pombe kali
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 249
- 489
Nikiwa kama Mwana Ukonga na mwananchi ninaejua siasa za Ukonga naomba nikiri kwa niaba ya wana Ukonga kuwa tunamuhitaji Jerry kuliko kitu chochote.
Hii ni kwa mustakabali wa maisha yetu, kubali kataa jimbo la ukonga ni miongoni mwa majimbo magumu ila sisi tuliozaliwa ukonga tunajua chanzo kiini na suluhu, ikumbukwe kuwa jambo la Ukonga lipo Wilaya ya Ilala, wilaya ambayo ni kubwa yaani inaanzia kariakoo mpaka chanika pia imepakana na kisarawe mkoa wa pwani kwa miaka yangu yote ambayo nimeishi ukonga nimegundua changamoto zifuatazo mosi ni miundo mbinu.
Tatizo la miundo mbinu ni kubwa kuliko tunavyofikiri kwani wakati wa masika watu hulazimika kupanga vyumba mjini kuepuka changamoto za usafiri ambapo huwa hakufikiki hapa naongelea maeneo kama mbondole,viwege, magole chakenke nk kwa watu wasio na akili lawama hizi huwa wanamtupia mbunge.
Bila kujua historia ya jambo husika wala kujua taratibu za serikali na michakato ya kumpata mzabuni nk, sababu ya kuwaelekeza wana ukonga kwamba tunamuhitaji Jerry ni kwamba huyu jamaa amekuwa jikoni kwa muda mrefu tangu akiwa Naibu Meya baada ya hapo amekuwa mjumbe kamati kuu ya chama.
Yaani jikoni kabisa hii imepelekea mpaka Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amiri jeshi mkuu kumuamini na kumpa uwaziri katika wizara nyeti sana ya ardhi, wana ukonga Mungu atupe nini tena ukizingatia maeneo yote niliyoyataja hapo juu yana migogoro ya ardhi mpaka kupelekea baadhi ya maeneo kuitwa maeneo ya uvamizi.
Mimi nashauri tuendelee kumng'ang'ania huyu home boy kwani yeye ndiye atatuvusha na kutupeleka nchi ya ahadi sababu ukonga anaijua vizuri na pia anaushawishi mkubwa hata kwa mkuu wa nchi na mamlaka zote, tusiache lulu hii ipotee.. kumbuka amepewa dhamana ya ardhi nchi nzima ya Tanzania.
Jimbo la Ukonga litakuwa tofauti baada ya muda mfupi sana.
Naomba kuwasilisha