Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

Eric,

Acha kupayuka ovyo, Zitto kakosa uhalai wa kuwa kiongozi kwa mujibu wa kifungu gani cha katiba yenu? acha blah blah umemwaga pumba tupu, kajipange uje upya au mwambieni baba mkwe amvue uanachama kabisa.

Philemon,

Eric Ongara mwanachadema (sijui ana cheo gani huko ) amekuja na shutuma na kumwaga matusi ya nguoni kwa Zitto. Huu ni muendelezo wa mashambulizi ya viongozi wa kada mbalimbali wa Chadema kwa Zitto.

Katika hali kama hii Zitto akijibu anaambiwa anavujisha siri! kakosa uhalali wa uongzozi nk.

Doule standards!

- Mkuu Masatu heshima mbele, toka jana nimekuwa nikizuiwa kuingia kutoa mawazo yangu kama yako kwa sababu sikubali mawazo ya mkubwa mmoja, wewe mkubwa I hope unazo nguvu kweli,

- Maana kama ni hizo nguvu uwe nazo kila kona sio JF tu! kwa sababu na wengine tunazo sehemu zingine ambazo huna, sasa it is only a matter of time!, hii ni mara ya pili unacheza huu mchezo, wewe umeanza kuna siku na mimi nitamalizia, ili nione kama kweli unazo hizo nguvu kila kona! That is a promise!

Respect.

Field Marshall Es!
 
Hivi kukemea kwake dhidi ya maovu ya Chadema ndio kigezo cha kumshutumu kwamba hana mapenzi na Chadema? Kumbe ukiwa kiongozi wa Chadema kamwe hutakiwi kukemea maovu ya Chadema hadharani hata kama maovu hayo ni pingamizi la juhudi za kumletea maendeleo Mtanzania!!

Nisingependa nishawishike kwamba ni Kweli chadema ina wenyewe...na nisingependa nishindwe kukubali kwamba "na wenyewe ni wachaga".

Zitto alitangaza kugombea na kisha akachomoa (sioni connection yoyote ya kukemea maovu ya Chadema). Kabla ya hapo, Zitto alifanya yafuatayo-

1. Alijiunga na kamati ya madeni ya Kikwete (akipingana na wenzake)
2. Aliungana na mafisadi kwenye issue ya Dowans
3. Hakujulikana msimamo wake kwenye bajeti ya serikali iliyopita.

Kukosa msimamo kwenye mambo muhimu ndiko kumemtoa Zitto kwenye hiyo sifa unayojaribu kumpa kuwa yeye ni mpiganaji kwenye vita muhimu ya kumletea mtanzania maendeleo (haya ni maoni yangu).

Hayo mengine ya uchaga na chadema nadhani unarudi kule kule kwenye ukabila na chuki zisizofaa ndani ya nchi na hivyo kukufanya wewe kuwa mtu mwenye chuki mbaya sana za kikabila na unayefaa kuogopwa kama ukoma.
 
- Mkuu Masatu heshima mbele, toka jana nimekuwa nikizuiwa kuingia kutoa mawazo yangu kama yako kwa sababu sikubali mawazo ya mkubwa mmoja, wewe mkubwa I hope unazo nguvu kweli,

- Maana kama ni hizo nguvu uwe nazo kila kona sio JF tu! kwa sababu na wengine tunazo sehemu zingine ambazo huna, sasa it is only a matter of time!, hii ni mara ya pili unacheza huu mchezo, wewe umeanza kuna siku na mimi nitamalizia, ili nione kama kweli unazo hizo nguvu kila kona! That is a promise!

Respect.

Field Marshall Es!

Huyu anayezuia watu kuchangia ashindwe na alegee.
 
Huyu anayezuia watu kuchangia ashindwe na alegee.

- You might be a smart man!, ila kwenye maisha huwa kuna kuzidiana ujanja na dunia ni ndogo sana sio kubwa sana.

- Sisi tunakuja kujadili taifa hapa kumbe kuna ambao wana agenda zao za kutumwa na wanasiasa mafisadi humu, atleast sasa I am glad kwamba nimeelewa maana kweli among all the people it was the right thing sana kunifanyia mimi, wazee wa sauti ya umeme, sasa ni zamu yangu kujibu, and I will.

Respect and Out!

FMEs!
 
- You might be a smart man!, ila kwenye maisha huwa kuna kuzidiana ujanja na dunia ni ndogo sana sio kubwa sana.

Vitisho tena?!

- Sisi tunakuja kujadili taifa hapa kumbe kuna ambao wana agenda zao za kutumwa na wanasiasa mafisadi humu, atleast sasa I am glad kwamba nimeelewa maana kweli among all the people it was the right thing sana kunifanyia mimi, wazee wa sauti ya umeme, sasa ni zamu yangu kujibu, and I will.
Respect and Out!

FMEs!

Na hao wenye agena zao ni kina nani? Wataje tu ili wajulikane na hoja zitajibiwa kwa hoja.
 
Zitto alianza hii safari pale alipokubali kujiunga na kamati ya madini ya Kikwete (bila kujadiliana na viongozi wenzake ndani ya chama) na hivyo kuondoa momentum ambayo wapinzani walikuwa wameipata baada ya kuibua skandali ya Buzwagi.

Watu wengi walimpinga hapa na kumuomba abadili mawazo lakini yeye akawakatalia kata kata kwa kudai kuwa anajua anachokifanya. Matokeo yake yanajulikana - suala la Buzwagi na migodi ya madini liliishia kwa mkulu Sinclair na mafisadi wenzake.

Baada ya hapo - na baada ya kupata pesa kibao kwenye kamati na tume za Kikwete - Zitto alibadilika sana kimtizamo na kiutendaji. Haikunishangaza pale alipoanza kuunga mkono mafisadi kuhusu ununuzi wa Dowans.

Zitto wa leo sio yule ambayo wazee wa CHADEMA walimpa issue ya Buzwagi ili ajijenge kisiasa. Ukaribu wa Zitto na Kikwete ni mkubwa sana kiasi cha kufunika juhudi binafsi ndani ya chadema kama chama chenye mpango wa kuingoa serikali ya Kikwete.

Safari ya Zitto kujiunga na Kikwete ilianza pale alipokubali uteuzi kwenye kamati ya madini. Yaliyobaki ni historia.
Nishawahi kusema kuwa Zitto sasa alikuwa amejaa kiburi sana na pengine kujiona kuwa ni yeye ndio Pekee katika CHADEMA. Kuna watu wengi sana katika CHADEMA kuwa lakini sio Active katika Politics za Tanzania. Lakini Zitto alikuwa ana jaribu hata timing yake ilikuwa Mbovu sana. Nilikasilika sana kuona anasema na kumwaga mambo haya hapa JF. Zitto sasa alishapoteza Dira yake Siku nyingi sana
 
Mpendwa Zitto,

U
kiacha suala la Dowans, kujitoa kwenye kugombea nafasi ya uenyeketi CHADEMA - Taifa, kumeonyesha kukosa kwako principles. Huku kunapelekea wewe kuyumba na kupoteza sifa za uongozi bora.

Samahani, ni principles zipi unazoongelea hapa?

Kuhamia CCM kutakuwa jambo la mbolea kwani huko hakuna watu wenye principles na pia unaweza ukawa juu ama ukapotezwa kabisa katika ramani ya siasa za Tanzania.

Si kweli kuwa CCM hakuna watu wenye principles. Wapo ingawa ni kiduchu na wameelemewa na wanasiasa hovyohovyo na wakifanya siasa katika mfumo fisadi....

omarilyas
 
Eric...ina maana wajumbe wa Chadema ni wajinga?..au wana akili za Kushikiwa? kiasi ambacho wanashindwa kutofautisha Mchango wa Zitto na Mchango wa Mbowe ktk Chadema?...!!!

Kwa Jinsi mnavyomtetea Mbowe kiasi Hiki...kama hawezi kusimama na Zitto ktk Uchaguzi wa Ndani, Je anaweza simama na Mgombea wa CCM ktk Kuchukua Mamlaka Makubwa ya Nchi...?

Hii imekaa kama ya CCM jinsi baadhi ya wazee wanavyopinga watu kuchukua fomu kugombea Urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2010.
Je hao wanahisi Kikwete hawezi kusimama na mgombea mwingine ndani ya CCM na akapita?
Ni rekodi ya uongozi inamsuta au???

All in all, Zitto alichemka sana alipounga mkono ule mpango wa Serikali/Ngeleja wa kununua mtambo wa Richmond/Dowans huku akijua hiyo inakiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Zitto alijua kabisa kuwa suala hilo si la Kamati yake ya Hesabu za Mashirika ya Umma, bali ni la Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, chini ya Mwenyekiti Shelukindo, ambaye kwa ujasiri aliingilia kati na hivyo kuokoa pesa za walipa kodi yaliyotakiwa kuchotwa kwenye 'dili' hiyo.

Hii iliongezewa nguvu na ufafanuzi wa kanuni uliotolewa na Spika Sitta.

Ukichunguza media coverage, hivi sasa ni vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM, Serikali na viongozi wa CCM ndio vinamshabikia. Hii imekaaje?

Ila hilo la Dowans analo tu...

Zitto alitangaza kugombea na kisha akachomoa (sioni connection yoyote ya kukemea maovu ya Chadema).

Zitto alishauriwa na "wazee wa chadema" hasigombee. Ni dhahiri hakujitoa kwa matakwa yake. Huu ni ukiukaji wa democracy ndani ya chadema. Katika hotuba zake mara nyingi amekuwa akiguswa na kufukuzana kulikoshamiri ndani ya chadema na ufujaji wa fedha za Chadema.

Kabla ya hapo, Zitto alifanya yafuatayo-

1. Alijiunga na kamati ya madeni ya Kikwete (akipingana na wenzake)
2. Aliungana na mafisadi kwenye issue ya Dowans
3. Hakujulikana msimamo wake kwenye bajeti ya serikali iliyopita.

---Nini kazi ya upinzani kama si kushirikiana na chama tawala kuleta maendeleo? Zitto anakosa gani kujiunga na kamati ya JK?

---Kwani upinzani ni kupinga kila kitu? Huo msimamo wa bajeti, ni wabunge wangapi msimamo wao unajulikana hata ndani ya ccm?

Chadema kweli hamnazo; yani you are so concerned na kuropoka kwa Zitto hata kama yote aliyoyasema ni ukweli 100%. Lakini kuweni makini, mana ni vigumu sana kuuficha ukweli.
 
kati ya controversial ambazo hana budi kurethink the direction in political race ni hizo;

Naamini ulikuwa na maana ya Controversies

1.Dowans; ulitaka tununue tu mitambo wakati wanaharakati wote wakikataa, na kufikia kuongea lugha zisizo na nidhamu kwa mh. Mwakyembe-people discredit for that!

Ina maana wanaharakati ambao wengi wapo nje ya sekta wanapokataa ndio lazima wawe right? Na kama kiongozi anapewa mitizamo na wataalamu ambayo inaonyesha umuhimu wa kufanya uamuzi mgumu, aache kuufanya mradi kuna wanaharakati wanakataa? Hivi wanaharakati ndio kina nani haswa? Mnataka tuendelee kuwa na viongozi wanaopita kufanya maamuzi yanayowahakikishia umaarufu wao tu bila ya kuheshimu ushauri wa kitaalamu? No wonder tunazidi kujaza na kuabudu mediocres ambao huishia kutupiga longolongo na ofa za kahawa....

2.Chairmanship;nakuunga mkono kujitoa kwa sababu ulikuwa umejichimbia kaburi la kisiasa, too eary kwa sisi kukuamini kama unaweza kuongoza chama cha vijana na wazee. nimestudy the way unawatreaty wazee, nikaona, bado, huwezi. the way ulivyodili na mwakyembe, sitta na slaa hivi majuzi, bado

Too early manake nini? So CCM wanaposema its too eraly to have full fledge democracy wako sawa?

wayfoward; stop politicing youth wing, sababu your very senior to them in national issues, ikiwezekana achana na vyeo ndani ya chama, show that u r loyal even out of system. stop connection with untrusted networks. otherwise mwakani utakuwa mwisho wa siasa zako, wakati siasa zitapokuwa tamu zaidi-when smart, neat and intellectual politics will prevail.

Huu uzembe wa kufikiri huu. Ni vipi iwe makosa kufanya siasa katika political party youth wing. Yaani haya madhila ya mfumo fisadi yametuchanganya akili kabisa. Kanisa na miskiti inapokuja na ilani za uchaguzi tunawashangilia, wanasiasa wanapofanya siasa ndani ya asasi za vyama vyao tunawakaripia...Hivi ni mdudu gani anatusmbua kiasi hiki?

Yawezekana kukawa na ongezeko kubwa la smart politicians (wajanjawajanja) lakini hili la neat and intellectuals i berg to differ. unawezaje kupata neat politicians katika mazingira ya siasa za matumbo zilizogubikwa na patronage mentality chini ya mfumo fisadi?

Mnapokosoa mjaribu kuja na critique zilizosimama jamani....ili wote kwa pamoja tuelimike.....

omarilyas
 
Zitto alishauriwa na "wazee wa chadema" hasigombee. Ni dhahiri hakujitoa kwa matakwa yake. Huu ni ukiukaji wa democracy ndani ya chadema. Katika hotuba zake mara nyingi amekuwa akiguswa na kufukuzana kulikoshamiri ndani ya chadema na ufujaji wa fedha za Chadema.

Kama yeye mwenyewe amesema kuwa anakubaliana na ushauri wa wazee na kujitoa basi jamii itamchukulia Zitto na maneno yake. Hayo mengine ni ya kwako mwenyewe.

---Nini kazi ya upinzani kama si kushirikiana na chama tawala kuleta maendeleo? Zitto anakosa gani kujiunga na kamati ya JK?

---Kwani upinzani ni kupinga kila kitu? Huo msimamo wa bajeti, ni wabunge wangapi msimamo wao unajulikana hata ndani ya ccm?

Chadema kweli hamnazo; yani you are so concerned na kuropoka kwa Zitto hata kama yote aliyoyasema ni ukweli 100%. Lakini kuweni makini, mana ni vigumu sana kuuficha ukweli.

Ni kweli sio kazi ya upinzani kupinga kila kitu au kutoshirikiana na chama tawala kwenye maendeleo ya nchi.

Lakini kumbuka kuwa, kamati ya madini ni kitu tofauti. Kabla ya hii kamati ya Zitto, kulikuwa na kamati na tume kibao zimeundwa kuchunguza na kutoa ushauri kuhusu masuala ya madini. Kabla hayo mapendekezo ya kamati na tume zilizopita hayajafanyiwa kazi, kamati nyingine ikiundwa ni upotevu na uharibifu wa muda na pesa za watanzania.

Zitto alilijua hili, aliambiwa na wenzake kuhusu hili lakini bado tu alijiunga na Kikwete kuwapotezea muda na pesa watanzania. Je ile kamati ya Zitto imeleta nini tofauti na kile kilicholetwa kabla?

Je issue ya Buzwagi ambayo ndiyo ilianzisha yote haya ilishughulikiwa? Kuna wakati chama kilicho madarakani.

BTW ... kuita watu kuwa hamnazo hakujengi hoja yako zaidi ya kukuonesha vile ulivyo. Mtu mwenye chuki za ajabu (ohh nimekumbuka, kuwa ulipondea wachaga somewhere hapo juu) za kikabila.
 
Zitto alijua kabisa kuwa suala hilo si la Kamati yake ya Hesabu za Mashirika ya Umma, bali ni la Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, chini ya Mwenyekiti Shelukindo, ambaye kwa ujasiri aliingilia kati na hivyo kuokoa pesa za walipa kodi yaliyotakiwa kuchotwa kwenye 'dili' hiyo.Hii iliongezewa nguvu na ufafanuzi wa kanuni uliotolewa na Spika Sitta.

Suala lolote la kibajeti la mashirika ya umma linaangukia katika kamati ya Zitto. Kina Shelukindo na Sitta waliingilia kuendeleza vita yao dhidi ya MTANDANO MASLAHI ambao waliamini ripoti ya Richmond ingewamaliza lakini wakajikuta makosa yao ya kuficha uchi wa chama chao kama alivyosema baadae Mwakyembe, yamefanya the whole RICHMOND saga kuwa another CCM survival spin ambao daima hukosa nia ya dhati ya kushughulikia wakosaji...

