Wana JF kuna utapeli ambao kwa sasa umeenea maeneo ya kariakoo, najua wapo matapeli miaka yote ila nimeona niwatahadharishe wale ambao wanadhani hawapo. Juzi nilikuwa mtaa ule ambao vifaa vingi vya Ujenzi huuzwa, ni bahati mbaya sana kuwa pamoja na kuishi hapa mjini muda mrefu sifahamu sana mitaa hiyo kwa majina, wakati naendelea na shughuli zangu mara akatokea mtu mmoja ambaye anakila sifa za kuitwa mheshimiwa, alikuwa amevalia suti na vikwelombwezo vyote, tulipokutana alianza kutabasamu na kunichangamkia kana kwamba tunajuana, alinisabahi kwa kuanza hivi,
Tapeli '' aisee mbona kama nakufahamu?
Nikamjibu inawezekana
Tapeli - Hivi hujawahi kuishi mikoa ya Arusha , Tanga au Mbeya? wewe ni mwenyeji wa wapi? aliuliza maswali yote hayo kwa mpigo
Nikamtajia.
Tapeli - Ooooha sawa, akajitambulisha kuwa yeye ni Daktari wa Upasuaji pale Hospital ya wilaya (wilaya ninayotoka). Huna ndugu yako ambaye ameshalazwa pale, MIMI nikamwamnia wapo wengi, akadai kuwa anafahamiana na ndugu yangu mmoja anaitwaaaa .. hakutaja jina mimi nikamtajia mmoja a yeye akadakia ''aah ndiyo mbona tunafahamiana naye sana? akadai wanafahammiana.
baada ya hapo daktari yule akaniambia kuwa yeye ni mwenyeji wa Mkoa ambao mimi nimetoka na kwambwa anafahamiana na Mdogo wangu huyo na kwamba anamsaidia sana anapokwenda kutaka matibabu.
Aliendelea kunieleza kuwa ametokea mnazi mmoja, kuna Daktari mwenzake ambaye amekwemnda kumuomba amsaidie kiasi cha fedha, maana yeye ametoka mtwara kwenya mazishi ya Baba mkwe wake yeye na familia yake na anaelekea wilaya ambayo amenitajia kuwa ndiko anakofanyia kazi( kumbuka hiyo ndiyo wilaya ninayotoka), akaendelea kunieleza kuwa amefika na ndege ya asubuhi kutoka huko mtwara, na kwamba pale Airport alikodi taxi kwenda Ubungo akidhani kuwa ni sh. 10,000 kumbe ni sh. 40,000, ambazo ndizo alizokuwa amebaki nazo kama nauli yake pamoja na famila yake, hivyo alikwenda hapo Mmnazi mmoja kwa Rafiki yake ambaye ni Daktari ili amuongezee lakini kwa bahati mbaya hakumkuta hivyo akaomba nimpatie kiasi hicho cha sh. elfu 40 atanirudishia kwa kumpatia mdogo wangu ili aniletee. kabla ya hapo alikuwa amekwisha niuliza kuwa mimi hapa mjini ninashuguli gani.. pamoja na kwamba mimi sio mtu wa kutaja ofisi ninayofanya kazi niliona nimtajie kwani sikuwa na shaka kuwa mtu niliyekuwa nazungumza naye ni tapeli, hii ilikuwa mapema sana wakati maongezi yetu hayafika mbali hivyo alijua fedha atapata.
kutokana nakudai kuwa yeye ni mwenyeji wa Mkoa ninaotoka, na ukizingatia kuwa wenyeji wa mkoa ule hupenda sana kuzungumza kilugha, ilibidi niingie moja kwa moja..... looooo hapo ndiyo dili lilipoanza kuyeyuka, maana nilimuona akibadilika taswira, nikamhoji inakuwaje yeye ni mwenyeji wa kule tena mtu mzima hajui lugha? akasema unajua mimi sikukulia kule nilirudi ukubwani....
hapo nilishtukia dili na nikajiridhisha fika kuwa hapa kuna kitu, nilichokifanya nilimweleza kuwa pesa niliyokuwa nayo haitoshi kumpatia ila kwa kuwa yeye ni maarufu aende tu akawaambia makondakta wa mabasi yaendayo huko anakokwenda watamwelewa...
Hiyo ndiyo kosakosa ya kutapeliwa niliyokutana nayo Kariakoo, hivyo be careful unapokuwa Kariakoo na maeneomengine hapa jijini.