Je, toyota IST inafaa kwa safari za mkoani?

Kikubwa ni service ya gar yako!Hakuna gari inayozuiwa kufanya masafa marefu!Kama gari yako haina service ya kutosha usiende tu hata Morogoro!Lakini hata iwe Passo Piston 3 utafika safari yako ya kilometa zisizopungua 1,500,000 that means nakuondoa shaka kuhusu IST!Itafika bila kupumzika popote!Kama ni dereva mzoefu wa Njia haswa kutoka Igunga mpaka Nzega ambako sio nzuri saana unatoboa tena mapemaa saa 4 usiku maximux hours unakuwa umefika!Lakini kwa ugeni na kuogopa Tochi utafika saa 6 au 7 usiku!!
 
Habari wanajamvi,

Nimetokea kuipenda sana gari toyota IST. Kilichonifanya niipende ni ulaji wake wa mafuta, haina gharama kwenye mafuta. Sasa swali langu je mtu akiamua kusafiri na IST kutoka DAR kwenda Mwanza atatoboa?

Nisaidieni please. Kama kuna mwenye ushauri pia niambieni
Ni moja ya gari bora sana.tumia gari kijana.ulaji was mafuta in mzuri sana,ni nzito barabarani na INA mwendo sana
 
Mimi nilisafiri na Passo Piston3 kutoka Dar mpaka Mwanza nilitoka Dar saa 9 kama na nusu nikaingia Mwanza saa 2 usiku wala sikupata tatizo lolote njiani wala sikupigwa Tochi ilikuwa mwaka jana mwezi wa 10 na niliendesha mwenyewe muda wote wa safari.
 
Ukiwasha A.C feni huwa zinazuguka na kupumzika kwa muda mfupi..
Ndio feni zinakuwa zinawaka ila upulizaji wa feni ya ac unapokuwa umewasha unakuwa mdogo ila mvumo wa gari ndio utaona umeongezeka na mshale wa rpm kama gari yako inauo mshale huo itaona umepanda kidogo either kufikia kwenue moja au juu ya moja ni tofauti na upulizaji wa feni pindi maji yanapokuwa yamepata moto na yanahitaji kupoozwa kwenye rejeta feni inapuliza kwa kasi zaidi na mvumo wa gari utabakia vile vile ila mvumo wa feni ndio itausikia zaidi na mshale wa rpm hautapanda utabaki pale pale ulipokuwepo kama gari ilo silence hautapanda wa hautashuka ila mvumo wa feni ndio utausikia imeongeza kumbuka ac inatumia zaidi compresor na condensor katika kuleta hewa ya baridi ndani ila kumbuka mfumo wa ac hata kama umeiwasha muda wote na gari unaitumia kufuta utaratibu nilioelezea hapo juu haina madhara yoyote kwenye gari yako.
 
Inatoboa...

Nimewahi kutoka Arusha hadi Dar kesho yake nikaunga Mwanza(nililala Singida) na baada ya siku tatu nikapiga Mwanza to Arusha kupitia babati bila tatizo lolote.

Hivyo kama gari haina shida then hamna sababu ya kuhofia.
 
Ipo vizuri tu nimeisha safiri nayo Dar to Kahama achia mbali hizo njia za ndani ndani huko kwetu kikubwa kabla ya kuondoka fanya services, mwaga oil pia nunua oil filter nzuri at least ya Tsh 20,000/30,000 zipo zinazofanya kazi kwa km 10,000 acha hizi za elfu tano

IST inaenda vizuri tu kama haina shida mkoa wowote kutoka Dar
 
Kwani hiyo Toyota IST na Toyota Volt ipi inafaa zaidi kwa matumizi ya kawaida nyumbani.
 
Unaweza ifananisha na passo,swift,corolla Suzuki escudo,fun cargo,sienta,porte,Prado Tx old model,nk?
 
Back
Top Bottom