Ahahaha sawa mkuu wangu kaa lingekuwa swali la kihuni na kilevi mbona umelijibu au nawe mlevi na mhuni kama mimi?.. Tuache mas-hala cheti cha ndoa hakiwezi kukuhakikishia kwamba wao ni wazazi wako kwa sababu sio cheti kinachozaa mtoto bali kitendo cha wazazi wako kukutana kimwili.Hilo ni suala la kihuni na kilevi..lakini ntakujibu hivi..sikuuliza hati yao ya ndoa kwani wote wawili walinipenda na kunipa malezi mazuri na elimu ya kuweza kupambana na maisha.hivyo sikua na sababu ya kuhoji ..lakini wangeniacha na kuhangaika na ulimwengu na kunitupa kama mtoto wa kambo basi nigedai hati kujua kama kweli wao ni wazazi wangu...ama ni mtoto wa kulea ...
na kama unaleta mfano ndoa katika muungano basi wanandoa wakikosana huachana ....Mkandara ufisadi na uongo na mbini chafu zilizotumikia kufikia muungano ndio mambo ambayo tunataka kuyafuatilia ili mchawi apatikane...
Hivyo hata kama watakutesa watakutenga ythe Only way kwako wewe kuhakikisha kama kweli ni wazazi wako ni swala la wewe mwenyewe kufanya DNA maana mwenye mashaka ni wewe. Na hata ukikuta hawa ni wazazi wako ama sio wazazi wako bado haitajibu swali gumu ambalo wewe unataka kulifanya nalko ni kujikata. Hivyo basi kama unataka kujikata iwe kwa taabu au mafanikio unaweza kabisa kufanya maamuzi hayo bila ruksa yao..
Na ndivyo tunacvyowaambia ya kwamba Hati ya Muungano baina ya Tanzania na Zanzibar ipo na picha zimewekwa kuonyesha kilichofanyika. Zanzibar wanayo copy yao na Bara na viongozi wetu hawana sababu wala jukumu la kutuonyesha isipokuwa tunaweza kudai kutokuwepo Usiri ktk makubaliano haya kama vile wenzetu Marekani walivyofanya BOFYA japokuwa kizazi hiki hakiwezi kuelewa sababu zilizolazimisha muungano huo ili hata vyuoni wanafunzi wanajifunza sheria wapate kuelewa na wanalinda kitu hiki kwa kupitia sheria uhalali upi. Hata Marehemu Profesa (RIP) aliandika makala zake akijiuliza sababu na utata ulofuatia makubaliano haya..
Maadam tulishaungana na wengi wetu ni kizaiz cha Muungano huo, uhalali wa ndoa hauwezi kabisa kuleta ufumbuzi wa matatizo ya Wazanzibar wala wabara isipokuwa kero zilizopo ktk muungano kama alivyoanisha Profesa ndizo za kuzitafutia Ufumbuzi na kama haiwezekani ni bora mwenye kuitaka talaka kama kweli ni mawazo ya baraza la Mapinduzi basi wajitoe, na kama ni mawazo ya wananchi wa Zanzibar majibu lazima yatoke ktk kiungo cha Muungano wetu nacho ni Baraza la Mapinduzi. Na amini maneno yangu mchawi sii yeyote bali Ukweli usipokubalika ya kwamba serikali ya Zanzibar ina wenyewe na wenyewe ndio hawataki kabisa kusikia habari za kuvunja Muungano maana ndio hifadhi yao wao..
Hawa ndio wabaya wao kama sisi tunavyopambana sasa hivi na CCM bara kutokana na imani waloijenga ya kwamba CCM ina wenyewe na wenyewe ndio watawala. Vita hii naweza sema ilianzishwa na CUF kupambana na viongozi wa CCM visiwani hadi kufikia karibu na ushindi lakini kama wanavyodai CCM wana silaha nyingi na za kila aina. Wakawazidi ujanja CUF kwa kujenga chuki baina ya chama hicho na Chadema wakati hawa wote walikuwa na agenda moja.
Kumwondoa CCM madarakani, hivyo walipojitenga wakifikiria Wazanzibar wanaweza kuwa na UMOJA kudai serikali yao bila kujua kwamba CCM wanajua fika hawakubaliki na wakijitenga CUF itaendelea kupambana na CCM mpya ya Zanzibar sijui wataitwa ASP au nini na uhasama utarudi palepale na itaishia CUF kuchukua madaraka. Hili ni swala ambalo baraza la mapinduzi hawataki kabisa kusikia kama CCM wanavyohaha kusikia Chadema inaweza chukua nchi mwaka 2015.... Akili mu kichwa!