Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

....kuna juhudi ya dhati ya kubagua section ya watanzania..huu ni ubaguzi...wewe fikiria imefikia mahali watu wanaoogopa vivuli ..viongozi wakubwa kabisa wamefikia mahali ..wanapita baadhi ya maeneo hasa ya pwani wakiwahuburia wazee wao wasiwauzie watanzania wenzao ardhi au tuseme kuzuia kuwakaribisha....kinyume cha katiba ya nchi waliyoapa kuilinda inayosema kuwa watanzania wana freedom of movement....chuki hii inaazia juu....hawa ni wafuasi tu kwa kile kilichojificha kwa wanaowatuma...kwa kujuwa au kutojuwa!!

Haya yote nimeyasikia na ndio maana mimi huwapiga nondo kali sana wale wote wenye chuki za kidini na kikabila hapa jamvini. Kuna sehemu hapo pwani huwezi kununua kiwanja kama wewe ni mkiristo au kabila fulani.

Watu inabidi sasa wanatumia wakazi wa Pwani kuwanunulia viwanja maana wao pekee hawawezi kupewa (kutokana na maagizo ya kijinga toka kwa watu wasioitakia mema Tanzania).

Kazi kweli kweli
 
U need to find a hoby badala ya kuwa mropokaji kiasi hiki!

Eric baba, hayo mawazo yako wala usifikiri kila mtu anawaza kama wewe!

Kwangu mimi Zito mpiganaji na kiongozi mzuri, andika weeeeeeeee jaza hata thread zote kwangu mimi ni hivyo hiyo haitabadilika; sijamjua leo wala jana!

Pili, weka dhamana au insuarance kuwa wengine woote wapiganaji hawawezi kuhudhiwa na kubadilika; ama sivyo kutakuwa hakuna mpiganaji !

swala la kuwa huyu jamaa atakufa kisiasa pia ni theory is not practical, na wote wanaosema hivyo ni kujaribu kutabiri kama akina Yahaya!

Tukiwa wakali kuwalinda wale wapiganaji wetu tutawaokoa wengi, tukiwa waandika nakala kama wewe tutaua wengi mwishowe utabaki wewe peke yako maana wooote watachukuliwa na upepo.

Uwazi wa Zito ni mzuri ndugu , ni picha tunapata kuwa ni jinsi gani vyama vinavyojiita mbadala vinaishi, Zito angekuwa wa kujikomba angekaa kimya!

KWA NAKALA YAKO UNAPROVE PIA KUWA ZITO YUKO JUU SANA ZAIDI YA CHADEMA, CCM huwa hawafanyi ujinga huu, angekuwa mdogo; why all this unconvicing articles!

Mwambie Mtei na Chadema wote kuwa habari zenu tumezipata na mnavyoishi humo, hamna tofauti na CUF, NCCR, TLP.

Shida ilikuwa nini si angeachwa ashindwe kwenye kibox cha kura, wewe hili hufikirii??

swali la kumalizia, tunawalindaje hawa wapiganaji?? maana juzi tu ulikuwa unampenda Zito , leo humtaki, kesho utamkacha Slaa, maana tuhuma zipo tu, na tusivyopenda vithibitisho!

why are we not believing in them, when then we will belive them as true dream leaders??

Mtu gani mkweli atakayeingia kwenye siasa na kuishi namna hii??

ETI KULINDA CHAMA THIS IS POPPYCOCK !!!, AKILINDE KISHA WAJE KUCHUKUA NCHI, SI KAMA YA KENYA YA KUMUONDOA MOI, THEN WAO HAWATAKI KUTOKA, THUBUTU !!! better this what is CHADEMA ANYWAY , mjinga sana wewe!!

Upumbavu huu anaouvumbua Zitto badala ya kufurahia ndio mnasema kulinda chama, TOFAUTI YA HII NA CCM ni nini then

Kwa wataka mabadiliko tusio na makundi this was good movies, kuona kumbe hakuna cha CHADEMA wala CCM, wala CUF , TLP, NCCR, we are long way to true revolution, lets think another way!

ETI KULINDA CHAMA!!! huu ujinga hausameheki, NDIO MNAISHI NA WANAWAKE WAZINZI ETI KULINDA NDOA!

mchaga nini wewe!!!!!!!!!!
 
Just delete that "mchagga thing" inatugawa na haina mantiki katika undugu wetu wa kitaifa!!

What if is true?? jamani kunya anye CCM akinya CHADEMA karanga? wote tunapige kelele ili kusiwa na ukabila, kama Zito angeruhusiwa huoni kuwa wangeondoa hilo wingu maana lipo na lilikuwepo! kama CHADEMA tunakiamini kwa nini tusikionye leo?
 
Haya yote nimeyasikia na ndio maana mimi huwapiga nondo kali sana wale wote wenye chuki za kidini na kikabila hapa jamvini. Kuna sehemu hapo pwani huwezi kununua kiwanja kama wewe ni mkiristo au kabila fulani.

Watu inabidi sasa wanatumia wakazi wa Pwani kuwanunulia viwanja maana wao pekee hawawezi kupewa (kutokana na maagizo ya kijinga toka kwa watu wasioitakia mema Tanzania).

