Katika siku za karibuni tulipewa taarifa na Mamlaka ya Hewa kuwa kutakuwa na mvua ya el Nino na hivyo wananchi wachukue tahadhari zote kuhusiana na mvua hizi. Walitutahadharisha kuwa mvua hizi zingeanza mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu. Leo ni tarehe 8 Oktoba, 2023 na kuna joto kali sana na hakuna dalili ya kunyesha kwa mvua. Ninachouliza Je, tuamini taarifa zenu?. Kama kuna kasoro kwenye taarifa zenu za awali kwa nini msitujulishe tena sisi wananchi?.