Je, ziwa Nyasa limetwaliwa na Malawi kinamna?

Kwanini rais asiwaamuru JKT wajenge ukuta ili tuwe na letu na Malawi wabaki na lao permanent.
 
Wamalawi huliita ziwa Malawi hivyo kama umesearch ramani ya Malawi lazima lije kwa jina lao.

Hilo ziwa wakilichukua ni mwanzo wa vita ya III ya dunia.
Vyovyote utakavyo search mkuuu mpaka haupo katikati kama maziwa mengine.
 
Namna Google inavyofanya kazi ni kuwa ukiwa Pakistan unatakiwa uone ramani ya Kashmir inayotambuliwa na Pakistan, ukiwa India unatakiwa uone ramani hiyohiyo inavyotambuliwa na India na hivo zitaonekana tofauti. Ndo maana mwaka jana mwishoni Russia waliitaka Apple ramani zao zioneshe Crimea ni sehemu yake, wakabadilisha lakini ukienda Ukraine utaona Crimea hiyohiyo inaonekana ni sehemu ya Ukraine. Hivo basi Tanzania tulitakiwa kuijulisha Google ifanye marekebisho. Hata hivo jina la Nyasa tunalijua sisi pekee maana hata kwenye mikataba halikuitwa hivo. Assume ziwa Tanganyika Wakongo waliite kilugha chao unadhani kuna jumuiya ya kimataifa italitambua jina hilo.
 
Back
Top Bottom