Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,016
- 9,885
Rangi nyingine zilizuiwa bila kutoa sababu huku maafisa wa forodha wakisema kuwa rangi nyeupe ni rangi ya bahati. Rais Gurbanguly Berdimuhamedov alianza kutumia msafara wa magari meupe kusafiri kwenye matukio ya umma, na karibu maafisa 160 wa ngazi ya juu, ikiwa ni pamoja na wakuu wa vyombo vya habari vya nchi, haraka wakafuata nyayo, kulingana na shirika la habari la RIA Novosti la Urusi mwezi wa Septemba 2014.
Sheria za rangi ni mojawapo tu kwenye orodha ndefu ya sheria, ambayo ni pamoja na marufuku ya uingizaji wa magari ya meupe, magari ya kifahari, na magari yenye namba za usajili zilizobinafsishwa au madirisha yenye tinted.
Watu wa Turkmenistan wamezoea vizuizi vya ajabu katika maisha yao ya kila siku, ambavyo mara nyingi inaonekana kama vimeletwa kwa mapenzi ya rais. Mnamo mwaka wa 2014, wakazi wa mji mkuu, Ashgabat, walipinga baada ya mamlaka kuamuru kuondoa air conditions kwenye majengo ili kuboresha muonekano wa jiji. Serikali pia imekuwa ikitumia mabilioni ya dola kurekebisha mji mkuu kuwa "mji mweupe" kwa kufunika majengo yote makubwa na marumaru.