Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?

WAAACHE HAO WAZEE WA KANISA WATAFUNE SADAKA NA KUJITAFUNIA VIKONDOO

SIKILIZA UKWELI HUU

http://www.mzalendo.net/habari/video...tu-wa-zanzibar

Acheni udini hapa, kwani Field Marshal John Okello kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar alikuwa dini gani? alikuwa raia wa nchi gani?:sick:

Artilce of the union.

The 'article of the union' was ratified by Karume snr. through the presidential decree No.5 which gave him powers to enter into any agreement on behalf of his country. The 'articles of the union' was furthermore approved by the revolutionary council, it is believed that some members showed some reservation however, Kassim Hanga managed to emotionally convinced them all to agree.
Contrary to popular belief of the Pascolians:sick:, the legality/presence of the ratified 'articles of the union' was validated/confirmed by Judge Nyalali commission in 1991.
 
acheni udini hapa, kwani field marshal john okello kiongozi wa mapinduzi ya zanzibar alikuwa dini gani? Alikuwa raia wa nchi gani?:sick:

artilce of the union.

the 'article of the union' was ratified by karume snr. Through the presidential decree no.5 which gave him powers to enter into any agreement on behalf of his country. The 'articles of the union' was furthermore approved by the revolutionary council, it is believed that some members showed some reservation however, kassim hanga managed to emotionally convinced them all to agree.
Contrary to popular belief of the pascolians:sick:, the legality/presence of the ratified 'articles of the union' was validated/confirmed by judge nyalali commission in 1991.

KWANI WAKATI PENGO ANAPOTOA AMRI , MUUNGANO USICHOKONOLEWE YEYE ANAKUWA NI MJUMBE WA NEC CCM AU CHADEMA??? AU

wewe ndiye ulikuwa katibu wa blm au babu yako ???

Usituletee maneno ya propaganda za kanisa tafadhali

ANGALIA MWENYEWE HAO WALIOKUWA KWENYE BLM UNALODAI WALIUKUBALI MUUNGANO WANASEMA NINI

Video:Kwanini tusiirejeshe jamhuri ya watu wa Zanzibar? | Mzalendo.net
 
Udini ndio unakusumbua Kamwemwe, hujajibu swali kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar Field Marshal John Okello alikuwa dini gani na raia wa nchi gani?:sick:

Karume snr, Kassim Hanga na wenzao waliridhia muungano bila ya kushikiwa mtutu wa bunduki. Ni kama vile kondoo anapoingia machinjioni bila kulazimishwa, sasa inakuweje leo muanze kulaumu watu wengine??:confused2:
 
Udini ndio unakusumbua Kamwemwe, hujajibu swali Field Masharl John Okello alikuwa dini gani na raia wa nchi gani?:sick:

Karume snr, Kassim Hanga na wenzao waliridhia muungano bila ya kushikiwa mtutu wa bunduki. Ni kama vile kondoo anapoingia machinjioni bila kulazimishwa, sasa inakuweje leo muanze kulaumu watu wengine??:confused2:

UDINI SIKUUANZISHA MIMI ALIUANZISHA NYERERE

HUYO ULIYEMTAJA NI MTUMISHI WA KANISA KUTOKA UGANDA KATIKA ILE PROGRAMU YA KANISA YA KUIFANYA AFRIKA MASHARIKI KUWA KATIKA UKRISTO

SOMA HII KITU , DECEMBER 1993

MJADALA unaendelea nchini kote juu ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na muundo wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Inavyoelekea yapo matatizo, dosari na sababu za msingi zilizopelekea wananchi kuhoji muundo wa sasa wa Muungano na kuleta hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ni yenye kuundwa kama si leo kesho.

Lakini wapo pia wanaopinga kabisa kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.

Aliyejitokeza kwa nguvu na kwa ukali hadharani kupinga hoja hiyo ni Mwalimu Julius Nyerere, katika kupinga hoja hiyo Mwalimu anatoa hoja zifuatazo:

Hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika imeletwa kwa kuwachoka Wazanzibari na Waislamu. Ufupi wa maneno Mwalimu Nyerere anadai hoja ya kuundwa Serikali ya Tanganyika imetokana na chuki za kidini - Wakristo kuwachukia Waislamu.

Hoja haipo katika sera za CCM na taratibu zimekosewa.
Kuundwa kwa serikali ya Tanganyika kutavunja Muungano na kutavunja Tanganyika pia.

Ukizingatia sifa nyingi ambazo Nyerere alijilimbikizia wakati wa utawala wake na sasa si vigumu kuelewa kwa nini anapinga kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. Mambo yake yote aliyoyaanzisha kwa vishindo huku akisifiwa kuwa zidumu fikra zake, yamekuwa yakiporomoka moja baada ya jingine huku mwenyewe akiona. Lililosalia ni Muungano; nao ukiporomoka haitaleta picha nzuri katika historia yake katika siasa.

Lakini lililo gumu kueleweka ni hatua ya Mwalimu Nyerere kutumia Turufu ya udini kuwagawa Wabunge; wana-CCM na Wa-Tanzania kwa ujumla katika suala hili. Kauli hiyo ingesemwa na Muislamu ingepewa mtizamo tofauti na labda isingeeleweka hasa miongoni mwa Waislamu. Lakini kusemwa na Mwalimu Nyerere kunaleta mkanganyiko zaidi. Kwanini; (udini ulikuwa umejengeka). Hali hiyo ilipelekea Masheikh kumlalamikia lakini akawanyamazisha kwa kuwashutumu kuwa wanachanganya dini na siasa. Miongoni mwa Masheikh hao wapo waliofukuzwa nchini; waliowekwa kizuizini, waliofukuzwa katika chama na kadhalika.

Sheikh Hassan bin Amir katika waraka wake kwa Waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa unajengwa Tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:

Kuingizwa nchini Tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya bendera ya Tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama Mama Maria na mtoto mchanga na nyuma yake maandiko 'MARIA MTAKATIFU ULINDE UHURU WA TANGANYIKA'.

Gazeti la KIONGOZI la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha Bwana George Kahama akipewa cheo cha dini na Pope kwa kuwakilisha serikali ya Tanganyika katika mkutano wa Makanisa ya Roma.

Mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, Baraza Kuu la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika lilitoa matangazo kuwa Uhuru wa Tanganyika ulikuwa 'Chini ya Msalaba'.

Tarehe 17/5/1963 Makanisa yalifanyia mkutano wao ndani ya Bunge.

Alipokufa Pope Yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima!

Kabla ya kifo chake Pope Yohana wa 23 alimletea Mheshimiwa Nyerere barua ya pongezi kwa kuupanua Ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na Pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa kwenye gazeti la Tanganyika Standard.

Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: "KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC". Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.

UKIMALIZA, SIKILIZA HIZI VIDEO TAFADHALI ,UTAPATA MAJIBU YAKO YOTE

Video:Kwanini tusiirejeshe jamhuri ya watu wa Zanzibar? | Mzalendo.net
 
UDINI SIKUUANZISHA MIMI ALIUANZISHA NYERERE

HUYO ULIYEMTAJA NI MTUMISHI WA KANISA KUTOKA UGANDA KATIKA ILE PROGRAMU YA KANISA YA KUIFANYA AFRIKA MASHARIKI KUWA KATIKA UKRISTO

SOMA HII KITU , DECEMBER 1993

Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: "KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC". Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.

UKIMALIZA, SIKILIZA HIZI VIDEO TAFADHALI ,UTAPATA MAJIBU YAKO YOTE

Video:Kwanini tusiirejeshe jamhuri ya watu wa Zanzibar? | Mzalendo.net

Mashaallah, yaani unafurahisha sana, kwa hiyo unadai mwanamapinduzi Field Marshal John Okello ni mkristu aliyetumwa!!! ina maana hata mapinduzi basi huyatambui/haramu sio?. Ina maana wewe ni neo-Shamtean?

Ushauri wangu kwako na akina Pascolians kama kweli mna nia ya kurudisha Zanzibar kuwa huru ni bora mkabadili mbinu za mapambano. Haina haja ya kulaumu watu wengine na kupenyeza hisia za udini kwenye hili jambo, makosa mlifanya wenyewe huko nyuma, mikataba mlisaini na kuridhia bila kulazimishwa na mtu.

om7_scaled.jpg

whiter-zanzibar-5.jpg
 
MWANAKIJIJIN WEWE NI MCHOKOZI TU

NIMELETA LINK YA MAHOJIANO YA KATIBU WA BLB LA WAKATI ULE NA KAELEZA KWA UREFU LEO NAKULETEA VIDEO HIZI

LABDA UTAELIMIKA ZAIDI WEWE NA HO WENGINE WANAOFUATILIA MIJADALA HII

Video:Kwanini tusiirejeshe jamhuri ya watu wa Zanzibar? | Mzalendo.net
Mkuu wangu unaweza kabisa kuirejesha kama walivyoijiuliza Libya maana ule ukoo wa Mfalme walipiga mahesabu ya kurudi na wakaanzisha kitu kama hiki. Wakawachochea wananchi wake kumchukia Ghadaff na kwamba Libya wanayoitambua ni ile ilopata Uhuru mwaka 1951 baada ya Sultan kujitangazia Uhuru wa kifalme akimweka wairi mkuu.. Toka walipopinduliwa na Ghaddaff wamekuwa wakitafuta njia za kuurudisha utawala wa kisultan na kusema kweli wamefanikiwa na hakika leo wanawafukuza watu weusi kama mbwa kutokana na kwamba Ghadaff aliwapenda watu wote. Haya tunayajua yanakuja Zanzibar ni chaguo lenu wenyewe.

Kwa hiyo mnaweza sana kuirudisha Zanzibar na bendera yenu ya sultan kama walivyofanya Libya maana hizi ndizo mbinu mpya wanazotumia kuwakamata vibaraka kama nyie msojua mbele wa nyuma isipokuwa Uzanzibar, na Inshaallah namuomba Mola awajaalie mpate nguvu mrudishe Jamhuri ya watu wa Zanzibar halafu cha moto mtakiona muanze tena kufur za kumlalamikia Mungu.

Ila nataka ufahamu ya kwamba hakuna Muungano wowote ulowahi kufanyika ulihitaji ratification ya Bunge au baraza zima isipokuwa bunge ndilo hulazimika kufuata sheria ilopitishwa kama vile sisi leo ni wanachama wa JUMUIYA ya African Union (AU) mpya ambayo viongozi wetu waliweka saini mwaka 2000 bila wewe na mimi kuridhia - BOFYA na hata ile ilotangulia ya mwaka 1965 kujiunga na OAU sidhani kama kuna kikao chochote kilifanyika kuridhia bali executive board yetu inayotuwakilisha ktk vikao hivyo ndio wahusika wakuu na ndio maana mara kwa mara vikao vya AU na UN kuna watu maalum kuwakilisha. Na hizi ni JUMUIYA tu ambazo zinaingiwa na nchi lakini sii Muungano unaounda NCHI bado mnataka kina nani wahusishwe?.. Hivyo basi nakuomba pia msome Abdulrahman Babu ktk kuundwa kwa muungano maana huyu ndio turufu ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

Kifupi Pasco kala vichwa kibao hapa kwa sababu hata hao Maprofesa hawajui haswa kilichotokea ktk Mapinduzi ya Zanzibar isipkokuwa speculations ambazo hawawezi kuzithibitisha hadi kesho. Na kwa bahati mbaya sidhani kama kuna mtu ambaye kwa undani anajua kilichotokea maana hata hilo baraza la Mapinduzi wenyewe ni wachache sana walifahamu kuwepo kwa Mapinduzi ya January 1964 maana ilikuwa siri na isingefanikiwa kama kila mwanchama au mjumbe wa ASP angejua kinachoendelea.
 
Mashaallah, yaani unafurahisha sana, kwa hiyo unadai mwanamapinduzi Field Marshal John Okello ni mkristu aliyetumwa!!! ina maana hata mapinduzi basi huyatambui/haramu sio?. Ina maana wewe ni neo-Shamtean?

Ushauri wangu kwako na akina Pascolians kama kweli mna nia ya kurudisha Zanzibar kuwa huru ni bora mkabadili mbinu za mapambano. Haina haja ya kulaumu watu wengine na kupenyeza hisia za udini kwenye hili jambo, makosa mlifanya wenyewe huko nyuma, mikataba mlisaini na kuridhia bila kulazimishwa na mtu.

om7_scaled.jpg

whiter-zanzibar-5.jpg

uniite majina yoyote, niamini au nisiamini mapinduzi haitobadilisha ukweli aliosema Okelo mwenyewe.

SOMA KITABU AMBACHO ALIKIANDIKA OKELLO Kinaitwa Revolution in Zanzibar ????

KITAFUTE MAANA KILIPIGWA MARUFUKU

Humo utayasikia maneno yake mwenyewe huyo Okello , usisikilize propaganda za kanisa, please
 
Good luck with your endeavors...:sick:

Btw, kama una mda soma makala ya Prof. Othman kuhusu uhalali wa muungano kwenye linki hapa chini:
http://zanzibardaima.wordpress.com/...zibar-african-initiative-or-cold-war-rivalry/
 
uniite majina yoyote, niamini au nisiamini mapinduzi haitobadilisha ukweli aliosema Okelo mwenyewe.

SOMA KITABU AMBACHO ALIKIANDIKA OKELLO Kinaitwa Revolution in Zanzibar ????

KITAFUTE MAANA KILIPIGWA MARUFUKU

Humo utayasikia maneno yake mwenyewe huyo Okello , usisikilize propaganda za kanisa, please
Acha wewe unaamini watu ambao wameandika kitabu kwa ajili ya biashara? Okello alikuwa primary school drop out hakumaliza hata darasa la nne hakujua kusoma wala kuandika. Kiswahili chenyewe kilimpiga chenga na hata kiingereza ndio kabisaa -sasa ameweza vipi kuandika kitabu au haya ndio ya elimu mpya ya mtoto kushinda mtihani wa darasa la saba lakini hajui kusoma wala kuandika..

Ila nachoweza kusema ni kwamba.. Je? unajua ya kwamba Okello alikuwa mwanachama hai wa ASP? na kama alikuwa mwanchama aliponda mawe ya kokoto huko Pemba ilikuwaje yeye ndiye awe kiongozi wa Mapinduzi bila viongozi wa ASP kujua na hata baada ya masaa 24 ya Mapinduzi, Yeye Karume na Babu waitangazie dunia kuwepo kwa serikali ya Mapinduzi? Hawa watu waliweza vipi kukutana au kuandaa utoaji habari huo ikiwa hayakuwepo maandalizi? Okello alitumiwa kwa kazi maalum yenye lawama na baada ya hapo akatemwa..

Akili za mbayuwayu mkuu wangu, changanya na za kwako mkuu wangu....
 
Mashaallah, yaani unafurahisha sana, kwa hiyo unadai mwanamapinduzi Field Marshal John Okello ni mkristu aliyetumwa!!! ina maana hata mapinduzi basi huyatambui/haramu sio?. Ina maana wewe ni neo-Shamtean?

Ushauri wangu kwako na akina Pascolians kama kweli mna nia ya kurudisha Zanzibar kuwa huru ni bora mkabadili mbinu za mapambano. Haina haja ya kulaumu watu wengine na kupenyeza hisia za udini kwenye hili jambo, makosa mlifanya wenyewe huko nyuma, mikataba mlisaini na kuridhia bila kulazimishwa na mtu.

om7_scaled.jpg

whiter-zanzibar-5.jpg
duh! halafu muungano wenyewe ulifanyikia huko huko zanji bari, maana ungefanyikia tanganyika tungeambiwa jamaa walishikiwa bunduki au walikuwa mateka. au samaki mkubwa kula samaki mdogo.
 
duh! halafu muungano wenyewe ulifanyikia huko huko zanji bari, maana ungefanyikia tanganyika tungeambiwa jamaa walishikiwa bunduki au walikuwa mateka. au samaki mkubwa kula samaki mdogo.

Jamni si hapa tunawaona wanabadilishana hati za muungano??????????? ziko wapi hizi hatii ???? nani anao??? mwenye nao aulete....ukweli ya walicho ungana hakijulikani...hizi hati ambayo nyerere na karume walisain hazipo sasa uhalali upo wapi...tutajuaje walisani kitu gani hawa ???/ pasua akili...ujiulize...kwa nini wanauficha? kwa nini hawataki watu waujue? kwanini kwa nini.....tatizo ccm bas ndio wanatuhangaisha akili...hawa ndio wanatuficha ukweli
 
Macos, nimewahi kuuliza hivi wewe umewahi kuiona hati ya ndoa ya baba yako na mama yako?.. na unapotaka kukiona unakuwa na sababu gani haswa? kujua kama ilikuwa ndoa ya kweli (kanisani, msikitini au City hall) ipi ndio halali kati ya hizo...Je, kujua kama wewe ni mtoto wao wa damu au unataka haswa kufuatilia kitu gani?.
 
Hilo ni suala la kihuni na kilevi..lakini ntakujibu hivi..sikuuliza hati yao ya ndoa kwani wote wawili walinipenda na kunipa malezi mazuri na elimu ya kuweza kupambana na maisha.hivyo sikua na sababu ya kuhoji ..lakini wangeniacha na kuhangaika na ulimwengu na kunitupa kama mtoto wa kambo basi nigedai hati kujua kama kweli wao ni wazazi wangu...ama ni mtoto wa kulea ...
na kama unaleta mfano ndoa katika muungano basi wanandoa wakikosana huachana ....Mkandara ufisadi na uongo na mbini chafu zilizotumikia kufikia muungano ndio mambo ambayo tunataka kuyafuatilia ili mchawi apatikane...
 
Mkuu wangu unaweza kabisa kuirejesha kama walivyoijiuliza Libya maana ule ukoo wa Mfalme walipiga mahesabu ya kurudi na wakaanzisha kitu kama hiki. Wakawachochea wananchi wake kumchukia Ghadaff na kwamba Libya wanayoitambua ni ile ilopata Uhuru mwaka 1951 baada ya Sultan kujitangazia Uhuru wa kifalme akimweka wairi mkuu.. Toka walipopinduliwa na Ghaddaff wamekuwa wakitafuta njia za kuurudisha utawala wa kisultan na kusema kweli wamefanikiwa na hakika leo wanawafukuza watu weusi kama mbwa kutokana na kwamba Ghadaff aliwapenda watu wote. Haya tunayajua yanakuja Zanzibar ni chaguo lenu wenyewe.

Kwa hiyo mnaweza sana kuirudisha Zanzibar na bendera yenu ya sultan kama walivyofanya Libya maana hizi ndizo mbinu mpya wanazotumia kuwakamata vibaraka kama nyie msojua mbele wa nyuma isipokuwa Uzanzibar, na Inshaallah namuomba Mola awajaalie mpate nguvu mrudishe Jamhuri ya watu wa Zanzibar halafu cha moto mtakiona muanze tena kufur za kumlalamikia Mungu.

Ila nataka ufahamu ya kwamba hakuna Muungano wowote ulowahi kufanyika ulihitaji ratification ya Bunge au baraza zima isipokuwa bunge ndilo hulazimika kufuata sheria ilopitishwa kama vile sisi leo ni wanachama wa JUMUIYA ya African Union (AU) mpya ambayo viongozi wetu waliweka saini mwaka 2000 bila wewe na mimi kuridhia - BOFYA na hata ile ilotangulia ya mwaka 1965 kujiunga na OAU sidhani kama kuna kikao chochote kilifanyika kuridhia bali executive board yetu inayotuwakilisha ktk vikao hivyo ndio wahusika wakuu na ndio maana mara kwa mara vikao vya AU na UN kuna watu maalum kuwakilisha. Na hizi ni JUMUIYA tu ambazo zinaingiwa na nchi lakini sii Muungano unaounda NCHI bado mnataka kina nani wahusishwe?.. Hivyo basi nakuomba pia msome Abdulrahman Babu ktk kuundwa kwa muungano maana huyu ndio turufu ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

Kifupi Pasco kala vichwa kibao hapa kwa sababu hata hao Maprofesa hawajui haswa kilichotokea ktk Mapinduzi ya Zanzibar isipkokuwa speculations ambazo hawawezi kuzithibitisha hadi kesho. Na kwa bahati mbaya sidhani kama kuna mtu ambaye kwa undani anajua kilichotokea maana hata hilo baraza la Mapinduzi wenyewe ni wachache sana walifahamu kuwepo kwa Mapinduzi ya January 1964 maana ilikuwa siri na isingefanikiwa kama kila mwanchama au mjumbe wa ASP angejua kinachoendelea.

huo muungano uliosema wa OAU wapi umeona VAT wanakwenda asubuhi kwenye nchi wanakusanya pesa yote ya kodi jioni wanarudi Dar-salaam na vikapu vyao vya pesa. mwisho wa mwezi nchi mnaipa 4% ya hiyo pesa ??? huu kama si umafia ni kitu gani?? Hata mkoloni mweupe alikuwa hafanyi wizi huu

Mkiambiwa mnakuja juu ahhh! hizo ni kero za Muungano , Kwa Mtindo huu kweli vijana wameamua na msifanye mchezo

NA LIWE LIWALO MUUNGANO UTAVUNJIKA TU...

MPAKA KIELEWEKE KAMA WASEMAVYO VIJANA HAKUNA CHA KERO WALA KARA YA MUUNGANO NA MAFIA HII
 
4. Kila mtu anaelewa Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ulitiwa saini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Mjini Zanzibar Hapa nitawapa tuu ilivyokuwa kabla na kilichofuata.
Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, na Nyerere kumsaidia Karume kumshughulikia Johh Okello, Karume alikuwa bado ana wasiwasi wa kudumu kwake kama Mwenyekiti wa BLM, kwa kuzingatia Karume hakushiriki mapinduzi yale, Kiongozi wa mapinduzi alikuwa ni John Okello, Karume alikimbilia bara kujificha! (Japo ilikuja kutangazwa ati alikuwa akiwapeleka wanae Amani na Ali waliokuwa wakisoma kwao Karume (Malawi). Okelo ndie alikuwa Mwenyekiti wa BLM na alimuita Karume kuwa mtangazaji kufuatio kuwa na Kiswahili safi. Karume akamzunguka Okello na kwa kusaidiwa na Nyerere, Okello alishughulikiwa na Karume kuitwaa nafasi ya Mwenyekiti wa BLM!.Kwa vile Karume hakushiriki actively kwenye mapinduzi halisi, alikuwa na wasiwasi wakati wote kuwa wale makamanda wangemrudi!, thanks kwa ulinzi wa askari 300 wa Nyerere, vinginevyo hata hiyo 1971, asingefika!.

Mwezi Machi, 1964, Nyerere alizungumza na Karume kuhusu Muungano, Karume alikubali hapo hapo na kutaka Press Conference iitishwe siku hiyo hoyo watangaze kuwa wameshaungana na kuwa nchi moja, Nyerere Rais, Karume Makamo. Mwalimu alimgomea Karume na kumwambia afanye siri ili taratibu zifuatwe.

Mwanzoni mwa Aprili, Mwalimu alimuita AG waTanganyika, Rowland Brown na kumwambia aandae mkataba wa muungano na uwe siri. Kule Zanzibar, Karume akampa likizo AG wa Zanzibar, Wolfgang Dourado ili isitie kauzibe. Akatafutwa Mwanasheria wa Uganda, Daniel Wadada Nabudere (kakaye mwandishi mashuhuri, David Wadada Nabudere) kutoa ushauri kwa Karume kuhusu muungano.

Tarehe, 22 April, 1964 Nyerere aliyeandamana na Rashidi Kawawa, Oscar Kambona na Job Lusinde walitua ghafla Zanzibar na kwenda moja kwa moja Ikulu ya Zanzibar, wakiwa na hati za muungano na Karume alitakiwa azisaini. Wakati wa utiaji saini huo, ulishuhudiwa pia na Abdallah Kassim Hanga, Abdul-Aziz Ali Twala na Salim Rashidi.

Karume alitaka kumtumia mwanasheria huyo wa Uganda kusaini kwa niaba ya mwanasheria mkuu wa Zanzibar, ila Nabudere akakataa na kusisitiza lazima zisainiwe na Mwanasheria wa Zanzibar!. Ndipo Rowland Brown akatinga na Solicitor General wa Tanganyika, PRN Fifoot aliyesimama nafasi ya Dourado!. Hati za muungano zikasainiwa!. Baada ya hapo Nyerere na ujumbe wake wakawaa pipa lao na kurejea Dar!.

Mkumbuke mpaka Karume anasaini, hajaliambia chochote BLM, siku hiyo jioni Aboud Jumbe aliyekuwa Pemba, ndipo akaelezwa na Karume kilichotokea asubuhi, akashangaa sana!. Jambo kubwa kama hilo limefanyika vipi, BLM, hawajui kitu!.

Ni baada ya kusainiwa, Bunge la Tanganyika likatunga sheria ya Muungano, ili kuuthibitisha hati zile, 'ratification', na BLM nalo lilipaswa kukaa na kuridhia hati zile!.

Muungano Ulithibitishwa rasmi na Bunge la Tanganyika kwa kutungiwa sheria na na ikatolewa uthibitisho mwingine uliosainiwa na Fifffoot kuonyesha kuwa BLM liliketi na kuridhia, lakini kiukweli BLM halikukaa, kujadili, wala kupitisha chochote kule Zanzibar!. Kila kitu kilifanywa bara!.

Aprili 27, 1964 Nyerere na Karume, walitinga katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano zilizosainiwa na Nyerere na Karume, na documents za ratification na tangu hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Siku hiyo ya Aprili 27, 1964 ndio siku wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil. Kati yao, Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai. Baada ya hapo, Bunge la Muungano likakamata madaraka yote!.
 
Kuridhia Muungano kwa Tanganyika na Zanzibar, ratification
1. Msingi mkuu wa ratification mkataba wa muungano ni kifungu hiki kwenye hati za muungano.
Article VIII of the Articles of Union provides:" These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples Republic of Zanzibar in conjunction with the cabinet of ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of United Republic and of Zanzibar in accordance therewith2. Lengo la kifungu hicho, ni kwa vile muungano ni mkataba wa kimataifa, ili mkataba huo upate uhalali wa kisheria katika nchi husika, lazima mkataba huo uridhiwe na nchi husika, hivyo kifungu hicho kilimaanisha bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi, walipaswa waridhie mkataba huo kwa kuutungia sheria mahsusi ili kuuhalalisha kisheria ndani ya nchi zao!.

3. Baada tuu ya hati za Muungano kutiwa saini ile Aprill 22 kule Zanzibar, Mwanasheria Mkuu Tanganyika enzi hizo, Rowland Brown aliandaa ratification na kupelekwa kwenye kikao cha bunge la Tanganyika, likapitisha ratification ile asubuhi ya Aprili 26, 1964 kwa kutunga sheria No. 243 ambayo ilitangazwa kwenye gazeti la serikali ya Tanganyika, GN No. hivyo kutimiza matakwa ya kile kifungu namba viii cha mkataba wa muungano.

4. Wakati hayo yakiendelea huku Tanganyika, Zanzibar nao kupitia Mwanasheria Wake Mkuu, Wolfgang Dourado, alipaswa kuandaa hiyo sheria ya ratification kule ikiitwa Decree, ili Baraza la Mapinduzi likae na kuipitisha hivyo kuutambua rasmi muungano kisheria. Hili halikufanyika lkwa sababu Dourado alipewa likizo ya siku 7 akapumzike nje ya nchi!. Aliporudi, seven day leter, akakuta game over!. Akaishia kulalamika kichini chini maana angetoa sauti, sijui kama hata unywele ungepatikana!. Ushahidi ni kauli ya Dourado Mwenyewe "I myself have been the Zanzibar Attorney General and Minster responsible for justice between 1984 and 1989. At that time I managed to peruse all the statute books of Zanzibar from 1964 and 1979 when the Revolutionary Council was acting as a legislative Assembly cum the Cabinet. No ratification law or any law to that effect is there. I was not myopic, but even if I was, the first Attorney General of Zanzibar after the Revolution had also testified the same that no law ratifying the Articles of unionexists on the Statute Books of Zanzibar." Dourado aliyasema hayo katika andiko lake la "The Consolidation of Union" alilowasilisha kwenye semina ya Tanhanyika Law Society, Julai 7, 1983 hapa jijini Dar es Salaam.

5. Mpaka Mungu amemuita Dourado mbele ya haki, msimamo wake ulikuwa "No law ratifying the Articles of the union of 1964 exists on the statute books of Zanzibar., I as a Principal Legal adviser to the Zanzibar government was not consulted ……… Zanzibar therefore did not have legal or constitutional advice from its Principal Legal adviser."

6. Badala yake, Solicitor General wa Tanganyika, PRN Fifoot ndiye alieandaa ratification document ya Zanzíbar ambayo aliisaini yeye na kumpatia Karume ile April, 27, 1964, Karume aiwasilishe kwenye bunge la Tanganyika ile siku Nyerere na Karume walibadilishana hati pale Karimjee. Hati ya aliyoiwasilisha Nyerere was a genuine ratified document iliyokuwa ratified na bunge la Tanganyika!. Hati aliyowasilisha Karume, was a fake one as if ni BLM ndilo nalo limefanya hiyo rafication kama lilivyofanya bunge la Tangayika!, It was just a make belive, kuizuga jumuiya ya kimataifa na hapo ndipo hata hao CIA na iteligensia yao wakaingizwa chaka na kubaki kupiga tarumbeta ya ratification kuwa ilifanyika!.

7. Hata kama Fifoot aliiandaa hiyo ratification ya Zanzibar, kwa nini hakumpa Douradau naibu wake, ili aisaini na kuipitisha kwenye kikao cha BLM ili angalau ionekane ilipitishwa Zanzibar?!.Kwa vile Zanzibar hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa Bunge, Baraza la Mawaziri na Mahakama, kwanini ile ratification iliyoandaliwa bara, isipelekwe tuu na kupigwa rubber stamp kwenye BLM ili kuipa uhalali kuwa ni kweli BLM waliridhia na kuratify?!.

8. Siku ile ya April 27, 1964, wakati Nyerere na Karume walipotinga ndani ya bunge la Tanganyika, kubadilishana hati za muungano zilizo kuwa ratified,Nyerere aliwasilisha hati halali ya muungano ilikuwa ratified kihalali na bunge la Tanganyika na kutangazwa rasmi kwenye gazeti la serikali, GN lakini Karume aliwasilisha ile hati iliyosainiwa na Fifoot alijifanya Dourado na kuziwasilisha hati za muungano kwenye bunge la Tanganyika as if ni kweli BLM lilikaa likajadili na kuridhia hizo hati za muungano, na Karume sio tuu amesaini hizo ratification bila kuzipitishia BLM, bali pia amezitungia Decree na kuitangaza katika GN hiyo hiyo ya Tanganyika japo kwenye GN ya Zanzibar sheria hiyo haipo!.

9. Kisheria, kwenye sheria ya mikataba, place of contact maters much as far as domestic laws are concerned, Ule mkataba wa muungano ni international contract, unaweza kusainiwa popote ndio maana Mwalimu Nyerere na time yake, walifunga safari kwenda Zanzibar. Process ya ratification sio international contact, ni domestic contact kutumia domestic laws (municipal) ambapo ratification hupaswa kufanywa na bunge husika likiwa nchi husika. Bunge la Tanganyika lilitimiza wajibu wake hivyo ratification ya Tanganyika ni legal. Kitendo cha ratification ya Zanzibar kuandaliwa na Fifoot wa Tanganyika na kusainiwa nae, halafu Karume kukabidhiwa sheria hiyo wakati sgeria za Zanzibar kwa wakati huo zilikuwa Decrees na kuiwasilisha bunge la Tanganyika, tangazo la ratification kutolewa kwenye GN ya Tanganyika na sio ya Zanzibar, ni mambo yanaifanya hiyo ratification kuwa voidable na sio void!

10. Hoja ya "privity' to contract na "capacity" to contract pia ipo kwa Karume kama Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, alikuwa na capacity to contact kama Karume kwenye zile articles of union, lakini kwenye Ratification, Karume hakuwa na Capacity ya kusaini sheria ambayo haikutungwa na BLM, na kusainiwa na Fifoot badala ya Dourado, na sheria hiyo kutopitishwa na BLM lakini akaiwasilisha as if imeridhiwa na BLM!, na Fifoot hakuwa na capacity to contract kwa niaba ya Dourado!, tena (ninahisi Fifoot alifanya "misrepresentation kujifanya Dourado ndio maana kuna uwezekano mkubwa, Karume hakupewa tena zile original documents!, alikuja mikono mitupu, na kurudi mikono mitupu ndio kule Zanzibar, hizo documents are no where to be seen!!). Emphasis mine!
11. Hata hivyo, kuna mabishano makubwa kati wanazuoni na wasomi mbalimbali wa sheria kuhusiana na hii issue ya ratification. Mwalimu wangu, Prof. Shivji amesema japo hakuna kumbukumbu zozote kuwa BLM liliridhia, kwa vile BLM limeipitisha sheria ya muungano, huko ndiko kuridhia kwenyewe!, kwa hiyo kwa Shivji, muungano uliridhiwa!.

12. Aliyekuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kwenye BLW, Hon. Abubakar Khamis Bakary ambaye ndie aliyetoa posa ya ndoa na CCM kule BLW na kuunda SUK ambapo kama mshenga, amezawadiwa uwaziri wa sheria anapingana na Prof. Shivji kwa kusema kuwa sheria ambayo haikutungwa na BLM wala haikupitishwa na BLM, sio sheria halali kwa Zanzibar!.

13. Pamoja na Kutofautiana na Shivji kuhusu uhalali wa ratification, lakini Mhe. Bakari anakubaliana na Shivji kuwa muungano ni halali, kwa sababu, licha yakutokuwepo official ratification kutoka Zanzíbar, hakuna Wanzanzibari wowote waliochukua hatua zozote za kupinga au kulalamika, hivyo hiyo ni dalili kuwa Wanzanzibari wameukubali muungano impliedily not expressly!.

14. Mwanasheria mwingine wa Zanzibar, al maaruf, Ali Salehe, mwandishi na mtangazaji wa BBC, yeye anashikilia, kwa kwa vile muungano haukuridhiwa, lazima uridhiwe ili kuupa nguvu ya kisheria Zanzibar!. Hivyo anasema ratification ifanyike!. Na hapa ndipo na mimi niliposimamia kuwa Wanzanzibari wafanye ratification kama kweli hawautaki tena muungano, BLW likatae ku ratify ili mlango wa kutokea uwe wazi, wide open!.

15. Prof. Haroub Othman ametofautiana na Shivji kwa kusema wajumbe wawili wa BLM, Abrahman Mohamed Babu na Khamis Abudulah Ameir, walimweleza kuwa BLM walijadilili hati za muungano na kuridhia! (bila maandishi wala kumbukumbu?). Prof. Haroub anadai siku anaelezwa hayo walikuwa club ya YASU akiwa anacheza na katoto fulani ambacho kalikuwa bado hata hajabalehe, kakiitwa Ali Juma Shamhuna!.

16. Kufuatia uwepo wa document ya ratification huku bara, na Zanzibar kimataifa ilikufa rasmi siku ile ya April, 26, 1964, hakuna tena anaejali kama hizo ratification documents zili fojiwa huku bara, ndio maana hata tume ya Nyalali, ilizihalalisha na kimataifa everthing is ok na humo humo ndimo hao majasusi wa Marekani, walikolalia na wote wanaoamini muungano uliridhiwa, japo ni kweli kwa bara muungano uliridhiwa kwa kauli na matendo, kwa Zanzibar, uliridhiwa kwa kauli bila matendo!, na sasa tunasikia kauli za kupinga na matendo ya akufukuzaye!.

17. Kiukweli Karume aliliendesha BLM kibabe sana, yeye kama Rais, Jaji Mkuu na Spika, wale wote waliopingana naye, hakuna ajuaye kilichowakuta ili walishughulikiwa kimya kimya na hata miili yao haikubahatika kuonekena (inasemekana walining'inizwa jiwe shingoni na kutoswa baharini!. Kina Babu kuona hivyo, wakajitimkia zao kabla ya kuwakuta, hayajawakuta. Uvumilivu ulipowashinda waliobaki, nao wakamshughulikia Karume!. (Naamini inteligensia ya Mwalimu alishauona mwelekeo wa Karume kwenye majaaliwa ya muungano, hivyo nae akaacha ya kumkuta yamkute, muungano udumu!.

18. Baada ya Karume, Aboud Jumbe akaukwaa urais. Dourado akamjulisha Jumbe kuhusu kukosekana kwan proper ratification na iliyopelekwa UN is fake!, wakaandaa document kuujulisha ulimwengu kuhusu hilo!. Seif Sharif akamtonya Nyerere, Jumbe akashughulikiwa ipaswavyo, huku Dourado akaozea jela!. Tukatangaziwa "kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar" bila kuelezwa kisa ni absence ya proper ratification!.

19. Wanzanzibar ni watu wazito sana kujifunza, licha ya kujua kilichomkuta Jumbe kilihusu kuutishia muungano, Dr. Salmini nae akataka kucheza karata yake zile siku zake za mwisho mwisho alinukuliwa akisema, wao wanayatambua yale mambo 11 tuu ndio ya halali, hivyo akajenga hoja kubadili katiba aongeze kipindi cha tatu ili ayashughulikie!. Tiss ilimshughulikia yeye na timu yake yote wakatupwa kando!. Hamshaghai kwa nini Salmin baada ya kustaafu hakuitwa popote kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli rasmi?, na yule dada yetu naye akaporwa!.

20.Kupitia hoja hizo na nyingine ambazo sikuzitaja, Mimi Pasco wa JF, kwa Mamlaka niliopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chini ya Kifungu cha "Freedom of Expressions", Sasa Natamka Wazi kuwa Muungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar, Haukuwa Ratified Properly in Zanzibar!. Ila pia Nasisitiza, Muungano Huu ni Halali, japo ulikosa uhalali kwa njia ya Expressly in Zanzibar, umepata uhalali huo Impliedly!.
 
Acha wewe unaamini watu ambao wameandika kitabu kwa ajili ya biashara? Okello alikuwa primary school drop out hakumaliza hata darasa la nne hakujua kusoma wala kuandika. Kiswahili chenyewe kilimpiga chenga na hata kiingereza ndio kabisaa -sasa ameweza vipi kuandika kitabu au haya ndio ya elimu mpya ya mtoto kushinda mtihani wa darasa la saba lakini hajui kusoma wala kuandika..

Ila nachoweza kusema ni kwamba.. Je? unajua ya kwamba Okello alikuwa mwanachama hai wa ASP? na kama alikuwa mwanchama aliponda mawe ya kokoto huko Pemba ilikuwaje yeye ndiye awe kiongozi wa Mapinduzi bila viongozi wa ASP kujua na hata baada ya masaa 24 ya Mapinduzi, Yeye Karume na Babu waitangazie dunia kuwepo kwa serikali ya Mapinduzi? Hawa watu waliweza vipi kukutana au kuandaa utoaji habari huo ikiwa hayakuwepo maandalizi? Okello alitumiwa kwa kazi maalum yenye lawama na baada ya hapo akatemwa..

Akili za mbayuwayu mkuu wangu, changanya na za kwako mkuu wangu....

Hukunijibu hili suali! umegeuka komba kula embe hili kidogo na lile kidogo japo hana njaa lakini aharibu tu huku akirukia matawi mengine

suali:

Huo muungano uliosema wa OAU wapi umeona TRA / VAT wanakwenda asubuhi kwenye nchi wanakusanya pesa yote ya kodi jioni wanarudi Dar-salaam na vikapu vyao vya pesa. mwisho wa mwezi nchi mnaipa 4% ya hiyo pesa ??? huu kama si umafia ni kitu gani?? Hata mkoloni mweupe alikuwa hafanyi wizi huu

Mkiambiwa mnakuja juu ahhh! hizo ni kero za Muungano , Kwa Mtindo huu kweli vijana wameamua na msifanye mchezo

Tuje hapo uliporukia :

Alikuambia nani maneno hayo , Okello au baba yake Okello , kwa vile hakujua kuandika ndio serikali ikaogopa watu kuutambua ukweli ikapiga marufuku hicho kitabu???

By the way, hata Thabit Kombo hakuandika kitabu ameandikiwa , nikuulize alifika darasa la ngapi???
au kitabu chake tusikisome???

Hayo unayoyaandika umeyatoa kitabu gani ??? HAYO MAANDALIZI YALIKUWEPO ZAMANI NI KWELI NA YANAENDELEA

Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: "KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC". Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.

ANGALIA HUU MKANDA PIA

http://www.youtube.com/watch?v=XmHMwKaLSqM
 
Pasco I hope umemaliza hilo darasa ulilotutisha nalo. Kama umemaliza basi umeshindwa kabisa kuonesha kuwa BLM halikuridhia muungano. Inaonekana umetafsriri kwa Kiswahili maandishi ya watu wengine ambayo umeshindwa kuyawekea shaka ya kisomi. Umeyakubalikuwa ni kwel bila kuyahoji na kutuletea tuyaamini kuwa ni kweli.
 
Back
Top Bottom