Je, WWI ilipiganwa katika Ardhi ya Tanganyika?

Wildlifer

JF-Expert Member
May 12, 2021
1,884
5,194
Salam wanahistoria.

Ninasoma Tasnifu ya Wangari Mathai iitwayo Unbowed, Kwenye sura ya Kwanza, nimekuta maelezo kuwa kuna wakenya waliletwa Tanganyika kupigana Vita ya Dunia, kati ya Muingereza dhidi ya Mjerumani. Katika kusoma kwangu historia sina kumbukumbu kusoma kuwa vita ya kwanza ya Dunia ilipiganwa kwenye Ardhi ya Tanganyika, nimewahi kusoma watu walichukuliwa hapa kwenda nje ya nchi kama Burma n.k kupigana upande wa Muingereza. Je, kinachoelezwa hapa ni sahihi?
Screenshot_20230131-175340_1.jpg

Screenshot_20230131-175421_1.jpg

Cc: Mohamed Said Red Giant joka kuu
 
Salam wanahistoria.

Ninasoma Tasnifu ya Wangari Mathai iitwayo Unbowed, Kwenye sura ya Kwanza, nimekuta maelezo kuwa kuna wakenya waliletwa Tanganyika kupigana Vita ya Dunia, kati ya Muingereza dhidi ya Mjerumani. Katika kusoma kwangu historia sina kumbukumbu kusoma kuwa vita ya kwanza ya Dunia ilipiganwa kwenye Ardhi ya Tanganyika, nimewahi kusoma watu walichukuliwa hapa kwenda nje ya nchi kama Burma n.k kupigana upande wa Muingereza. Je, kinachoelezwa hapa ni sahihi? View attachment 2501860
View attachment 2501861

SHAJARA ZA VITA ZA LANCE CORPORAL KLEIST SYKES
VITA VYA KWANZA VYA DUNIA 1914- 1918

1675194119635.jpeg

Kleist Sykes (1894 - 1949)

Utangulizi

November 11, 1918 ndiyo siku Vita Vya Kwanza Vya Dunia vilimazilizika na dunia inaadhimisha siku hii.

Kleist Sykes hajaacha kunishangaza kila ninapoyaangalia maisha yake kupitia mswada alioandika kabla hajafa mwaka wa 1949 mswada ambao alimwachia mwanae Abdul Sykes na yeye Abdul akampa binti yake Aisha Daisy Sykes na Daisy akiwa mwanafunzi wa Historia Chuo Kikuu Cha Afrika Mashariki, Dar es Salaam akaandika ‘’Seminar Paper,’’ ‘’The Life of Kleist Sykes, ’’ (1968).

Mwalimu wake wa historia John Iliffe, aliitia ‘’paper,’’ hii kama sura moja katika kitabu alichohariri, ‘’Modern Tanzanians,’’ (1973).

Nimeupitia mswada wa Kleist na kunyambua kile Waingereza wanakiita: ‘’War Dairies,’’ yaani Shajara za Vita, Kleist akieleza maisha yake katika Vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 – 1918) akiwa askari katika jeshi la Wajerumani.

Baadhi ya askari hawa kutoka Tanganyika walipigana katika vita hivi alikuwa ndugu yake Kleist, Schneider Abdillah Plantan ambae baadae alishiriki katika harakati za kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

***​

''Miezi michache kabla Vita Vya Kwanza Vya Dunia haijaanza Ujerumani ilimteua Lettow-von Vorbeck kama Kamanda wa Majeshi ya Ulinzi ya Ujerumani katika Tanganyika.

Askari wa zamani Waafrika waliopigana chini yake, pamoja na Kleist wanamkumbuka kwa mapenzi kama mtu mwema na askari shujaa.

Kleist aliingizwa ndani ya jeshi la Wajerumani tarehe 13 November 1906 akiwa kijana mdogo sana wa umri miaka kumi na mbili na akapigana katika vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918).

Katika jeshi Kleist alipata mafunzo ya mawasiliano.

Baada ya miezi mitatu alihamishwa na kupelekwa Bataliani ya Pili kama karani katika Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam.

Alibakia hapo hadi mwaka 1914.

Vita vilipoanza, bataliani ya Kleist iliondoka Ukonga ikaelekea Mwakijembe, Tanga ambako kulikuwa na mashambulizi kutoka majeshi ya Waingereza kupitia mpaka wa Kenya.

Katika bataliani hiyo alikuwapo Schneider, mtoto wa Affande Plantan.

Kleist alikuwa anazungumza Kijerumani na juu ya yote hayo alikuwa vilevile ni mtoto wa kulea wa Affande Plantan, kiongozi wa askari wa Kizulu katika utawala wa Wajerumani.

Kwa ajili hii Kleist alipewa heshima ya pekee na akapewa nafasi kuwa mpambe wa von Lettow Vorbeck.

Kumshuhudia kijana wa Kiafrika katika sare ya jeshi la Kijerumani akiongea Kijerumani huku anatembea nyuma ya von Lettow-Vorbeck, Mkuu wa Majeshi ya Wajerumani Tanganyika, bila shaka kuliwavutia wengi, hata Wajerumani wenyewe.

Hii ilikuwa nafasi hasa iliyostahili mtoto wa askari ambae baba yake aliwasaidia Wajerumani kuiteka Tanganyika.

Kama mpambe kazi yaje ilikuwa kushughulikia mambo yote ya Kamanda Mkuu.

Alikuwa na jukumu la kuangalia chakula na usafi wa sare za von Lettow-Vorbeck, pamoja na mahitaji yake mengine.

Alikuwa ndiye mtu wa kwanza Lettow-Vorbeck kukutananae asubuhi na wa mwisho kabla hajalala.

Ilikuwa kazi yenye kumpa hadhi, mamlaka na heshima mbele ya askari wenzake. Utanashati wa Kleist katika mavazi na nidhamu yake katika maisha yake ya kawaida tu, yalitokana na kipindi hiki alichokuwa jeshini.

Inaaminika kuwa hata ile hulka yake ya kuweka shajara na kuandika kumbukumbu muhimu ya mambo yake, yanatokana na uzoefu aliopata katika kipindi hiki akiwa jeshini.

Inasemekana hii ndiyo miaka ambayo ilijenga silka na maisha ya Kleist.

Shajara zake za vita ni kielelezo binafsi kuhusu kampeni za Wajerumani na Waingereza wakati wa Vita Kuu Vya Kwanza.

Shajara hizo zinaeleza kwa ukamilifu hali ya mambo yalivyokuwa kwa askari wa Kiafrika katika mapambano waliyoshiriki dhidi ya Waingereza.

Kupitia maandishi ya Kleist unaweza ukaelewa ile chuki ambayo Waarabu walikuwanayo dhidi ya Wajerumani.

Pambano la Kleist la kwanza dhidi ya Waarabu waliokuwa washirika wa Waingereza lilikuwa katika sehemu moja ijulikanayo kama Mwele Juu karibu ya Tanga.

Mbinu ya Lettow Vorbeck ilikuwa kuvuka mpaka wa Tanganyika na Kenya ili kukata mawasilano ya reli kati ya Mombasa na Kisumu.

Reli hii ilikuwa jirani na mpaka wa Tanganyika.

Ilikuwa mwendo wa siku chache kuifikia reli hii na kuikata Kenya na njia yake kuu kutoka Mombasa.

Lakini jeshi la wanamaji wa Kiingereza lilikuwa Mombasa kwa hiyo bandari ya Mombasa ilikuwa imesalimika na manowari za Kijerumani.

Ilikuwa wakati bataliani ya Kleist ipo Korogwe, mji uliopo maili chache kutoka Tanga, katika kijiji kiitwacho Semanya ndipo Kleist alipopokea habari kuwa Affande Plantan, baba yake Schneider na mlezi wake amefariki Dar es Salaam.

Plantan alikuwa amekufa kwa homa ya matumbo tarehe 11 December 1914.

Wajerumani walisimamisha vita kwa siku saba kwa heshima ya Affande Plantan.

Wajerumani hawakuwa wezi wa fadhila walitambua kuwa alikuwa Affande Plantan waliekujanae kutoka Msumbiji kuja kuiteka Tanganyika.

Alistahili kila aina ya heshima aliyostahili askari shujaa, hata kama alikuwa mamluki.

Baada ya hapo Kleist na kamapani yake walielekea Tanga ambako kulikuwa makao makuu ya jeshi la Wajerumani wakati wa vita.

Hapo hakukaa kwa muda mrefu kwa kuwa ilibidi kuomba likizo kurudi Dar es Salaam kumuangalia mama yake Bi. Kwemah aliyekuwa mgonjwa.

Alikaa Dar es Salaam kwa siku kumi akimuuguza mama yake kisha akarejea Tanga na akapewa kuongoza askari wanane katika divisheni ya kampani.

Tarehe 24 December, 1915 kamapani yake iliamuriwa kwenda Mwakijembe na kisha Mwele Ndogo kuipokea 4th Reserve Company.

Waarabu walichukua nafasi hii ya msahambulizi ya Waingereza dhidi ya Wajerumani kulipiza kisasi dhidi yao.

Waarabu waliungana na Waingereza kuwatimua Wajerumani Tanganyika.

Bado baadhi yao walikuwa na kumbukumbu ya kitendo cha kikatili cha Wajeruani kwa shujaa wao Abushiri ambae walimnyonga mwaka 1889.

Historia ikajirudia upya; Kleist na Schneider waliingia katika mapigano Mwele Ndogo dhidi ya adui wa zamani wa baba yao na adui wa Wajerumani Waarabu.

Mapambano haya yalifanyika siku ya mkesha wa Krismasi mwaka wa 1915 katika sehemu ile ile ambayo Sykes Mbuwane na Affande Plantan mamluki wa Kizulu waliteremka kwenye meli kuja kuwaongezea nguvu Wajerumani waliokuwa wakipigana na Waarabu na machifu.

Kwa saa kumi kuanzia alfajir hadi muda mchache kabla ya jua kuchwa, Wajerumani walibanwa katika mashambulizi makali.

Kleist akapandishwa cheo na kuwa Lance Corporal kwa mchango wake katika pambano lile.

Siku mbili baada ya pambano hilo Kleist na kampani yake waliamuriwa kwenda Kahe.

Kleist Alibakia Kahe kwa mwezi mmoja kisha wakapata amri ya kwenda Voi, Kenya mji uliopo mpakani.

Wakati wakiwa njiani kuelekea Voi, Kleist akaugua na ikabidi arudishwe Mombo, mji uliokuwa na mbu wengi kwa ajili ya mto uliokuwa unakatiza hapo mjini.

Kleist alibaki akiugua hapo Mombo hospitalini kwa miezi miwili.

Kutoka Mombo akaelekea Handeni.

Mwezi Aprili 1916 habari zikamfikia bado akiwa katika uwanja wa mapambano kuwa mama yake Bi. Kwemah amefariki dunia.

Mwaka wa 1916 Jeshi la Kiingereza lilikuja kuungwa mkono na askari kutoka Afrika ya Kusini walioshuka na meli Mombasa.

Chini ya uongozi wa Jenerali Smuts walivuka mpaka wakaingia Tanganyika kupitia Namanga na Taveta.

Haukupita muda mrefu mji wa Moshi ukatekwa.

Batalioni ya Kleist ikawa sasa inarudi nyuma kuelekea Dodoma kulipokuwa na boma la Wajerumani.

Si tu kuwa kikosi cha Kleist kilikuwa kinaandamwa na majeshi ya Waingereza, vikosi vya Wabelgiji navyo vilikuwa vimevuka mpaka kutoka Belgian Congo na kuingia Tanganyika.

Wabelgiji waliteka Kigoma, Ujiji na Tabora.
Mambo yalikuwa yamewachachia Wajerumani.

Afya ya Kleist kwa wakati ule ikawa mbaya sana.

Alifanyiwa uchunguzi Morogoro na akaonekana hawezi kuendelea kuitumikia katika kampeni yake.

Afya yake haikumruhusu kupigana vita na ikabidi aachwe nyuma Mahenge wakati wenzake wakikimbia huku wakifukuzwa na adui.

Kampani ya Kleist ilikwenda Chenene ambako walipambana kwa bunduki na vikosi vya Afrika ya Kusini kwa saa mbili.

Kampani ile ikakimbilia Gode Gode, wakiponea chupu chupu.

Kleist akakamatwa mateka mwezi Septemba 1917.

Von Lettow Vorbeck mwishowe alifanikiwa kuvuka reli ya kati akavuka mpaka na kuingia Msumbiji, wakati huo ikijulikana kama Portuguese East Africa, akanusurika kutekwa yeye na askari wake.

Kwa askari wa Kizulu hii ikawa ni nusra kwao kwa kuwa walikuwa wamerudishwa nyumbani.

Wakati von Lettow Vorbeck amefanikiwa kuponyoka kukamatwa, mpambe wake Kleist alitekwa na jeshi la Wabelgiji na wao wakamkabidhi kwa Waingereza.

Waingereza walimtia Kleist kifungoni katika kambi ya mateka wa vita.

Askari waliokuwa mateka pamoja na wagonjwa walichukuliwa na Waingereza na kutiwa kwenye kambi iliyokuwapo Kilosa.

Kleist alikubali ukweli kuwa sasa yeye amepoteza hadhi yake kama askari, ni mateka, kwa hiyo akawa anasubiri hatima yake.

Alibakia ndani yake kambi ile na yeye mwenyewe anaeleza katika kumbukumbu zake kuwa hakuwa na kinyongo chochote kwa maadui zake.

Kleist aliweza hata kufanya urafiki na maadui zake ambao walikuwa wamemtia kifungoni.

Kutokana na hali yake ya afya, Kleist hakuweza kufanya kazi zote za sulubu kama ilivyo desturi kwa wafungwa.

Hali yake ya afya haikuwa inaonyesha dalili zozote za kupata nafuu, Kleist aliachiwa mwaka 1917 kwa hisia labda akiwa nje ya kambi, afya yake itarudi.

Mwezi Novemba 1918 vita vikaisha huko Ulaya.
 
Asante sana. Naomba nitaisoma kesho kwa utulivu zaidi, kisha nitasema neno.
 
SHAJARA ZA VITA ZA LANCE CORPORAL KLEIST SYKES
VITA VYA KWANZA VYA DUNIA 1914- 1918

View attachment 2501922

Asante sana Mzee MS. Mengi sikuwa nayajua.
 
Shukraani Maalim M.Said kwa maelezo yako ,yapo super Nami imebidi niingie kwenye networks nijisomee zaidi kuhusu WWI battles ndani ya nchi yangu Tanganyika, nimesoma pale Selous Game Reserve ilipigwa battle moja matata sana ,na Col.Lettow alichokifanya he defended the line ili waingereza wasiyafikie maji, na alifanikiwa na askari wengi wa kiingereza walikufa kwa kiu, pia Col.Lettow alifanikiwa kuwapa motisha wapiganaji wake ambao walihamasika sana, pia alipokimbilia Mozambique aliwanyanyasa sana Wareno pamoja na kuwa na jeshi dogo, alipora vyakula na silaha nyingi, another interesting news ya Col.huyu wa kijerumani hakutekwa kwenye uwanja wa medani, he surrended kijiji fulani hapo zambia with dignity baada ya kupewa taarifa ya kushindwa kwa vita kwa ujerumani in Europe, alijisalimisha na pistol 🔫 yake kiunoni na kofia ,mkanda,buti zake!,pia kuna another good story kuhusu hii vita kuhusu ile meli ya kijerumani ambayo ilikuwa inaingia baharini na kuzinyanyasa sana meli na uingereza na washirika wake na kurudi kujificha kwenye mto, ilichukua muda kugundulika na ikapigwa pale mtoni, waziri wangu wa utalii na balozi wangu wa ujerumani mngeitangaza hii history ya meli hii hapo ujerumani tungepata euro 💶 nyingi tu, tuendelee kulala
 
Nkanini,
Hiyo video hapo chini huyo anaezungumza Kijerumani jina lake ni Thomas Plantan.

Huyu ni mtoto wa Chief Mohosh Shangaan aliyekuja Tanganyika na Hermann von Wissman na jeshi la mamluki wa Kizulu kuja kusaidia Ujerumani washinde vita dhidi ya Abushiri bin Salim Pangani na Mtwa Mkwawa Kalenga.

Chief Mohosh alikuja kujulikana kama Affande Plantan Tanganyika.

Thomas Plantan anazungumza katika kumbukumbu ya Paul von Lettow Vorbeck mwaka wa 1964.

Welldone mkuu kwa kutunza hizi kumbukumbu, hatuna political will wa kuutumia utajiri huu kutuingizia kipato hasa cha utalii, tuna kumbukumbu nyingi sana za wajerumani nchi yetu hii, pia sijui kama tuna majumba ya ukumbusho wa history yetu, sijui kama Kinjikitile kumbukumbu zake zipo displayed somewhere ndani ya nchi yetu
 
Msiba mkubwa.
 
Nkanini,
Hiyo video hapo chini huyo anaezungumza Kijerumani jina lake ni Thomas Plantan.

Huyu ni mtoto wa Chief Mohosh Shangaan aliyekuja Tanganyika na Hermann von Wissman na jeshi la mamluki wa Kizulu kuja kusaidia Ujerumani washinde vita dhidi ya Abushiri bin Salim Pangani na Mtwa Mkwawa Kalenga.

Chief Mohosh alikuja kujulikana kama Affande Plantan Tanganyika.

Thomas Plantan anazungumza katika kumbukumbu ya Paul von Lettow Vorbeck mwaka wa 1964.

Sijaelewa kinachosemwa kwenye Video. Ila kwenye Comments, kuna ujumbe huu wa mchangiaji;

Picha [hiyo ya Video] ilipigwa katika makaburi ya jumuiya ya madola jijini dar es salaam ambapo wanajeshi wa kijerumani waliofariki dunia katika Vita ya Kwanza ya Dunia wamezikwa karibu kabisa na makaburi ya wakoloni wa kijerumani ambayo yamesahaulika kabisa kwa sababu hakuna nia kabisa ya ujerumani kuyadumisha. [Serikali ya] Uingereza hugharamia utunzaji wa makaburi ya Wajerumani katika makaburi kadhaa nchini Tanzania, Ambayo ni ya Dar na Iringa.
 
Nkanini,
Hiyo video hapo chini huyo anaezungumza Kijerumani jina lake ni Thomas Plantan.

Huyu ni mtoto wa Chief Mohosh Shangaan aliyekuja Tanganyika na Hermann von Wissman na jeshi la mamluki wa Kizulu kuja kusaidia Ujerumani washinde vita dhidi ya Abushiri bin Salim Pangani na Mtwa Mkwawa Kalenga.

Chief Mohosh alikuja kujulikana kama Affande Plantan Tanganyika.

Thomas Plantan anazungumza katika kumbukumbu ya Paul von Lettow Vorbeck mwaka wa 1964.

Tafsiri ya kinachosemwa kwenye video hiyo;

"In, memory of,
We, the old Herrschaften, they slept herew e can not forget Lettow-Vorbeck

We wish him that he will not forget us,
we, the german soildier, otherwise we would not fear god in the world."

This askari is not speaking german properly and the connection between those sentences are not correct. But let me conclude this:
Paul von Lettow-Vorbeck was the general of the askari-troops in German East-Africa, today it is called Tanzania.
 
My...
Ahsante sana.
 
Ilipiganwa sana. Tena ilikuwa kali. Ndiyo kisa cha kuzamishwa kwa MV Liemba ili isikamatwe na maadui. Manowari ya kijerumani iliyoitwa Konigsberg iliharibiwa kwenye mto Rufiji ilikokimbilia. Kuna vitabu vinaelezea vita hiyo, kama Mimi and Toutou go Forth na General wa kijerumani wakati huo Paul von Lettow Vorbeck ameandika kuanzia maandalizi hadi vita kwenye My Reminescences of East Africa. Kiufupi hadi vita inaisha Tanganyika ilikuwa bado haijatekwa sababu ya huyu jamaa.
 
Asante kwa rejea hizo. Nime'pirate' tayari hicho kitabu. Nitakipitia, na nitashare nililoyapata.
 
Attachments

  • Screenshot_20230205-143640.jpg
    Screenshot_20230205-143640.jpg
    113 KB · Views: 14
Ndio,si ndio maana wakaleta Mv liemba wajerumani, na hapo rufiji nasikia kuna meli ya vita ilizamishwa pia

MV Liemba haina uhusiano wowote ule na Vita, Meli iliwekwa kuhudumia Koloni la Mjerumani lililojumuisha Tanzania ya leo (ukiondoa Zanzibar), Burundi na Rwanda, na hata Ziwa Tanganyika kulikuwa na Bandari na cranes na reli ya Kati iliishia Ziwani na haya yote yalifanyika kabla ya Vita Kuu kuanza.
 
Ilipiganwa sana. Tena ilikuwa kali. Ndiyo kisa cha kuzamishwa kwa MV Liemba ili isikamatwe na maadui. Manowari ya kijerumani iliyoitwa Konigsberg iliharibiwa kwenye mto Rufiji ilikokimbilia. Kuna vitabu vinaelezea vita hiyo, kama Mimi and Toutou go Forth na General wa kijerumani wakati huo Paul von Lettow Vorbeck ameandika kuanzia maandalizi hadi vita kwenye My Reminescences of East Africa. Kiufupi hadi vita inaisha Tanganyika ilikuwa bado haijatekwa sababu ya huyu jamaa.

MV Liemba ni Ziwa Tanganyika na haina uhusiano na Vita ya Dunia, ni meli iliyowekwa kuhudumia Ziwa Tanganyika, na inatumika mpaka leo hii!
 
MV Liemba haina uhusiano wowote ule na Vita, Meli iliwekwa kuhudumia Koloni la Mjerumani lililojumuisha Tanzania ya leo (ukiondoa Zanzibar), Burundi na Rwanda, na hata Ziwa Tanganyika kulikuwa na Bandari na cranes na reli ya Kati iliishia Ziwani na haya yote yalifanyika kabla ya Vita Kuu kuanza.
Mkuu,unasema meri ya kivita haikuwa na uhusiano na vita, seriously ?
During World War I the Germans converted Goetzen to an auxiliary warship under the name SMS Goetzen. They gave her a 10.5 cm (4 in) gun from the light cruiser SMS Königsberg, a ship no longer operational and which her crew later scuttled in the mouth of the Rufiji River. She also received an 8.8 cm (3 in) gun, one of two that Königsberg had brought out from Germany to arm auxiliary cruisers should the opportunity arise. Lastly, the survey ship SMS Möwe contributed two 37 mm Hotchkiss revolver guns to Goetzen's armament.[14]

The Germans appointed Oberleutnant zur See Siebel captain of Goetzen. Under his command Goetzen initially gave the Germans complete supremacy on Lake Tanganyika. She ferried cargo and personnel across the lake between Kigoma and Bismarckburg (now Kasanga, Tanzania), saving troops from a two-week overland march, and provided a base from which to launch surprise attacks on Allied troops. It therefore became essential for the Allied forces to gain control of the lake themselves.
 
Back
Top Bottom