Kazi kweli kweli


..mkubwa wao alitoa maagizo juzi akiwa lindi akizindua barabara inayolipiwa mkopo wake kwa kodi zetu wote ...aliwaambia """ sasa barabara hiyo msimuuzie mtu yeyeto ardhi..."....nikajiuliza kama ni barabara imeanza kujengwa tangu enzi ya nyerere,mwinyi,mkapa,na sasa wanaendelea ...sikupata kumsikia mkapa mfano pamoja na kutokea huko pwani ya mtwara na kujenga sehemu kubwa ya barabara akiwaagiza wakazi wasikaribishe watanzania wenzao....ujinga kabisa..kukaribisha wasomali sawa ..lakini watanzania wenzenu tatizo....

juzi waziri mmoja akiwa bagamoyo ...akawaambia kuwa wanapeleka pale bandari ;;;na EPZ na akawataka watu pale wasimkaribishe mtu kufaidi hayo matunda.....kwa kuuza ardhi...,sasa tunaenda wapi????...hiyo EPZ na BANDARI si inajengwa kwa kodi za wote...kwa nini wazuie watanzania wenye nia ya kutega uchumi pale wasichukue fursa kwa usawa....???.... afteral bandari hiyo na epz hazikuwa na sababu badala yake wangejenga EPZ mtwara au tanga...waunganishe na uganda kwa tanga na malawi na zambia kwa mtwara...hakuna sababu ya kujenga bandari mpya bagamoyo just 30km away the dar es salaam port....
 

Mara nyingine hutokea mtoto akawa maarufu kuliko baba aliyemzaa ..... sishangai hali hiyo ikitokea kwa Zitto na Chadema!!
Ni mtazamo tu
 
Kunya, kulawiti, ujinga, upumbavu etc halafdu Zitto akijibu anatoa siri!
 
Utetezi kuwa yeye ni binadamu ana nyama na kuwa anaudhika kama binadamu ni upumbavu. Ni sawa na mlevi anaebaka kwa kisingizo cha msukumo wa pombe, kwanini hakuna msukumo wa mlevi mwanaume kulazimisha kulatiwa? Kwa nini bado kuna uangalifu wa kuchagua vitendo

Eric,

Acha kupayuka ovyo, Zitto kakosa uhalai wa kuwa kiongozi kwa mujibu wa kifungu gani cha katiba yenu? acha blah blah umemwaga pumba tupu, kajipange uje upya au mwambieni baba mkwe amvue uanachama kabisa.

Philemon,

Eric Ongara mwanachadema (sijui ana cheo gani huko ) amekuja na shutuma na kumwaga matusi ya nguoni kwa Zitto. Huu ni muendelezo wa mashambulizi ya viongozi wa kada mbalimbali wa Chadema kwa Zitto.

Katika hali kama hii Zitto akijibu anaambiwa anavujisha siri! kakosa uhalali wa uongzozi nk.

Doule standards!
 
Shida Salum, maarufu kama First Lady ameshukia Dr Slaa na kumtuhumu kwamba amemuita mwanae kuwa ni fisadi. Shida Salum ambaye ni mama mzazi wa Zitto Kabwe aliyesama hayo katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA(BAWACHA).

Akifungua mkutano huo, Dr Slaa alisema kwamba wanawake wa CHADEMA wawe mstari wa mbele katika kupiga vita ufisadi na kuhakikisha kwamba mafisadi hawasambaratishi CHADEMA.

Dr Slaa akatoa mfano wa jinsi ambavyo mafisadi walitaka kuichafua CHADEMA wakati wa kifo cha Wangwe na kufikia hatua ya kupika habari kwamba Mbowe alifukuzwa na mapanga Tarime.

Dr Slaa alisema kuwa huo ni mkakati wao kwa kuwa hata wakati wa hoja ya BOT walifikia hatua hata ya kuutumia usalama wa taifa kutimiza azma hiyo kwa kunukuu barua yao ya kuzuia hoja hiyo.

Dr Slaa alisema kuwa CHADEMA ndio mbadala wa CCM hivyo inatazamwa kwa matumaini na watanzania wote na kuwataka wanawake wawe mstari wa mbele kulea chama.

Mara baada ya Hotuba hiyo, Mama Shida ambaye alikuwa ni mgeni waalikwa kwenye ufunguzi wa mkutano huo kama Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Ulemavu(CHAWATA) alinyoosha kidole kusema neno.

Moja kwa moja akamlaumu Dr Slaa kwa kumuita mwanae kuwa ni fisadi. Akamtaka afahamu kuwa makao makuu ya chama hicho yamejaa uchafu.

Hata hivyo, Dr Slaa ambaye katika hotuba yake hiyo hakusema popote kuwa Zitto ni fisadi alimshukuru Mama Zitto kwa swali lake, na kumweleza kuwa kama ofisi ya katibu Mkuu inauchafu basi ni jukumu la yeye na Naibu Wake ambae ni mwanae Zitto Kabwe kuundoa ama kuwajibika.


