wa zion
JF-Expert Member
- Mar 23, 2013
- 222
- 477
Nitaanza kwa kushare my own experience, miezi kadhaa iliyopita niliitwa kwenye shirika moja kubwa sana hapa Tanzania kwa ajili ya kufanyiwa usahili wa nafasi fulani waliyoitangaza, kwa kutokujua nikafanya maandalizi ya kutosha ili siku ikifika nikapambane.
Bahati nzuri mmoja wa wafanyakazi wenzangu niliofanya nao kazi hapo awali alitokea kwenye hii taasisi tulifanya nae kazi kwa muda na akaitwa kurudi kwenye hili shirika alipotokea, kwa furaha nikampigia simu kumuambia nimechaguliwa kufanya interview kwenye shirika lao, Jibu nililokutana nalo sikuamini masikio yangu " omba Mungu hizo ni formalities tu maana tayari kuna mtu wa ndani "
Nilikosa nguvu lakini nikajipa moyo kwamba acha niende nitapambana hata kama wana mtu wao, siku ikafika mapema nikafika eneo la tukio ndani ya dakika chache nikapelekwa chumba cha kufanya mtihani wa kuandika jamani ule ulikua sio mtihani bali kukomoana waliweka kabisa kwamba kila swali hakikisha unajibu kwa 2 page, maswali yalikua matatu kila swali moja lilikua lina page mbili hadi tatu za kusoma tu swali na kuna kipengele A na B ukiangalia uwe umeandika(type kwenye laptop) almost 12 pages ndani ya saa moja. kwa kweli nilikaa mule ndani kama 20 minutes nikitafakari nakanyanyuka nikamuita HR wao nikamwambia nimeahirisha kufanya akaniambia fanya basi hata oral interview nikagoma maana bado nilikua msindikizaji tu wa yule walienae.
Je, yalishakukuta? ulifanyaje?