Je unakumbuka viwanda hivi?

Kamongo

JF-Expert Member
Mar 20, 2009
1,956
2,072
Wana jf leo nataka kuwakumbusheni ya viwanda ambavyo vilifanya kazi kwa ufanisi ila vikafa kama Tameco,Ufi,ZZK,SUNGURA TEX,TANGANYIKA Packars,je tatizo lilikuwa wapi?na tunashindwa kuvifufua
 
Tatizo ni ujinga na ulimbukeni. Tulishindwa kutofautisha siasa na ufundi (technical Issues) Kila kitu kilitokana na siasa hata kama ni cha kifundi. Mfano Ajira zote hata za mainjinia zilitegemea wanasiasa waamue (Interviews ziliendeshwa na wanasiasa hata hawajaenda shule) Wanasiasa walikuwa wana sauti kubwa kuliko mainjinia na wakurugenzi. Matumizi ya mapato yalitokana na maamuzi ya wanasiasa kwanini viwanda hivyo visifikisike?
 
Inauma sana tulikuwa tunakula beef za tanganyika packers,maziwa ya Kcc,mikate ya siha,leo kila kitu china
 
Kiwanda cha Magunia (Tanzania Bag) -Moshi

Kiwanda cha Ngozi (Tanaries)- Moshi

Kiwanda cha Vipuri vya mashine (Mashine Tools)- Moshi

Kweli inasikitisha sana...! Vyote hivi vimekufa kabisa hakuna hata majengo yake tena....!
 
Hakika nikikumbuka mambo hayo huwa ninamlilia Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Alikuwa mzalendo mpenda nchi na wananchi wake. Viongozi wa sasa ni zero, hakuna kitu.
 
Hakika nikikumbuka mambo hayo huwa ninamlilia Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Alikuwa mzalendo mpenda nchi na wananchi wake. Viongozi wa sasa ni zero, hakuna kitu.

Huyo baba wa taifa alishindwa kuweka hivyo viwanda katika mfumo wa biashara, KAMA ALIVYOSEMA BABA VUNJO, alianzisha vizuri uendeshaji zero.
 
Hakika nikikumbuka mambo hayo huwa ninamlilia Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Alikuwa mzalendo mpenda nchi na wananchi wake. Viongozi wa sasa ni zero, hakuna kitu.

Hivi viwanda vilikuwa vianendshwa na walipa kodi, kila mwaka vina- Bail out na serikali, havikuleta faida kwa sababu ya ufisadi uliofanyika walikuwa wanalindwa na Mwlm Nyerere, pia uungilio wa siasa ulichangia kuuwa viwanda

Viwanda hivi vilikuwa mzigo mkubwa kwa wananchi, ilitubidi tulipe kodi ya kichwa kwa kila mtanzania ili tuweze kunusuru viwanda.
 
Hivi kipi bora KODI ya kichwa au VAT na PAYE?

Bora ingerudi hiyo then wafute VAT naamini watanzania tungekuwa na akili, kuna watu hawajuhi kuwa wanalipa kodi kupitia VAT.
 
Pamoja na maamuzi ya kisiasa, viliuawa na soko huria na menejiment za ovyo.
 
Kiwanda cha Magunia (Tanzania Bag) -Moshi

Kiwanda cha Ngozi (Tanaries)- Moshi

Kiwanda cha Vipuri vya mashine (Mashine Tools)- Moshi

Kweli inasikitisha sana...! Vyote hivi vimekufa kabisa hakuna hata majengo yake tena....!

mkuu hapo kwenye red umenigusa....... yaani kile kiwanda si mchezo...... halafu nikwambie...... kile kiwanda Mwalimu JKN alipewa zawadi personally... lakini kwa uzalendo wake alikifanya ni cha taifa...., je angepewa EL ingekuaje

Way forward

mimi nashauri serikali ambayo ni makini na inapenda maendeleo ivifufue hivyo viwanda through a modality known as native empowerment (hii ni trade mark yangu) south africa wanayo black empowerment.... yaani tunatafuta watanzania wazalendo waaminifu na wachapakazi tunawawezesha na kuwapa udhamini kwenye financial institution .... pia tunawapa mikataba na masharti makali..... halafu tunawapa viwanda hivi waviendeshe na faida wanayopata watachangia huduma za afya na elimu..... ajira zitapatikana na kodi za nchi watalipa...... nchi itakwamuka na hiyo itakua ni endelevu pamoja na kuanzisha viwanda vingine vipya through transfer of technology mechanism
 
Wana jf leo nataka kuwakumbusheni ya viwanda ambavyo vilifanya kazi kwa ufanisi ila vikafa kama Tameco,Ufi,ZZK,SUNGURA TEX,TANGANYIKA Packars,je tatizo lilikuwa wapi?na tunashindwa kuvifufua

Nafikiri suala la msingi hapa ni kuvifufua kwani vingine vimegeuzwa kuwa nyumba za popo na vijiwe vya wavuta bangi.

Mfano pale kibaha , sijui kile kiwanda cha TANITA ( kiwanda cha korosho) sasa hivi wakubwa wanafikiria nini.

TAMCO kiwanda cha ku-assemble SCANIA , wale jamaa walikuwa wanaagiza vipuri na wana-assemble pale njia panda ya kuelekea SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA , naona siku hizi kuna tapeli mmoja pale TAMCO , lk siyo ile TAMCO ya zamani. Halafu kitu cha ajabu ni kuwa ile Mgt ya TAMCO walikuwepo wa-nordic pale sijui what went wrong

SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA limedumaa , basi ni matatizo juu ya matatizo...
 
Back
Top Bottom