NINA IMANI
Senior Member
- Jan 8, 2014
- 113
- 15
Naomba kuuliza msimu mzuri wa kulima vitunguu maji na soko linakuwa la uhakiki ni upi? Asante.
naomba kuuliza msimu mzuri wa kulima vitunguu maji na soko linakuwa la uhakiki ni upi? Asante.
kilimomaarifa.tajiri Mungu akubariki hapa tunajifunza mengi mno na unajibu kila unachoulizwa kwa ufasaha na kwa moyo mkuu tofauti na wengine wanaouza ushauri huku JF ilhali hata unapomuuliza kitu hajibu kwa ufanisi.
naomc kuuliza hiyo AQUA STIKER HUWA INAUZWA SH NGAPI?
Prishaz
KWA MBOLEA ZA VIWANDANI, HASA WAKATI WA KUPANDIKIZA MICHE SHAMBANI
KIPIMO NI KWAMBA, ILE SIKU YA KUPANDIKIZA MICHE INATAKIWA KILA SHIMO LIPATE MLS 250 ZA MAJI YALIYOCHANGANYWA NA MBOLEA. HAYO MAJI YENYE MBOLEA NDIYO HUWA TUNAYAITA KAMA STARTER SOLUTION, HII INASAIDIA SANA KUUFANYA MMEA KUPATA STRONG SOLUTION IMMEDIATELY UNAPOKUWA TRANSPLANTED. MMEA UNAPOWEKWA KATIKA SHIMO, MAJI YA KWANZA KUNYONYWA NA MMEA YAWE NI HAYO YENYE MBOLEA.
SASA MBOLEA ZA KUPANDIA NI, DAP, NPK (17;17;17), YARA MILLER WINNER, TSP, MINJINGU MAZAO ETC, KWA HIYO UTACHUKUA GRAM 100 ZA MBOLEA MOJA WAPO (HASA NAPENDEKEZA PANDIA DAP, AU YARA MILLER WINNER) UTAYEYUSHA KATIKA MAJI LITA 20, THEN KWA KILA SHIMO UTAWEKA HIZO MLS 250 KAMA STARTER SOLUTION NDIPO UPANDIKIZE MCHE. HIVYO UNAIWEKA IN FORM OF SOLUTION SIYO KAMA
"USIFANYE KINYUME, CHA KUPANDA MCHE KWANZA NDIO UWEKE HIYO STARTER SOLUTION"
Nimeipenda hii sana huenda ikawa na matokeo ya haraka mno nina hoho zangu ziki kitaluni ntafanya hivo pia.
KIONGOZI
NTAKUELEZA ZAIDI KATIKA MATIKITI MAANA NIKO NA UZOEFU NAYO
KAMA MAZAO YOTE YANATAMBAA SI VIZURI SANA UKICHANGANYA
TIKITI,
UDONGO NA JOTO
Usiwe wa kutuamisha maji
Ukiwa Tifutifu, AU kichanga Tifutifu (Clay loam) na hali ya joto kiasi angalau 15- 35 degree inatosha sana
Linahitaji maji mengi mwanzoni lakini kadri linavyoendelea maji unapaswa kupunguza
MUDA WA KUOTA
Ukisia mbegu huchukua siku 5 hadi 10 kuota
KAMA SHAMBA LIKO TAYARI BY NOW, UKIPANDA SIKU 75 HADI 90 (AINA ZA MBEGU ZILIZOPO SOKONI KWA SASA NI HYBRID -ZEBRA, 1. SUKARI F1, 2. MSHINDI, 3. JULIANA ETC) UNAVUNA TIKITI KWA HIYO UNAMIEZI 3, OKT, NOV NA DEC WAKATI TUNAKABIA MWAKA MPYA UNAVUNA.
KWA TIKITI JITAHIDI SANA KUPANDA KWA NAFASI
KAMA UTALIMA MATUTA BASI TUTA LIWE LIMEINUKA KIASI KUJA JUU WALAU SM 20 HIVI LIWE NA UPANA WALAU WA SM 45 HADI 60, UPANDAJI, KUTOKA SHIMO HADI SHIMO SM 90 HADI 100, NA KUTOKA KATIKATI YA TUTA HADI TUTA LINGINE NI MITA 1.5=SM 150, KWA HIYO KWA MATUTA YANAYOFUATANA TIKITI ZIIKIANZA KUTAMBAAA UNAZILAZA ZINAKUTANA KATIKATI YA HIZO TUTA MBILI
KAMA UTAAMUA KUPANDA KWA MAJARUBA KAMA HAYA YA MPUNGA, AMBAPO WATU WENGI HUMWAGIA KWA KUTENGENEZA MITALO YA KIENYEJI YA UMWAGILIAJI BASI, JARUBA LAKO LINAPASWA KUWA NA UPANA WA MITA 3 NA UREFU WOWOTE ULE HATA WA MITA 5 ILI MRADI UWEZE KUMUDU KUINGIZA MAJI.