..........ndiyohiyo
 
Asante, kaka wewe nawe umetoa hoja! hobby(sio hoby) yangu ni kuropoka!

Ni lugha yangu ya tatu hiyo ila nashukuru kwamba nimeeleweka na ujumbe umefika. Tujaribu o gea mambo ya msingi badala ya kukazana kuvamia watu wa nasaba fulani waliotoka maeneo flani. Pia tujaribu kuelewa ni nini kinajadiliwa kabla ya kukurupuka na kuanza kumvamia mwandishi badala ya kujibu hoja kwa kujenga hoja... Ukitaka mpanda Eric personally mfuate PM kama ambavyo umenifata mimi..!
 
Ni lugha yangu ya tatu hiyo ila nashukuru kwamba nimeeleweka na ujumbe umefika. Tujaribu o gea mambo ya msingi badala ya kukazana kuvamia watu wa nasaba fulani waliotoka maeneo flani. Pia tujaribu kuelewa ni nini kinajadiliwa kabla ya kukurupuka na kuanza kumvamia mwandishi badala ya kujibu hoja kwa kujenga hoja... Ukitaka mpanda Eric personally mfuate PM kama ambavyo umenifata mimi..!


Kumbe ulivyoandika muda ule, ulijenga hoja kwa kusema unaropoka? au unaona kuna mtu anatishika na lugha hizo humu? wengine tushatukanwa sana tu, sasa ukitokea wewe unaadika unaropoka haugusi kitu.

Ebu angalia post yako hii ya pili ilivyojaa utu na hekima, jribu kufikiri kama ingekuwa ndiyo umendika muda ule!

wengine wanavyofanya wanaread btn lines na kukosoa na kujenga hoja kila mstari, ukichukua post ya mtu nzima na kusema unaropoka, huwi tofauti na huyo aliyeropoka, tena inakuwa aibu mtu wa heshima kama wewe kumwambia kichaa kama mimi unaropoka, maana kuropoka inaweza ndio ikawa mimi na kila mtu ananijua kwa hivyo!

Ebu tauche hayo naona umekuja kikubwa inaweza ukawa hukunielewa, lakini nimemjibu kwa mawazo yangu, si unajua JF, we dare talk openly! kuna watu tuna matatizo ya ubongo na maisha , ninapofanya kosa jaribu kunielekeza kama ulivyofanya hapa! mkuu ndio maana linaitwa jamvi

Thank though, you are good man to me!
 
Zitto alianza hii safari pale alipokubali kujiunga na kamati ya madini ya Kikwete (bila kujadiliana na viongozi wenzake ndani ya chama) na hivyo kuondoa momentum ambayo wapinzani walikuwa wameipata baada ya kuibua skandali ya Buzwagi.

Watu wengi walimpinga hapa na kumuomba abadili mawazo lakini yeye akawakatalia kata kata kwa kudai kuwa anajua anachokifanya. Matokeo yake yanajulikana - suala la Buzwagi na migodi ya madini liliishia kwa mkulu Sinclair na mafisadi wenzake.

Baada ya hapo - na baada ya kupata pesa kibao kwenye kamati na tume za Kikwete - Zitto alibadilika sana kimtizamo na kiutendaji. Haikunishangaza pale alipoanza kuunga mkono mafisadi kuhusu ununuzi wa Dowans.

Zitto wa leo sio yule ambayo wazee wa CHADEMA walimpa issue ya Buzwagi ili ajijenge kisiasa. Ukaribu wa Zitto na Kikwete ni mkubwa sana kiasi cha kufunika juhudi binafsi ndani ya chadema kama chama chenye mpango wa kuingoa serikali ya Kikwete.

Safari ya Zitto kujiunga na Kikwete ilianza pale alipokubali uteuzi kwenye kamati ya madini. Yaliyobaki ni historia./QUOTE]

Kimsingi Zitto, ni kijana aliyetufaa na anaeendelea kutufaa katika siasa za Bongo kwa nafasi aliyonayo. Binafsi, mwenendo na baadhi ya hoja zake zimekuwa sometimes zikinitatanisha kiasi cha kutamani kujua historia yake hasa akiwa UDSM kwani alikuwa pia akishiriki siasa za wanafunzi. Nimebahatika kuongea na watu takribani 12 waliokua nae UDSM including room mates. Ningependa kuwashauri wadadisi wengine wafanye upembuzi zaidi juu ya hili, lakini ninachoweza kusema Nafasi ya Uwenyekiti wa CHADEMA ni kubwa kwa Zitto na haingekuwa na maslai kwa CHADEMA. Kama alishauriwa ajitoe katika kinyang'anyiro cha uwenyekiti basi nadhani lilikuwa ni wazo zuri tu.
 
We can not under estimate nguvu ya mafisadi. Naamini maneno ya Mzee Mtei kuwa mafisadi wamepenyeza rupia Chadema. Kuna uwezekano kuwa haya tunayoyaona ni matokeo ya operesheni hiyo. Kama Chadema wakionesha maturity kwenye ku-deal na hili litakuwa jambo la maana na itaweka mazingira mazuri ya chama kujijenga. Lakini kama kesho wakifanya fyongo watawapa CCM a big greenlight.

