JICHO PEVU: JK usimshauri tena raisi mwingine kuhusu usalama na amani ya nchi yake

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Mheshimiwa raisi, awali ya yote hongera kwa hotuba yako ya mwisho wa mwezi maana ilijaa lugha tamu ya kidiplomasia inayo onyesha ni namna gani ulivyo muungwana na usiye penda magovi au migogoro na nchi majirani zetu kwenye ukanda wetu. Hotuba yako imeonyesha ni namna gani una dhamira ya dhati ya kuona utulivu una shamiri kwenye nchi majirani zetu. Hotuba yako ilionyesha ukomavu mkubwa sana wa dhamira ya kuona amani ambayo ni tunda la haki ikitamalaki kwenye nchi za wenzetu, katika kipindi chako dhamira yako ulisha ionyesha na ukaitenda kwa vitendo nchi jirani ya kenya, ulifanya hivyo kwa Commoro na Madagascar, huko kote uliko toa ushauri wako hukuwahi kutukanwa wala kubezwa bali ulipewa sifa na kuonekana shujaa na hata ulipo amua kutumia vikosi vya majeshi yetu hakuna aliye hoji dhamira yako ya kuitafuta amani. Kwa majirani zetu wa Rwanda imekuwa tofauti, wao ushauri wako kwao imekuwa nongwa, wamekubeza, wamekutukana, wamekunanga na wamefikia hata hatua ya kukutishia kukupiga.

Binafsi ulipo toa kauli kule Kagera kuwa majeshi yetu yako imara na mipaka yetu iko salama huku ukitahadharisha atakaye leta chokochoko kukiona cha mtema kuni nilijua unajibu mapigo kwa kagame, kumbe hukuwa na maana hiyo wala dhamira hiyo, niliogopa nikajua unataka twende tukamchape kagame. Mungu ashukuriwe hekima ya kidiplomasia bado iko kifuani pako japo mwenye jicho la tatu akikusoma katikati ya mistari anaona fukuto lisilo kuwa na afya kati yako na kagame.

Hata hivyo, baada ya kusikiliza hotuba yako, leo nataka kuwa mshauri wako kuhusiana na dharau, matusi na dhihaka zilizo onyeshwa na wanyarwanda, kwako na kwetu sisi watanzania, najua una washauri wengi na wabobezi kwenye mambo mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, kitamaduni, kijamii na hata kiimani, najua washauri wako wanafanya kazi yao vizuri usiku na mchana kwa weledi na kwa ufanisi wa hali ya juu.

Busara imenituma kukushauri, mimi ni muungwana wa kijiwe cha kahawa nisiye kuwa na wadhifa wala hadhi ya kukuona ninapo jisikia kufanya hivyo kwa muda wowote lakini najua nina uwezo wa kukufikia kwa njia ya maandishi ambayo kwangu ina nguvu kuliko kuja kubisha hodi kwenye nyumba tuliyo kupangisha.

Kabla sija kushauri naomba nianze kwa kunukuu maneno yako kwenye hotuba yako ya mwisho wa mwezi, umesema "Ushauri si shuruti, ushauri si amri, una hiyari ya kuukubali au kuukataa" kwa heshima na taadhima naomba ushauri huu ninao kupa wewe usiukatae kwa sababu eti si shuruti au amri. Wewe nifanye mimi mjinga na upokee tu maana nataka kukuepusha na kikombe cha matusi na dharau kutoka kwa viongozi wa nchi nyingine ambao huenda baadae ukajisikia kuwashauri kama ilivyo tokea kwa Kagame na wao kuamua kufuata mkondo aliofuata Kagame na kuamua kuporomosha matusi na kejeli kwetu halafu dunia nzima ikajua tena kuwa ile nchi ya Nyerere iliyokuwa inaheshimika sasa hivi imekuwa ubao wa matusi na kejeli. Wapo watakao sema Nyerere amekufa na heshima ya nchi yake na walio baki wote ni dhaifu tu! japo inawezekana kuna wadhaifu wachache.

Mheshimiwa raisi, kipindi hiki achana kabisa na nia au dhamira ya kutoa ushauri kwa kiongozi yoyote mwenye nchi yenye mgogoro wa amani, natambua unajua kuwa amani ni tunda na zao la haki bali amani si tunda na zao la maombi kama baadhi ya viongozi wa chama chako wanavyo potosha. Lakini pia natambua kuwa haki ina mbegu ya upendo ndani yake. Hivyo kabla hujatenda upendo kwa mtu mwingine lazima ujipende kwanza wewe mwenyewe na kabla ya kuonyesha njia ya haki ni lazima wewe mwenyewe ujitendee haki na kuonyesha kweli kuwa haki imetendeka.

Msingi wa mimi kukushauri usimshauri tena kiongozi mwingine wa nchi nyingine umelala kwenye mafundisho ya dini zetu tunazo ziabudu, dini zote zinatabia moja kuu, zinafundisha upendo na kutendeana haki huku zote zikiamini kuwa haki ndio msingi wa upendo na amani.

Mafundisho ya dini yanatufundisha kuusema ukweli hata kama uta umiza vishikizo vya mioyo yetu, lakini pia mafundisho hayohayo yanatufundisha kuondoa kibanzi kwenye macho yetu kabla hatuja fikiria kuondoa boriti kwenye macho ya wenzetu, hii ni misingi muhimu sana tuliyo wekewa kwenye mafundisho ya dini zetu na naamini ni udhaifu wa kutokufuata mafundisho haya ndio kumesababisha wanyarwanda kutudharau, kukudharau wewe na hata kukutukana kama nilivyo kusikia ukilalamika.

Katika kipindi cha uongozi wako hasa n'ngwe hii ya mwisho kumekuwa na matukio mabaya sana naya Kuogofya ambayo pia naamini hata shetani ametushangaa sisi kama watanzania kwa matukio mabaya yaliyotokea na kuwa tabia ambayo hatukuwa nayo mwanzoni! Wapo watanzania wenzetu walio uwawa au kupoteza maisha mikononi mwa polisi, kumetokea vifo vingi vyenye utata, kuna watu walitekwa, wameteswa na kung'olewa meno na kucha bila hata ganzi haya yote yametokea na sauti za watanzania zikapazwa lakini jitihada zako za dhahiri za kukomesha vitendo hivi hazija onekana kwa dhati. Ndio maana nikasema nikushauri kwa dhati ya moyo wangu ili uhakikishe kwanza haki inatendeka nyumbani kwako kabla ya kwenda kushauri kwenye nyumba ya Kagame.

Japo kabla yako nilisha hadithiwa kuwa yaliwahi kutokea mauwaji ya Mwembe chai na vurugu za uchaguzi wa zanzibar ambazo zilisababisha vifo vya makumi na wakimbizi kule shimoni (mombasa) nchini Kenya wakati wa mzee mkapa lakini pamoja na hayo nimejikuta najiuliza maswali.

• Umethubutu vipi kwenda kumshauri Kagame apatane na waasi wakati wewe umeshindwa kutekeleza ombi la muda mrefu la barua ya chama hasimu (chadema) kwa chama chako kuhusu kuunda tume huru ya kimahakama itakayo ongozwa na majaji kuchunguza vifo vyenye utata vilivyo tokea kwenye mikutano ya chama hicho pamoja na vifo vingine vyenye utata?!

• Umethubutu vipi kwenda kumshauri kagame wakati wewe ni amiri jeshi mkuu wa majeshi na jeshi lako la polisi kwenye ripoti mbalimbali linaonekana kuwa ni jeshi ambalo linakiuka haki za raia ikiwemo kubambikiza kesi na kutunga mashtaka ya uongo na kesi za ugaidi ambazo hazipo? Ulisha kaa na Polisi kama amiri jeshi mkuu kukomesha tabia hii ili litende haki kwa watanzania?

• Umepata wapi uhalali wa kimaadili (moral authority) kutumia busara kumshauri Kagame aongee na wakinzani wake kisiasa wakati wewe umeshindwa japo kukaa na viongozi wa upinzani husasi chadema kujadilina nao na kujua sababu za wao kukamatwa mara kwa mara na kuwa na kesi za mfululizo zisizo kuwa na kichwa wala miguu huku jeshi la Polisi likiwaandama kuliko linavyo wandamana na kuwanyamazia viongozi wa ccm hata wanapo toa kauli zenye utata?!

