JF Karibuni Tanzania Professionals Network

Mr. Mtsimbe nakubaliana nawe sana kwa uliloanzisha, nami nipo mbioni kuwasiliana nawe na kujiunga na TPN kama mmojawapo wa Diaspora kwani baadhi yetu tunataka kuja nyumbani sasa.

Na nilikujua toka wakati wa Mnazi Mmoja Applied Computer nikiwa mwanafunzi wako.

Nakutakia kila la kheri na nimekuwa nafuatilia maendeleo ya TPN toka wakati bado kamati ya uanzishwaji.......hongera kwa juhudi zako binafsi na wale wote waliofanikisha ikafikia hapo.

Tupo pamoja, na tunakuja.........!!!!!!

Unataka kujiunga na TPN kutokana na kufahamiana na Mtsimbe toka Mnazi Mmoja ama kutokana na kuelewa Sera kamili za TPN?

Yaani umefuatilia TPN toka bado Kamati ya Uanzishwaji mpaka leo hii hukupata Hamasa ya kujiunga nayo? Mpaka moto huu ambao umewashwa hapa JF ndo umekufumbua macho? Hukuwahi wish kwamba ungekuwa among wanaotajwa kama Founding Members wa TPN?

Kuna namna hapa!!!
 
Mr. Mtsimbe nakubaliana nawe sana kwa uliloanzisha, nami nipo mbioni kuwasiliana nawe na kujiunga na TPN kama mmojawapo wa Diaspora kwani baadhi yetu tunataka kuja nyumbani sasa.

Na nilikujua toka wakati wa Mnazi Mmoja Applied Computer nikiwa mwanafunzi wako.

Nakutakia kila la kheri na nimekuwa nafuatilia maendeleo ya TPN toka wakati bado kamati ya uanzishwaji.......hongera kwa juhudi zako binafsi na wale wote waliofanikisha ikafikia hapo.

Tupo pamoja, na tunakuja.........!!!!!!

Kipanga Mweupe karibu sana. Kwa wale wenzetu wanaopanga kurudi nyumbani, tungependa kuifanya TPN iwe kama Labour Exchange Centre ya Professionals na pia Business and Projects Exchange Centre. We do hope this will assist our brothers and sisters who would like to come back home, to be sure of what they will do when they are back.

Nashukuru kwa kuweza kunikumbuka. Hakika ni miaka mingi sana. Karibu tuungane, wakati ni huu sasa. AGM itakuwa mwezi wa nane.
 
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, napenda kuwapongeza TPN kwa kualika wana JF ktk umoja wao. Nafikiri ukijiunga na Tpn au umoja wowote ule ni opportunite kubwa ya kujiendeleza wewe mwenyewe na Taifa kwa ujumla. Nadhani ndani ya TPN kuna wataalamu mbalimbali na wazoefu wa Viwanda, usafiri, banks, ustawi wa jamii, uongozi bora, mikataba, biashara za nje na ndani nk. Ila nitoe angalizo kidogo kwani tuna profesional societies nyingi Tz lakini hazina msaada sana hasa kwa mwananchi wa kawaida. Hebu tumieni wazoefu ndani ya TPN kusaidia kupunguza kero hapo bongo. Kuna kero ambazo nahisi kama Society TPN mnaweza kujaribu kuzishughulikia zikamsaidia hata mtanzania wa kawaida, mfano usafiri mkakopa mabasi makubwa sio vipanya from outside na kumanage ipasavyo si mtakuwa mmesaidi while nanyi mkiingiza kipato. Who knows mnaweza kujidevelop na kuanzisha even kiwanda in the future. Ndio watu wanavyofanya nchi za wenzetu. Hebu jaribu kuafatilia history ya makampuni makubwa duniani yalianza na yameendelea vipi. Wazo langu binafsi
Once again Thanks TPN


F2S nimekupata . . . TPN inachofanya kwa sasa ni kumobilize na kuhamasisha members wake wafanye miradi mbalimbali kwa kadiri wanavyoweza kuibuni na kui-present. Sasa hivi kuna walioungana kuendesha miradi fulani fulani. Nadhani ni mwanzo mzuri. With time miradi itakuwa mingi.

TPN kama Network haifanyi biashara lakini mipango yake ni kuwawezesha wadau wake wafanye mambo makubwa ya kuleta mabadiliko ya kweli katika nyanja mbalimbali.
 