Uzuri wa CCM ni chama ambacho popularity yake haijajengeka kwa individual personalities, imejengeka kwenye collective personality ya chama. Hata JK akiondoka leo bado CCM ni CCM tu, lakini inatia shaka kiasi kwa upande wa upinzani na CHADEMA as well. Inatia shaka zaidi kwa kitendo alichokionesha Zitto na kimezusha maswali Mengi kama kweli Zitto Kabwe. Is this Zitto Kabwe we know, the one we call him a hero, a camouflaged Zitto?? Is Zitto Kabwe we have seen in the past two weeks, a selfish one, the one who needed elders to tell him that personal rift will cause cancer in the party, a real Zitto ?? sijui kama ni kweli tatizo ni ugomvi binafsi kati yake na Mnyika na Mrema, au na yeye amelambishwa asali chafu na kusahau umuhimu wake kwa Tanzania hasa kwenye kipindi hiki tunapoendelea 2010. Who knows, ni yeye mwenyewe anayejua ukweli.

Lakini kusikia ushauri wa wazee ni credit kwa Zitto, na wazee kuplay role ndani ya Chadema ni credit pia na ni utamaduni wetu watanzania, na inaonesha kuwa kuna effective internal mechanism inayoweza kufanya kazi ya kukilinda chama. Kwa hiyo the whole thing ni kuwa imeonesha wekaness na strength ya Chadema. Lakini blow aliyotoa Zitto kwa Chadema ni kubwa na itakuwa na madhara makubwa sana kwa Chama 2010.
Zitto naona upo online hapa, do not take it personal. Najua umewafurahisha baadhi na umetusikikisha baadhi pia.
 
Lazima tukumbuke haki huambatana na wajibu.

Kaka kwa umri wako kukumbatia theory za kuhalalisha ugandamizaji kam huu unatutisha sana endapo utapewa uheshimiwa wenye makali ya dola

Jaribio lolote la kulazimisha wanachama wachague kati ya mtuhuru,Zitto au slaa ni fikra muhali za kihuni ambazo zinaweza kukijeruhi chama.

Unataka kusema kuwa wanaCHADEMA hawana uwezo wa kuchagua viongozi wao?



CHADEMA ina wafuasi wengi lakini ni wachache waliojitokeza mbele katika siasa za moja kwa moja.Hivyo CHADEMA inahitaji majabali haya machache kuendelea kuwemo katika safu moja ili kukiandaa chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu.Tayari kulikuwa na wazo la kutumia "utatu mtakatifu" yaani Mtuhuru,Slaa na Zitto katika kuipasua na kiitesa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwakani na hatiame kukiandaa vyema chama na mwaka wa “mavuno” mwaka 2015.

Kaka hata mimi naomba utokee muujiza hili lifanikiwe. Lakini swali kwa unavyomjua MTUHURU wako unadhani anaaminika hata kumpendekeza Zitto kuwa Katibu wake? Na kama kulikuwa na mpango huo iweje Slaa aache kuchukua fomu za kugombe umakamo?

Zitto alikuwa ana wajibu wa kutafakari namna ambavyo "haki" yake ya kugombea ingesababisha mnyukano ambao ungeibua athari za muda mrefu kwa chama na wagombea. Hatuwezi kuhujumu demokrasia ndogo kwenda kuathiri demokrasia Pana.Hatuwezi kutetea udhofishaji wa CHADEMA Kwa kiisngizio cha demokrasia na kwa wakati huo tukiua demokrasia pana yani ushindani wa CCM na CHADEMA.

Kwa hiyo kwako wewe unaona ni sawa kabisa kuacha CHADEMA iliyojaa wasiokuwa tayari kupractice demokrasi kuwaongoza watanzania kufanikisha demokrasia pana. Unataka kusema wale mafisadi wa kenya walivyowalaghai wakenya na dudu lao waliloliita NARC na kuja na madudu kama ANGLO LEASING Scandals ndio mfano wa kuigwa kwa watanzania?

Kugombea kwa Zitto kungefaidisha zaidi CCM zaidi ambavyo ingefaidisha CHADEMA. Kama CCM wangeombwa ushauri basi wangesisitiza Mtuhuru na Zitto washindane. Hivyo uamuzi wa awali wa Zitto kugombea ulikuwa tayari una manufaa kwa wapinzani wa CHADEMA Hususani CCM.

Kama sio kujua kuwa mmoja wao angekosa ustaarabu wa kutumia siasa safi kufanya kampeni zake, uoga wa kutowashindanisha unatokea wapi. Yaani mnataka kusema yale mawazo ya wahafidhina wa CCM kuwa kumshindanisha JK na mtu mwengine kutavunja chama yana maniki. Ilikuwaje mkaanza kuwabeza wale kina mama na wazee wa watu walipoandamana kuwatisha wanaCCM wengine wenye nia ya kushindana na JK 2010? Au kwa sababu huyu ni mswahili Jakaya ni sawa lakini sio "mstaarabu" FREEMAN AIKAELI?

