DOKEZO Jeshi la Uhamiaji wamenirudisha Nyumbani wakidai sipo Fiti. Nimepoteza dira ya maisha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nawasalim kwa jina la JMT, Naamin kila mmoja wetu ni mzima wa afya na kwa wenzetu ambao hawako sawa kiafya basi mwenyezi Mungu awafanyie wepesi...
Pole sana dada yangu Kwa changamoto hii uliyopata.Kila jambo Lina kusudi lake.Kaa mshukuru Mungu na umuombe sana akuvushe kipindi hiki Cha majaribu haya.Usikate tamaa,jambo lolote unalowaza ambalo ni la Mafanikio tekeleza.Kikubwa Usikate Tamaa na Mungu atakubariki.

Mwisho wa yote Kwa mawazo yangu ulivyosema kozi ya Uhamiaji,na unasema Kuna mtu alikushika mkono kwanini hujamtafuta Tena? Au ukiona Haina haja.

Lakini pia mawazo yangu yawezekana labda umri ndio kitu kilichokuondoa kwenye kozi,waliamua kusema Afya Kwa kuwa huwezi hoji KOKOTE kwani majibu Siri Yao.Umri Wakati wa Tangazo ulisemaje? Na wewe uliajiriwa kwenda kozi kama mtaalamu au vile vigezo vya kidato Cha nne au sita?

Samahani lakini Kwa haya maswali.
 
Pole sana dada yangu Kwa changamoto hii uliyopata.Kila jambo Lina kusudi lake.Kaa mshukuru Mungu na umuombe sana akuvushe kipindi hiki Cha majaribu haya.Usikate tamaa...
Amen, nashukuru sana kuhusu kigezo cha umri kilikuwa sawa, kwa sababu natimiza miaka 30 mwezi wa 10 mwaka huu na niliingilia kwa digrii na kwa digrii kigezo cha umri ilikuwa ni kutokuzidi miaka 30.

Na kuhusu mbanga aliyenisaidia baada ya kutoka nikampigia simu akasema tayari tumeshachelewa majina yameshatumwa makao makuu hivyo hana cha kufanya tena .. basi ikawa imeisha
 
Nawasalim kwa jina la JMT, Naamin kila mmoja wetu ni mzima wa afya na kwa wenzetu ambao hawako sawa kiafya basi mwenyezi Mungu awafanyie wepesi...
Nilikua na wazo la kwenda uhamiaji jpo kwa njia za panya lilivotoka lile tangazo

Ila Mzee akanambia wakija kufanya ukaguzi na ukikutwa na hatia yni unafukuzwa chuo dah nikasema bora nusu shari kuliko shari kamili

Mtoa mada pole sanaa tafuta hospitali hizi ukapige day worker
 
Mkuu usikate tamaa, magumu haupitii peke yako, angalia thread zangu nyuma uone watu tulivyotoka mbali, watu tumepiga koz 3 months kiwila tukaja kuambiwa unfit wakat imebak miez mi3 tumalze koz lakn tukarud bado tukapambana, mambo ni mengi.
Dah naweza kuhisi maumivu uliyopitia, pole sana mkuu, haya maisha haya kweli ni fumbo kubwa sana na laiti kama tungepewa macho ya kuona ya mbeleni, naamin kuna maamuzi mengi tuliyoyafanya tusingeyafanya...
 
Shahada ya Maabara za kisayansi. Plz fadanua. Nini unaweza kufanya kwa uhanisi kupitia fani hii
Fani niliyosoma inaitwa "Biotechnology and Laboratory Science' kupitia fani hii naweza kufanya kazi Hospitali kwenye upande wa Molecular diagnostic, naweza kufanya kazi kwenye Taasisi yoyote inayojihusisha na utafiti iwe upande wa magonjwa ya binadamu, tafiti za kilimo na mifugo, kwenye maabara za viwandani kama Laboratory Analyst, maabara za migodini pia kama Laboratory Techologist, kufundisha baadhi ya masomo katika vyuo vya kati vya kilimo na mifugo, pia ningekuwa na mtaji ningeweza kujiajiri kwa kufungua ofisi inayojishughulisha na utoaji wa ushauri wa jinsi ya kudesign maabara za kisasa, uuzaji wa kemikali za maabara, vifaa vya maabara, vifaa tiba na vya kujifunzia.
 
Hata maabara za shule unaweza kuzisuka vizuri?
 
Back
Top Bottom