Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Bubu Msema Hovyo, kisa chako ni kizito na kimenigusa sana . . .

I am starting to think sijui tuandike kitabu cha "VISA VYA JKT" . . . very interesting
Ilikuwa operation vyama vingi,tulikuwa pamoja mkuu,huyo Sgt mlimbila alikuwa akiwaingilia makuruta na wake Wa mastaff kimiujiza,
 
Mkuu sijakupata, unatunyima raha, kama ni blue print fafanua kwa lugha ya uungwana tuelewe.

Umenikumbusha mambo ya kuoga na Mestin pale maji yanapokosekana na bado unatakiwa utakate. Ni kweli watu hawakuwa na aibu ya utupu.

Siku moja kamanda moja mwenye nyota mbili sikumbuki jina, alikuwa na binocular wakati tunakata kuni. Akaniambia " Kijana tunajua mambo mengi sana mnayo fanya ila tunamezea wakati mwingine" nilipomwuliza kwa nini akanipa binocular na kulielekeza wapi niangalie, huwezi amini, kulikuwa na askari kuruta wa jeshi wa kike na kiume wakifanya kamchezo kabaya . . . baada ya kukata kuni. Du, nilibaki hoi sana
Duh sina mbavu!
 
Dah nakumbuka 841kj pale mafinga .... Jkt ya zaman ilikuwa na mafunzo mazur sana... Sitawasahau makamanda hawa. Lt nkya, Lt liundi, Lt alloys, na wiliam Sagala... Mpaka leo nina alama mgongon na mkono wa kushoto... Nilichimba handak kwa sahan na panga
umenikumbusha mbali nkya na alloys ni noma hasa kipindi cha pori mlima nguruwe na kuzima moto msitu sao hill
 
Mim sitasahau jkt .nakumbuka nilijiunga jkt nikapangwa jkt mgambo kabuku 835kj ilikuwa noma sana sitaweza kumsajau capt laiza alikuwa akionekana kombania watu wanalia hata bado mazoez hajatoa.nakumbuka siku moja kulikuwa na mvua sana usiku wakat wa mkesha makamanda wa E coy na F coy waliungana wakatufanyia kitu ambacho hadi leo ninapokumbuka nakuwa mpole sana walikuwa na upupu wakaumwaka lile eneo tunalofanya mazoez wakawa wa wanatuambia tulale chin na stik nyingi tu roll zile tope zilikuwa zinawasha sana tulijikuna sana hadi asubuhi ule usiku ulikuwa wa mateso coz uwasho na stick za kutosha.sitaweza kusahau jkt(mwana ukome)
 
Mim sitasahau jkt .nakumbuka nilijiunga jkt nikapangwa jkt mgambo kabuku 835kj ilikuwa noma sana sitaweza kumsajau capt laiza alikuwa akionekana kombania watu wanalia hata bado mazoez hajatoa.nakumbuka siku moja kulikuwa na mvua sana usiku wakat wa mkesha makamanda wa E coy na F coy waliungana wakatufanyia kitu ambacho hadi leo ninapokumbuka nakuwa mpole sana walikuwa na upupu wakaumwaka lile eneo tunalofanya mazoez wakawa wa wanatuambia tulale chin na stik nyingi tu roll zile tope zilikuwa zinawasha sana tulijikuna sana hadi asubuhi ule usiku ulikuwa wa mateso coz uwasho na stick za kutosha.sitaweza kusahau jkt(mwana ukome)
Dah poleni sana mkuu,lile eneo la E coy na F coy nalikumbuka sana lilivyokuwa lipo hovyo mno.Mimi nilikuwa B coy ila wale wa E na F coy tulikuwa tunawaonea sana huruma.Mimi nilipita juzi juzi tu sio miaka mingi
 
Dah! umenikumbusha mbali sana mkuu..1991/92 op. vyama vingi..Makutupora A-coy tulipangwa kumwagilia bustan.. Lakini baadae tukahamishiwa Bulombora, D-coy. Namkumbuka afande Mnzena, Mtekere, afande Sezero, coplo Ngoma, afande Mbewa na afande machachali mikwara mingii Stanslaus Makoba ''kadebra'' baiskeli yake iliandikwa ''sereuka mwana wa ndege..mnafiki hakosi sababu'' Kombania hii kulikuwa na vijana akina Robert Nyamhanga, Prudence Timanywa, Mongu Manumbu, Mpemba Francis, Safari Lucian, Redemtus Shoto, Privatus,Anterius Sostenes, Joe Kihampa (TBC1) na wengine. Akina dada kulikuwa na Kore Ally Sadick, Rose Manyama, Judith Schirima, na wengine wengi. Nakumbuka umoja, ushirikiano wa kusaidiana kuepuka visanga baina ya makuruta nk. Siku tukipokea ''kichele'' tulikuwa tunakwenda kijiji cha Kaseke kutumia. -J4 wa D-coy
Kaka usipasahau na muyobozi au ilagala gerezani

Sent from mTalk
 
Naona Mlale tupo wachache sana huku ww utakua mtoto wa Mpuku.hahahaa
Tupo Mlale Tupo. Afande Nguvu ya Nyani, Rweikiza. Sabuni, Mande, Chuma, Matron Grace na MWajuma Magagula na Lusonga sitaenda tena. Maafande wa Mlale watanisurubu! Dah Shamba la Embakasi. Ukarimu wa Wangoni watani zangu! Jamani ni kumbukumbu nzuri. Wimbo wangu daima ulikuwa ' Nimeuona mpilipili na maua yake nselema......' Ile nyumba ya mbao iliyokuwa ikihamishwa na Kuruta Dah!
 
Nawakumbuka makuruta wen zangu Itende JKT kina Calman Mkenda, Eliasi Ndutu,Mapinduzi Mwawalo, Anatalia Luwungo, Mpendwa Chitegile,Predikanda Chandalala,na wengineo wengi, lakini tulikuwa na kina Afande James,CO wetu kipindi hicho alikuwa Afande Martin Madatta, na II I/C wake ail kuwa Marehemu Major Mande, Adjutant ails kuwa Afande Mrope, na Mp Comander alikuwa Juma Ing'aa Kama sijakosea. Hakika maisha hale yalikuwa Matamu balaa japo ili kuwa ni Operasheni Oljoro
 
1989/90 program ya chama Nilianzia Mlalakua nikapigwa bogi kwenda D-tach mbweni nikawa kitengo cha kuziba masufuria na upishi maharaghwe hayanachumvi baadae nikahamishiwa Mlale JKT kwa kanali Mtono (RIP) combania C chini ya Afande Meja Mwankina, Nguvu ya Nyani, Pilato, kashumba, makala..........kuna mengi ya kukumbuka nilianza kitengo cha Bustani, kufatua matofali ya udongo kila siku mtu mmoja ufyatue matofali 2500 makumbuka kuna siku Mtono alikuja kwenye kitengo chetu akayakanyaga matofali kama 200 akisema siyo mazuri hivyo niyarudie nilisimamaa nikamwangalia kwa uchungu na hasira lakini sikuwa na la kufanya zaidi ya ndiyo afande baadaye nikapelekwa kuchoma mkaa pembezoni mwa mlima Renji kuelekea Mlandizi sikukaa sana kwenye Mtaa nikapelekwa kwenda kuanzisha shamba jipya LINDIPUNDIPU aaaha kule kazi ilikuwa pevu kwani vitanda vilikuwa chanja tulizotandika nyasi juu yake ilikuwa ni shida watu waliumwa huko balaa.........kulikuwa na rafiki yangu mmoja alikuwa na YG wake ambaye CO alikuwa anavunjanae murua wa jeshi....akapanga aende nae Mjini Songea ndipo mimi na rafiki yangu pamoja ma msichana mmoja kukapelekwa D-tachi ya matarawe (sabasaba) pamoja na mali ya Mzee wale wasichana waliondoka na CO kwenye Maruti sisi tulifuata kesho yake na Isuzu ya jeshi baada ya Order kuletwa shambani........Tulienjoy sana D-tach kwani tuliletewa Paja la ng'ombe watu wanne tu na tulikuwa tunapika wenyewe tukawa tunakata nyama tuaenda kuuza kwenye bar.....baada ya week tatu tukarudi kikosini..........Nimekumiss Mlale, Chipole ,magagura, lusonga, Usiku nilikuwa nawauzia mihogo ya kuchemsha kwenye mahanga wakati nipo kitengo cha matofali nilikuwa tunaiita Meno ya Tembo.........
 
Tupo Mlale Tupo. Afande Nguvu ya Nyani, Rweikiza. Sabuni, Mande, Chuma, Matron Grace na MWajuma Magagula na Lusonga sitaenda tena. Maafande wa Mlale watanisurubu! Dah Shamba la Embakasi. Ukarimu wa Wangoni watani zangu! Jamani ni kumbukumbu nzuri. Wimbo wangu daima ulikuwa ' Nimeuona mpilipili na maua yake nselema......' Ile nyumba ya mbao iliyokuwa ikihamishwa na Kuruta Dah!
Nguvu ya Nyani ( mwaliko) anapanda juu ya Mti asome namba ya kiatu wakati wa kwata......Msambaa yule.....Matron Grace alikuwa Mzuri kweli....... 1989/90 Program ya Chama
 
Nguvu ya Nyani ( mwaliko) anapanda juu ya Mti asome namba ya kiatu wakati wa kwata......Msambaa yule.....Matron Grace alikuwa Mzuri kweli....... 1989/90 Program ya Chama
Wow Sawa kabisa sawa kabisa! Yaani I wish kama tungekutana woooote tuliopitia Mlale na Maafande wetu. Dah Nguvu ya Nyani atakuwa Mtu mzima sana sasa na Grace naam She was Beautiful and Humble!
 
Nimefurahishwa sana niliposikia umoja wa wana jkt 833KJ oljoro operesheni miaka 30.A uhuru,hawa jamaa wamejipanga na kuunda umoja wao walifany bonge la get together party pale leaders.Naomba mwenye contacts zao nasi tuweze kuandaa kama wao.Wanasaidiana sana
 
Kwa kweli nimesisimka sana kwa yote; kwani limepelekwa mbali sana na kila mchangiaji.

Mimi nilianzia mgombo-kabuku tanga na kumalizia maramba; 1989\90.lamsingi kwa wadau wote ili historia isipotee; ni vyema ifanyike documentation na hatimaye itayarishwe video series\film.
Hapo tutakuwa tumejitendea haki wadau wote na jkt kwa ujumla.

Napendekeza iundwe team ya kukusanya matukio na habari zote zilizotokea; ili iandikwe healthy script itakayotoa best and exciting picture of what really happened in those camps.

Duh, nilikuwa Mgambo JKT operesheni Nidhamu 1986/87 Kombania C kombania ya demo. Kabla sijaripoti pale ilikuwa nimepangwa kwenda Masange Tabora lakini ajabu siku mbili mfululizo train haikupita pale Korogwe station kumbuka tulikuwa tunapewa hati za kusafiria bure ikiitwa warrant.

Sasa siku ya pili nilikuwa na baba mzazi akatokea afande na kutuchangamkia ile mzee kusema tumekosa usafiri yule afande akaunganisha kuniambia njoo Mgambo kila kitu kipo kama ulaya nikakubali. Walitupokea kwa ukarimu na upole sana nadhani kwa kuona watu wengi walikuwa wanatoroka. Lakini lo mafunzo yalipofunguliwa ndipo tulipogundua jeshi siyo mchezomchezo.
Kisa kimoja kidogo ntakieleza hapa siku ya pili kambini tulipelekwa kusomba tofari na maji katika ndoo, sasa kuna kuruta raia mwenye asili ya kihindi alibandikwa ndoo ya maji kichwani, ilikuwa shida yaani ni kutetemeka na kuyumbayumba, basi afande akamkemea na kumwambia wewe kesho utatoroka, na kweli jamaa siku ya pili hatukumuona tena.
Kuna mikasa mingi sana fikiria ilikuwa ni mwaka mmoja siyo mchezo. Hata hivyo sijutii kupitia JKT kuna mengi yametujenga kuwa hivi tulivyo.
 
binafsi nakumbuka sana nkiwa 834kj makutupora jkt operesheni kikwete awamu ya tatu mwaka 2015 tulikamatwa usiku tukiwa tumelala hangani wenzetu wakiwa mkesha kiukweli doso tulilopewa na ma MP kila nkikumbuka huwa naumia roho kuna wenzetu baadhi walilazwa
 
Nakumbuka tulikuwa tunabeba matofali baada ya kutoka shambani,njaa ilikuwa inauma sana, na muda wa kula ulipitiliza sana,mmoja wetu akaamua kuanzisha wimbo fulani wa FRELIMO ambao wote tunaitikia,wimbo ni wa huzuni sana.
Yule afande nae akahuzunika sana,hivyo basi akapiga marufuku mtu yeyote kuimba.Haikusaidia wimbo ukaanzishwa na wote wakaitikia huku tofali zinabebwa na muda ushakuwa kiza.
Afande akawaka tukapewa adhabu mchanganyiko,halafu tukarudishwa kubeba matofali,tulipoanza kubeba tu daah wimbo ukaanzishwa na wooote tukaitikia afande akawaka hasira balaa,ikapigwa kipenga,wakaja maafande wengine tukapewa adhabu hapo ishakuwa usiku hasa,kisha tukarudishwa kubeba matofali aisee wimbo ukaanzishwa tena na safari hii alianzisha mwanamke na watu wakaitikia huku wanalia na tofali zinabebwa........
.........daah itaendelea.......
 
Back
Top Bottom