Je tunahitaji report ya CAG au tunahitaji Internal Controls?

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Hii ni kwa wale wazee wenzangu ambao enzi zetu auditor alionekana kama askari polisi au ametumwa kutafuta mwizi

Kuna wakati huwa nacheka ofisi haina Controls zozote za pesa miaka nenda rudi halafu kila mwaka unatuma auditors wakafanye kitu gani?

Mapungufu ya Control za ndani kuna wakati yalimkasirisha Rais Marehemu JPM na kuamrisha pesa zote za serikali kwenye Benki za biashara ziende Bank of Tanzania na yeye akajikuta ameingia kwenye mkumbo ule ule wa kutoweka kwa 1.5 Trilioni halafu zigo akadondoshewa Prof Assad Mkaguzi mkuu ajibu kama pesa zimetoweka au La! pale Ikulu Dar

Kwa tukio la 1.5 Trilioni lilionyesha kuna mapungufu makubwa kwenye internal control yaani mtu anaweza badili matumizi ya pesa zilizopangwa na Bunge atakavyo yeye kwa mamlaka yake na hakuna control yeyote iliyopo ya kumdhibiti mtu huyo

Cha kushangaza na kuchekesha zaidi bado watu hao unawatungia sheria kuwa "Wafanye lolote lile la uwizi au ufisadi hawatashtakiwa na mtu yeyote kwa makosa ya uwizi na ufisadi walipokuwa madarakani"

Unapunguza control ya kuwashtaki halafu unamwambia auditor akakague ofisi ya Jaji mkuu na Spika wabunge huku si kupoteza muda wa auditor?

Enzi hizo za sisi wahenga Mkaguzi hakutoa taarifa wala hakutoa hadidu za rejea alivamia ofisi ghafla kama vita lakini bado watu waliwadhibiti auditors na waliendelea na kazi mpaka wakastaafu ingawa baadhi walifungwa kwa fitina ndani ya ofisi lakini sio kutokana na report ya CAG kuwa wamekwapua pesa

Dunia ya kidigital watu wanajua auditor anakuja lini na hadidu za rejea ni zipi, Tatizo la sasa ni vijana kutafuna pesa na kusahau kuweka document sawa, Lakini ukiwapa muda kelele zote hizo zinaisha

Auditing sio vita wala mapambano, Audit ni kelele kama kelele zingine tu zinazohitaji uzuiaji, Na kuna mbinu nyingi za kuzuia kelele za auditor

Document na receipt zinazokosekana kwenye maswali ya auditor zinajibika na Kutengenezwa

Ukisikia auditor anabweka ujue kuna document kadhaa kutokana na muda wahusika walishindwa kuweka sawa lakini ukiwapa muda maswali yote ya auditor yana majibu

Auditor akishapewa document zake basi wananchi mtasubiri Audit ya mwaka mwingine na mtapiga kelele tena za wizi zilizozoeleka miaka nenda rudi

Zamani enzi zetu auditor alidhibitiwa kwa kulambishwa asali na kupewa mapochopocho mfano gunia la mchele, gunia la mahindi, na wakati mwingine anakabidhiwa mrembo, Baada ya week zake za Audit anarudi kwenye Familia yake na full gunia za mchele na mapochopocho hapo tegemea hati safi

Ukisikia watu wamepata hati chafu ujue kamati ya fitina na Majungu haikujipanga vizuri, Waliojipanga vizuri auditor hawezi toa hati chafu

Laiti kama watu wangejua maana ya auditing Tanzania wasingepiga kelele eti kuna wizi unafanyika kila mwaka

Hakuna uwizi unafanyika kila mwaka bali kuna mapungufu ya internal control za taasisi husika

Mtapiga kelele kila mwaka lakini tiba ya mambo haya ni katiba mpya

Katiba yetu kuna mahala inajichanganya sana na kuna muda watu hawajui mwisho wa mamlaka yao

Kuna watu wanaambiwa toa pesa hiyo ya barabara ikajenga shule ya kata, Akija auditor anaona kuna makosa lakini huyu mtumishi ameamrishwa

Bila katiba mpya itakayotofautisha mamlaka ya wanasiasa na Serikali basi tegemea report ya CAG ile ile na wanaosomewa ni wale wale na wezi ni wale wale (Nukuu ya Tundu Lisu)
 
Ni kweli kunahitajika Mifumo ya Ufuatiliaji na Udhibiti (Monitoring and Control Systems) Serikalini na Taasisi zake siyo kwa ajiri ya kupunguza gharama za uendeshaji bali kuchukua hatua haraka penye dalilibm za ubadhilifu.

Kinachotokea na kuendelea kwa sasa ni kutegemea ripoti ya CAG wakati ubadhilifu umekwishafanyika.

Katiba mpya haibadili tabia za watu ambazo hutegemea uwezo na usimamizi wa Kiongozi wa juu katika Kaya, Jamii, Taasisi, Kampuni, Serikali nk. Kama huyo Kiongozi hajali au naye ni mhusika hakuna shaka kuona mambo ya hovyo
 
Huwezi control binadamu lkn unaweza kumbadilisha.

Watendaji wale wale walibadilika wakati wa magu na wamerudi tena kitabia wakati huu.

Tatizo la taifa ni maadili na kukosa watu wenye roho za kupenda kuwahudumia wengine. Wengine huita kukosa wito.
Nchi imekuwa ktk utawala wa tabaka moja toka uhuru.
Tunahitaji serikali jumuishi ili tuweze kujikwamua ktk janga hili.
 
Very correct , andiko Lina Afya ingawa limekuja kisela sana !
I'd u strengh internal controls, the best will be achieved
 
Ni kweli kunahitajika Mifumo ya Ufuatiliaji na Udhibiti (Monitoring and Control Systems) Serikalini na Taasisi zake siyo kwa ajiri ya kupunguza gharama za uendeshaji bali kuchukua hatua haraka penye dalilibm za ubadhilifu.

Kinachotokea na kuendelea kwa sasa ni kutegemea ripoti ya CAG wakati ubadhilifu umekwishafanyika.

Katiba mpya haibadili tabia za watu ambazo hutegemea uwezo na usimamizi wa Kiongozi wa juu katika Kaya, Jamii, Taasisi, Kampuni, Serikali nk. Kama huyo Kiongozi hajali au naye ni mhusika hakuna shaka kuona mambo ya hovyo
Mkuu Fikiria utetezi wa Mwigulu bungeni kuhusu matumizi ya pesa za serikali

Anajitetea kuwa kila pesa inaidhinishwa na Rais hata kama Bunge limepitisha Rais anaweza badili matumizi yake

Wewe kama Mkaguzi Umepewa kazi ya kukagua kwa hali kama hii ya Rais kuwa na Mamlaka ya kubadili matumizi ya pesa za wananchi atakavyo utakagua kitu gani? Na hata ukiandika report unafikiri Rais atachukua hatua au kuna Bunge la kumchukulia Rais hatua
 
Very correct , andiko Lina Afya ingawa limekuja kisela sana !
I'd u strengh internal controls, the best will be achieved
Mfano mwezi ule ambao karibu na kuandaliwa budget au kufunga mwaka wa serikali ndio watu wanapiga sana pesa ndio wakati Invoice za malipo ya uwongo zinaandaliwa ili kufunga mwaka uliopita

Zitatafutwa supporting document kuidhinisha kila malipo watu waliyopanga kupiga pesa kwenye miezi ile kuelekea kufunga mwaka

Na uwizi huu ni Syndicate bahasha zinagawiwa kutoka Uhasibu mpaka ofisi za RAS na wakuu wa Mikoa mpaka madiwani wanapewa bahasha
 
Back
Top Bottom