Jeshi la Polisi laanza Uchunguzi wa Kifo cha Nusura Hassan Baada ya taarifa za Kifo kutapakaa mitandaoni!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,121
Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishna Misiime amesema Jeshi lake limeanza Uchunguzi wa Kifo cha mwanafunzi wa UDOM Nusura Hassan kilichotokea mkoani Kilimanjaro

Kamanda amesema tukio hilo limezua Mjadala mkubwa mitandaoni likimuhusisha Naibu waziri wa Tamisemi mh Dugange

Tusiime amesema Uchunguzi huo utamshirikisha pia Mkemia mkuu wa Serikali na Watu mbalimbali watahojiwa

Sabato njema!
 
Kwa upande wangu sijawahi ona mwanafunzi wa chuo akafariki bila Tanzia. Udom wameikana Tanzia yao na mpaka sasa hawajatoa taarifa ya kifo cha mwanafunzi. Je kweli hajafa? Au kuna shida gani juu ya kifo chake?
 
Hili tukio polisi wasitupiwe lawama, lazima Naibu Waziri aseme ukweli, sbb kama watachunguza simu ya binti, wataona kila kitu, huu uchunguzi utakuwa rahisi ikiwa uwazi utatawala, kama binti alikuwa kwenye ajali, matokeo ya uchunguzi mfupi tu jibu litolewa kwa public.
 
Back
Top Bottom