Jenga ngome yako, Usikubali kuishi kimazoea

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,179
52,892
Kwenye maisha kumbuka jambo moja, wenzako wanapoleta mezani chakula halafu wewe huleti, inawezekana wewe ukawa ndiyo chakula chenyewe. Unaelewa hilo? Duniani hakuna kitu cha bure zaidi ya salamu, ukiona unatumia kitu cha bure, inawezekana wewe ndiyo ukawa bidhaa yenyewe.

Ndugu zangu hakuna kitu muhimu kwenye maisha yako kama marafiki. Marafiki ndiyo wanaweza kukufanya wewe kufanikiwa ama kutokufanikiwa. Tunatakiwa kuwa makini sana kwenye kuchagua marafiki.

Kwenye mahusiano yangu yoyote, kitu ambacho nafocus nacho ni marafiki wa msichana wangu. Marafiki zake ndiyo watakaoniambia niendelee kuwa naye ama niachane naye. Unapoungana na wezi wawili na kutembea nao, jua wewe ni mwizi wa tatu, muda ukifika utaamini hilo.

Chagua marafiki unaoendana nao. Halafu kumbuka si kila mtu anatakiwa kuwa rafiki. Wengine wafanye kuwa washikaji. Mtaani vijana wengi wanataka niwe rafiki yao ila mimi nimeamua kuwafanya kuwa washikaji tu. Unajua kwa nini? Ni kwa sababu nitakapokuwa nao, urafiki ukadumu, lazima na mimi nitakuwa kama wao, nitafikiria kama wao, na nitaishi kama wao.

Mpaka uwe best friend wangu kuna vitu naviangalia, baadaye nikiona hatuendani kwa mambo kadhaa, sioni shida kukufana mshikaji wangu tu.

Kuna watu wengi walifeli kwa sababu ya marafiki, na kuna watu wengi walifaulu kwa sababu ya haohao marafiki. Google ilianzishwa na marafiki wawili, Facebook ilianzishwa na marafiki. Biashara kubwa dunia ukifuatilia zilianzishwa na marafiki, hebu mwangalia rafiki yako, unahisi unaweza kutengeneza naye biashara? Unahisi ana uwezo wa kusimamia biashara? Kama una wasiwasi naye, achana naye mshikaji wangu.

Wewe na rafiki yako lazima muwe na ndoto kubwa, ndoto za pamoja. Kama ndoto yako ni kununua V8 siku moja, basi rafiki yako nawe awe na ndoto kama hiyo, sio unakuwa na rafiki ambaye ndoto yake ni kununua IST. Unapokuwa na ndoto kubwa, tafuta rafiki mwenye ndoto kubwa pia.

Una ndoto ya kuanzisha kampuni, halafu unakuwa na urafiki na jamaa mwenye ndoto za kupiga picha na Diamond siku moja. Ndugu yangu, huyu rafiki atakurudisha nyuma, wakati utakapokuwa unarudi nyuma hutogundua, utakuja kugundua siku ambayo utakuwa tayari umefika hapo nyuma.

Watu wengi mitaani wanalalamika eti mtu akipata pesa tu, anabadilisha marafiki, anakuwa si rafiki tena na wale washikaji mitaani. Hiyo ni kweli kabisa. Lini umeona mtu amekuwa tajiri halafu ana urafiki na wale washikaji wa mitaani?

Unapofanikiwa na kupata pesa, sasa ni muda wa kubadilisha kampani yako. Hutakiwi tena kuwa na urafiki na wale washikaji wa mtaani, wale wafanye wana, unawasabahi, unawa pesa, unakaa nao kwa dakika hata tano na kusepa.

Unapokuwa na pesa, ili upate pesa ni lazima uwe ma urafiki na watu wenye pesa, huu ukweli hatuupendi sana sisi masikini. Yaani tunataka leo Diamond amepata pesa, basi aje kijiweni, akae nasi kama zamani, tutakuwa tunakosea sana. Ukifanya hivyo, huna muda mwingi utarudi ulipotoka.

Ukisoma kitabu cha 50 Cent ameelezea hili, anasema washikaji wengi wanfeli kwa sababu wanataka kuwa na urafiki na watu wa mitaani kwao na ndiyo maana wengi wanauawa. Washikaji wa mitaani wanakuwa na chuki, watafanya kila njia wakumalize.

Angalia mfano kama jamaa wa Migos, ameuawa mtaani kwao alipokwenda kutembea na kucheza kamari, wanamuziki wengi wa Marekani wanauawa mitaani kwao walipokulia, kwa nini? Washikaji walioachwa mitaani bado wanakuwa na chuki mioyoni. Mshikaji wa kitaa ni rahisi kukufanyia ubaya. Unapinga na hilo?

Unapopata pesa, kuwa karibu na watu wenye pesa, ambao wana ndoto kubwa. Haiwezekani leo mtu anaendesha Range Rover ya milioni 90 halafu kila siku yupo na mshikaji mwenye baiskeli. Hatukudharau, ila najaribu kukwambia ukweli jinsi picha halisi ya maisha ilivyo.

Kama una Range Rover, rafiki yako wa kwanza awe yule mwenye Range Rover, mawazo yenu yanaweza kuwa sawa kabisa. Hili matajiri walijua sana na ndiyo maana unasikia mtoto wa tajiri fulani kamuona mtoto wa tajiri fulani. Mto wa pesa unaflows sehemu yenye pesa.

Sisi mtu akipata pesa na kubadilisha marafiki tunaanza kulalamika. Sasa bro! Mtu ana bilioni kumi kwenye akaunti, akikuomba ushauri wa biashara utampa ushauri wa biashara gani? Manake kwenye ushauri huo lazima uingizie masuala ya kodi, kodi zitakuwaje, wafanyakazi watalipwaje, faida yake itapatikanaje…sasa wewe unajua masuala ya kodi na wakati huna biashara yoyote ile?

Braza unamiliki baiskeli, kwanza kuwa na urafiki na mtu mwenye baiskeli, muwe na ndoto sawa kwa sababu ukimtafuta mtu mwenye gari, urafiki wake mkubwa utakuwa wa watu wenye magari.

Unapokuwa na pesa, pesa zinakuja zenyewe, unashangaa mtu ana pesa halafu anapata mazali ya kupata pesa zaidi. Huwa hivyo, pesa humfuata mwenye pesa. Hata mitaani tunaona, mtu akiwa mzee wa wanawake, unashangaa wanawake wanamfuata tu, yaani hapati hata kazi kuwapata, sio kama mwenzangu na mimi.

Ukizoea kupata pesa, pesa zinakuja zenyewe, ukizoea kupata wanawake, wanawake wanakuja wenyewe. Ukiwa unapatwa na mikosi, unashangaa tu mikosi inakuandama kila siku. Mwili wako unapozoea kupata magonjwa, unashangaa tu magonjwa yanakuandama. Huwa ipo hivyo.

Kama unamchukia msela kwa sababu sasa hivi ana pesa na hayupo karibu na nyie tena, bro tafuta pesa acha makasirikio.
Screenshot_20230224-022444_1.jpg
 
Tunatafuta pesa, tunaweka kanuni nyingi ili kuishi kipesa.Tunatengana na so called washikaji wa kijiweni, kwa vile tu tumepata pesa.Lakini tukifilisika tunarejea tena vijiweni kwa jamii ile ile ambayo tulikuwa nayo na baadae tukaimbia baada ya kupata pesa.Mwishowe kumbe tukiwa na pesa au tukiwa hatunazo tunatakiwa kuwa na UTU tu.Wakati mwingine pesa huzaa uadui tu.ANYWAY ZITAFUTENI ILA ZISIWAGEUZE WANYAMA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom