Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Aisee sikia kwa mtu tu yasikupate wewe!

Nakumbuka mwaka 2013 ulikuwa kama mwaka wa mikosi kwangu,mwaka huo nilikuwa nauguza baba yangu miezi miwili hospitali kwa tatizo la kansa.Mwezi wa sita akafariki,sijapoa na machungu ya msiba mwezi wa nane nikaachishwa kazi.Baada ya kuachishwa kazi,niliandamwa na matatizo lukuki ambayo nikianza kusimulia hapa naweza nikaishia kulia tu.

Kwa ufupi amani kwenye ndoa yangu ikaisha kabisa,nikagombana na mke wangu(nahisi kwa kuwa maisha aliyozoea akawa hayapati tena),akaamua kuondoka nyumbani kwenda kwao,kuna nyumba niliyokuwa najenga,akabeba hati zote za manunuzi ya kile kiwanja akaondoka nayo.Nimekaa miaka miwili bila kazi mpaka mwaka huu ndo nimeamua kujiajiri mwenyewe.Daah,ngoja niishie hapa wakuu!Inaumiza sana.
VIP huyo mke alirudi? Ulikuwa umezaa nae?
 
Aisee sikia kwa mtu tu yasikupate wewe!

Nakumbuka mwaka 2013 ulikuwa kama mwaka wa mikosi kwangu,mwaka huo nilikuwa nauguza baba yangu miezi miwili hospitali kwa tatizo la kansa.Mwezi wa sita akafariki,sijapoa na machungu ya msiba mwezi wa nane nikaachishwa kazi.Baada ya kuachishwa kazi,niliandamwa na matatizo lukuki ambayo nikianza kusimulia hapa naweza nikaishia kulia tu.

Kwa ufupi amani kwenye ndoa yangu ikaisha kabisa,nikagombana na mke wangu(nahisi kwa kuwa maisha aliyozoea akawa hayapati tena),akaamua kuondoka nyumbani kwenda kwao,kuna nyumba niliyokuwa najenga,akabeba hati zote za manunuzi ya kile kiwanja akaondoka nayo.Nimekaa miaka miwili bila kazi mpaka mwaka huu ndo nimeamua kujiajiri mwenyewe.Daah,ngoja niishie hapa wakuu!Inaumiza sana.
Pole sana, Mungu atyakusimamia. Matatizo kiubinadamu tunayaona mabaya lakini yanajenga. Mungu akuzidishie.
 
Your the strong girl and i've got no doubt for that

You had every good song for every mood and that's the greatest faith to survive with!
I ain't that strong swts, but behind me is a very strong God. Trust me kuna muda kama binadamu wengine nakata tamaa pia, najifungia chumbani nalia weeee but nikimaliza nashukuru Mungu coz several times nimeshawahi hisi like "I'm never gonna make it", but Mungu akanivusha katika magumu yangu. So naamini kwa yote yatakayonipata, Mungu ana makusudi na mimi and Yes navuka kutoka stage moja kwenda stage nyingine kubwa zaidi. The key is to be Grateful always. Don't complain, Just Praise Always...Kama hakina faida na mimi, Mungu asingeruhusu kinipate
 
Hiyo hali inaweza ikakufanya ukafanya Maamuzi magumu ila ukijua kama kuna mapito hapa duniani unavumilia tu Maana maisha ni kutesa kwa zamu
 
Hustle ninayokumbuka ni ile ya kula mlo mmoja kwa siku tena kwa shida alafu asubuhi ukiamka unasikia jamaa anamtoa demu alie lala nae elfu kumi
Inauma sana bty nashukuru Mungu maisha yanakwenda

Huyo demu huwezi jua nae alikuwa anapeleka hiyo pesa kwa waliolala njaa jana kabla hajaja kulala na mchizi.
 
Hapa nina maanisha kufirisika/kufulia kukosa uhakika wakupata angalau chai kwa siku kutengwa na ndugu. Kukosa kazi muda mrefu, kuugua na watu kukutenga, kukosa kodi ya nyumba/mahali pa kulala, kusingiziwa kwamba hutafuti kazi au kusemwa umelogwa ndugu kusema una laana.Kukatishwa tamaa kwamba Mungu kakuacha,kwamba unasali uongo
kudharauliwa na mambo kama hayo.

Je uliweza vipi kuchomoka katika hali hiyo?

UMENIKUMBUSHA MBALI SANA.
Nimezaliwa katika kijiji kimoja kinaitwa Kayombo, huko Bukene, Nzega, Tabora. Nilipitia maisha magumu kwa kweli, lakini tu niseme kwamba, yawezekana mimi sikupita maisha magumu, bali wapo wengi ambao pengine walipitia magumu zaidi yangu.

Nilikuwa napenda kusoma toka nikiwa shule ya msingi, na aidha kwa mipango ya Mungu, ama kutamani niwe kama wengine, nilikuwa na ndoto kubwa sana siku moja niwe mmoja kati ya wasomi nchini, japo sikujua msomi katika kitivo gani, ila tu nilichokuwa nakijua ilikuwa tu siku moja nami niitwe msomi. Nakumbuka mwalimu wangu nikiwa darasa la tano, aliniuliza swali, ningependa kuwa nani maishani. Nilichomjibu ni kwamba, 'nataka kuwa waziri' wala uwaziri wenyewe sikujua maana yake.

Nilikuwa nikiishi na mama yangu kipenzi, na nikiwa kama mtoto wa kiume pekee na wa mwisho kati ya watoto wengine saba, nyumbani mimi ndiye nilikuwa faraja ya mama, kazi zote za kiume mimi ndo nilikuwa wa kuzifanya kutokana na ukweli kwamba, baba alifariki dunia nikiwa na umri wa miaka mitatu, kwa mujibu wa maelezo ya mama yangu.

Kutokana na familia yangu kutokuwa na uwezo wa kutosha, niliingizwa katika shirika moja la WORLDVISION INTERNATIONAL, shirika ambalo silipendi kama nisivyompenda shetani katika maisha yangu, kama mtoto mfadhiliwa aishie katika mazingira magumu, na nilikuwa mmoja kati ya watoto wanne tarafa ya Bukene tuliochaguliwa kuliwakilisha shirika hilo kwenye maombolezo ya MTOTO WA AFRIKA mkoani Shinyanga mwaka 2005, sherehe ambayo hufanyika kila siku ya Tarehe 16 June, safari ambayo huwa naisemea kama safari iliyofungua ukurasa mpya katika maisha yangu.

Nilifanikiwa kumaliza elimu ya msingi na kufaulu kwa ufaulu mkubwa tu (alama 213/250), nikapangiwa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule moja ya kata, karibu kabisa na nyumbani. Maisha nyumbani kiukweli yalikuwa magumu, maana nililazimika kujishugulisha na kazi anuai ambazo kwa namna moja, ama nyingine zilitakiwa zinipatie kipato ambacho angalau ningeweza kununua mahitaji nyumbani na kununua nguo zangu pamoja na ada, na moja kati ya kazi nilizozipa kipaumbele ilikuwa ni kukata na kuchoma mkaa.

Kama nilivyosema hapo juu kwamba, kati ya mashirika ambayo sipendi hata kuyasikia ni WORLDVISION INTERNATIONAL, na hapa sintozungumza ni kwa sababu gani, nitatoa mawasiliano ili nipate kukupatia kitabu changu kinachokwenda kwa jina la A SPITTING COBRA, nilichokiandika si punde, kwa muktadha wa riwaya ya wasifu (AUTOBIGRAPHICAL NOVEL).

MAISHA MAGUMU AMBAYO SINTOYASAHAU.