SASA KWA JARUBA TUNAPANDA PEMBENI KATIKA ANGLE HIZO. KUTOKA SHIMO HADI SHIMO NI HIZO SM 90 (=futi tatu), AMBAPO SASA YAKIAANZA KUTAMBAA UTAYALAZIA KATIKATI HAPO KATIKA HUO UPANA WA MITA 3, SO YA KULIA YATAKUJA HAPO CENTRE, YA KUSHOTO , KASK, NA KUSINI HIVYO HIVYO YANAKUJA KULALA HAPO
MBOLEA ZA KUPANDIA NI MUHIMU SANA
UKIPATA YARA MILA WINNER ( NAMBA HIZI 15:9;20 AINA YA NPK) ITAKUFAA KILA SHIMO UNALOWEKA MBEGU MOJA WEKA GRAMA 10 YA MBOLEA SWA NA KIJIKO KIMOJA KIKUBWA CHA WALI. ZITAOTA BADA YA SIKU 5 HADI 10
AFTER ONE MONTH, UTAWEKA MBOLEA YA KUKUZIA KAMA CAN AU UREA
MAUA YAKIJA JITAHIDI UPATE BOOSTER (HIZO NI MAALUMU KWA AJIRI YA MAUA NA MATUNDA
ZIPO BOOSTER ZINAITWA STAARTER- MFANO HALISI ZILIZOPO MADUKANI NI POLYFEED STARTER-HIZO HUTUMIKA KUPIGA MAUA WAKATI WA MAUA
MATUNDA YAKIJA UTAWEKA POLYFEED FINISHER-HIYO NI KUIMARAISHA MATUNDA, NA PIA UTAFUTE MBOLEA INAITWA YARA NITRABOR (HII INA Calcium na Nitrojen kwa wingi) , husaidia kuzuia tikiti kunyauka, na kuzoa katika kitako-Ugonjwa unaitwa Blosom End Rot
WAKATI WOOTE WA MAISHA YA TIKITI USISAHAU DAWA ZA WADUDU, WANAOKATA MAUA , NA KUTOBOA MATUNDA, DAWA KAMA DUDU ALL AU SELECRON, AU MATCH, AU KARATE MOJA WAPO YATOSHA KUMALIZA WADUDU
LAKINI WAKATI WA KUPIGA HIZI DAWA KUWA MAKINI SANA USIPIGE MCHANA, UTAUWA NYUKI WA KUFANYA UCHAVUSHAJI KUTOFANYIKA-HAPO UTAPATA DIFORMALITIES NYINGI SANA KAMA SHAPELESS KATIKA MATUNDA, PIGA ASUBUHI SANA AU JIONI SANAA,
PIA KAMA UTAONA KUNA HALI YA UKUNGU (UNYEVU NI MWINGI AU BARIDI USIKU AU MCHANA) NI MUHIMU KUWEKA DAWA ZA JAMII YA COPPER, KAMA BLUEE COPPER, AU EBONY KUZUIA UKUNGU,
NI MUHIMU SANA KUHAKIKISHA TIKITIKI ZAKO ZINAPATA MAJI WALAU MARA 3 KWA WIKI, ILI KUPUNGUZA WATER SRESS
GHARAMA ZA MBEGU
KWA EKARI MOJA UTAHITAJI Gram 300 za mbegu , ambapo jumla ya gharama za mbegu ni kati ya tsh 200,000 hadi tsh 300,000
MAVUNO
Kwa kuwa kwa nafasi tajwa hapo juu utakuwa na mashimo yasiyopungua katiya 2000 hadi 3000 Kwa ekari moja. Hivyo kila shimo au kila kamba ya tikiti ikikupa matikiti matatu means utakuwa na mavuno ya vichwa vya tikititi kati ya 6000 hadi 9000, ambayo ni sawa na wastani wa tani 12 hadi 18 kwa ekari moja
Karibu Kiongozi