Je, TFF mnazingatia matumizi ya dawa haramu Michezoni?

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Dawa haramu. hizi ni dawa zilizopigwa marufuku kutumika na wachezaji either wa Mpira wa miguu, riadha au hata masumbwi kwani dawa hizi zinavichocheo ambavyo huweza kumfanya mchezaji kucheza bila kuchoka kwa muda mrefu either kwa kumpa nguvu, kusisimua misuli na pia kupunguza utendaji kazi wa moyo/ cardiac output.

Ni madawa yanayokemewa sana kutumika michezoni na mashirikisho yote ya mpira kuanzia ngazi ya nchi mpaka Ulimwenguni, tumeshuhudia wachezaji kadhaa wakipigwa marufuku kucheza mpira kwa miaka mingi kwa kisa matumizi dawa haramu michezoni hata Tanzania kuna wachezaji washakutana na kadhia hii.

Kwa kipindi cha karibu sijasikia shirikisho letu la mpira wakitilia mkazo juu ya matumizi ya madawa haramu michezoni kama hakuna wachezaji katika ligi yetu wanaotumia madawa hayo its fine na hongera.

Tumeshudia michuano ya Caf iliyotamatika wiki kadhaa zilizopita nao walikua makini sana kupima wachezaji either baada ya mechi au kabla ya mechi na wanaweza kutumia mkojo, au hata damu.

Kwanini nawashauri TFf kutilia mkazo hapa, mpira wetu kwa sasa umekua na janja janja nyingi pamoja na muingiliano wa wachezaji wa mataifa tofauti huku kila mmoja akiwa na tabia zake.

Kwa utafiti wangu mdogo kuna wachezaji wa timu moja kubwa tu nchini leo ntaipa jina X kuna baadhi ya wachezaji wao wakiitwa timu ya taifa aloo wanakua kwenye viwango vibovu sana kama vile kuchoka mapema, kushindwa hata kutuliza mpira, ila wakirudi kwenye timu yao utadhani sio wale naendelea na tafiti zangu ntarudi na majibu hapa.

TFF fanyeni surprise siku moja mpime wachezaji kwani sheria zinawapeni mamlaka.
 
Umengea vitu vya umuhmu sana ila watu wanashndwa kuchandia vtu vya umuhmu
Ila ni kweli asemacho mleta mada ni muhimu wachezaji au mchezaji mmoja kupimwa km ametumia dawa za kuongeza nguvu..na hii mara nyingi inafanyika kipindi mpira umeisha kwa timu maalum kutea mchezaji mmoja tika kila timu na kuwapima

Ngoja nicheki kanuni inasemaje kwa ligi yetu
 
Ila ni kweli asemacho mleta mada ni muhimu wachezaji au mchezaji mmoja kupimwa km ametumia dawa za kuongeza nguvu..na hii mara nyingi inafanyika kipindi mpira umeisha kwa timu maalum kutea mchezaji mmoja tika kila timu na kuwapima

Ngoja nicheki kanuni inasemaje kwa ligi yetu
Nashukuru sana kwa mchango wenye tija naomba ukizipata uje nazo hapa wote tufahamu.

Naona kama TFf huu upande wamejisahau sana wanadili na ushirikina ila huku wamepaacha kabisa.
 
Nashukuru sana kwa mchango wenye tija naomba ukizipata uje nazo hapa wote tufahamu.

Naona kama TFf huu upande wamejisahau sana wanadili na ushirikina ila huku wamepaacha kabisa.
Mkuu nichungulia kanun zao i za 2021-22 sijaona hicho kipengele wala kanuni

Nadhani waanze kufikiria usemalo
 

Attachments

  • KANUNI-TPL-2021-22-1.pdf
    12.2 MB · Views: 2
Unafiki Sio Mzuri.....!

Tunaomba Uitaje tu hiyo timu Uliyoipa jina 'X'...

Japokuwa Machale Yameshaanza kutucheza kuhusu iyo timu X...!

Kuna beki Wa timu ya Taifa wanaotokea hiyo timu X huwa wanachomesha sana...
 
Back
Top Bottom