Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,397
- 24,391
Ilipoingia 1978, November/December hadi 1979, jeshi lilipitia "baptism of fire" wakati wa Vita ya Kagera.
Kimsingi baada ya vita ile ikadhihirika kuwa Defence Policy iko safi na inafanya kazi katika mazingira ya wakati ule.
Najua leo jeshi liko complex kuliko wakati huo na lina vyuo vyake ambavyo ni Think Tanks, kama National Defence College pale Kunduchi.
Sasa leo kuna vita hivi vya Ukraine na vile vile Israel na Hamas. Mbinu zilizojitokeza na kuwa very effective katika kushambulia adui, ni matumzi ya Drones na Missiles.
Huko Ukraine drones zimekuwa a weapon of choice katika ku target sehemu za adui kwa pande zote.
Hamas juzi kwa vifaa ambavyo waweza kufikiri ni vya mchezo mchezo tu, katumia drones ambazo zimechakaza vibaya miuondombinu ya kijeshi ya Israel iliyokuwa mstari wa mbele.
Kwamba wameuawa wanajeshi zaidi ya 300 wa Israel katika mashambulio, hilo na jambo kubwa sana.
Maoni yangu ni; Jeshi letu vile vile litazame upya Defence Policy yake ili matumizi ya vifaa hivi viweze kujumuishwa katika ulinzi wa nchi yetu.
Nawaza tu!