Je, VAR kwenye michuano ya AFCON imeongeza au imepunguza ladha?

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,144
15,144
Wakuu nini mtazamo wako kuhusu matumizi ya VAR kwenye michuano hii ya AFCON 2023 inayoendelea. Je,unaona imeongeza ladha au imepunguza ladha ya mpira?

Screenshot_20240207-234956.jpg
 
Inategemeana na matokeo ya uamuzi yalivyo athiri timu yako.

Kama VAR kwa upande wa timu yako iliamua kitendo ambacho kilienda kuinufaisha timu yako unauoishabikia basi hapo lazima uifurahie VAR

Ila kama ndio timu yako imekuwa victim kila tukio linaloamuliwa na VAR imekuwa ikiadhibiwa basi lazima uichukie.

Ila in general VAR imekuja kuleta radha kamili ya soka, mshindi apatikane kwa njia za halali.

Japo zipo baadhi ya acts unaona haziamuliwi ipasavyo na hili sio tatizo la VAR ni yule refa anayetafsiri hilo tukio.

Ndio maana watu wanafikiria uwezekano wa kuja na mfumo wa roboti lenye AI ambalo litakuwa programmed litaweza kuamua mechi bila kuwa na mihemko.
 
AFrica ina marefa bora sana kuliko ulaya basi tu.

Hii michuano ya Afcon imenionesha hilo jambo kuanzia maamuzi ya marefa uwanjani bila Var hadi maamuzi ya marefa kwa kusaidiwa na Var.

Simaanishi hakuna mapungufu la hasha ila tupo vizuri sana tofauti na michuano mingi ya ulaya inavyochezeshwa.

Mfano hakuna ligi ulaya inaendeshwa kihuni kama Epl na wakati kuna Var lakini wale marefa hawana tofauti na wa Nbc premier league.
 
Kiukweli VAR nimeanza kuielewa sasa

Kwenye michuano hii imetumika vizuri sana kwa kufuta makosa mengi ambayo refarii na wasaidizi wake wasingeweza kuyaona bila VAR

Mfano SA vs Nija bila VAR SA alikua anaumia bao nyingi lakini VAR ikamaliza utata

Refarii pia wamekua wepesi kuomba VAR review pale wachezaji wanapo omba hivyo

So far so good
 
Back
Top Bottom