Jifunze kumbusu mwenzio kila mara;usisubiri mshahara mezani umpe busu

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Ni kubusu tu!



Usiweke kiwango cha chini kumbusu mume wako au mke wako.

Hakikisha unambusu kila siku kabla ya kuagana asubuhi, muda wowote mchana na kabla ya kulala usiku hata usiku wa maneno ukikumbuka kwani kubusu ni kipimo cha hali ya mapenzi katika ndoa​
 
Busu hiloooooooo pokea! Busu husaidia kuwezesha moto wa mahaba kuendelea kuwaka kati ya wapenzi.
Kumbuka mpenzi wako huhitaji kujisikia yupo appreciated na zaidi anapata mapenzi (love and affection) kutoka kwako na njia nzuri ni kumpa busu.

Bahati mbaya ni kwamba wanandoa wengi wameshikwa na kunaswa na mtego wa u-busy hadi imefika wanasahau kuwabusu wapenzi wao.
Niambie wewe unayesoma sasa hivi hapa umembusu mke wako au mume wako lini?
Nahisi umesahau!

Plainly; mahusiano yanahitaji kazi, hasa kwa huyo special someone wako in your life kama ulifanya kazi kumpata kwa nini sasa ulegeze kamba, kaza uzi hakikisha uzi uleule uliotumia kumpata ndo huohuo unatumia kudumisha penzi na si kudumu tu bali linakuwa sustainable.

Kubusu hujenga intimacy kati ya mke au mume pia hufanya bonding iwe strong na kuhufanya wewe mwenyewe ujisikia vizuri na afya njema.

Nini faida za kubusu kiafya?
Busu ni afya kwa meno yako, wataalamu wamefanya tafiti na kugundua kwamba busu kuzuia plague kujijenga kwenye meno na hii ina maana utapunguza safari kwa daktari wa meno.

Busu ni afya kwa moyo wako (heart) kwani wakati wa kubusiana mnazalisha adrenaline ambazo husababisha moyo kuongeza speed na damu kwenda sehemu zote za mwili.

Kila mwanaume au mwanamke ambaye humuaga mwenzake asubuhi kwa busu utafiti unaonesha anaongeza miak 5 zaidi kuishi duniani.
Kama huwa hubusu wakati unaagana na mwenzi wako asubuhi unajipiga panga miaka 5 kuishi.

Kubusu hukuongezea self esteem na kujisikia upo appreciated kwani busu ni tamu na raha.

Mabusu hupunguza kuzeeka (aging) kwani mnapobusiana huhusisha misuli zaidi ya 29 kwenye eneo la mashavu na shingo.

Kubusu huchoma calories kati ya 6 – 12 na mkiongeza na love making huweza kufikia 300 na utajisikia raha.

Kubusu huondoa stress, huweza kutoa ocytocin, homoni ambayo hufanya mtu kujisikia vizuri.

Hakikisha unapobusu ni zaidi ya sekunde 10 ili kupata matokeo.

Hivyo basi wewe na mpenzi wako go ahead, kwa afya na furaha sherehekea kila siku kwa kupigana mabusu.

Je, kuna aina ngapi za mabusu?

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom