Jenerali ulimwengu achafua hali ya hewa mkutano wa kutathmini APRM kwa kuhoji kura za urais za 2010

mkuu..hilo swali alinamajibu ila ikitokea sikumoja jack zoka akaulizwa nadhani yeye ndye atakaetupatia majibu mazuri ila kiukweli..ni uzembe wa tume yetu ya uchaguzi.
 
Mimi nnayo, JK alishinda kwa kishindo kwa asilimia zaidi ya 60! Unabisha? Hayo ndiyo matokeo ya kina ya kura za urais, ya ubunge siri yangu! Hahahaaaaa! Tanzania ina wenyewe na wenyewe ndiyo sisiem!

Vyovyote vile, uchaguzi umepita na Rais kapatikana.
Lakini wenye akili na mapenzi mema na nchi yetu lazima tuhoji ili kuinusuru nchi na machafuko yasiyo lazima.
Mwakani Kenya wanachagua Rais, tunapata somo, tuige mfano wa Tume mpya ya Kenya kwenye kupiga kielectronik
 
Umewahi kufikiri hata ofisi ya Msajili wa vyama haijui matokeo ya kura za urais kwa kila jimbo.
Labda rais alipigiwa @ national level tu, majimboni tulikuwa tunapiga kura za wabunge tuuu, bro Tanzania tamu sana kukaa tu na kufikiri vile mambo yanaenda unaweza tamani kupigana ili hali ibakie kuwa hivi tu na vituko visituishe
 
Mimi nnayo, JK alishinda kwa kishindo kwa asilimia zaidi ya 60! Unabisha? Hayo ndiyo matokeo ya kina ya kura za urais, ya ubunge siri yangu! Hahahaaaaa! Tanzania ina wenyewe na wenyewe ndiyo sisiem!
Elewa swali kabla ya kujibu. Swali linauliza "Kuna anayejua matokeo ya kurauraisi kwa kila jimbo la uchaguzi?"
Jibu linapaswa kuwa:
  1. Rungwe Mashariki...............XXX
  2. Rungwe Magharibi...............XXX
  3. Bukoba mjini......................XXX
  4. Musoma vijijini...................XXX
Kusema alipata 60% sio jibu sahihi kwa swali hili. Linaweza kuwa sahihi kwa swali lingine lakini sio hili. Subiri Jenerali aulize swali lingine litakalohitaji jibu hili. Swali hili linaweza kuwa: "Raisi, wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, katika uchaguzi mkuu wa October 2010, alipata kura asilimia ngapi ya wapiga kura wote waliojitokeza kupiga kura?"
Jenerali hajauliza swali hilo kwa sababu kila mmoja, hata mjinga anajua kwa kuwa ndizo zilizotangazwa na Tume ya Uchaguzi. Kura hizi zilipaswa zitokane na kura za kila jimbo la uchaguzi ambazo hakuna anayezijua. Kwa mantiki ya kawaida ni kuwa kura za kila jimbo ni siri ya Tume ya Uchaguzi.
Nguzo mojawapo ya utawala bora ni UWAZI (TRANSPARENCY). Kama hakuna uwazi, taarifa haziwezi kufuatiliwa zikajulikana chanzo chake, utawala bora ni ndoto. Nguzo ya pili ni ushirikishwaji (participation). Kama wananchi hawakushirikishwa kumchagua Rais wao, Rais amewekwa na USALAMA wa Taifa, Utawala bora ni zero.
Kama 2+2= 4, haiwezekani 2+ = ikawa 4
 
hivi kibonde wa clouds kwanini asijifunze kutoka kwa jenerali ulimwengu?

Mkuu atakula wapi? Njaa haina aibu. Uongo na kujipendekeza ni sehemu ya maisha yao ili tu mkono uende kinywani. Watu kama hawa ni wabaya sana.
 
Hata kama kwa viboko tena vile vya mkoloni wa kijerumani Mkuu Aweda M P hlitakaa lijibiwe swali la Jenerali ulimwengu,ni kwamba halina jibu.na kama kuna mtu analeta ubishi wa kilimbukeni na itikadi bandia za kichama aende NEC ith official letter aki-request kupewa matokeo ya uchaguzi wa rais kwa mwaka 2010 kwa ukamilifu wake aone kama atapatiwa kitu.hapo ndipo utakapopata jibu la kuwa watu wanapozungumzia utawala bora ni gelesha ya kwenye vmaandishi tu,uhalisia haupo.
Nakushukuru mkuu Aweda kwa kutumegea ulichokisikia katika mkutano huo.
 
Wa Tz ni wazembe, mazezeta acha tutawaliwe maana hata maana ya democracy hatujui, the right to vote, to elect and to be elected to be representative. Wizi tunauona hatuchukui hatia, haki inapiganiwa, linda kura ili upate kiongozi wako. Mfano ubungo, arumeru mashariki, watu walikomaa kikaeleweka, kwa mpendazoe zingepatikana picha tu za yale masanduku ingekuwa safi,
 
Matokeo ya kura za Urais kwa kila jimbo hayakutangazwa au yaliyotangazwa yanadaiwa si ya kweli?
 
kURA ZIPI ZILIZOCHAKACHULIWA?HIZI ZA UDIWANI JUZI AU?WAPINZANI WA BONGO MNA SAFARI NDEFU SANA AISEE,KILA KUKICHA WARSHA,MIAMSHO,MAKAONGAMANO N.K. LAKINI UKIJA UCHAGUZI WANANCHI WANAWAKATAA

Mkuu, suala si tu haki itendeke, BALI ionekane imetendeka. Wanasheria wanasema ithibitike pasi na mashaka, yaani beyond reasonable dout.
 
usalama wa taifa walikesha kutiki kura za ndiyo za jk ni jambo ambalo liko wazi na linafahamika kwa hyo ulimwengu alikuwa sahihi kwa sababu majimbo yote yalificha kura za uraisi na dk slaa alitumia busara sana kukaa kimya kutoingiza nchi hii kwenye vita kwa sababu ukweli wote ulijulikana
 
Wakuu,
Nilipata fursa ya kuhudhuria kikao cha kutathmini mchakato wa APRM kilichoandaliwa na asasi ya kimataifa ya OSEA ktk hoteli ya Kilmanjaro DSM wiki hii.

