emmarki
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 682
- 918
Kwa wale wanaopenda kujiunga na JKT kwa mwaka huu nafasi ziko wazi. mchakato unaanzia Wilayani kwako. Tembelea ofisi ya wilaya yako kwa maelezo zaidi.
=========
Jeshi la kujenga taifa JKT limetangaza nafasi ya kujiunga na mafunzo ya jeshi hilo kwa kujitolea kwa mwaka 2017 ambapo vijana kutoka Tanzania bara na Visiwani wanaruhusiwa kuomba. Mkuu wa JKT Meja Jenerali Michael Isamuhyo amesena utaratibu wa vijana kuomba nafasi hizo unaratibiwa na wakuu wa mikoa na wilaya.
TAARIFA KWA UMMA
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo anawatangazia vijana wote wa Tanzania Bara Na Visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea mwaka 2017.
Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo, unaratibiwa na ofisi za Wakuu wa mikoa na wilaya ambapo muombaji anaishi.
Zoezi la kuchagua vijana litaanza Mwezi Novemba 2017 na vijana watakaochaguliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 04 mpaka 09 Desemba 2017.
Jeshi la Kujenga Taifa linaendelea kusisitiza kuwa nafasi za vijana kujiunga na mafunzo ya JKT haziuzwi, aidha yeyote atakaye husika na utapeli wa kuuza au kununua nafasi hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria.