Je wajua tofauti ya mwanamke na mwanaume kisaikolojia

uvugizi

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,235
874
1 Petro 3:7 " kadhalika ninyi waume kaeni na wake zenu kwa akili ; na kumpa mke heshima , kama chombo kisicho na nguvu ; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima , kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.""

Wanasaikolojia na biolojia wamefanya utafiti ambao umetusaidia kuwabaini hawa viumbe me/ke.

Imebainika tatizo kubwa la kimawasiliano kati ya mwanaume na mwanamke ni kwa sababu kila mmoja hamjui mwingine.

Ellen Goodman katika research yake na kitabu chake ,, titled in a different voice ""ana share na wewe vipengele vichache muhimu kati ya tofauti hizo.

1)UWEZO WA MAWASILIANO NA LUGHA YA MWILI

Sehemu ya mawasiliano ya mwanamke katika ubongo ( akili) ni kubwa kuliko ya mwanaume . Mwanamke ana uwezo mkubwa wa kuongea kuliko mwanaume . Mwanamke anaongea maneno 25,000 kwa siku , wakati mwanaume anaongea 12,500 kwa siku . Mwanamke anasikiliza neno kwa neno na ni mwepesi sana kuelewa lugha ya mwili ,,,, hapa kama ni security intelligence ni wazuri sana .

2) KUSHIRIKISHANA NA KUTATUA MATATIZO.

Wanaume wanapenda sana kujitegemea katika kipengele hiki, wanapenda kutatua matatizo wao wenyewe bila hata kuyaongelea sana . Kinamama wao wasipo shirikisha matatizo yao kwa marafiki na watu wengine wanakuwa wanachanganyikiwa zaidi , hata kama hao wanaowashirikisha hawana majibu. Kipengele hiki ndiyo chanzo cha migogoro ya NDOA

3) MVUTO NA MAPENZI

Eneo la ubongo la matamanio ya mapenzi ( sexual desire) kwa mwanaume ni kubwa sana, ndiyo maana wanaume wanahisia Kali za kimapenzi kuliko wanawake

4) HASIRA NA USULUHISHI

Mwanamke kibayolojia ana wire katika ubongo wake wa kuepusha ugomvi ,, ugomvi kwake si sehemu yake sana mpaka pale tu atakapoguswa asili yake , inaamika anakuwa mkorofi kuliko mfano kuuchukia ule uanamke wake ,, kinyume chake ni kuusifia asili yake .Watafiti wanasema akili ya mwanamama inatatua ugomvi kwa haraka , mwanaume akili haitendi kwa haraka yaani hakubali amani kwa haraka.

5) KUFIKIRI KIMANTIKI NA KIHISIA

Mwanaume anaweza kuamua maamuzi yeyote bila kuathirika kihisia , mwanamke ni tofauti, atakishikilia hicho kwa muda mrefu. Mwanamke daima huwa hakubali matokeo ya hicho kitu ,,, mwanamke atalifanya tukio ,,,, tambua kwamba mtu asiyekubali matokeo huyo kisaikolojia huwa hayupo na ni rahisi kufanya lolote.

Kwa Majumuisho mwanamke ana hemisphere ya emotion na logic na mwanaume vivyo hivyo ,,,, ila mwanamke anatawaliwa na hemisphere ya emotion zaidi ,Mwanaume ya logic zaidi..... Kwa hiyo mwanamke ana uwezo mkubwa wa kumdhibiti Mwanaume , kwa sababu kisaikolojia Emotion ndiyo inayoendesha dunia siyo logic. Na ndiyo maana mwanamke alitengenezwa awe msaidizi kwa mwanaume kwa mujibu wa biblia,,,, tazama mwanamke akiwa na pesa mume hana ,, ndoa ipo njia panda .

Mwanaume na Mwanmke au mke na Mume wakitofautiana ndani ya ndoa ,, maana yake LOGIC + EMOTIONS ,,,,, vimegongana na matokeo ni frustration

Nayakumbuka maandiko matakatifu yanasema ,,,,,KAENI NA WAKE ZENU KWA AKILI ,,,,,

Be inspired
 
Nimeketi hapa mbele kwa dereva kwakuwa kuna vipengele vya bibble nawasubiri wajuvi waje.
 
Back
Top Bottom