Inalekea kulikuwa na makundi ya muda mrefu ambayo Zitto anayafahamu kwa mujibu wa maandiko yake hapa, na pengine ndio msukumo wake kugombea. Kama ndivyo,Zitto amepwaya kiungozi kwa kuamua kugombea kwa msukumo wa kukuza na kumaliza kundi jingine.Umbea, majungu na husda haviwezi kamwe kufaulu kama kichocheo cha kuwa mwenyekiti wa chama kitaifa.

Makundi hayakuanza na Zitto ila yameanza na utamaduni wa kufukuzafukuza kila anayetofautiana na maslahi ya wachache yanayopewa jina la maslahi ya chama. Na usimsingizie Zitto kuwa aligombea kukuza ama kumaliza kundi jingine. Kama kitu alichokuwa anasisitiza kuwa kinatia umuhimu wa yeye kugombea ni kusamehe wale wote walionewa kwa kufukuzwa ama kusimamishwa uanachama mara baada ya kuonyesha tofauti zao na mwenyekiti wao. Na hili amelisema hata alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari. Sasa hii ya kumaliza kundi jingine yametka wapi. Usitie shaka Zitto hana roho ya korosho na wala utamaduni wa kuweka vinyongo na pia best wako Mnyika kamwe hawezi kugeuka adui wa Zitto kwani wametoka mbali. Kidudu mtu ambaye anapaswa kunyamzishwa ni mwengine ambaye sidhani kama ana umuhimu sana kwako.

Zitto anaelewa kanuni, mazoea na taratibu za uendeshaji wa chaguzi zake za ndani. Kama alikuwa na nia njema alipaswa kuwa ameepika michakato hii ili isije ikadhuru nia yake ya kugombea na pengine kuwa na athari hasi kwa taathira ya chama kwa ujumla wake. Uzembe wake katika kutathmini hili ni hujuma za wazi dhidi ya haki yake kama mgombea na ustawi wa chama kwa ujumla wake. Ushauri uliotolewa na kamati ya wazee wa chama ni jambo ambalo Zitto alipaswa kuling’amua hata kabla.Pengine lengo lilikuwa kukivua nguoa chama au kuwashwa na msisimko wa ndani.

Dogo umefikia lini umri wa Wazee wa Chama unakuja na mawazo mgando kama haya. Yaani U-CCM umewaathiri namna hii. Kama ninyi mliokulia katika enzo za siasa za ushindani mnafikiria hivi iweje leo muwashangae MAGOGO yaliyofubaa ya CCM?

Ipo changamoto ya chama ya kuwa na utegemezi usio wa kwaida kwa mtuhuru, slaa na Zitto kutokana na mitaji yao mikubwa ya kisiasa. CHADEMA inao watu wengi wenye weledi wanaoweza kutoa mchango mkubwa katika medani ya siasa, hivyo kunapaswa kuwa na mkakati kambambe wa kuzalisha na kutambulisha kwa umma wanasiasa wengi zaidi.”Utatu mtakatifu “uliapaswa kuwa nyenzo ya kutengeneza mabingwa wapya. Zitto kwa uzembe au kiburi aliamua kupuuza hali halisi ya chama na kuamua liwalo na liwe! Suluhisho lake la mvutano wa ndani lilikuwa ni kusambaratisha wapinzani wake wa ndani na pengine kukisambaratisha kabisa chama kwa ujumla wake.

Aliyechukua fomu na kujaza kuomba ridhaa ya wanachama wake kuwa kiongozi wao na waliotumia bisara zisizo na hakima kumshinikiza ajitoe kwa kuogopa athari za siasa chafu za KIJANA wao na baadae wafuasi wake kuendeleza kumwaga sumu dhidi ya mwenzao, ni yupi ambaye anataka kukisambaratisha CHAMA?


Maandiko ya Zitto kama majibu ya Tuhuma dhidi zake JF
kwanini hakuna msukumo wa mlevi mwanaume kulazimisha kulatiwa?

Ina maana huyajui haya kama yanatendeka?

Ikiwa wabaya wake ni John Mrema na John Mnyika, kwanini ameamua kugombana na chama kizima? Uchaguzi wake makini wa maeneo ya kugusa katika majibu yake ni kielelezo cha mpangalio uliojaa uovu, fikra duni na nia mbaya, mathalan maelezo yanayoibua hisia kama suala la marehemu wangwe ni kielelezo halisi kuwa Zitto ana nia mbaya na CHADEMA. Huwezi kujisaidia katika kisima ambacho unatumia kwa maji ya kunywa na kupikia kisa umekasirishwa na mwanakijiji mmoja.

Ni wapi Zittoa amesema hawa ni wabaya wake. Na kama wakati Zitto anakubali ushauri wa wazee wao wanaingia mitandaoni na kwa waandishi wa magazeti kuendeleza propaganda zao kama walizotumi kumfrustrate Kaborou na Chacha Wangwe ulitaka Zitto awanyamazie. Ili iweje? Watu wazoee uzandiki wao hadi waamini?

