Je, unakijua kikosi cha KM?

maishapopote

JF-Expert Member
May 28, 2009
3,278
5,518
View attachment 142139

Wadau kuna vikosi vingi hapa nchini vya usalama wa wananchi,viongozi na Taifa ambavyo havijulikani kabisa kwa wananchi,sasa nimeamua kwa mtiririko kama wa series nitakua nakuja na kikosi kimoja kimoja kwa nia ya kuwafahamisha ili wakati mwingine tuwe na uelewa kidogo kuhusu usalama wetu,viongozi wetu,na nchi yetu kwa ujumla...na leo nawaletea kikosi cha KM maana yake Kikosi maalumu cha jeshi la magereza....

Kikosi cha KM kama ilivyoainishwa ni kikosi cha jeshi la magereza ambacho hutumika kutuliza fujo na kazi maalumu za jeshi la megereza kwenye magereza zote hapa nchini,Kikosi hichi kinaundwa na vijana shupavu wenye urefu usiopungua futi sita na lazima uwe na miraba minne,mavazi yao yanajumuisha ngao,nguo ngumu kwa ajili ya kujikinga na mabuti magumu sana yenye chuma kwa mbele.

utendaji wa KM ni wa ajabu sana,kwa mfano ikajulikana na mkuu wa gereza kuwa kuna watu wanataka kuanzisha fujo ya jumla gerezani? hii huwa inajumuisha wafungwa wengi sana,au kuna wafungwa wanapanga kutoroka kwa kutumia nguvu mkuu wa gereza hatawaambia kitu lakini siku hiyo mtakapofunguliwa milango ya sero zenu ili muende kazini hapo ndo ghafla mtakutana na KM mbele yenu,kwa idadi ya kutosha na hamtaona askari hata mmoja wa magereza mliemzoea,halafu wao watawatangazia kua mvue nguo zote na wao huanza kichapo cha kufa mtu bila kuwaambia sababu,mtapigwa kinyama sana hadi mtalainika tu halafu ndio wanaweza kuanza kuwahoji mkiwa hoi kabisa.

KM wanaogopeka kwasababu ni wakatili sana,utendaji wao ni wa kikatili zaidi ya field force,wao hawaogopi kitu maana kule gerezani haki ni ndogo mno,KM wengi wanavuta bhangi na wanalipwa mshara kidogo sana,na mara nyingi hawana kazi yoyote,ni hao tu wafungwa wakorofi wanaowaogopa tu! na nia hao tu ambao wana uwezo wa kutuliza ghasia kubwa kabisa gerezani.

sio kila gereza lina KM,mara nyingi vikosi vyao vipo sehemu zenye magereza makubwa tu lkn hupelekwa kwenye magereza madogo kama kukiwa na matatizo kama niliyoyasema hapo juu,kitu kimoja ambacho ukimuuliza mfungwa yeyote kuhusu KM atakujibu ni kwamba hao ni wanyama na sio binadamu,na wanawaogopa sana.

ukiwa mfungwa mkorofi,utapangiwa kwenda kufanya kazi katika kikosi cha KM kwa maana kambini kwao,maana wana kambi tofauti,hilo tu ni adhabu tosha kwa mfungwa na niamini hakuna mfungwa anaetaka mazoea na KM kwa namna ya aina yoyote ile.KM ni hatari kwa mfungwa kuliko mfungwa mwenzake hatari......

kama kuna maswali au una unachotaka kuongezea unaweza,na kesho kama sitabanwa nitawaletea habari kuhusu kikosi cha upelelezi cha jeshi( military inteligency agency) ambacho kipo Lugalo

Shukrani!
 
Kikosi cha KM kwa picha hiki hapa wadau

KM.jpg
 
Back
Top Bottom