Jenerali ulimwengu achafua hali ya hewa mkutano wa kutathmini APRM kwa kuhoji kura za urais za 2010

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Wakuu,
Nilipata fursa ya kuhudhuria kikao cha kutathmini mchakato wa APRM kilichoandaliwa na asasi ya kimataifa ya OSEA ktk hoteli ya Kilmanjaro DSM wiki hii.

Kikao hicho kiliwashirikisha vyama vyote vya siasa, ofisi ya msajili, Asasi za kiraia, wabunge, waandishi wa habari viongozi wakubwa wa serikalini, Maprofesa kutoka ndani na nje nk.

Kulikuwa na wasemaji kutoka ndani na nje ya nchi wakiwepo wabunge wajumbe wa APRM wa kwetu na kutoka nchi mbali mbali wakiwepo mmoja wa profesa kutoka ghana aliyewasilisha mada.

Kama kawaida kulikuwa mjadala mzito wengine wakisema kiwango cha utawala bora nchini kinaridhisha na wengine wakisema hakiridhishi.

Mmoja wa wasemaji jenerali Ulimwengu ktk dakika zake za mwisho alichafua hali ya hewa pale alipouliza swali lililoshindwa kujiwa na wote waliokuwemo ktk ukumbi huo.

Aliuliza, wakati tunapojadili utawala bora je, kuna mtu yeyote miongoni mwetu anayejua matokeo ya kura za urais za mwaka 2010 kwa kila jimbo ktk ukumbi huu?

Swali hilo lilibadilisha kabisa hali ya hewa humo ndani hata wale waliokuwa wanasema TZ kuna utawala bora walikaa kimya na wote tukatazamana.

Mwandishi moja akaendelea kuweka chumvi kwenye kidonda kwa kusema yeye alizitafuta na hakufanikiwa.
Hali hiyo ilimfanya mwongoza kipindi kumkaribisha msemaji wa OSEA kufunga mkutano huo ktk mazingira hayo yasiyo na jibu na swali hilo.

My take,
Naomba kutoa changamoto kama kuna mwanajf mwenye jibu la swali la Jenerali UlImwengu atupe kwa faida ya wanajf wote.
 
Nadhani watakuja na majibu ya kuchakachua kwa swali la Jenerali Ulimwengu,kama waliweza kuchakachua kura basi wataweza pia kuja na majibu ya swali husika kama kawaida yao.

Tunapenda kuona watanzania wenye uwezo wa kujipambanua na kuuliza maswali magumu ambayo majibu yake huwa ni kigugumizi kwa serikali kama alivyofanya Ulimwengu
 
Mimi nnayo, JK alishinda kwa kishindo kwa asilimia zaidi ya 60! Unabisha? Hayo ndiyo matokeo ya kina ya kura za urais, ya ubunge siri yangu! Hahahaaaaa! Tanzania ina wenyewe na wenyewe ndiyo sisiem!
 
Imefika wakati sasa kwa tume ya uchaguzi,kutumia mifumo ya kisasa ya kielektroniki,yenye uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu kwa muda mrefu,
 
NEC ni wapuuzi. Mfano mzuri ni aliyekuwa waziri wa Maliasili 'mwizi' Maige alibeba mabox ya kura za urais za jimbo la Msalala na kukimbia nayo kwenye gari chini ya ulinzi wa polisi na usalama wa taifa. I can testify this in court

2015 kazi itakuwa pevu!
 
hajui huyo. Atajulia wapi? Mkuu fanya uchunguzi kuhusu jimbo la Msalala halafu uje uitoe kwenye Malumbano ya Hoja!

Mkuu, majimbo mengi yamenda ccm 2010 kwa staili hiyo hiyo ya Msalala. Jana nilitoa maoni yangu hapa Dsm kwenye tume ya katiba kuhusu umuhimu wa tume huru ya uchaguzi japo najua imesemwa sana. 2015 ili tukae na amani yetu tunahitaji tume huru ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom