Je, ulishawahi fika kwenye Interview ukaghairi kufanya?

Me naitwa daily but siendi sometimes mpaka wanapiga cm tena wananipa siku ingine siendi pia
 
Naona wadhaifu mpo mnajazana negative energy; well, huwa inasaidia kufanya uone tatizo hilo lipo kwa watu wengi, LAKINI mwisho was siku inakula subconscious yako, unakuwa unajiona wewe ni mtu wa KUKOSA tu;

Refer nyuzi za RAKIMS & Pasco

Mchawi wako ni maneno uiambayo nafsi yako; INSHORT kilicho katikati ya wewe na mafanikio yako ni WEWE mwenyewe
 
Niliienda kwenye interview moja kulikuwa kuna nafasi 7 waliita watu mia mbili, tukaingia kwenye kuandika, wakachuja ,tukabaki hamsini, tukaenda kwenye vitendo, sasa cha ajabu kuna watu pale walikuwa wanajitolea na wenyewe walikuwa pamoja na sisi, nikasikia wanaambizana ,hawa wanapoteza mda wao tu,hizi nafasi zina watu mda mrefu.

Nilikaa nikajiuliza, hapa nakula hoteli na nalala gest, hii gharama ya nini yote, nafasi 7 na watu wapo walikuwa wanajitolea na sisi wageni tumebaki 43 ,huyu mwenyeji walie kaa nae siku zote akijitolea kwa uchungu wote wamuache wanichukue mimi ambaye ndo kwanza wananiona leo, nitakuwa na upepo gani??!, Sikukaa sawa bwana mmoja akanifata kama utani akaniambia hii interview ni kutimiza wajibu tu, nafasi walishakaba watu kitambo, niliangaria hali nikaona utoboaji si mrahisi. Nikarudi gect kuchukua vyangu na baada ya mda nikafatilia nikaambiwa waliokuwa wanajitolea walipewa kipaumbele chapo watu wote walikuwa na sifa.

tatizo hawajui wanatupotezea muda na pesa kutufanya mbuzi wa kafara
 
Jana nilikuwa na interview wilaya ya kongwa nafasi ni 7 wameita watu 600+ nikapiga garama za kwenda na kurudi ni kam laki.
Nilichofanya nimenunua mitetea 10 ya elfu 8 na pumba za mayai kwanzia next week nianze vuta mpunga
Ndio zile nafasi za watendaji kata au..?
 
Mashirika mengi ni very corrupt. Baada ya tangazo kw chini wanaandika "_ _ _ is an equal opportunity employer , women and disabled people are advised to apply. Hapo nafasi ina mtu teyar wanakamilisha formalities tu.
 
Ulifnya uamuzi sahihi sn mkuu unajua kuna interview zingne hazizingatii utu kabisa af utakuta wanaandika eti wana guarantee equal opportunity shame on them, kuna interview moja ya TPB miezi kadhaa iliyopita ni aibu sn wametangaza wakaita watu nilipoenda nikakuta watu km 2k na wengine walipangiwa mchana so I think we were abt 3 to 4k nilijitayarisha vzr hee kufika c nikakutana na interview ya multiple choice ok haikuwa issue bt nilichoka sn waliposema matokeo yanatoka cku hyo hyo jioni wkt interviewee wa mchana walichelewa kumaliza ss utajiuliza walisahihishaje apo km co mazingira ya kuingizana wazi wazi ndo mana nasuggest ata hawa TPB nao wapitie utumishi tuu japo uko napo kuna uozo bt kdg afazali
Nitaanza kwa kushare my own experience, miezi kadhaa iliyopita niliitwa kwenye shirika moja kubwa sana hapa Tanzania kwa ajili ya kufanyiwa usahili wa nafasi fulani waliyoitangaza, kwa kutokujua nikafanya maandalizi ya kutosha ili siku ikifika nikapambane.

Bahati nzuri mmoja wa wafanyakazi wenzangu niliofanya nao kazi hapo awali alitokea kwenye hii taasisi tulifanya nae kazi kwa muda na akaitwa kurudi kwenye hili shirika alipotokea, kwa furaha nikampigia simu kumuambia nimechaguliwa kufanya interview kwenye shirika lao, Jibu nililokutana nalo sikuamini masikio yangu " omba Mungu hizo ni formalities tu maana tayari kuna mtu wa ndani "

Nilikosa nguvu lakini nikajipa moyo kwamba acha niende nitapambana hata kama wana mtu wao, siku ikafika mapema nikafika eneo la tukio ndani ya dakika chache nikapelekwa chumba cha kufanya mtihani wa kuandika jamani ule ulikua sio mtihani bali kukomoana waliweka kabisa kwamba kila swali hakikisha unajibu kwa 2 page, maswali yalikua matatu kila swali moja lilikua lina page mbili hadi tatu za kusoma tu swali na kuna kipengele A na B ukiangalia uwe umeandika(type kwenye laptop) almost 12 pages ndani ya saa moja. kwa kweli nilikaa mule ndani kama 20 minutes nikitafakari nakanyanyuka nikamuita HR wao nikamwambia nimeahirisha kufanya akaniambia fanya basi hata oral interview nikagoma maana bado nilikua msindikizaji tu wa yule walienae.

Je, yalishakukuta? ulifanyaje?
 
Halafu hii ya women are encouraged to apply imekuwa kama maigizo maana hata matangazo ya madereva unakuta wanasema hivyo
Kwani madereva wanawake hawatakiwi au hawapo mkuu?
Yaani tena kwa mfano kwenye hizi NGOs, kama wewe ni driver mwanaume ukienda interview ukakuta kuna mdada nae ameitwa kwa nafasi hiyo hiyo, na labda nafasi ilikua moja, hesabu maumivu.
Ni very likely atachukuliwa mdada... Labda tu itokee huyo mdada awe ni mbovu sana.....
Maana madereva wadada wapo wachache, na NGOs zinawapenda kwa sababu inawafanya waonekane wapo gender sensitive kwa donors wao ambao wengi wanapenda sana gender balance.
Kamugy T
 
Kwani madereva wanawake hawatakiwi au hawapo mkuu?
Yaani tena kwa mfano kwenye hizi NGOs, kama wewe ni driver mwanaume ukienda interview ukakuta kuna mdada nae ameitwa kwa nafasi hiyo hiyo, na labda nafasi ilikua moja, hesabu maumivu.
Ni very likely atachukuliwa mdada... Labda tu itokee huyo mdada awe ni mbovu sana.....
Maana madereva wadada wapo wachache, na NGOs zinawapenda kwa sababu inawafanya waonekane wapo gender sensitive kwa donors wao ambao wengi wanapenda sana gender balance.
Kamugy T
Thanks Dkt kwa taarifa.
 
Back
Top Bottom