Jiji la Mbeya kama kijiji

Mbunge Zitto Kabwe alitoa takwimu hizo kwenye page yake ya facebook muda si mrefu!Mtwara,Lindi then Tanga kwa umaskini Tanzania!!
Tanga ilikuwa zamani bhana, enzi zile miaka ya 80 wakati nasoma Usagara Sec, Tanga ulikuwa ni mkoa wa 2 au wa 3 kwa ukubwa kama sijakosea. Lakini tokea walipoua viwanda vya Mbolea (TFC), CIC, Sikh Saw Mills, Chuma (T) Ltd, NASACO, BANDARI, Shirika la Reli, Zao la Mkonge nk, kila kitu kimeanguka chali imebaki Kiwanda cha Saruji tu...
 
Kwa hiyo kama hamna NSSF,PSPF na wengineo ndiyo HAMNA maendeleo?Mwanza na Moshi ambao hao NSSF wanajenga wanaishinda Mbeya nn?Labda ndiyo tuanzie hapo!!
Pamoja na kuanzia hapo, pengine ningekuuliza vile vile,
Je waridhika na maendeleo ya Jiji la Mbeya?
Jiji ambalo hata mkuu mmoja wa mkoa Daniel Ole Njoolay aliwahi kuliita kijiji kikubwa.
Jiji halina jengo la hadhi, halina ukumbi wa mikutano wa hadhi, halina hoteli yenye heshima, hoteli zote ni za wawekezaji wadogo wadogo.

Sasa Malafyale kama umeridhika na hilo then you have very low standards indeed!
 
Last edited by a moderator:
Kwakweli, mimi naona tatizo la mbeya ni serikali na mashirika yake , pamoja na mashirika binafsi, kutowekeza jijini mbeya.

Kwa vyovyote mbeya huwezi kufananisha na majiji mengine ya siku nyingi kama dar. Vipo vigezo vingi sana. Wengi wametetea hapa kuwa mbeya inaendelezwa na watu wa kawaida waishio mbeya, mimi ingekuwa kushauri serikali ningetumia jiji la mbeya ili kuiletea neema tanzania kwakuwa iko mpakani mwa nchini nyingi; malawi, zambia, congo na nchi za mbele zaidi kuelekea south africa.
Kwanini balozi zote ziwekwe dar, headquarters zote dar, pia wangegawanya baadhi ya shughuli kubwa za kitaifa na kimataifa ziwe zinafanyika kwenye majiji nje ya dar mf mikutano ya sadc, kufanya hivyo kungewalazimu serikali kujenga hayo mahotel na miundo mbinu bora zaidi ya hii, na si serikali tu bali hata wadau kama nssf na wajasiliamali ungeona mara moja nao wanakuja kuwekeza katika mambo kibao ya kimaendeleo jijini.
Nasema serikali kwanza ifanye hivyo, then private sector wataingia kiurahisi bila kuitwa. Kwasasa fursa za uwekezaji zipo, ila serikali haijachagiza zaidi mf ni vema uwanja umejengwa, tena mzuri, kidogo mambo yamebadilika, lakini bado kwanini wasiamue kuelekeza baadhi ya ndege za nje kutua na kutokea mbeya? Dar inachangizwa zaidi na serikali yenyewe, kuwepo kwa ikulu, maofisi ya wizara zote na mawakala wao kumepelekea hata sekta binafsi kuelekeza nguvu zao karibu nao. Sasa mtu ajenge hotel ya nyota 3 au 5 mkoani wakati hakuna wateja wa uwezo huo?
 
Pamoja na kuanzia hapo, pengine ningekuuliza vile vile,
Je waridhika na maendeleo ya Jiji la Mbeya?
Jiji ambalo hata mkuu mmoja wa mkoa Daniel Ole Njoolay aliwahi kuliita kijiji kikubwa.
Jiji halina jengo la hadhi, halina ukumbi wa mikutano wa hadhi, halina hoteli yenye heshima, hoteli zote ni za wawekezaji wadogo wadogo.

Sasa Malafyale kama umeridhika na hilo then you have very low standards indeed!

Mkuu naona unajichanganya sana
1.Umesema Mbeya hamna hotel yenye hadhi then ukageuka ukasema Mbeya ina hotel zote ni za wawekezaji wadogo wadogo!Wapi hapa TZ kuna hotel nzuri zisizo za wawekezaji wadogowadogo?

2.Mbeya hakuna jengo la hadhi?Una maana gani hapo?

3.Olle Njoolay anatoka Arusha/Manyara,anakotoka kunaizidi Mbeya?Kwa lipi?
 
huyo azusa angalia tu argument yake utajua ni mweupe kichwani,anazungumzia uzuri kwa kuangalia na macho yake na kisha ana conclude mzunguko wa pesa! Kazi ipo

ujue hata viongozi wetu wanabahatisha kufanya maamuzi wengi wao
 
A City in da house baby!!!!!!!!!!!! kitu Arusha bana!!!

DSC00930.jpg






DSC00903.jpg

DSC00911.jpg
 
Mbeya City ongeeni kwa picture bana kama hizi za Arusha.....A City in da house....

02Reception.jpg








DSC00934.jpg







DSC00928.jpg










DSC00907.jpg
 
du, karne hii bado mtu unafikiria habari kijiji na uchawi,umefirisika kimawazo kwelikweli,wenzako tunawaza jinsi ya kufanikiwa wewe unawaza uchawi, mchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe.wacha wanambeya tufurahie maisha yetu,chakula tele,huduma za jamii zakutosha, hata wewe mwenyewe tunakulisha pamoja na uchawi unaouzungumzia,pia angalia mbeya inavyochangia kwenye pato la taifa, halafu uendelee kuongea
 
kwa akili yako jiji linaloweza kuwa kitovu cha utalii kwa africa kama arusha linapaswa kuwa kama arusha ilivyo?. pia hotel za kitalii ujenge mbeya na hamna watalii ili iweje?.
Watu wangekuwa na akili kama yako, basi Mwanza injengwa kwa vile watalii wanaenda kutazama sangara!
 
mie nimezaliwa mbeya na kukulia huko.nakubaliana nawe mkuu,upo sahihi kabisa hasa suala la wafanyabiashara kukimbilia mikoa mingine ni kweli kabisa.wafanyabiashara wengi wamehama huu mkoa kwa sababu ya mazingira magumu ya kibiashara yanayosababishwa na viongozi wa mkoa huu.pia wengine walifikia hata hatua ya kujiua kama yule mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina la mgeni maarufu kama milamo.

hiyo bado sio point ya msingi kuzaliwa au kuwa mmbeya akuumanishi una hati miliki ya mbeya. mbeya ni ya watanzania wote kama unavyoweza kuishi sehemu yoyote ile tz bila bugdha ndio maana hata hao wafanyabiashara wa hapo wengi wametoka iringa na wametumia fursa hiyo kama watz tena muwashukuru ndo wanaoukuza mji. mwanza na arusha imekuwa juu kwa sababu watu wametumia fursa za kibiashara vizuri hata s.h. amon anatokea mbeya lakin anawekeza huko unaogopa kushika jembe alaf unataka maendeleo kingine ni vimila vyenu vya kurithi mtu akijenga nyumba ajengee na ukoo asipofanya hivyo mnamuondoa
 
kwa akili yako jiji linaloweza kuwa kitovu cha utalii kwa africa kama arusha linapaswa kuwa kama arusha ilivyo?. pia hotel za kitalii ujenge mbeya na hamna watalii ili iweje?.

Hapo umenena mkuu....Arusha ndio kitovu cha utalii Africa nzima....ilipaswa kuwa mbali mno.......hizo ndio changamoto...:suspicious:
 
Watu wangekuwa na akili kama yako, basi Mwanza injengwa kwa vile watalii wanaenda kutazama sangara!
mwanza ina watu laki saba na nusu utafananisha na mbeya ya watu laki tatu na themanini?. mwanza pia ni centre ya biashara ya lake zone tofauti kabisa na mbeya. tumia akili wewe.
 
hakuna jiji tamu kama dar es salaam mkuu usidanganyike na kelele za wakuja
 
Kwa chakula ni hapo city pub,ila huduma zao vilevile bado zipo chini.IMBOMBO SYA BAN'TU
 
Back
Top Bottom