Kama mada tajwa juu, maisha magumu niliyopitia ambao unaweza kuyasoma pia katika kitabu changu, ni pale nilipokuwa kidato cha kwanza, nilikutana na kesi nikiwa na rafiki yangu, kuwa tumefanya mapenzi mchana kweupe, na kupewa suspension ya wiki mbili na kuripoti na wazazi. Niliamua kuondoka nyumbani nikiwa nimekata tamaa kabisa ya kusoma tena. Najua wengi watajiuliza, 'suspension ya wiki moja tu ndiyo ilinifanya niondoke nyumbani na kukata tamaa kiasi hicho!'. Mengi utayasoma kwenye kitabu hicho ikiwa ni pamoja na swali hili, lakini tu kwa ufupi ni kwamba, nilamua kutoroka nyumbani na kukimbilia mkoa jirani wa Shinyanga, ambapo wala sikujua naenda kufikia wapi, ila tu nachoweza kusema ni kwamba, ilinibidi nilipofika Shinyanga kulala nje na nililala kama siku tatu, nikiwa na machokoraa wengine.

Ndipo nilipopata msamalia na kuhifadhi kwake na kunifanya kama sehemu ya familia yake. Mengi nimeyapitia ambayo ningependa ku-share jamvini ili tujifunze kitu, lakini niseme, fuatilia kitabu changu cha A SPITTING COBRA, na kupata copy yake, niandikie pepe anwani hujumasr@gmail.com au kwa simu nambari +255 785 777 710, nitakupatia copy hiyo.

Kwa sasa nipo chuo kikuu cha Dodoma, nasoma shahada ya Elimu katika sanaa ( Bachelor of Education in Arts (Linguistics).

Nikisema maisha magumu, simaanishi kwamba nimeyasoma kwenye kitabu, bali nimeyaishi.


 
Hayo yote uliyoyaandika , ndio nayapitia sasa. Tena yamekuwa kwa muda mrefu sana.

Ilifika mahala nikaenda SCOAN Nigeria kwa PTB Joshua kwa njia ya bara bara ( nilitumia siku 76 kufika)

Nimekuwa kiroho sana. But matatizo yapo pale pale. Na yanazidi kuongezeka mpaka kukimbiwa na watu wa karibu kabisa, uliowasomesha na kuwainua juu.

Wakwe kukuona kama mwehu, mke kukuona hufai , na kuudharau Wokovu wako.

Mara waseme sitaki Kazi, na kwamba nachagua Kazi. Wakwe wanamsisitiza mke wangu aachane na Mimi kuwa nampotezea muda, sina Kazi.

Nakuwa karibu sana na Mungu kila mara. Na ninafunga na kuomba kila mara.

Hii ni sehemu ambayo naitumia kusali mchana na Usiku..., asubuhi mchana jioni.

Usiku kabla ya saa 6 , Then saa 7-8 , na saa 9-10.

Nimetandaza vyeti vyangu vyote kuanzia chini hadi Postgraduate, na mahitaji ya watu wengine.

Natumia muda kuwaombea maadui

f077592e4c5aa05c1d2e35ac99a56ca1.jpg
ulie anzisha thread umeyazua sasa
 
Kutokana na maelezo yako, unavita kubwa katika ulimwengu wa roho, na vita vyako hutashinda kwa nguvu za kimwili. unahitaji maombi maalum ya ukombozi, ndio umeokoka lakini kuna vifungo utakuwa umefungwa kwavyo na inahitaji maombi maalum na ufunuo kwaajili ya kuvi deseable, inaonekana umekuwa ukiomba mara zote bila kujua specific nini cha kuombea, umekuwa ukiomba kwa ajili ya kupata kazi, lakini shida sio katika kupata kazi.

Ni kosa kubwa sana katika maombi kuomba bila target, au kulenga wrong target. kama inashindikana kabisa ni vizuri kuwa na mfungo wa utakaso na maombi katika Roho. ROMANS 8:26-28. MATTHEW 17:21. Ina bidi ufanye mfungo wa maombi kuomba Roho mtakatifu akufunulie ( akuonyeshe) wapi palipo na tatizo ili uweze ku deal direct na chanzo.

Kaa chini tafakari, angalia historia ya maisha yako, ya wazazi wako. kuna mahali palifanyika agano fulani la kiroho? Je kuna jambo wewe ulowahi lifanya ambalo linaweza kuwa sababu ya milango kufungwa? jaribu kuangalia hata yale madogo ambayo unaona ni irrelevant. Fanya sala ya toba ya ukombozi ( special deliverance) na kama kuna mahali kwa namna moja au nyingine unahisi ulifanya jambo ambalo lilimuumiza mtu sana, katengeneze nae, machozi ya mtu ni mabaya sana.
mungu hana specific principles kias mpaka asijue nini unataka omba hata meli kama alitaka kukupa baiskel atakupa hyo baiskel .....MUNGU Mkubwa
 
Nina Vita kubwa sana katika Ulimwengu wa Roho, kwasababu shetani na majeshi yake yote wananifahamu vizuri sana , that I am a noble person ( A righteous branch and the repairer of the broken walls) ; Naelewa kuwa wanaumiza vichwa sana jinsi ya kunimaliza kwa muda mrefu wameshindwa.

Wakati nazaliwa, nilizaliwa nikatoka na chupa ya uzazi kama mnyama; na hata baada ya kuipasua chupa wakanikuta kondo la uzazi limeniviringa mara tatu shingoni.

Nikiwa na 3 years, niligundulika kuwa ni bubu, nikakatwa karimi.

Baadae nikapata mke mwenye HIV+ na nimeishi nae kwa zaidi ya 8 years bila kupata maambukizi wala watoto wangu kupata maambukizi. What a mighty God.

So nina elewa kuwa Mwili wangu sio wa kawaida, kwasababu ya kuepuka vifo vingi sana. Niliwahi kutekwa na Magaidi zaidi ya mara 2 na hawakuweza kunifanya kitu.

I know the truth, wa haya yote. Sio kwa nguvu zangu.
kazi IPO enhe
 
Daah!!.,umesema kila kitu
Heaven ujue haya maisha mambo hayawezi kua sawa kila siku na matatizo hayana kwao ndio maana yapo kwetu kila siku yanashinda

Ila nina imani hiyo pia yana faida ndio maana yanatupata na BWANA hutupa vizingiti anavyoamini tunavimudu..lets just keep in faith! :) :)
I ain't that strong swts, but behind me is a very strong God. Trust me kuna muda kama binadamu wengine nakata tamaa pia, najifungia chumbani nalia weeee but nikimaliza nashukuru Mungu coz several times nimeshawahi hisi like I'm never gonna make it, but Mungu akanivusha katika magumu yangu. So naamini kwa yote yatakayonipata, Mungu ana makusudi na mimi and Yes navuka kutoka stage moja kwenda stage nyingine kubwa zaidi. The key is to be Grateful always. Don't complain, Just Praise Always...Kama hakina faida na mimi, Mungu asingeruhusu kinipate
 
Daah!!.,umesema kila kitu
Heaven ujue haya maisha mambo hayawezi kua sawa kila siku na matatizo hayana kwao ndio maana yapo kwetu kila siku yanashinda

Ila nina imani hiyo pia yana faida ndio maana yanatupata na BWANA hutupa vizingiti anavyoamini tunavimudu..lets just keep in faith! :) :)
AMEN
 
kipindi hiki ni kipimo cha uvumilivu na uaminifu kwa Mungu, baadhi na wengine kushindwa kuhimiri hali hii lakini kubwa zaidi ukipitia hali hiyo ni mpito wa wewe kuwa mwalimu na msaada kwa wengine kuwasaidia kuwashauri na kuwajenga ktk misingi ya uvumilivu....kama mti unahimili hali ya kudumu kusimama pahala pamoja kwa maisha yake yote sembuse binadamu! binadamu anazunguka anatembea...mti ukikosa maji unavumilia hadi mvua zinaunyeshea, jua kali linawaka mti unavumilia hadi mawingi yanaweka kivuli hauondoki..kwa nini wewe utake kujiua bila kuonyesha kiwang cha uvumilivu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom