Jerry Silaa: Rais lazima awe jasiri sio kulialia

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
JerrySlaa(1).jpg

Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa amefunguka na kusema kuwa mtu ambaye atagombea nafasi ya Rais mwaka 2015 anapaswa kuwa ni mtu jasiri mwenye maamuzi sahihi, na si mtu ambaye atakuwa analialia au kulalamika.


Jerry Slaa alisema haya alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpka saa kumi Alasiri.


Jerry Silaa alionesha wazi kuwa nafasi ya urais si nafasi ambayo inaweza kuongozwa na kila mtu kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiona wanaweza kuongoza taasisi hiyo ya urais na ndipo hapo alipotoa mfano wa baba na mtoto, kuwa nyumbani mtoto analia lakini baba halii.
"Nikiteuliwa kugombea urais nitakubali, jukumu hili lazima alibebe mtu,lakini mtu huyo anapaswa kuwa jasiri mwenye maamuzi sio kulialia.


nyumbania analia mtoto baba halii."
Kauli ya Silaa ni wazi inaonesha kuwa viongozi ambao wamekuwa si watendaji badala yake muda mwingi wamekuwa wakilalamika hawatufai katika nchi hii kwani kuna mambo mengi ambayo yatahitaji maamuzi yao na watashindwa kufanyia kazi, hivyo amewataka wananchi kutowachangua viongozi ambao wamekuwa mizigo na si wawajibikaji kwa wananchi.


"Tanzania kuna uongozi wa "kibaba" yaani kuna viongozi wanadhani uongozi ni haki yao ya asili. ni vyema viongozi tukaamka tuwatumikie watu na mkituona hatuwajibiki msituchague katika uchaguzi"


Lakini mbali na suala la uongozi Jerry Silaa alijaribu kuongelea suala la miundombinu na mafuriko katika jiji la Dar es Salaam na kusema kuwa majanga ya mafuriko kwa wahanga wa Jangwani wamejitakia wenyewe na wao ndiyo wamekuwa chanzo cha maafa hayo katika maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na kujenga katika eneo ambalo ni njia ya maji na kusababisha maji hayo kushindwa kupita ipasavyo.


"Mnyamani tunajenga mtaro na tunawaangalia kibinadamu wahanga wa mafuriko, ila hao Jangwani wamejitakia wenyewe, maana toka 2012 msimamo wa serikali ni wakazi wa mabondeni wanajitakia wenyewe mafuriko, na kuwatia hasara wana Dar es Salaam wote, madaraja yanakatika kwa ajili maji yamekosa pa kupumua sababu watu wamejenga. Mwaka jana hasara ya miundombini 20 Bilioni mpaka leo hatujamaliza kukarabati na bado mingine imekatika. Ukijiheshimu nawe utaheshimiwa na ndio uzuri wa uongozi wa vijana,ukija kihivyo utajibiwa kihivyo,mfikishie ujumbe wake huu. Ila Na nitoe Pole kwa wanaochelewa makwao barabara zikifungwa."


KUGOMBEA UBUNGE 2015
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pia amefunguka juu ya kutaka kugombe nafasi ya ubunge mwaka huu, anadai kuwa amekuwa akishawishiwa na watu wengi lakini atafanyia kazi hilo ili aone kama anaweza kufanya maamuzi ya kuwawakilisha wananchi bungeni kupitia chama chake cha CCM.
Jerry Silaa: "Deo nashukuru,nimeshawishiwa sana na wengi wana sababu kama ulivyo wewe "nimeona unaweza sana" naendelea kutafakari ili nikifanya maamuzi niyasimamie na yawe ya dhati.


Mbunge anapaswa kuonyesha tofauti kwenye jimbo letu ,kama huna nia ya dhati ni bora uache."
Jerry Silaa : "Wapo kina Deo Kidunda wengi wanaonishauri,kunitaka na kuniunga mkono, mvumo umekuwa mkubwa na mimi nina maoni yangu,namaliza manispaa June nakabidhi kazi ya watu nitafanya maamuzi sio yenye maslahi kwangu bali kwa watanzania" Aliongeza Silaa Mbali na kuonyesha kuguswa na kushawishiwa na watu wengi lakini pia Kiongozi huyo ambaye ananafasi katika Chama Cha CCM alikiri wazi kuwa katika chama chake kuna baadhi ya viongozi ambao wamekichafulia Chama chao ingawa yeye anaamini CCM ni chama bora.


"Bado CCM ni chama bora na si kampuni ya mtu, inawezekana kukawa na viongozi waliotuangusha ni wachache tunajipanga vyema. Hata familia hamzaliwi sawa"


RUSHWA TANZANIA
Inafahamika suala la rushwa limekuwa ni changamoto sana kwa nchi nyingi barani Afrika na imekuwa changamoto kubwa zaidi katika serikali ya awamu ya nne ya Tanzania na kupitia Kikaangoni Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe alikiri wazi kuwa udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete ni kushindwa kudhibiti rushwa, Jerry Silaa naye leo amefunguka njia ya kuweza kuzibiti rushwa Tanzania ni kuweka mifumo katika teknlojia na si kitu kingine.


Jerry Silaa: "Degree yangu ya kwanza ni Bsc Electonics naamini nchi hii ukileta technology rushwa basi. nani amewahi mpa rushwa mtumishi wa facebook amfungulie account??? technology ndio itafanya hati ya ardhi isiwe na rushwa,TRA isiwe na rushwa, Tender isiwe na rushwa"


UCHAGUZI KUAHIRISHWA OKTOBA
Wakati viongozi wa vyama vya upinzani nchini wakiwa na wasiwasi na hofu ya kuarishwa kwa uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwa kufanyika mwezi wa Kumi, kutokana na kusuasua kwa mchakato wa uandikishwaji katika daftari la kudumu la wapiga kura, Jerry Silaa amesema kuwa kuaHIrishwa kwa uchaguzi kwa hali ya kawaida sio Demokrasia ila inapobidi inawezekana kuarishwa.


Jerry Silaa: "Kwa hali ya kawaida hapana sio democrasia, ikibidi ndio. Mwaka 2005 mgombea mwenza wa Chadema alikufa zikaongezwa siku 15"


Chanzo:IPP Media
 
Back
Top Bottom