Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Kwann ukiwa katika hali ngumu watu wansajiweka mbal nawe? na wanajisogeza kwa yule alie vizuri kiuchumi,kimaisha etc..
Binaadam tutaacha lini huu unafki?
Mi nshaapa hakyamama siku mtu anikute nashine mwenye pesa asijisogeze kwangu..

Wasamehe banaa. But indeed inabidi kuwa makini na watu wanaoitwa marafiki
 
Ndugu, ni vigumu sana kuelewa ninayopitia. Na kile ninachopata baada ya maombi.

Bila kufanya hivi , tayari ningekuwa nimeishajinyonga zamani au kufa.

Last week nilipata attack nikiwa bafuni naoga, nilianguka ghafla...damu zilitoka nyingi sana... ( nakumbuka , mchana yake kuna mtu alinitamkia atanifanya kitu kibaya - jioni nikapatwa na hali hii)
ecc23a8c060db886933b6764fb298519.jpg


Ni watu wachache sana wakianguka bafuni kama nilivyoanguka wanapona. Mara nyingi huwa wanapata stroke au kufa.

Nimenusurika kufa mara nyingi sana Ndugu. Huwezi kunielewa kwa kusoma hapa.
Mungu akusaidie tu, there is no way unaweza kumuacha. Endelea kupambana. Lakini pia unapopita katika wakati kama huu ni vema ukaweka mapenzi yako pembeni na kumuuliza nini mapenzi yake au anataka ufanye nini.

Kuna watu wanapitia magumu kama vile Yona, unajikuta umemezwa na Samaki kwasababu umekataa kusudi la Mungu analotaka kukutumia. All in All Mungu akusaidie.
 
Unakua huna hela kiasi kwamba hata ukikwea daladala na kumuona konda ana mihela ile unatamani kumnyang'anya.

Enzi za chuo hii ilintokea sana maana safari ya kutoka Udsm hadi Mabibo kwa miguu si ya kitoto, halaf ukifika hostel wachanganya Maji na sukari unakandamiza kitu cha mkate. Umasikin ni kitu cha kulaani sana jaman
Unakua huna hela kiasi kwamba hata ukikwea daladala na kumuona konda ana mihela ile unatamani kumnyang'anya.

Enzi za chuo hii ilintokea sana maana safari ya kutoka Udsm hadi Mabibo kwa miguu si ya kitoto, halaf ukifika hostel wachanganya Maji na sukari unakandamiza kitu cha mkate. Umasikin ni kitu cha kulaani sana jaman

jamani jamani jamani,, hapo mabibo to UD ni mbali kweli kiasi unasema ulipitia wakati mgumu??

anyway inategemea ulikulia malezi gani, inawezekana ulianzia familia ya mboga saba
 
Mkuu unaijua njaa lakini? Hapo umetoka lecture choka mbaya, jua na joto la dar walijua kiongozi? Jumlisha na stress duuuuh
jamani jamani jamani,, hapo mabibo to UD ni mbali kweli kiasi unasema ulipitia wakati mgumu??

anyway inategemea ulikulia malezi gani, inawezekana ulianzia familia ya mboga saba
 
Maisha ni kama chakula leo ugali kesho wali, ndizi ,makande,pilau, mihogo, baga na maisha bila changamoto ni sawa na kula chakula cha aina moja kila siku lazima utakichoka hivyo changamoto huongeza ladha ya maisha ndg zangu hakuna aliezaliwa na mali wote tumezaliwa hatuna hata chupi kikubwa hautakiwi kukata tamaa, kuwa mnyonge na wala kuendekeza shida kiasili shida tumeumbwa nazo haziepukiki so usipate presha na kujiona unazo peke yako. Pambana kadri uwezavyo utimize malengo yako usitegeme msaada wala huruma ya mtu utalemaa.
 
aca657e5d4dab19132bab5158b47f679.jpg

Hapa nina maanisha kufirisika/kufulia kukosa uhakika wakupata angalau chai kwa siku kutengwa na ndugu. Kukosa kazi muda mrefu, kuugua na watu kukutenga, kukosa kodi ya nyumba/mahali pa kulala, kusingiziwa kwamba hutafuti kazi au kusemwa umelogwa ndugu kusema una laana.Kukatishwa tamaa kwamba Mungu kakuacha,kwamba unasali uongo
kudharauliwa na mambo kama hayo.

Je uliweza vipi kuchomoka katika hali hiyo?
Kupitia maisha magumu ni bahati ndg zangu binaadam wengi hawajapitia hiyo mi naifananisha elimu adimu sana ambayo unapata kufahamu roho za binaadam wenzako na kukufunza jambo kubwa ambalo litakua dira ya maisha yako na unaweza kwenda kuishi popote bila matatizo tumeona wengi waliokulia maisha ya kishua leo mwisho wao umekua m bovu kutokana na kukosa hii elimu, usiichukie changamoto mungu anaweza akakupa na ndiyo ikawa njia ya mafanikio yako..
 
Kuna watu wanatake advantage hivyo wanajaza thread kwa vihadithi vyao. Huwa najiuliza, kuwa kiongozi ni lazima utoe motivation speech? kwasababu kibaiolojia pale unachocheza nacho ni Adrenalin tu.

Shida ni kwa kila mtu, ila haimaanishi kila shida ni kubwa kuliko ingine. Mimi nimeshawahi kupresent ushuhuda wangu humu jamvini kupitis IDs tofauti na kwa maneno tofauti, kila aliyecomment alihitimisha kuwa mimi ni "Surviver". Inamaanisha shida sio shida kubwa hadti tu pale inapohatarisha uhai wako kwa miaka mingi mfulizo...hivyo wewe utaitwa survivor.

Wengi humu mmezaliws kwenye familia za wazazi wote wa pande mbili, umaskini wa familia yenu uliyopelekea kukuza kwa shida haumaanishi kuwa wewe umepitia shida, unamaanisha umekulia tu kwenye hali duni iliyopelekea iwe vigumu kufanikiwa kwenye mambo mbalimbali ya kawaida kama vile ajira, mahusiano au uchumi.

Tuulizeni tuliopitia shida.
Mkuu pole sana
umeeleza vyema sana
Tofauti kati ya shida na hali duni
 
The world is not fair!!
Ila jamani usiombe kufilisika tena bora ubaki na huo umaskini wako uliozoea kuliko kuzishika afu zikaja kupeperuka utajuta!
Kuna watu tulichezea maisha hii nchi hii ilifikia mtu akilalamika hali ngumu ya maisha unamshangaa huyu jamaa niaje!
ila sasa ndo unaona kwann hali ni tete asubuhi unajibonda mihogo unavuta ndefu hadi usiku unajibonda ugali kachumbari unalala lazma uombe kifo
daah!acha kabisa!!
mi hata sisemi yaani!
maisha niliyoyapitia hapo kati!only God knows!!
Naomba Mungu yasijirudie kwa kweli maana nusu nichizike!
Aiseeh!siongei mengi kwa Leo!
 
daah!acha kabisa!!
mi hata sisemi yaani!
maisha niliyoyapitia hapo kati!only God knows!!
Naomba Mungu yasijirudie kwa kweli maana nusu nichizike!
Aiseeh!siongei mengi kwa Leo!
Maisha bana yakikugeuka unaweza kuokota makopo.me toka january mwaka huu niliachishwa kazi dahhh we acha tu nilikuwa kibonge cha mtu sshv nimebaki skeleton
 
Yan hizo zote nimeshazipitia siwez kuja kusahau kwenye maisha yangu kabisa nilala chin kwa kulalia nguo zangu na kula mkate kama chakula kwa muda wa wiki nzima. Kuna wakati nilitaman kujiua niliumwa vibaya sana halafu hakuna mtu sio rafik wala ndugu anayekupa ushirikiano wa dhati. Oh MGD sitak kukumbuka kabisa.
acha kabisa!!!Haya maisha mpk unamuuliza Mungu uliniumba ili niteseke au?!
unakaaa usiku mpk kunakucha usingizi hauji na unatamani kusikuche!
Ndugu wanakudharau mpk watoto wadogo mnoo!!
yaani jamani nyie!
 
Maisha bana yakikugeuka unaweza kuokota makopo.me toka january mwaka huu niliachishwa kazi dahhh we acha tu nilikuwa kibonge cha mtu sshv nimebaki skeleton
yaani tena hata chizi ana afadhali!
pole sana hapo sasa kwenye shida ndo pakujua rafiki wa kweli ni yupi!
nimesuffer sana na life but thnx to lord nlisimama imara mpk sasa yaani naomba Mungu nisirudi kule!
 
UMENIKUMBUSHA MBALI SANA.
Nimezaliwa katika kijiji kimoja kinaitwa Kayombo, huko Bukene, Nzega, Tabora. Nilipitia maisha magumu kwa kweli, lakini tu niseme kwamba, yawezekana mimi sikupita maisha magumu, bali wapo wengi ambao pengine walipitia magumu zaidi yangu.

Nilikuwa napenda kusoma toka nikiwa shule ya msingi, na aidha kwa mipango ya Mungu, ama kutamani niwe kama wengine, nilikuwa na ndoto kubwa sana siku moja niwe mmoja kati ya wasomi nchini, japo sikujua msomi katika kitivo gani, ila tu nilichokuwa nakijua ilikuwa tu siku moja nami niitwe msomi. Nakumbuka mwalimu wangu nikiwa darasa la tano, aliniuliza swali, ningependa kuwa nani maishani. Nilichomjibu ni kwamba, 'nataka kuwa waziri' wala uwaziri wenyewe sikujua maana yake.

Nilikuwa nikiishi na mama yangu kipenzi, na nikiwa kama mtoto wa kiume pekee na wa mwisho kati ya watoto wengine saba, nyumbani mimi ndiye nilikuwa faraja ya mama, kazi zote za kiume mimi ndo nilikuwa wa kuzifanya kutokana na ukweli kwamba, baba alifariki dunia nikiwa na umri wa miaka mitatu, kwa mujibu wa maelezo ya mama yangu.

Kutokana na familia yangu kutokuwa na uwezo wa kutosha, niliingizwa katika shirika moja la WORLDVISION INTERNATIONAL, shirika ambalo silipendi kama nisivyompenda shetani katika maisha yangu, kama mtoto mfadhiliwa aishie katika mazingira magumu, na nilikuwa mmoja kati ya watoto wanne tarafa ya Bukene tuliochaguliwa kuliwakilisha shirika hilo kwenye maombolezo ya MTOTO WA AFRIKA mkoani Shinyanga mwaka 2005, sherehe ambayo hufanyika kila siku ya Tarehe 16 June, safari ambayo huwa naisemea kama safari iliyofungua ukurasa mpya katika maisha yangu.

Nilifanikiwa kumaliza elimu ya msingi na kufaulu kwa ufaulu mkubwa tu (alama 213/250), nikapangiwa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule moja ya kata, karibu kabisa na nyumbani. Maisha nyumbani kiukweli yalikuwa magumu, maana nililazimika kujishugulisha na kazi anuai ambazo kwa namna moja, ama nyingine zilitakiwa zinipatie kipato ambacho angalau ningeweza kununua mahitaji nyumbani na kununua nguo zangu pamoja na ada, na moja kati ya kazi nilizozipa kipaumbele ilikuwa ni kukata na kuchoma mkaa.

Kama nilivyosema hapo juu kwamba, kati ya mashirika ambayo sipendi hata kuyasikia ni WORLDVISION INTERNATIONAL, na hapa sintozungumza ni kwa sababu gani, nitatoa mawasiliano ili nipate kukupatia kitabu changu kinachokwenda kwa jina la A SPITTING COBRA, nilichokiandika si punde, kwa muktadha wa riwaya ya wasifu (AUTOBIGRAPHICAL NOVEL).

MAISHA MAGUMU AMBAYO SINTOYASAHAU.


Kama mada tajwa juu, maisha magumu niliyopitia ambao unaweza kuyasoma pia katika kitabu changu, ni pale nilipokuwa kidato cha kwanza, nilikutana na kesi nikiwa na rafiki yangu, kuwa tumefanya mapenzi mchana kweupe, na kupewa suspension ya wiki mbili na kuripoti na wazazi. Niliamua kuondoka nyumbani nikiwa nimekata tamaa kabisa ya kusoma tena. Najua wengi watajiuliza, 'suspension ya wiki moja tu ndiyo ilinifanya niondoke nyumbani na kukata tamaa kiasi hicho!'. Mengi utayasoma kwenye kitabu hicho ikiwa ni pamoja na swali hili, lakini tu kwa ufupi ni kwamba, nilamua kutoroka nyumbani na kukimbilia mkoa jirani wa Shinyanga, ambapo wala sikujua naenda kufikia wapi, ila tu nachoweza kusema ni kwamba, ilinibidi nilipofika Shinyanga kulala nje na nililala kama siku tatu, nikiwa na machokoraa wengine.

Ndipo nilipopata msamalia na kuhifadhi kwake na kunifanya kama sehemu ya familia yake. Mengi nimeyapitia ambayo ningependa ku-share jamvini ili tujifunze kitu, lakini niseme, fuatilia kitabu changu cha A SPITTING COBRA, na kupata copy yake, niandikie pepe anwani hujumasr@gmail.com au kwa simu nambari +255 785 777 710, nitakupatia copy hiyo.

Kwa sasa nipo chuo kikuu cha Dodoma, nasoma shahada ya Elimu katika sanaa ( Bachelor of Education in Arts (Linguistics).

Nikisema maisha magumu, simaanishi kwamba nimeyasoma kwenye kitabu, bali nimeyaishi.
Hongerah sana mimi mmojawapo ntahitaji hicho kitabu. Kitu nilichojifunza watoto hawa wa mitaani wengi wao ni intelligent! Kwani najaribu kuwaza utaondokaje nyumbani na kwenda kuishi mitaani ukiwa mtoto mdogo bila akili ya ziada ya kuweza kuishi? Basi niishie hapo kwani mengine nitayapata kwenye kitabu! Historia kama hizi zitapunguza hata unyanyapaa kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Ni jukumu la serkali na jamii kusaidia ili kusiwe na vulnerable kids, elimu bure ni njia mojawapo.
Ushauri kwa mara nyingine kwa Mheshimiwa Rais vunja wizara ya Afya na hii ya ustawi wa jamii ( hii ishughulikie masuaaya jinsia, wanawake na vijana ( kuwaanzishia ujasiriamali), wazee na walemavu iwe na wizara yake inayojitegemea as Wizara ya Afya kwa changamoto zake pia ibaki ikijitegemea. Ukitaka watendaji wa hii wizara inayohusu Ustawi wa jamii wakereketwa tupo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom