JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro imemhukumu kifungo cha miaka saba jela Donati Phabian baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia Alfred Damas kwa madai ya kumkuta akizungumza na mtalaka.
Phabian alifanya kitendo hicho baada ya kuwakuta wawili hao barabarani katika Kijiji cha Lugangwa, Tarafa ya Matombo Mkoani Morogoro.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Paulo Ngwembe alisema amezingatia kwa kina mazingira yaliyosababisha mauaji hayo na kuona kuwa ni mazingira ya kukosekana kwa utu.
Jaji alisema mshtakiwa aliamua kujichukulia sheria mkononi kwa kumuua mwanaume aliyemkuta amesimama njiani akizungumza na mwanamke ambaye yeye alikuwa mke wake huku akiwa tayari ameshampa talaka.
Licha ya mshtakiwa kufika kituo cha polisi kujielezea kuwa alifanya hivyo kwa sababu bado ana mapenzi na mkewe na asingependa awe na mtu mwingine, alisema hilo ni jambo la mapenzi ya kitoto na kwamba kama angetaka usuluhishi wangeenda mbele ya wazazi wao.
Alisema kimsingi inaonyesha mshtakiwa alijipeleka polisi kwa kulinda usalama wake na si kujutia makosa yake kwamba adhabu hiyo ya miaka saba jela, itamfanya ajutie makosa yake na kuwa fundisho kwa wengine.
Hata hivyo, Jaji Ngwembe alisema hati ya kukata rufani dhidi ya adhabu hiyo iko wazi kwa mshtakiwa pale atakapotaka kufanya hivyo.
Awali, Wakili wa Utetezi, Kisawai Mandela, aliiomba mahakama kumpa mshtakiwa adhabu yenye huruma kwa sababu ni mtendaji kosa kwa mara ya kwanza na ana watoto ambao wanamtegemea.
Naye Wakili wa Serikali, Evelyne Ndunguru, aliiomba mahakama kumpa mshtakiwa adhabu itakayolingana na kosa alilolitenda ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia za kujichukulia sheria mkononi.
Akisoma shtaka, karani wa mahakama hiyo, Lilian Kombe, alidai kuwa mshtakiwa alifanya kosa hilo mwaka 2021 kwa kumuua mwanamume kwa kumchanja na kisu mwilini mbele ya ndugu wawili wa mwanamke huyo, jambo lililosababisha kifo chake papo hapo.
Wakati huo huo, Amelda Ngagiri (60) mkazi wa kijiji cha Nyandira, wilayani Mvomero amehukumiwa kifungo cha nje kwa miezi 12 na kupewa adhabu ya kusafisha eneo la kituo cha afya Nyandira baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia.
Jaji Ngwembe alisema ameamua kutoa hukumu hiyo kwa mshtakiwa huyo kutokana na umri wake mkubwa na afya yake kuwa si nzuri na kwamba anapaswa kusafisha kituo hicho na akishindwa atakwenda jela miaka minne.
Awali karani Lilian Kombe alidai kuwa tukio hilo lilitokea Mei 25, 2020 majira ya usiku katika kijiji cha Nyandira ambapo mshtakiwa huku akijua kufanya hivyo ni kosa, alimuua kwa kumshambulia na gongo aliyekuwa amelewa.
Source: IPP