Ndugu Mtsimbe,

Katika kuboresha muundo wa jumuia yako, ni vizuri muweke sections zinazotenganisha taaluma mbali mbali ndani ya TPN. Kwa mfano mimi ni mwanachama wa IEEE (Institute of Electrical and Electronics Engineers) ingawa mimi siyo mhandisi wa umeme kama ambavyo ungetegemea, bali ni mhandisi wa mitambo (Mechanical Engineer). Ila kwenye IEEE kuna Automatic Control Society (ACS) ambayo ndiyo imenifanya niwe mwanachama wa IEEE. Vivyo hivyo huko kwenye TPN, ni vizuri muweke vijumuia vidogo vidogo kama hivyo ambavyo vinawakutanisha watu wa fani moja. Hiyo itakuwa na kivutio cha kuleta professionals mbali mbali wakitegemea kukutana na wenzao wenye backgrounds zinazofanana.
 
Ndugu S. Mtsimbe,

Mimi kama mmoja watanzania ambao wangeweza kujiunga na TPN nina machache ambayo ningependa kushauri na kupata ufafanuzi kabla ya kujiunga.

1. Nimepitia tovuti yenu, nimekutana na makosa kadhaa ya wazi ya lugha. Nadhani ni vizuri tovuti hii kwa sababu inawakilisha Tanzanian Professionals basi iwe na utaalamu wa hali ya juu. Napendekeza TPN itafute wahariri wazuri (tunao wengi) ili kuipitia. Mfano mdogo tu (na ipo mingi) mtu akisoma vision ya TPN kwenye ukurasa wa mbele haieleweki mpaka akifungua ukurasa wa objectives, ndio anaelewa. Wageni wenu wakitaka kuijua TPN watataka kusoma Vision. Wakishindwa kuielewa vision, wameshindwa kuielewa TPN.

2. Nashauri pia muwe makini sana na matumizi ya takwimu na taarifa mnazoweka kwenye tovuti. Ikiwezekana muonyeshe vizuri wapi mmepata (vyanzo) takwimu hizo. Kwa mfano, mkisema tanzania ni nchi maskini sana yenye watu zaidi ya "50% below poverty line...", basi mueleze chanzo. Kwa sababu hatuna hakika kama hiyo ndio takwimu sahihi. Na nadhani ni muhimu pia kuzipa takwimu nguvu - zimzungumze zenyewe bila kuweka maneno yoyote yanayoweza kuleta hisia za kuongezea "chumvi".

3. Jingine ambalo yawezekana ni swala la muonjo tu (na hili linaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu) na labda sio muhimu sana ni muonekano mzima wa tovuti hiyo. Kwa mawazo yangu tovuti hii inaonekana kama ya jumuiya kibiashara au klabu zaidi kuliko kitaaluma. Ingependeza kama mngekuwa na vitu vichache sana kwenye ukurasa wa mbele na rangi chache zaidi, kwa maana nyingine kusiwe na makeke mengi sana.

4. Mwisho, ningependa pia kujua umuhimu wa lugha ya taifa katika taasisi hii. Kwa sababu hii imekuwa ni conflict kubwa kwenye taaluma zetu hapa nyumbani na kumezuka mjadala mkali sana kwa miaka mingi wa athari ya lugha ya taifa na ya taaluma mashuleni kwenye maendeleo ya taifa. Na kwa sababu TPN itawajumuisha watu mbali mbali hata wasioweza kuelewa lugha ya kiingereza (kutokana na mission ya TPN). Je, mmefikiria swala hili na je kwa sababu hii ni taasisi ya wataalamu wa kitanzania na kwa sababu moja ya matatizo ya msingi ya watanzania ni wataalamu wetu kutumia mbinu za mataifa mengine kutatua matatizo yetu "local", je si vizuri chombo hiki kikalifanya hilo kuwa moja ya maswala muhimu kwa sababu kwa mataifa mengi yaliyoendelea huko ulaya na Asia ya kusini lugha imekuwa ni sehemu muhimu ya maendeleo ya kiuchumi.
 
F2S,

Tuwape mda tu hawa TPN labda hapo mbeleni watatuonyesha mambo makubwa nafikiri changamoto zako wataziona.

Thanks GM, something is already happening . . . . hoping that in August AGM we will have a new TPN more stronger and effective.

Our Treasurer is heading to Dodoma this week to open up a chapter. We have been informed by interested parties and members of TPN in Dodoma that more than 30 people has confirmed for a meeting.
 
Sanctus,

I think we have reached somewhere, I am now accepting your "Karibu" it is time for action, I am on my way to TPN's office to register myself. I believe that Mjenga Nchi ni Mwananchi.

We will discuss all TPN's shortfall live. However, not under this name. When is the next members meeting?

See you there Mr President and God bless you.

Njimba

Mzalendo Njimba, karibu sana katika Mtandao wa kweli . . . . Our next meeting is scheduled to take place on 31st August 2008. I forsee there might be some constitution changes. Also, we need to expand the leadership base as we have grown and there are so many challenges which needs collective leadership, so we may be requesting members to join the leadership team.
 
GM,

I can see tunafikiria kitu kimoja na kwa wakati mmoja!

what a coincidence!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Njimba

Wazalendo . . . mkishaanza kuona mitazamo yenu inafanana, ina maana muelekeo ni mzuri. Collective positive minds and attitudes is what will bring changes in this country.
 
Bwana Mtsimbe..usiishie hapa tu sasa na kwa michuzi,..juhudi zifanyike kujinadi zaidi kwa jamii ili waweze kuelewa mnafanya nini na mna vision ipi....i hope mtapata member wengi zaidi na wenye mawazo chanya zaidi yakukipeleka chama chenu kwenye mafanikio mnayoyataraji...msichoke..pigeni mzigo ..tafuteni kondoo wa bwana...chama kiwe na nguvu..natumaini kuna vichwa vingi tu (Professionals) nje ya chama chenu vyenye uwezo mkubwa sana na machungu yanayohitajika kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu tatizo wanakosa nafasi ya kuonyesha na kutumia uwezo wao ili wasaidie kusukuma gurudumu hilo...so ingekua vyema chama chenu kikawa kama daraja lakuwatoa huko walipo..kuwaleta pamoja na kutengezeza mazingira ambayo yatawafanya wajisikie na kuguswa kutumia uwezo wao wote na nguvu zao katika kuliletea taifa letu maendeleo ya kweli.........wako wengi sana lakini wanakosa morali na hari ya kuliinua taifa lao..so wanaishia kujinufaisha wenyewe na elimu zao..which is not wrong but ingefaa zaidi kama wangejijali wao na taifa lao kwa pamoja...but tatizo tunarudi pale pale wanakosa sehemu na mazingira muafaka yakutoa mengi yalio kwenye vichwa vyao kulisaidi taifa....

so this is your challenge bw. Mtsimbe.

Mzalendo Wakunyuti, nashukuru sana kwa mawazo yako mazuri. Nikitumia lugha ya kigeni . . "You have hit the bulls eyes". Nitafikisha maoni yako TPN na tutayafanyia kazi yote. Kama utakuwa DSM tarehe 31 August 2008 karibu katika AGM .
 
Mimi ni mwanachama wa TPN, ingawa sijapata muda kujishugulisha rasmi.

Sidhani kama bwana Sanctus Msimbe anataka nikajiunge pale kama Fair Player, anachotaka yeye ni kujiunga kwa jina langu halisi la Mwakaleli Donatus. Siri yangu ya kujiita FairPlayer itabakia yangu.

Hoja ya majina halisi sioni mantiki yake kwa hapa JF

Asanteni sana

Mzalendo FairPlayer, hakika umenena, na hoja ya kutumia majina halisi hapa JF tumeshakubaliana kuwa haifai labda tu kwa sababu maalumu sana.

Tafuta muda ndugu yangu uanze kujishughulisha rasmi TPN. Njooni wote tushauriane na kusaidiana nini cha kufanya. Nadhani uwezo tunao mkubwa sana kama wote kwa pamoja tukiamua. AGM itakuwepo tarehe 31 August 2008.
 
Mimi ni mtaalamu wa kupindua Nchi vipi nije?

Du Mwanawani hii ni kali sana . . . LOL. Nadhani tunaweza kukutumia ndani ya TPN, si kwa kuipindua serikali iliyopo madarakani bali kwa kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii ili kuuondoa umasikini na kubadilisha hali za maisha ya Watanzania kuwa bora. Njoo tujadiliane . . .
 
Unataka kujiunga na TPN kutokana na kufahamiana na Mtsimbe toka Mnazi Mmoja ama kutokana na kuelewa Sera kamili za TPN?

Yaani umefuatilia TPN toka bado Kamati ya Uanzishwaji mpaka leo hii hukupata Hamasa ya kujiunga nayo? Mpaka moto huu ambao umewashwa hapa JF ndo umekufumbua macho? Hukuwahi wish kwamba ungekuwa among wanaotajwa kama Founding Members wa TPN?

Kuna namna hapa!!!

Mzozo, katika kipindi kifupi ambacho nimekuwa katika uongozi nimejifunza mengi sana kuhusu wanataaluma wetu. Ukiacha wachache sana wengi wanapenda ku-observe kwanza wajue muelekeo . . . Watch and See . . . With time mambo yatabadilika.
 
Ndugu Mtsimbe,

Katika kuboresha muundo wa jumuia yako, ni vizuri muweke sections zinazotenganisha taaluma mbali mbali ndani ya TPN. Kwa mfano mimi ni mwanachama wa IEEE (Institute of Electrical and Electronics Engineers) ingawa mimi siyo mhandisi wa umeme kama ambavyo ungetegemea, bali ni mhandisi wa mitambo (Mechanical Engineer). Ila kwenye IEEE kuna Automatic Control Society (ACS) ambayo ndiyo imenifanya niwe mwanachama wa IEEE. Vivyo hivyo huko kwenye TPN, ni vizuri muweke vijumuia vidogo vidogo kama hivyo ambavyo vinawakutanisha watu wa fani moja. Hiyo itakuwa na kivutio cha kuleta professionals mbali mbali wakitegemea kukutana na wenzao wenye backgrounds zinazofanana.

Ndugu yangu Kichunguu, kuna mambo moja au mawili ningependa kuyagusia . . . Kwanza kuundwa kwa TPN hakukuwa na maana ya kuchukua majukumu ya vyama vingine vya kitaaluma ambavyo tayari vinafanya kazi yake vizuri. TPN inashirikiana vizuri sana na vyama hivi na ndiyo maana baadhi ya vyama hivi viongozi wake ni members wa TPN na wengine pia ni viongozi wa TPN.

Madhumuni makubwa ya TPN ni kushughulikia mambo ambayo taaluma moja peke yake haiwezi kuyamudu hasa ya kiuchumi nk. Hata hivyo mawazo yako ni mazuri sana ina nawezekana kabisa ndani ya TPN tukawa na vikundi vya wanataaluma zinazofanana. Nitayawakilisha TPN.
 
Mzalendo Wakunyuti, nashukuru sana kwa mawazo yako mazuri. Nikitumia lugha ya kigeni . . "You have hit the bulls eyes". Nitafikisha maoni yako TPN na tutayafanyia kazi yote. Kama utakuwa DSM tarehe 31 August 2008 karibu katika AGM .

Ahsante Kwa ukaribisho wako Bw. Mtsimbe. Tuombe Mungu yote yatawezekana.
 
Zimwi likujualo halikuli likakwisha, lakini kwa JF CCM wakijua jina lako halisi umejiingiza kifungoni kimawazo. We unafikiri wakijua kuwa wewe ni Ofisa IKULU na upo JF si ndio watajua kuwa mvujisha siri. Hivi hivi anonimity ndio watajirekebisha maana humjui nani adui yako na hivyo itakufanya uwe katika mstari ulionyooka kila wakati. Mnaojitambulisha ni vizuri kwani role yenu humu ni kusoma Ila wapo wenye role ya kijasusi humu. Yaani wafukua habari ili kuisaidia nchi hawa waendelee kuwa ANONIMOUS
Ndugu yangu HOFSTEDE sikubaliani na wewe suala moja kwamba kila tatizo ni CCM hapana. Bwana Sanctus alichoeleza yeye ni kitu tofauti kabisa na suala la taaluma sasa hiyo CCM huko kwenye taaluma inatoka wapi labda kuhusu hili suala la ajira nakubaliana na wewe kama utakuwa umeajiliwa ikulu na ikafika mahala wana taaluma mnakutana uso kwa uso hapo kuna utata, Lakini na imani mtandao wa TNP unajitegemea utakapojiunga huko siyo lazima ujitangaze kuwa wewe ni JF member
 
Back
Top Bottom