Kikao hicho kiliwashirikisha vyama vyote vya siasa, ofisi ya msajili, Asasi za kiraia, wabunge, waandishi wa habari viongozi wakubwa wa serikalini, Maprofesa kutoka ndani na nje nk.

Kulikuwa na wasemaji kutoka ndani na nje ya nchi wakiwepo wabunge wajumbe wa APRM wa kwetu na kutoka nchi mbali mbali wakiwepo mmoja wa profesa kutoka ghana aliyewasilisha mada.

Kama kawaida kulikuwa mjadala mzito wengine wakisema kiwango cha utawala bora nchini kinaridhisha na wengine wakisema hakiridhishi.

Mmoja wa wasemaji jenerali Ulimwengu ktk dakika zake za mwisho alichafua hali ya hewa pale alipouliza swali lililoshindwa kujiwa na wote waliokuwemo ktk ukumbi huo.

Aliuliza, wakati tunapojadili utawala bora je, kuna mtu yeyote miongoni mwetu anayejua matokeo ya kura za urais za mwaka 2010 kwa kila jimbo ktk ukumbi huu?

Swali hilo lilibadilisha kabisa hali ya hewa humo ndani hata wale waliokuwa wanasema TZ kuna utawala bora walikaa kimya na wote tukatazamana.

Mwandishi moja akaendelea kuweka chumvi kwenye kidonda kwa kusema yeye alizitafuta na hakufanikiwa.
Hali hiyo ilimfanya mwongoza kipindi kumkaribisha msemaji wa OSEA kufunga mkutano huo ktk mazingira hayo yasiyo na jibu na swali hilo.

My take,
Naomba kutoa changamoto kama kuna mwanajf mwenye jibu la swali la Jenerali UlImwengu atupe kwa faida ya wanajf wote.

Fungua website ya Tume ya Taifa ya uchaguzi utayaona , mbona yako kule. Ulimwengu, amechanganyikiwa tangia alipoambiwa yeye sio raia, huo ni wivu alio nao ulimwengu tangia system ilipomwacha
 
:cheer2: :cheer2:.............Tanzania bado inapita katika mchakato wa wananchi wake kujitambua.....hili somo la uraia bado ni tatizo.... elimu ya uraia ielekezwe katika maeneo yote..... kuna watu ambao ni mashabiki wa upinzani, na wanazo kadi za kupigia kura lakini hawaendi kupiga kura... wako watu ambao hawana vitambulisho vya kupigia kura lakini hawafanyi jitihada zozote kupata vitambulisho hivyo.... hata inapotolewa taarifa na tume ya uchaguzi kwamba waende kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho hivyo ... hawaendi... hapo ndo pa kuanzia.... hata kama kuna kuchakachua watu wajitambue wakapige kura....... unajua hata kama refa anaiuma timu yenu... jitahidini kufunga magoli ya mbali muone kama refa atakataa kila goli.....:target:
 
Kusema ukweli mie sijaelewa msingi wa swali hili alilouliza bw.Ulimwengu.Nasema hivyo kwa sababu sote ni mashahidi kuwa tume ya uchaguzi ilikuwa ikitangaza kura za mgombea ubunge na uRais kwa kila jimbo.Sasa alikuwa akimaniisha washiriki kama walikariri matokeo hayo vinchwani mwao au ni vipi? ufafanuzi tafadhali!
 
Nashangazwa kuona karibu kila mdau anasubiria 2015 kwa kigezo kutakua na katiba mpya, me naamin mwizi ni mwiz tu alafu ukizingatia ameshakua jambaz sugu!. nadhan tungejipanga na huu mfumo wa kielectronia na elimu zianze kutolewa mapema labda tunaeza fikia lengo la 2015 ikiwemo na kutunza kumbukumbu.
 
hivi kibonde wa clouds kwanini asijifunze kutoka kwa jenerali ulimwengu?

Jenerali Ulimwengu huwa hategemei mkate wake kwa kufanya kazi za kiuhouseboy kama kina Ritz, Kibonde, nngu007, Rejao na wengine ambao bila kusujudia mafisadi mkono hauendi kinywani. Ana fikra pana sana na ndizo zinazomwezesha kuendesha maisha yake bila ya kuwa tegemezi kama niliowataja hapo juu. Ukiwa mvivu wa kufikiri utaishia kuishi kwa kujikomba komba tu maisha mwako.
 
Umewahi kufikiri hata ofisi ya Msajili wa vyama haijui matokeo ya kura za urais kwa kila jimbo.

Duh!!!!!!!!!! Hiii kali akya mama, yaani mimi na ujanja wangu sijawahi kufikiri hivi aisee na kama ni kali basi kweli kuna watu wanatufanya mazuzu!!!!!!????? yaani hii ni kali akya mungu, lkn yana mwisho tu!!!!!
 
Swali zuri sana
Ni kweli. Lakini limechelewa mno. Jenerali na sisi wengine tulikuwepo mwaka 2010 matokeo yalipotangazwa. Tatizo jingine kubwa ni KATIBA yetu ya sasa. Hairuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa na chombo chochote au yeyote yakishatangazwa na Tume ya Uchaguzi. Jenerali wetu anaweza kukamatwa akahojiwa kwa swali hili?
 
Back
Top Bottom