• Nimejiuliza, umepata wapi mamlaka ya kimaadili kumshauri Kagame aongee na waasi wapinzani wakati wewe kupitia hotuba yako ya mwisho wa mwezi ulisha wahi lalamika kuwa chadema wanafanya maandamano ili kuondoa serikali iliyoko madarakani kihalali kama ilivyo tokea Misri na Libya huku ukiwa hujawahi kukaa na chadema hao hao ukawauliza kama ni kweli walikuwa na mpango huo?! Na mlifikia muafaka gani ili wauache mpango wao maana uliwatahadharisha wananchi juu ya maandamano ambayo ni haki ya kiraia?

• Bado najiuliza, umepata uhalali gani wa ki-maadili kumshauri Kagame aongee na wapinzani waasi wakati wewe umeshindwa japo kuwapa pole chadema (chama pinzani hapa nyumbani) ambao ni wahanga walio lipuliwa mabomu kwenye mikutano yao kadha huku wewe ukikaa kimya na kushindwa kutoa japo pole wakati si kawaida yako kwenye mambo ya misiba?!

• Naendelea kujiuliza, umepata uhalali gani wa kimaadili kumshauri Kagame aongee na wapinzani waasi wakati waziri wako mkuu akitoa amri zenye utata mara kadhaa kupitia bunge?! Mara anaye uwa albino naye auwawe, mara "liwalo na liwe", mara "wapigwe tu maana sasa tumechoka" hivi nyinyi mlio choka mnatoaje ushauri kwa wengine ambao hawaja choka?!

Raisi wangu, dawa pekee ya kuepuka matusi na kejeli na kutuepusha sisi na kikombe cha kejeli dhidi ya mataifa mengine achana na habari za kutoa ushauri kwa wengine, tukae chini tumalize matatizo yetu, tutoe boriti kwenye jicho letu ndio turuke kiguu na njia kwenda kuwa shauri wengine wenye matatizo. Kaa chini utatue sintofahamu ya Mtwara na ikiwezekana anza hapo hapo ikulu kwa kuwauliza walio tangazia taifa kuwa viongozi wa CUF walio pata kibao kutoka kwa wanajeshi kule Mtwara eti ni vibaka, ikulu yako ina halalisha vibaka wale mkong'oto na sio kufikishwa kwenye vyombo vya sheria?!

Mheshimiwa, Sisi yetu yanatushinda kwa nini tuwe na upendo wa mshumaa wa kumulikia wengine huku tukiteketea?! Amani yetu inapotea kutokana na haki kukandamizwa kwa nini tusijenge misingi na nguzo imara za haki zitakazo simika amani ndio tutoke kwenda kushauri wengine na wengine watakao taka waige kutoka kwetu?

Chukua ushauri wangu ninao utoa kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu na kwa kuwa tuko kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa ramadhani kabla ya kufungua kwa sikukuu ya eid nikutakie funga njema na Eid Mubarak Sheikh Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Sidhani kama kuna sababu yeyote itayomfanya mtu yeyote asitoe ushauri wowote.

Vilevile sidhani kama ushauri ni lazima ufuatwe.

Na amani siyo tunda la haki. haki inaweza kuvunja amani, na amani inaweza kuvunja haki.
 
Mohamedi Mtoi maneno ya busara sana haya, naomba washauri wa JK wamwambie asome khabari hii hapa JF neno baada ya neno, kifungu baada ya kifungu halafu atafakari then achukue hatua mara moja..
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la Kikwete hana Hekima, yeye amekariri tu kuwa atapata sifa kwa kuropoka.

Hivi kama kweli Kikwete alikuwa na nia njema kwa Kagame na Nchi ya Rwanda kwanini ushauri wake asingempa Kagame kwenye Kikao cha Faragha na sio kumwambia hadharani?

Kulikuwa kuna haja gani kwa Kikwete kuja hadharani kusema kuwa 'Amemuamuru' Rais wa Sudan awakamate mara moja wahusika wa mauaji ya Askari wa Tanzania Darful?
 
ndani ya CCM mbona sijawahi ona mtu akitumia muda wake mwingi na akili kuandika makala nzuri na tamu kiasi hiki?hakuna wenye akili?au wana akili za kutuka dr slaa,lema na mbowe tu???
asante bro mohamed Mtoi
 
Last edited by a moderator:
ndani ya CCM mbona sijawahi ona mtu akitumia muda wake mwingi na akili kuandika makala nzuri na tamu kiasi hiki?hakuna wenye akili?au wana akili za kutuka dr slaa,lema na mbowe tu???
asante bro mohamed Mtoi

Matusi kwa viongozi wa upinzani ndio yanayo lipa mkuu! Bila shaka mgao unaendana na idadi ya matusi. Ha ha ha.
 
Last edited by a moderator:
Kuna chuo kimeanzishwa pale Kunduchi cha National Defence.........naimani viongozi wengi wa vyama vya siasa Tanzania watapata fursa ya kwenda kujifunza pale, kwa vile sio chuo cha kijeshi pekee...! Kuna mambo mengi kuhusu national defence ambayo sio rahisi kwa raia tu wa kawaida kuyaona. Tulipokubali mwaka jana kuwapa uraia watu 165,000 toka Burundi haikuwa jambo rahisi, sasa usipoweka mambo yako sawa hii hali itaendelea kuwa hivyo kila machafuko yatakapotokea nchi jirani. Wale wakimbizi wa Rwanda kule Ngara walilazimishwa kuondoka kinyume na kanuni za kimataifa, laiti wasingewalazimisha mpaka leo tungeendelea kuwa nao kama walivyobaki Congo, idadi yao ilikuwa 500,000. Embu jiulize, pamoja na kuwalazimisha kurudi kwao bado wapo kadhaa walikataa katakata mpaka tukawapa uraia wanyarwanda 30,000. Kwa machafuko ya miaka ya tisini tu tayari tumewapa uraia wakimbizi karibu 200,000 achana na wale waliongia kinyemela na kujificha. Idadi hiyo ni kubwa kuliko hata baadhi ya makabila hapa kwetu.....! Sasa watu wanafikiri aliyosema Kikwete ni ya Kikwete, no hayo ni ya Tanzania kama taifa...!
 
kwangu mimi sion kosa alilolifanya mh Rais wetu na wala kumshauri PK kwenye mkutano wa AU pia sio kosa.
PK unless ana kitu kingine ila kama ni huu ushauri tu basi ameprove kuwa mtu wa ajabu sana mbele za watu wengi duniani.
Binafsi namwona PK kama rais ambaye anapenda kuona wanyarwanda wakiteseka na kusulubiwa pasi sabab za msingi.

so far JK lichungulia mbali anajua fika kwamba haya mapigano mwishowe ni mzigo wa wakimbizi kwa TZ na ndivyo walivyozoea na akikaidi siku akiingia vitan wasije kuomba hifadhi kwetu hatutawapokea.
 
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ametufundisha nini kuhusu majirani zetu?

wewe ni lazima umekurupuka tu. hii mada wala hata haujaisoma! kama kweli umeisoma hebu twambie Mtoi kasema nini kuhusu majirani zetu? hasa Kagame... Mtoi kasemaje?
 
Mh.Kikwete, tatizo lake ni moja.....kutafuta makuu kupitia kuungwa mkono na Jumuiya ya kimataifa.

ingawa kauli yake haikuwa na ksoro sana kidiplomasia, lakini naye hana guts za kuendelea kumnyoshea kidole Kagame wakati vyombo vyake vya dola hapa Tanzania vinawatendea raia isivyo halali.
 
Mkuu nguvumali

Umeweka sawasawa kisu kwenye mfupa, na ndio maana ushauri wangu kwa mkuu ni kutaka kuondoa boriti kwenye jicho lake kabla hajaondoa kibanzi kwenye jicho la kagame.

Naamini akiamua anaweza, akisha jisafisha ana uwezo wa kwenda na kumshauri yoyote. Lakini kwa sasa apumzike kwanza maana kuna mambo mengi machafu yanayo mtia doa na Tanzania kwa ujumla tena mengine yakihusisha watumishi wa taasisi yake kama jinsi tunavyo soma kwenye baadhi ya vyombo vya habari hususani gazeti lililo fungiwa la mwanahalisi.
 
MIAKA YAKE MITATU ILIYOBAKI ATUMIE KUIJENGA TANZANIA YETU, atumie kuunganisha taifa lililosambaratika kwa matukio na mikasa ya kidini na kisiasa.
na ndio maana msimamo wake dhidi ya Rwanda na na mtizamo wa USA dhidi Rwnda unatazamwa kama wenye kutia shaka na hasira kwa serikali ya Kigali.
Sioni mantiki panaa ya kuendelea kubishana na Kagame , ambaye daima anapambana kujijengea umaarufu na nguvu ndani ya serikali yake na ndani ya mioyo ya wanyaruanda. sisi tusijitie ukiranja kama tu hagusi maslahi ya TAIFA LETU.
 
Mwandishi usichanganye mambo ya kitaifa na kimataifa. Kwa hoja zako Rais ataishia kuwa bubu.
 
Kuna chuo kimeanzishwa pale Kunduchi cha National Defence.........naimani viongozi wengi wa vyama vya siasa Tanzania watapata fursa ya kwenda kujifunza pale, kwa vile sio chuo cha kijeshi pekee...! Kuna mambo mengi kuhusu national defence ambayo sio rahisi kwa raia tu wa kawaida kuyaona. Tulipokubali mwaka jana kuwapa uraia watu 165,000 toka Burundi haikuwa jambo rahisi, sasa usipoweka mambo yako sawa hii hali itaendelea kuwa hivyo kila machafuko yatakapotokea nchi jirani. Wale wakimbizi wa Rwanda kule Ngara walilazimishwa kuondoka kinyume na kanuni za kimataifa, laiti wasingewalazimisha mpaka leo tungeendelea kuwa nao kama walivyobaki Congo, idadi yao ilikuwa 500,000. Embu jiulize, pamoja na kuwalazimisha kurudi kwao bado wapo kadhaa walikataa katakata mpaka tukawapa uraia wanyarwanda 30,000. Kwa machafuko ya miaka ya tisini tu tayari tumewapa uraia wakimbizi karibu 200,000 achana na wale waliongia kinyemela na kujificha. Idadi hiyo ni kubwa kuliko hata baadhi ya makabila hapa kwetu.....! Sasa watu wanafikiri aliyosema Kikwete ni ya Kikwete, no hayo ni ya Tanzania kama taifa...!
Hayo ni maneno yake na hao wanaojifanya wanajua usalama wa taifa wakati ni sifuri hata kazi yao hawaijui siku hizi si ya watanzania! wala si kweli national defence lazima ifundishwe chuoni..
 
Sidhani kama kuna sababu yeyote itayomfanya mtu yeyote asitoe ushauri wowote.

Vilevile sidhani kama ushauri ni lazima ufuatwe.

Na amani siyo tunda la haki. haki inaweza kuvunja amani, na amani inaweza kuvunja haki.
Hapo ndipo tunapochanganya mambo mkuu,watu wanajaribu kuibua mambo ya ndani ili kutafuta sababu ionekane JK kakosea vitu vya ajabu kabisa,kwani JK kukataa kukutana na DR wa ukweli Slaa ndio linatufanya tushabikie raisi wetu kutukanwa???Kwani vita vinavyoendelea DRC na Rwanda kwenyewe havituhusu???hatuna wakimbizi wao hapa???Au tunataka raisi wetu akienda kukutana na maraisi wenzie ajifunge plasta mdomoni asiongee chochote maana kuna baadhi ya maraisi atawaudhi???Hii si kweli mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.TUSICHANGANYE MADA HAPA,KILA MADA ILETWE KIVYAKE IJADILIWE.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
Pamoja na maneno mengi mazuri uliyotumia ktk kumshauri JK, Bado sioni tatizo ktk ushauri alioutoa Jk kwa PK.
Ndio anahitaji kutengeneza mambo nyumbani kwake, lakini wakati huohuo anahitaji kutuwakirisha nje. Tupende tusitake, bado yy ni rais wetu!
Kama rais wa Tz, anawakati mgumu sana kwa kutokuchua hatua muafaka kwa wakati, sasa ukiangalia kila sehemu ya Tz ni vurugu: muungano, siasa za ndani, uchumi,nk!
Nafikiri ushauri anaotakiwa kupewa ni kutokua na uchaguzi ktk kutoa maamuzi sitahiki.
Kama jinsi anavyopenda wengine wawe na amani, basi nasi tunamuhitaji awe kiongozi bora na sio bora kiongozi!
 
Asante Mohamed,
Ni bahati mbaya kuwa uchambuzi na upembuzi wako huu watauita majina mengi ili kuonesha "huna uzalendo wewe". Watashambulia nafsi yako, utu wako badala ya kujibu hoja au kukinzanisha hoja kwa hoja.

Ila niseme tu, naungana nawe ktk hayo maswali maana JK anataka kuwa champion wa convenience externals.

Jirani zetu hawawezi kumjua JK na wala haiwapasi kumjua kivile.....ila sisi Watanzania inatuhusu. Sasa kwa udhaifu wake binafsi na serikali yake umeiingiza Tanzania ktk mambo mengi tu mabaya kama vile udini, ukabila, ufisadi, rushwa, madawa ya kulevya, uhalifu na mauaji (holela na/au ya kupangwa) nk nk

JK ni Rais wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania. Sisi tunataka Rais wa Tanzania kwa ajili ya kila jema la Watanzania. Kwa hiyo kwa sehemu amejitakia. Kuna msemo unasema ...."hakuna kitu hatari kama 'nia njema'"
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
Pamoja na maneno mengi mazuri uliyotumia ktk kumshauri JK, Bado sioni tatizo ktk ushauri alioutoa Jk kwa PK.
Ndio anahitaji kutengeneza mambo nyumbani kwake, lakini wakati huohuo anahitaji kutuwakirisha nje. Tupende tusitake, bado yy ni rais wetu!
Kama rais wa Tz, anawakati mgumu sana kwa kutokuchua hatua muafaka kwa wakati, sasa ukiangalia kila sehemu ya Tz ni vurugu: muungano, siasa za ndani, uchumi,nk!
Nafikiri ushauri anaotakiwa kupewa ni kutokua na uchaguzi ktk kutoa maamuzi sitahiki.
Kama jinsi anavyopenda wengine wawe na amani, basi nasi tunamuhitaji awe kiongozi bora na sio bora kiongozi!
Tatizo liko kwenye "...kwa nia njema....nili.." Kuna msemo unasema "nia njema ni kitu hatari sana"
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
Pamoja na maneno mengi mazuri uliyotumia ktk kumshauri JK, Bado sioni tatizo ktk ushauri alioutoa Jk kwa PK.
Ndio anahitaji kutengeneza mambo nyumbani kwake, lakini wakati huohuo anahitaji kutuwakirisha nje. Tupende tusitake, bado yy ni rais wetu!
Kama rais wa Tz, anawakati mgumu sana kwa kutokuchua hatua muafaka kwa wakati, sasa ukiangalia kila sehemu ya Tz ni vurugu: muungano, siasa za ndani, uchumi,nk!
Nafikiri ushauri anaotakiwa kupewa ni kutokua na uchaguzi ktk kutoa maamuzi sitahiki.
Kama jinsi anavyopenda wengine wawe na amani, basi nasi tunamuhitaji awe kiongozi bora na sio bora kiongozi!

Mkuu.

Nimekusoma na kukuelewa sana ndugu yangu, kinachotakiwa ni JK kuweka mazingira safi nyumbani kwake kabla hajachukua ufagio na kwenda kufagia uwanja wa jirani. Unajua kuwa yametokea mambo makubwa sana yaliyo hatarisha amani ya nchi yetu lakini hakusimama kidete kuyasemea, hivi unakumbuka ule mlipuko wa lile bomu kule Arusha?! Wale walio kufa na Kanumba utanzania wao hauna heshima mbele yake?! Mbona ameshindwa kutoa hapa pole huku bunge nalo likikiuka kanuni na kuendelea na vikao wakati kuna jambo kubwa limetokea?!
 
Back
Top Bottom