Ikiwa ni kweli Mrema na Mnyika wamemtuhumu Zitto ni kwa nini kama kama kiongozi ameshindwa kutumia miundo ya chama kutataua? Na mbona amekishambulia chama kwa ujumla wake? Amekihusisha chama na uchaga( ni sawa na kuthibitisha propaganda za CCM au kuunga Mkono msimamo,mkakati na mtazamo wa CCM dhidi ya CHADEMA), maauji na matumizi mabaya ya fedha. Hizi sio tuhuma za kwa watu binafsi! Inaelekea anaowalenga wana mapenzi makubwa kwa chama zaidi yake, hivyo kete yake yeye ni kwa kuumiza kile kinachopendwa na hao maadui zake wa “kubuni”.

Unataka kuniambia kuwa Zitto angeenda kukimbilia kwa hao wazee ambao nao wanakuja kudai kuwa Zitto ana tuhuma za kuhonga vijana kwa ushahidi wa sms na vijikaratasi? Sijui kuhusu mauaji lakini unataka kusema CHADEMA hakuna tuhuma za matumizi mabaya? Hayo ya uchaga ni nani kama sio wenyewe wanayoyatengenezea mazingira ya kuyahalalisha. Tatizo hizi natural born arrigances zinawafanya muwe reckless kiasi cha kufanya yaleyale ambayo maadui zenu wangependa muyafanye ili muwathibitishie mapungufu yanu.

Hivi iweje mtu anayetumia fedha za chama vibaya, akatumia ukabila katika kufanikisha malengo yake akawa na mapenzi na chama chake na yule ambaye anamwambia kuwa acha kutumia ukabila ndiye akawa hana mapenzi nacho. Kwani haya yameanza kusemwa lini? jee kuna suluhu iliyofanyika kichama? Na imekuwaje kuwa hata alliances za utetezi wa MBOWE na mashambulizi dhidi ya Zitto zikawa na picha ya udini? sitaki nije kwa undani wake hapa lakini kama unahitaji nishtue nitakushukie the whole chain...

Ni kama anatuambia yeye haipendi CHADEMA kihivyo! wakiendelea kumgusa ataua chama! Huu ni ubakaji wa chama na kuibua hofu za kibazazi. Ni kama anawaambia wanaCHADEMA wasimuuzi lasivyo atanyea kisima?! Hatuwezi kuendesha chama kwa hofu na kuwaza ni lini Zitto atakunya katika kisima. Kuna maswala mengi ya kuwaza katika mustakabali wa nchi zaidi ya kunya kwa Zitto.
Kwa makusudi Zitto ameamua kupotosha suala la BAVICHA. Ushindi wa kafulila anauzungumzia anaujaje?. Nilibahatika kushuhudia uchagauzi ule, matokeo hayakutangazwa kutokana na idadi za kura kuzidi idadi ya wapiga kura. Hali ilivyoanza kuwa tete Zitto alitoa kauli tata kuwa vijana leo watatupiana ngumi na kutokomea, yeye kama kiongozi wa kitaifa anaamua kukimbia hali ile ulikuwa ni udhaifu mwingine mkubwa wa kiungozi wa Zitto.

Ulitaka abaki ili mtimize mpango wenu wa kumchoma visu?
Msiamazi baada ya kutangaza hali halisi ya zoezi la kura, aliwaapa wajumbe nafasi ya kutoa maoni yao ambao wengi walimtuhumu moja kwa moja Zitto pasipo kutafuna maneno kuwa alishiriki kuhujumu uchaguzi ule.

Tangu lini kumpigia kampeni mtu kukageuka kuwa kuhujumu uchaguzi?

hatukumsikia hata wakala wa kafulila akilalamikia kudhulumiwa. Ni aibu kwa Zitto kufanya jitihada za kuhalalisha uhuni ule. Ikiwa alibainie jitihada za hujuma dhidi ya Kafulila ni kwanini hakuziwasilisha katika kikao cha jumapili cha kamati kuu?

Tangu lini aliyeshinda uchaguzi akalalamika kuwa kadhulumiwa? angewasilishaje taarifa wakati wenye chama wameshinikiza hata majibu yasitolewe.


Kuhoji kamati ya wazee chini ya Mtei kuendelea kusimamia uchaguzi zinaozendelea wakati tayari baraza la wazee limechagua viongozi wake ni kielelezo cha kukosa uwajibikaji wa pamoja.

Yaani sasa mnataka hata watu wasihoji makosa ya kikatiba? Kazi kwelikweli.

Baada ya kikao cha kamati kuu jumapili iliyopita umma ulielezwa kuwa tofauti kati ya Zitto na Mtuhuru zimefutwa. Sasa hapa Zitto anaposema siku wakipatana na Mtuhuru wapambe nuksi watakoma anataka kusema nini? Kwamba walituzuga? Walifanya unafiki?

Kama msingeendelea na propaganda zenu dhidi yake ni wazi mambo yangekuwa shwari sasa. Kosa ni lenu mliochukulia uamuzi wake wa kujitoa kama weakness na mkaendeleza mpango wenu wa kummaliza kisiasa...Na msipoangalia mtaadhirika maana FREEMAN na ZITTO walijuana siku nyingi na wamefanya mengi pamoja.....wakati ninyi mnaendela na ujinga wenu huku wenzenu wanaangalia jinsi gani ya kufanya kazi pamoja huko mbele kuendeleza libeneke (ofcourse kama mmoja wao hajaendeleza chuki zake)


Jitihada za Kuiua CHADEMA ni jambo lisilovumilika kwa hali yoyote ile.Ni ushenzi na laana iliyo kuu. Naami hili ni jaribio la mwisho la CHADEMA kudhihirisha ukomavu wake wa kisiasa na kuwarejeshea matumaini watanzania. Upuuzi na udhaifu wa Zitto unaweza kusahihishwa

Wenye jitihada ya kuiua CHADEMA ni wale walio tayari kufanya lolote ili mradi kulinda vyeo vyao na maslahi yao hadi kuwafanya wazee kutumia busara isiyo na hekima kumshawishi Zitto kujitoa......

omarilyas
 
Dude appears arrogant, self-righteous, ego-tripping and not least has a tendency to draw (and relish in) attention to himself.

I bet in the back of his conceited mind he believes himself to be some kind of charismatic, young, uniquely ambitious, next generation political animal in the local political scene.

All the hype he receives on a daily basis in the tabloids as some sort of an up-and-coming political stalwart and stud (among the usually grey-haired CCM geezers and rest of the aging, tired-looking and boring political talking-heads) no doubt contributes to his big-headedness (or inflated sense of self-importance if you will)

But one thing I know for sure (and you can all agree with me - more or less), ni kwamba jamaa ana sura mbaya kama kiatu cha Baniani! Damn!
 
Dude appears arrogant, self-righteous, ego-tripping and not least has a tendency to draw (and relish in) attention to himself.

I bet in the back of his conceited mind he believes himself to be some kind of charismatic, young, uniquely ambitious, next generation political animal in the local political scene.

All the hype he receives on a daily basis in the tabloids as some sort of an up-and-coming political stalwart and stud (among the usually grey-haired CCM geezers and rest of the aging, tired-looking and boring political talking-heads) no doubt contributes to his big-headedness (or inflated sense of self-importance if you will)

But one thing I know for sure (and you can all agree with me - more or less), ni kwamba jamaa ana sura mbaya kama kiatu cha Baniani! Damn!

Well Mkuu, Zitto is no devil. Nakumbuka kauli ya FMES, "viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe" kwa hiyo ukumbuke kuwa unapomsema Zitto maana yake nini. Hii ni Tanzania ndugu.
 
Mkuu Eric,
Shukran sana kwa mwenye kusoma between the line ataelewa ni mambo gani yamekuudhi. Na hakika umeeleza kama mpenzi na mwanachama wa Chadema ambaye unatazama mbalii na nje ya kabati hili la Udini na ukabila kwani haya yote na matokeo ya hasira za watu wote humu..

Kitu kimoja tu, umeeleza mengi kuhusu Zitto na tumekuelewa lakini umeshindwa kuelezea pia Ukweli wa lawama za Zitto pamoja na hasira zake. Je, kuna ukweli gani?...hapa nikiwa na maana wazee wa Chadema na washabiki woote waliokuwa against Zitto nao wana makosa makubwa tu ambayo tunayafukia fukia na visigino nya miguu yetu.. Ubaya wa kinyesi hakiwezi fichika kwa mchanga kwani ni harufu yake inayowaudhi watu.

Yawezekana wazee wa chama walifanya hayo kwa nia nzuri kama Zitto lakini kama utakuwa makini utagundua kwamba ni WAPAMBE wa pande hizi mbili walomwagia Petrol cheche za Uchaguzi huu ambao nina hakika Zitto na wazee walishafikia muafaka...Sisi ndio tulomhukumu Zitto na wazee kama Yesu na waumini wake walivyohukumiwa na Wayahudi.

Kama mtakumbuka mwaka 2006 baada ya Uchaguzi mkuu nilikuuliza wewe kuhusu Uchaguzi ndani ya Chadema ktk viti vya wawakilishi wake ikiwa ni pamoja na Secretariet. Sikuona ushindani mkubwa zaidi ya kuwa uchaguzi ule ulipangwa watu wakagawana vyeo. Nilipinga mfumo mzima wa chama Chadema na hakika niliwakalia kooni vibaya sana..
Nilihoji pia kwa nini ktk kugombea kiti cha rais Mbowe hakupata mshindani wa kweli na tulizungumzia hoja hizi kwa mapana kiasi kwamba nilikuwa mchungu kwenu. hakika mwaka huu nilitegemea ushindani na mambo mengi kurekebishwa kwani hizi tuhuma za Uchagga na Udini zimekuwepo sii leo. Zipo miaka kibao na wala sii Zitto kiongozi wa kwanza ndani ya chama kulalamikia haya. Sisi sote tulitegema kutakuwa na mabadiliko mwaka huu na pengine kila mgombea kuanza kuipanga vizuri zaidi.

Mara zote uchochezi wa Demokrasia ktk chama na ushindani wake una malengo ya kukuza fikra huru za kuwasilisha sera za chama kwa wananchi. Ni kutokana na chaguzi hizi huwafanmya viongozi wetu wawe active, waweze kuonyesha uwezo wao wa kuongoza kwa sababu bila hivyo watapoteza kura na imani ya wananchi.

Kuzuia Demokrasia na uwakilishi wa mawazo ambayo hujenga sera na utekelezaji wake ni sawa na Taifa linalokuwa chini ya Udikteta. Kiongozi anakuwa hana sababu ya kufanya kazi kwa bidii kwani hana mpinzani. Kila anachofikiria yeye ndio kitakuwa, na kwa bahati mbaya ndivyo tawala za Kiafrika zinavyojiendesha..
Natofauti kati ya nchi moja hadi nyingine ktk maendeleo yake ni pale kuna Demokrasia ya kweli yaani kuna ushindani wa shina ktk chama kupropagate sera na Utekelezaji wake kichama na kwa mapana yake mrengo na sera Kitaifa.

Binafsi nilitegemea Zitto na Dr. Slaa kugombea kiti cha urais kwa tiketi ya Chadema lakini kama uloandika ndivyo Ilivyo (yaani mwenyekiti ndiye mgombea kiti cha Urais) basi chama Chadema wamecheza mbovu na rafu..isipokuwa kosa la Zitto linakuja tu ktk kuandika vitu ambavyo yeye mwenyewe aliafiki mwanzoni wakati wazee hao wa chama hawana UWEZO kulingana na katiba kumwengua.

Kukubali kwake ushauri wa wazee hao wa chama kisha akaja wageuka na kusema walimlazimisha hali akijua fika kwamba Kikatiba hawana uhuru huo ni kuonyesha uvivu mwingine wa kifikiri. Zitto alitakliwa kuendelea kipigana kama mama Clinton alipoambiwa ajitoe akazua hoja ya kwamba anashutumiwa kwa sababu yeye ni mwanamke!... Froim that day alipindua upepo wa kura..Kwa mamillioni wanawake walimuunga mkono na kumpa kila nguvu kuendelea hadi siku alokuja shindwa..

Wakuu zangu tusidanganyane hata kidogo.. Siasa ni mchezo mchafu, yaliyomkuta Zitto ni mambo ya kawaida kabisa ndani ya chama. hata huko Marekani ndani ya Demokratic wana tofauti zao na wana makundi ya kuunga mkono/kupinga sera na utekelezaji wake ikiwa wanaona hautakuwa na manufaa kwa wananchi wake. Obama leo hii anakabiriwa na Upinzani mkubwa toka ndani ya chama chake. na wapo viongozi wa chama chake wanampiga madongo ktk TV kila siku kuhusiana na mpango wake wa Afya kwa wote..Ni jukujmu la Obama kuwa convince wabunge wake kwamba mpango wake utakuwa na mafanikio ya kudumu na hautaiweka nchi ktk madeni na matatizo zaidi. Hii ndio Demokrasia ya kweli nasii kugombea vichwa vya watu kutokana na majina yao.

Ushabiki wote ulokuwepo hapa JF ni ushabiki wa vichwa vya watu..Tuanshindwa kuelewa kwamba ushindi wowote ule hutokana na team work. Tunacholalamika ni kuwekwa bench kwa Zitto na Mbowe kuchukua nafasi ya Goalkeeper wakati sisi sote sii makocha wa team Chadema. Hao wazee tunaowalaumu wana akili, hekima na busara kuona nje ya sanduku la ushabiki na kama wao ni washabiki basi tutawahukumu pindi Ushindi utakapo kosekana kwani hata Mkapa na JK walipogombea Urais wapo wana CCM wengi walipinga nyendo zilizotumika. yet CCM wameendelea kushinda na ndio Ilani kubwa ya chama.. To win by all means necessary!
Mkielewa undani wa maneno haya, kazi za wazee ktk chama mtaweza kuelewa kwamba Demokrasia pia nimfumo unaofuata mahesabu na sayansi kama majaribio yoyote yale ktk maabara..Mkikosea hesabu Demokrasia inaweza kuwa mbegu ya magugu na mtavuna magugu.

Kifupi tuachane na habari za Zitto na viongozi wa Chadema.. tuwe na subira tupate kujua kinachoajiri hivi sasa. Sote tulivutiwa na kugombea kwa Zitto na sote tulihudhunishwa na kujitoa kwake lakini hatuwezi kutunga visingizio ikiwa mchezaji wetu mwenyewe kavua njumu na kuondoka iwe kwa hasira au kutofahamu athari za maamuzi kama hayo...Alotuangusha sote ni Zitto, period!

Yaliyopita sii ndwele tugange yajayo... wazee walichemsha na mkuu wetu Zitto pia ka smell..hivyo mashambulizi yote yanazunguka pande mbili na hakuna mwenye nafuu kati yao. Kukikomboa chama ni kuachana na yote haya na tusubiri maamuzi ya wahusika na jinsi chama kitakavyo fikia maamuzi yake kwa manufaa ya chama na wananchi wote.
 
Last edited:
Back
Top Bottom