Ukichunguza media coverage, hivi sasa ni vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM, Serikali na viongozi wa CCM ndio vinamshabikia. Hii imekaaje?

Same question iende kwenye fact kuwa ukichnguza media coverage, hivi sasa ni vyombo vinavyomilikiwa na watu wa kutoka kabila na dini moja ya mshindani wa Zitto katika kinyang'anyiro ndani ya CHADEMA ndio vinavyoendesha political assasination process dhidi ya Zitto..IMEKAAJE?

U need to get closer to the game to understand it then utaepuka kujiuliza maswali rahisi kama hili unalo uliza....kuna mengi zaidi ya CCM, serikali, ukabila na udini...

omarilyas
 
Zitto alishauriwa na "wazee wa chadema" hasigombee. Ni dhahiri hakujitoa kwa matakwa yake. Huu ni ukiukaji wa democracy ndani ya chadema. Katika hotuba zake mara nyingi amekuwa akiguswa na kufukuzana kulikoshamiri ndani ya chadema na ufujaji wa fedha za Chadema.

---Nini kazi ya upinzani kama si kushirikiana na chama tawala kuleta maendeleo? Zitto anakosa gani kujiunga na kamati ya JK?

---Kwani upinzani ni kupinga kila kitu? Huo msimamo wa bajeti, ni wabunge wangapi msimamo wao unajulikana hata ndani ya ccm?

Chadema kweli hamnazo; yani you are so concerned na kuropoka kwa Zitto hata kama yote aliyoyasema ni ukweli 100%. Lakini kuweni makini, mana ni vigumu sana kuuficha ukweli.

Mkuu kuhusu Zitto kuingia kamati ya madini kuna kasoro moja kubwa sana. Zitto anawakilisha sera za Chadema ambazo zinahitaji nci yetu kuwa na hisa katika amshirika ya madini. Sasa ikiwa serikali yetu haina hisa ndani ya mashirika hayo, hakuna sera wala kifungu cha mtazamo wa chama chake (Chadema) umekubalika na serikali kuu kutumiwa ili kuboresha sekta ya madini. Zitto hakutakiwa kufanya kazi huko kwa sababu ni Kinyume cha katiba ya chama chake.
Siku zote wabunge wanashirikiana na serikali kuu ikiwa tu serikali kuu itakubali kubadilisha baadhi na sera zake na kufuata mkondo wa kati kaisi kwamba hata Wapinzani wanakuwa na mchango wa sera zao.. Lakini sii mtu kuingia kamati ambayo malengo yake ni kinyume kabisa chga mtazamo wa chama chako..
Anyway haya yalikwisha pita.. Zitto alichemsha, akachemsha na anaendelea kuchemsha kutokana na tatizo kubwa na siasa nchini. Yaani vyama vyote vya siasa havina mrengo, Zitto ni Conservative na anahusudu mrengo huo wakati Bongo kila mtu ana dini yake lakini unaambiwa nchi haina dini..hivyo hivyo principal hiyo ipo ktk Mrengo..
Hivyo itakuwa shida sana kwa wananchi kumwelewa Zitto na msimamo wake..Hii haina maana hafanyi makosa.
 
Last edited:
Same question iende kwenye fact kuwa ukichnguza media coverage, hivi sasa ni vyombo vinavyomilikiwa na watu wa kutoka kabila na dini moja ya mshindani wa Zitto katika kinyang'anyiro ndani ya CHADEMA ndio vinavyoendesha political assasination process dhidi ya Zitto..IMEKAAJE?

U need to get closer to the game to understand it then utaepuka kujiuliza maswali rahisi kama hili unalo uliza....kuna mengi zaidi ya CCM, serikali, ukabila na udini...

omarilyas

Omar,

Nilikuuliza jana kama unamsemea Zitto au unasema kwa niaba yako. Zitto alidai kuwa anaandamwa na wamachame (na wachaga?) lakini baadaye akaonekana kuback down.

Naona wewe leo umekuja full ... kudai kuwa Zitto anaandamwa na watu wa dini na kabila tofauti na Zitto.

Unaamini kuwa wanaompinga Zitto hapa na kwingine wanafanya kwa vile wao sio kabila au dini moja na Zitto! are you serious?
 
Back
Top Bottom