Jeshi letu linaonyesha umahiri wa kupigwa na tofali zama hizi!? Hawaoni wenzao huko duniani?

Sherehe za Muungano hazina mvuto kabisa. Ni bora tuwe tunapumzika kama tufanyavyo siku za Nyerere na Karume days. Vinginevyo Rais awe analihutubia taifa moja kwa moja toka Ikulu. Kama vipi yafanyike makongamano ya kujadili kero za Muungano.

Nimekuwa nikifuatilia maonesho ya mbinu za kijeshi za majeshi yetu kuanzia makomando mpaka jeshi la polisi, hakika hazioneshi kwenda na wakati.

Katika zama hizi za teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani na kurusha makombora ya masafa marefu... Ninyi mnaonesha kupigana na matofali na vipande vya mbao? Ni lini utakutana na adui umpige na tofali? Labda kama ni mbinu za kuwadhibiti wapinzani hapo sawa.

Mapambano dhidi ya wahalifu au Vita katika zama hizi yanafanywa kiakili na kiteknolojia zaidi. Mahitaji ya mtu anayeweza kuhimili kupigwa na nondo ama tofali yamepungua sana kama siyo kwisha kabisa.

Wahalifu wengi hawana maguvu ya mwili wala hawatumii nguvu katika kutekeleza mambo yao. Na hata wapiganaji wa zama hizi hawatumii tena magumi wala maguvu kubeba matofali. Kuna vifaa vya kiteknolojia vinavyofanya yote haya.

Niombe mtuoneshe mambo yanayoendana na mabadiliko ya zama. Onesheni show za kisasa kama zile za Korea Kaskazini.
Sexless ulipitia JKT? Au wewe ni wale ambao hawajawahi kupitia mafunzo hayo? Unaufahamu uaskari wa vita vizuri?
 
Embu acheni kukuza hili jeshi kwa kipimo cha M23 hao wabeba AK-47 na vibomu vya kutengeneza nyumbani.
Ingekua watu kama Al shabab au Boko haram sawa maaana wale wapo njema kila idara had mizinga wanayo so hao M23 ukiwaona tu km wanaumwa unyafuzi.
Marekani pamoja na teknolojia yake alitolewa jasho na vietcong (peasants) katika vita ya Vietnam
 
...Kama hujui si lazima kujibu kila thread.
Inaonekana wewe ni mwerevu sana
...We we ulifaulu au ulifeli?
Unazidi kuonyesha werevu wako, kuwa u genius kuliko wengine humu JF

...Kama kuvunja tofali la udongo ni ukakamavu vipi anayevunja msitu heka nzima kufungua Shamba?
Unatakiwa kuelewa kuwa huko kuvunja tofari, kukunja nondo kunakofanywa na hao askari ndio kunakufanya upate nafasi nzuri na uhuru wa kuandika kwenye hii forum kwa amani kabisa, wakati wananchi wenzio huko DRC, Garisa, Somalia, Chiboku Nigeria, Southern Sudan, etc hawana muda, amani na utulivu kama wewe. Muda wao mwingi wanautumia kulinda roho zao wenyewe, ila wewe unapiga tu kelele humu unajifanya unajua.

 
Hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini waasi wakikimbizwa ni kukimbilia Kenya,Congo,Rwanda,Sudan na nchi nyingine za Afrika mashariki na kati,na sio Tanzania?

Unajua wanajeshi wetu wanafanya nini huko mipakani kuzuia hilo?... Waulize watu wanaoishi mipakani ndio wanajua mziki wa JWTZ.

Wiki iliyopita zaidi ya wanajeshi 30 wa Tanzania wametunukiwa na UN.Wacongo wanalifagilia jeshi la Tanzania kuliko lao.

Katibu Mkuu wa UN alisema JWTZ ni jeshi lenye nidhamu na weledi wa juu kwenye mapambano kiufupi ni jeshi bora.

Amani unayoiringia kuna watu wanapoteza maisha yao kuilinda... Kuwepo na amani ya mda mrefu kiasi hichi ni ishara tosha jeshi letu liko imara sana.

Pole sana
 
Mkuu haya ya ufipa yanakujaje hapa kwenye masuala ya kitaifa? Jeshi halina chama, usimuabishe Polepole hapo Lumumba. Chukua buku 7 zako za leo lkn usirudie tena kutoa komenti dhaifu kama hii.
Ahsante kwa ushauri. Ila kumbuka pale walikuwa wakionesha ukakamavu kunogesha sherehe na si mbinu za medani.
Ninyi watu wa ufipa,kwakukosa pa kushika toka mumpokee bwana yule na kugeuka watetezi wa ufisadi na uovu,mmekuwa mkipinga kila kitu bila tafakuri.
Hivi unadhani hata umiliki manoari zote ulimwenguni,nyambizi zote,ndege zote zisizo na rubani kwamba we ndio mshindi? Muulize mmarekani analijua hilo vizuri.
 
Kuna raia waliomba wawe wanapeleka hayo matofali sijui ombi lao kama lilisikilizwa

mkuu Yale matofali sina uhakika kuwa yanafaa kwa matumizi ya kujengea maana haiwezekani tofali ya sementi ikapigwa nyundo moja ikawa mchanga kihasi kile
 
Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.

Wale walikuwa wanaonyesha onyesho la kufurahisha waliokwenda uwanjani na ukakamavu wao, ile ni sanaa kama sanaa zingine. Hawakuwa pale wakionesha mbinu za kupigana na adui.

Hivi majeshi yetu yanapofanya gwaride ina maana wanatuonesha mbinu yao ya kupigana na adui?

Wacheni kuwa mapunguani.
Nashukuru sana dada kwa hili jibu, nilitaka kusema jambo ila hili lako kwa mwenye akili timamu kakuelewa
 
Huh, mie nakutaka unifundishe wewe hawa wa huku watanipa matango poli tu

= pori

Kwa sentensi yako hiyo, kwanza unatakiwa ujifunze kuwa msafi wa roho kwa kuwaamini binadam wenzako, huwezi kuwahisi tu ni wabaya kabla hujauona ubaya wao. Hiyo ni roho ya kikafiri, achana nayo.
 
Yaani unataka ufananishe marekani/urusi/north korea na tanzania?

Jeshi lolote linamiliki siraha za aina flani kutokana na ulazima wa muda na tishio la adui

nchi za afrika tishio kubwa ni ugaidi na vita baina ya nchi jirani,sasa kama malawi hata AK 47 hana kunaulazima gani wanachi walale njaa/wafe kwa magonjwa kisa jeshi letu limiliki masiraha ya nyukilia kwa ulazima gani uliopo,acheni kuleta siasa kila sehemu

komondoo pia hufundishwa kutumia mwili kama siraha awapo vitani

jeshi ni jeshi,sio kampuni la mnyonge kila mmoja kujifanya mjuaji,

mtoa mada hata mguu pande unaonekana huwezi,ila kwenye kupondea hamjambo,wewe lala, kula, andika post ila ukumbuke kunawatu kila siku wanapelekwa nchi mbalimbali kuleta amani

na siku kikinuka wewe ndo utakua wa kwanza kuomba jeshi kutoa msaada mapema iwezekanavyo huku wewe ukiwa upo chini ya uvungu
 
Vita vyetu huku Africa havihitaji technology ya kisasa sana mkuu. Haya mazoezi ya kupiga vichwa matofali ndio yanafaa kwa mazingira ya huku kwetu. Huku majeshi yetu yana-deal na makundi kama M23, Alshabaab, Kony na watu wanaofanana na hao. Ukiwakamata huna haja ya kupoteza risasa unawapa vichwa vya kutosha tu mpaka wanakwenda kuonana na muumba wao.
 
Back
Top Bottom