Jenerali Mabeyo(JWTZ): Kuna Viashiria vinavyotishia Usalama wa Nchi. Hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo

siku zote mtu akifanya mambo mazur tu ni lazima aungwe mkono na watu na ukiona watu hawakuungi mkono yakupasa ukae chin ujiulize ni wapi umekosea ili ujirekebishe, wengi tunaamin kama mtu akifanya mambo mazur tu lazima akubalike tu
Ni ushauri mzuri, lakini tangu lini uliwahi kuona vichaa wamekaa chini wakipanga mambo mazuri yasiyoweza kuwadhuru watu wazima?!!!!
 
Jeshi libaki kambini mpaka litakapoitwa kama hatua ya mwisho ya juhudi nyingine zote za vyombo vya ulinzi.

Inakuwaje jeshi likatangaza military operations walizoamua wao wenyewe na ambazo Kamati y Bunge ya Ulinzi na Usalama haizijui?

Kofia na nyota 4 mbele, hivi huyu Jenerali wa kibongo amefanya nini cha kuitwa Four Star General?

Ukisikia mtu anaitwa four star general nchi za wenzetu yani anakuwa mtu ameshafanya ma life and death strategic decisions ya kijeshi...

Anakuwa ashakuwa bosi wa ma central command yanayoratibu military operations...

Anakuwa kaandika ma peace and security dossiers y kushauri a kubishana na wanasiasa wa wizara ya ulinzi na Ikulu...

Anakuwa ashawahi kuwa foot soldier kwenye ma battle fronts toka mdogo. Mabeyo hata Kagera kapigana?

Mkuu wa kikujibu ni tag
 
Siasa za maji machafu zimeingia hata katika jeshi letu sasa. Huyu baba ni msukuma na amewekwa ili awe controlled kama remote control from Magogoni na bwana Bombe Magufuli. Watu wasioweza kuendeshwa kwa kutumia remote hawana nafasi katika hii serikali ya Kidikteta.

amenunuliwa yaani pesa za walipa kodi zinatumika kuwaziba midomo watu walio katika mihimili ya serikali. Hakuna mahakama- Jaji mkuu amenunuliwa, Mkuu wa Polisi - Sirro Amenunuliwa, kuna viongozi wa dini nao walio nunuliwa. Asilimia 98 ya wabunge wa CCM wamenunuliwa, na sasa NIMESIKITIKA KUONA HATA MKUU WA MAJESHI NAYE AMENUNULIWA.
Unazingua bhana........
 
Fake news.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo amewataka Watanzania kujiepusha na vitendo vinavyoweza kutishia usalama wa nchi na kuharibu tunu ya amani iliyopo.

Ameeleza kuwa hivi sasa vipo viashiria vinavyotishia usalama wa nchi, na kwamba hatua zinachukuliwa ili kudhibiti hali hiyo.

Jenerali Mabeyo amewaomba Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli dhidi ya wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi za umma, kwa kuwataja hadharani watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Ametoa kauli hiyo jana wakati akifunga Maadhimisho ya Tamasha la Mashujaa wa Vita ya Majimaji katika Viwanja vya Makumbusho ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji mjini Songea.

Mabeyo amesema vita dhidi ya wizi na ufisadi, iliyoanzishwa na Rais Magufuli, si ya mtu mmoja, bali kila Mtanzania anapaswa kushiriki, kwani mali zinazoibwa na baadhi ya Watanzania, zinapaswa kuwanufaisha watu wote.

Mabeyo alisema badala ya kushughulika na uvunjifu wa amani, ipo haja ya Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo imedhamiria kuwatumikia wananchi kwa kuboresha huduma za kijamii ili kutoa fursa kwa wananchi kutumia muda wao kufanya kazi za kujiletea maendeleo.

Ametaja baadhi ya mambo yanayotishia usalama wa nchi kuwa ni matumizi mabaya ya utandawazi ambayo mbali na ya kuharibu utamaduni wa nchi, baadhi ya watu wanaitumia vibaya kwa kuhamasisha wananchi kufanya na kushiriki katika matukio ambayo yanaashiria uvunjifu wa amani na utulivu uliopo nchini kwa muda mrefu.

Jenerali Mabeyo alitaka shule za msingi, sekondari na vyuo nchini, kufundisha wanafunzi umuhimu wa kulinda, kutunza amani na wananchi kuishi kwa kupendana, badala ya kutumia muda wao kutafuta sababu za kutengana, jambo ambalo halina tija kwa taifa.

Wakati huo huo, Jenerali Mabeyo aliitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuboresha Makumbusho ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji ili yatumike kwa ajili ya utalii na kuliingizia taifa fedha nyingi.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Chiristina Mndeme alisema Serikali ya Mkoa wa Ruvuma, itaongeza nguvu katika kulinda mipaka yake ili wananchi wa mkoa huo waweze kuendelea na kazi za uzalishaji mali.
 
Kuna tatizo amabalo ccm bado hawalitambui. Labda ni mpango wa Mungu kwa Marne hii kuikomboa Tanzania.

Badala ya serikali na vyombo vya ulinzi na usalama kutatua matatizo yanayolalamikiwa na wananchi hadi kupelekea hali ya sintofaham na uratibu wa maandamano ya amani, imebaki inatoa matamko wakati hali halisi sio nzuri.
Mkuu wa jeshi, mshauri aliyekuteuwa mwambie hali halisi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa sio nzuri. Angalie amekosea wapi arekebishe , matamshi na vitisho havitasaidia tena, watu wamechoka wako tayari kwa lolote. Someni alama za nyakati. Acheni kulindana ni wakati wa kuambiana ukweli kama kweli nnaitaka amani ya Tanzania, anayeivuruga amani ya Nchi na Maghufuli na Makonda kwa uonevu dhidi ya wafanyakazi, mauaji ya RAIA, kesi za kusingiziwa, Uhuru wa maoni na kupata habari, Uhuru wa shughuli za kisiasa ambazo ni za kikatiba, matumizi mabaya ya madaraka na fedha za serikali(ujenzi wa uwanja wa chato na manunuzi ya ndege), binge kizazi, manyanyaso ya wapinzan na wafanyakazi, mikopo ya elimu ya huu, huduma finyu za afya hakuna madawa ya kitosha, ukabila udini na ukana aliyoujenga Maghufuli, hki ya uchaguzi kura kuibiwa wakishirikia na poloce huku wakiqanyima wapinzani form za kiapo,
Acheni unafki kumpamba Maghufuli na kuwakandamiza wananchi hamsaidii kuokoa amani ya nchi ndio kwanza mnazidi kuipeeka kwenye shimbo. Unafki mshahara wake mauti...ndio tunapoelekea ndugu mkuu wa jeshi.
Mmeuficha ukweli mnahubiri unafki kwa maslahi ya matumbobyenu.
 
Siasa za maji machafu zimeingia hata katika jeshi letu sasa. Huyu baba ni msukuma na amewekwa ili awe controlled kama remote control from Magogoni na bwana Bombe Magufuli. Watu wasioweza kuendeshwa kwa kutumia remote hawana nafasi katika hii serikali ya Kidikteta.

amenunuliwa yaani pesa za walipa kodi zinatumika kuwaziba midomo watu walio katika mihimili ya serikali. Hakuna mahakama- Jaji mkuu amenunuliwa, Mkuu wa Polisi - Sirro Amenunuliwa, kuna viongozi wa dini nao walio nunuliwa. Asilimia 98 ya wabunge wa CCM wamenunuliwa, na sasa NIMESIKITIKA KUONA HATA MKUU WA MAJESHI NAYE AMENUNULIWA.
Aseeeeeeeee
 
Tunahitaji tafiti na ushahidi gani tena kudhibitisha kwamba jeshi haliko compromised na ccm????

Leo CDF anatoa rai tuunge mkono juhudi za raisi dhidi ya ufisadi na .....Jeshi na siasa wapi na wapi na haya mambo yameanza lini hapa kwetu????

Nauliza hivi Je hili ni Jeshi la wananchi au jeshi la ccm?????

Hvi kwa matamshi ya huyu cdf wa ccm kuna sababu tena itakayonifanya nisiunge mkono April 26???????????
 
Hivi inaingiaje akilini mkuu wa majeshi kutumika kwenye majukwaa ya siasa? It is very disgusting you know!
KWA UTAWALA HUU DHALIMU:
1. Jeshi na siasa inaruhusiwa.
2. Police na siasa inaruhusiwa.
3. Siasa na dini inaruhusiwa.
4. DINI NA SIASA HAIRUHUSIWAI, hawa wanaikosoa sana serikali ya Mtukufu,Malaika, Mungu kwa was ccm Magu.
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo amewataka Watanzania kujiepusha na vitendo vinavyoweza kutishia usalama wa nchi na kuharibu tunu ya amani iliyopo.

Ameeleza kuwa hivi sasa vipo viashiria vinavyotishia usalama wa nchi, na kwamba hatua zinachukuliwa ili kudhibiti hali hiyo.

Jenerali Mabeyo amewaomba Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli dhidi ya wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi za umma, kwa kuwataja hadharani watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Ametoa kauli hiyo jana wakati akifunga Maadhimisho ya Tamasha la Mashujaa wa Vita ya Majimaji katika Viwanja vya Makumbusho ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji mjini Songea.

Mabeyo amesema vita dhidi ya wizi na ufisadi, iliyoanzishwa na Rais Magufuli, si ya mtu mmoja, bali kila Mtanzania anapaswa kushiriki, kwani mali zinazoibwa na baadhi ya Watanzania, zinapaswa kuwanufaisha watu wote.

Mabeyo alisema badala ya kushughulika na uvunjifu wa amani, ipo haja ya Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo imedhamiria kuwatumikia wananchi kwa kuboresha huduma za kijamii ili kutoa fursa kwa wananchi kutumia muda wao kufanya kazi za kujiletea maendeleo.

Ametaja baadhi ya mambo yanayotishia usalama wa nchi kuwa ni matumizi mabaya ya utandawazi ambayo mbali na ya kuharibu utamaduni wa nchi, baadhi ya watu wanaitumia vibaya kwa kuhamasisha wananchi kufanya na kushiriki katika matukio ambayo yanaashiria uvunjifu wa amani na utulivu uliopo nchini kwa muda mrefu.

Jenerali Mabeyo alitaka shule za msingi, sekondari na vyuo nchini, kufundisha wanafunzi umuhimu wa kulinda, kutunza amani na wananchi kuishi kwa kupendana, badala ya kutumia muda wao kutafuta sababu za kutengana, jambo ambalo halina tija kwa taifa.

Wakati huo huo, Jenerali Mabeyo aliitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuboresha Makumbusho ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji ili yatumike kwa ajili ya utalii na kuliingizia taifa fedha nyingi.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Chiristina Mndeme alisema Serikali ya Mkoa wa Ruvuma, itaongeza nguvu katika kulinda mipaka yake ili wananchi wa mkoa huo waweze kuendelea na kazi za uzalishaji mali.

Viashiria vya kutoka nje ya nchi au humu humu ndani? inavyoonekana unazungumzia vya ndani sasa IGP yeye atasema nini?

Mimi nafikiri mkae chonjo hiyo 26 April wanajeshi wafanye route march nchi nzima.
 
Amani ni utulivu wa kiakili,moyo pamoja na mazingira kwa ujumla. Amani hii ipo kwa kila mmoja?
 
Hahahahaa...anaendeshwa na kina polepole. Yaani pole pole ana nguvu kuliko yeye. Aki deal na wasiojulikana ntamuona ni mwanaume kweli kweli.

Mkuu wa majeshi namheshimu sana lakini kwa speech hii amejishushia heshima. Kama mkuu wa ulinza na usalama ktk mipaka ya nchi hii, anetaja hivyo viashiria ni vipi.

Lakini kwa kuwa anajua fika viashiria hivyo vinamlenga mtu fulani ameishia kusema tu kiujumlajumla.
Huwa naliheshimu sana Jeshi kupita maelezo, lakini tangu huyu jamaa ameteuliwa kuwa mkuu wa Majeshi nimekua kwenye wakati mgumu sana ma pia nimekua na simanzi.
Ila kwa heshima yangu kwa jeshi letu nimeamua kukaa kimya tu pasipokuongelea masuala ya Kijeshi.
 
Tanzania Tanzania hivi kila kituko lazima kianzie kwetu! Walipo tekwa ndugu zetu si serikali wala vyombo vyake vya ulinzi na usalama vilijitokeza kupinga vitendo hivyo viovu.

Walipo uwawa inaodawai wahamiaji haramu kwa mujibu wa waziri wa ulinzi bila kufanyiwa uchunguzi wa kina mlinyamaza.

Wakauwawa ndugu zetu askari polisi,kidogo mkastuka na kuanza operation kwa kuwa ni watumishi was chombo cha dola watumikao vilivyo,wote tukalaani bila ubaguzi kwa kuthamini haki na utu wa mtu.

Wakauwawa ndugu zetu huko Morogoro kwa kukatwa mapanga na kwa kuwa wametokea vyama vya upinzani si IGP wala mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama aliyestushwa. Ikaonekana marehemu wetu wamejiuwa wenyewe hawana haki ya kuwajua wauwaji.

Zimetumika silaha za kivita kufanya shambulizi kwa lengo la mauaji lakini hakutokea kamanda Mabeyo kustushwa wala kutoa kauli ya kulaani lakini hata ule uchunguzi tu eti bado una msubiri dereva wa Mh. Lissu.

Tuna tatizo gani Watanzania ikiwa maandamano ya amani yana ibua mpaka wakuu wetu wa majeshi kutoa vitisho ilihali matukio ya mauaji ya chuki ya kisiasa yaonekane ni jambo dogo na la kawaida.

Kuwatisha Watanzania wahanga wa mfumo kandamizi ni kinyume na misingi ya haki za binadamu na demokrasia kwa umoja wake. Watanzania wanalilia utawala wa sheria wenye kujali na kuzingatia ustawi wa taifa na watu wake.

Watanzania wamechoshwa na vitisho,kejeli,kupuuzwa na kudharauliwa utu wake. Wamechoshwa na maamuzi ya kibabe yanayo fanywa na sauti ya mtu mmoja. Kuendelea kututisha ni kutuongezea chuki dhidi ya serikali yetu iliyo shindwa kutekeleza matakwa ya jamii ya Kitanzania.

Hatuandamani kama wajinga,tuna andamana kwa faida yetu na vizazi vyetu tukibeba ujumbe utakao wakilishwa kwa sauti ya umoja wa wananchi.

Watanzania wana andamana kudai madai ya msingi na kurudisha ugatuaji wa madaraka unao zingatia weredi,haki na usawa. Watanzania wamechoshwa na mgawanyo wa makusudi wa matabaka na upendeleo miongoni mwao.

Haingii akilini Kimara wana bomolewa nyumba bila fidia wakati huo huo Mwanza wanazuia eti ni wapiga kura walio mchagua. Hivi makamanda hamkuiona hiyo ni dosari mkamshauri bwana Mkubwa juu ya athari ya ubaguzi huo.

Inasikitisha ina sononesha ikiwa hata majeshi yamekuwa bias bila kujali utaifa wetu. Kwa nini tunaingiza chuki ya kimamlaka ilihali sisi sote ni familia moja.

Sitaki kuamini kauli ya Mabeyo ni msimamo wa jeshi,ingekuwa polisi nisinge shangaa hao wapo bias siku nyingi wakiutumikia mkate wao wa siku.

Mko wapi viongozi wa dini,kimya chenu kinashiria nini au uoga wa kutembelewa na TRA. Matukio makubwa ya uvunjifu wa amani hamyakemei mna subiri mpaka tupigwe ndipo mtoe matamko wakati wa ibada za mazishi yetu!!!

Kila mmoja atekeleze majukumu take kwa haki kama waandamanaji watakapo tekeleza haki yao kikatiba.

TANZANIA YETU ITAJENGWA NA WALE WENYE MOYO SAFI SI VITISHO.
 
kwa hiyo ulishawahi ona polisi kabla ya kupiga virungu wanahoji mtu kuwa wewe kabila gani ni ukoo wetu au la au ulishawahi ona wanauliza vitambulisho kabla ya kukushushia virungu? Aisee unachekesha
Huna akili kama wao. Unapopiga risasi hovyo kama una akili unajiuliza jee hii ikimpata kaka au baba ambaye yupo hapa bila mid kujua nitajisikiaje?
Hivi kama aliyemshuti Akwilina akigundua ni Dada yake wa damu unadhani hata hiyo kazi ataitaka tena
 
Back
Top Bottom