GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Tatizo la vijana wa bodaboda ni kunywa pombe masaa yote, pombe zikifahamika kama visungura, Vijiwe ambavyo bodaboda zinapaki vijana wanakunywa pombe masaa ishirini na nne wakishushia na Mo energy.
Baada ya kushiba visungura akili za kawaida zinatoweka na sasa wanakuwa wanyama hawajali alama za barabarani, wanaendesha bodaboda kwa mbwembwe kwa kutumia mkono moja na wana overtake wapendavyo wao.
Mwaka 2019 ilitolewa hukumu mahakama ya kisutu ya kwenda jela maisha kwa vijana 8 baada ya kuchoma kituo cha polisi cha Bunju A kwa kutumia mafuta ya Petroli.
Baada ya hukumu ndani ya mahakama vijana walipiga mayowe na kugalagala chini huku familia zao na watoto nao wakipiga mayowe kwa mshindo wa vilio wa kutokuamini kama ndugu zao ndio kwaheri na mwanzo wa maisha tete kwa familia.
Bodaboda waliochoma basi la saibaba wanafahamika hapo Korogwe, Wameharibu mali za raia wasio na hatia, Wameharibu document muhimu za watu wasio na hatia waliokuwa wanasafiri na basi la Saibaba.
Tuwakumbushe vijana wa bodaboda wa hapo Korogwe na najua ni wengi na wataanza kuishi kama digidigi kwani kifungo cha miaka thelathini au maisha hakikwepeki kwao.
Yaliyotokea kwa vijana Bunju imebaki kuwa historia katika maisha yao na familia zao.
Hasira ni hasara.