JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

View attachment 1526957
Vladimir Putin akiwa Tanzania 1972 pamoja na Samora Machel na Emerson Mnanangwa(Rais wa Zimbabwe)

-Putin alikaa Morogoro Tanzania kwa miaka 4 (1973-1977)akiwafundisha wapigania uhuru wa kusini
Ila bongo kuna wakati tunaichukulia kimasihara sana, ila hapa kuna hatari sana angalia hata na watu waliopita hapa.. Noma sana, respect
 
"HISTORIA

Huyu ndiye mwenye Mzizima yake sasa

Anaitwa mzee Jumbe wa Tambaza, ambaye zama za kale kabla ya kuwepo kwa Dar es Salaam, alikuwa mmiliki wa eneo lote lililoitwa Mzizma.

Yani kuanzia kule Magogoni, Ikulu, hadi Daraja la Salenda (Selander Bridge), njoo Upanga kule shule ya Tambaza hadi Makao Makuu ya Jeshi, nenda hadi Kisutu kisha ingia Uhindini yote na Posta yake, yote ilikuwa miliki yake halali.

Miaka ya 1860s, alilimega eneo hilo kuanzia Magogoni hadi Salenda na kumuuzia Sultan Majid wa Zanzibar ambaye alitumia eneo hilo kujenga majengo ya chuo Kikuu cha Kiislamu cha Daru Salaam (hivi sasa Ikulu) na hostel zake ambazo sasa ni Hospital ya Saratani ya Ocean Road.

Zama za miliki ya mzee Jumbe wa Tambaza, eneo lile la Magogoni hadi Salenda lilijulikana kama Mzizima kutokana na utulivu wake pamoja na wanyama wakali waliokuwepo. Ikawa kila aliyepita eneo hilo lazima mwili wake uzizime.

Eneo lake jingine, ukiingia huku Barabara ya Bibi Titi hadi Kisutu na kuja huku kwetu Kariakoo, liliitwa Tindwa na ndio ulikuwa mji haswa wenye wakazi kama mia sita (600) hivi.

Kusanyiko la eneo lake la Tindwa, alilouza na jingine kuligawa bure tu na kugawa, na miji ya Kunduchi na Mbwa Maji, ndio iliyounda Jiji la Dar es Salaam hii ya sasa ambayo:

Jina hili la Dar es Salaam lilibadilishwa na Wajerumani toka jina la Daru Salaam lililotokana na jina asili la Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Daru Salaam chuo ambacho baadae Wajerumani walilifanya kama Ikulu baada ya kusafirisha Waislamu kimabavu miaka ya 1870s.
#IMENUKULIWAView attachment 2025692
Kwann wasungu waliyabadilisha majini asili ya waasisi wa maeneo na kubatiza majina yao.....ni chuki au ndo usungo tu?
 
View attachment 1519845
Wakongwe wanaikumbuka?? Mgiriki alivyoanzisha Sheraton akampa binti yake ikamshinda hii wakafunga December 1998 mpaka saivi wanaishi popo tu pale
.
.
.
.
.


Dar — es-Salaam - In A surprise move, the management of Motel Agip in Dar-es-Salaam, one of Tanzania's leading tourism and business facilities, this week confirmed plans to close the hotel despite indications that the hotel industry was picking up.


The 57-room hotel in downtown Dar is slated to close on December 18 after 35 years of operation. More than 150 workers will be laid off. The hotel's managing director, Mr. Emmanuel Mantheakis, told The East African that the decision to close down had been taken to allow shareholders to run other businesses.
Imeshindikana kabisa kufufua hii?
 
LEO KATIKA HISTORIA Huyu Ndie Mtu Aliejenga MUHIMBILI
HOSPITAL, Anaitwa Sewa Haji Paroo Alifika
Zanzibar Akitokea Ktk Miji Ya Bhuj Na Kutch
Na Mnamo Mwaka 1852 Alifungua Duka La
Bidhaa Mbalimbali Huko Zanzibar, Mnamo
1860 Akafungua Duka Lingine Kubwa
Bagamoyo Na Kuweka Makazi Yake, Biashara Zake Zikawa Kubwa Na Kuwa Tajiri Mkubwa Sana, Alisaidia Watu Wote Bila Kujali Rangi, Dini Wala Kabila Zao, Alinunua Majengo Mengi Na Kuyafanya Maeneo Ya Watu Wasiojiweza, Alijengaja Mashule Na Hospitali Kadhaa, Ktk Mji Wa Mzizima { Leo Inaitwa Dar es Salaam}.

Alijenga Hospitali Akaiita Sewahaji
Hospitali Ikitoa Huduma Bure, Mnamo
February 1897 Sheikhe Sewa Haji Paroo
Alifariki Dunia, Ilikuwa Ni Huzuni Na Simanzi
Kwa Wakazi Wa Bagamoyo Na Mzizima Kwa
Kuondokewa Na Sheikhe Sewa Haji
Aliependwa Sana, Baada Ya Kufa Kwake
Wakoloni Baadaye Wakabadilisha Jina Kutoka Sewahaji Hospital Na Kuiita Princess Magreth Hospital, Na Mnamo 1963 Iliitwa Muhimbili Hospital, Na Mojawapo Za Wodi Inaitwa SEWA HAJI,
Sheikhe Sewa Haji Alale Mahali PemaView attachment 2025734
Na apa pia walibadilisha jina......nahisi ata zile gunduzi za ki biological na physical hawa wasungu hawausiki nazo wamebambia tu...
 
Benjamin William Mkapa (wa kwanza kushoto) na rafikize Phillip Magani (Mwenye Kofia) na John Kambona (wa kwanza kulia) wakiwa wanafunzi Saint Francis College (sasa Pugu Secondary).

Picha kwa hisani ya Kitabu cha Historia ya Maisha ya Rais Mkapa: My Life, My Purpose.

#Maktaba YetuView attachment 2028856
Sasa mh. Hayati Mkapa ule unene ni wamadaraka ua...apumzike kwa amani
 
View attachment 1592121

Josina Machel. mwanaharakati, Mwanamapinduzi, Mpigania uhuru wa Msumbiji, Mke wa kwanza wa Samora Machel Rais wa Msumbiji. binafsi namlinganisha na TAMARA BUNKE mwanamke jasiri msaidizi wa Major Ernesto CHE Guevara ama Salia Sanches Mwanamke shupavu Msaidizi wa Fidel Castro
Licha ya harakati zake Josina hakuonja matunda ya uhuru. alifariki na kuzikwa Dar es Salaam kabla ya uhuru wa Msumbiji
Kaburi lake liko maeneo gani chief?
 
Marehemu suleimani mwanyiro mwenye gitaa akiwa na max bushoke enzi hizo
Screenshot_20211203-182825.jpg
 
Back
Top Bottom