GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Kwa katiba ya Tanzania ni mahakama tu ndio inathibitisha nani mwizi au sio mwizi na siyo ukaguzi wa CAG au kamati maalum ya bunge
Kama kila mwaka watu wanaiba mbona hawaendi mahakamani?
Kwa ufupi wabunge baadhi wa ccm wafundishwe maana ya ukaguzi au auditing
Ukaguzi unafanywa kwa kuwa na hadidu za rejea au references mara nyingi ni Sera na sheria
Mkaguzi anaangalia sera na sheria inasema nini kuhusu matumizi na ni kitu gani kimefanyika
Wamiliki wa sera na sheria ni bunge lenyewe,Serikali hapa mawaziri na makatibu wao pamoja na mahakama
Ukisikia watu hawajafuata taratibu tambua wamiliki wa hizo taratibu ndio wamewaambia wapindishe taratibu
Mawaziri na makatibu wakuu wana uwezo wa kuwachukulia hatua za nidhamu watumishi kama kweli wameiba pesa lakini kiuhalisia pesa hazijaibwa bali wao ndio wamewaelekeza watumishi wa chini kupindisha sheria
Wabunge wengi wa ccm wanatafuta umaarufu au upenyo wa kusikika ili walau wapate uteuzi wa Rais na kuwa mawaziri
Kelele bungeni bila mpangilio zina lipa sana ,kuna wabunge wamekuwa mawaziri kwa kelele zao bungeni ,Mifano ni mingi sana kuanzia Hussein Bashe,Kitila Mkumbo na Mwigulu mwenyewe alitolewa baada ya kupiga kelele wakati wa corona akarudishwa kuwa waziri
Mambo ya fedha yana sheria zake na kanuni zake zinazopangwa ,Pale kanuni isipofuatwa ya matumizi kwenye report ya CAG yanaitwa matumizi hewa au matumizi yaliyokosa uthibitisho
Wakati wa dharula serikali inabadili matumizi ya pesa iliyopangwa ili kupambana na dharula au wakati mungine kutoa pesa toka kifungu kimoja kuhamishia kifungu kingine kukidhi mahitaji,kwenye Auditing hili huitwa ni tatizo na matumizi yasiyofuata taratibu au sheria
Wabunge baadhi wa ccm wao kwa kufuata mkumbo wanasema pesa zinaibiwa na watendaji wa serikali,Tangu lini mtendaji wa serikali huko halmashauri akageuza matumizi ya pesa bila barua toka kwa wakubwa wake?
Maswali ya kujiuliza?
1.Ni nani anaethibitisha pesa zimeibwa ,Ni wabunge au Mahakama?
2.Na kama pesa zinaibwa ni watu wangapi wapo mahakamani kwa kosa la wizi kwenye kelele za wabunge?
3.Kwanini wananchi walipowatuhumu wabunge wamehongwa pesa za bandari hawakuchukuliana hatua za kinidhamu wao wenyewe? Au kwenda mahakamani ?
Ukifuatilia kelele za bungeni ni kelele za kutaka kusikika au umaarufu,Sifa ya mwanasiasa ni kutajwa tajwa mdomoni na watu ili usisahaulike wakati wa uchaguzi ndio maana wabunge wanaongea pesa zimeibwa lakini huyo mwizi anaiba kila mwaka bila kufikishwa mahakamani
Je, waliozidisha invoice kwenye ile ndege wapo mahakamani?
Je, waliosaini mkataba wa bandari wapo mahakamani?
Je, waliohamishia wanyama chato wapo mahakamani?
Je, walionunua mabehewa ya enzi za vita za vietnam wapo mahakamani?
Sifa ya mwanasiasa ni kutajwa tajwa midomoni mwa watu asisahaulike,Hakuna pesa kwenye report ya CAG aliposema imeibwa bali ni wabunge wenyewe na Mawaziri ndio wanapindisha kanuni na taratibu za matumizi ya pesa na mzigo anaangushiwa mtendaji wa halmashauri au Manispaa