w0rM
Member
- May 3, 2011
- 68
- 164
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema katika Ibara ya 1 inaeleza wazi kuwa Tanzania ni Nchi Moja na ni Jamhuri ya Muungano. Katika Ibara ya 2 (1) Katiba hiyo inaeleza wazi kuwa eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar.
1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
2. (1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
Kutokana na hapo ionaonesha wazi kuwa Nchi ni moja inayoitwa Tanzania ila ina muunganiko kwa Tanzania Bara (Tanganyika) na Tanzania Zanzibar (Zanzibar). Haijaeeleza kama Tanzania Bara au Zanzibar Bara zikiwa zenyewe zinatambulika kama Nchi
Lakini wakati huo huo, Katiba ya Zanzibar inatambua Zanzibar yenyewe kama Nchi na Tanzania yenyewe kama Nchi. Katika Ibara ya kwanza imeitambua Zanzibar kama Nchi lakini katika Ibara ya 2 Katiba ya Zanzibar imesema Tanzania imeundwa na Nchi mbili, Zanzibar ikiwa ni miongoni mwao
1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
2. Zanzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Je, Katiba hizi zinapingana zenyewe? Ipi inapaswa kufuatwa? Au ndio kwa sababu Katiba ya Jamhuri haijasema kwamba Zanzibar sio nchi basi tunafuata ya Katiba ya Zanznibar?