Je, Tanzania tupo tayari; BRICS nations offer alternative to West

Zulu Man Tz

Member
Sep 23, 2020
73
99
A new world order? BRICS nations offer alternative to West.

Mataifa yanayojumuisha umoja wa BRICS — Brazil, Russia, India, China, South Africa yamejipanga ili kutoa mbadala wa mfumo uliopo wa fedha kimataifa na na majarida makubwa ya kisiasa. Mfumo wa kimataifa wa fedha wa sasa unaendeshwa sana na siasa za Magharibi na Marekani kupitia World Bank na International Monetary Fund.

Tunajua kwamba G7 ni informal Forrum ambayo inajumuisha Mataifa makubwa yenye uchumi imara Ulimwenguni inayoongozwa na wakuu wa nchi hizo kama vile; Ujerumani, Uhispania, United Kingdom, Japan, Ufaransa, Italia na Canada ila Marekani ni mwanachama tuu kama vile alivyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya(EU).

Historia ya BRICS.

Mwaka 2001 Mkurugenzi wa Uchumi wa Multinational Investment Bank Jim O'Neill aliziunganisha nchi ya Brazil, India, Russia na China nakuitwa "BRIC" kwa mara ya kwanza. Lengo lilikuwa ni kuendeleza Uchumi ukue kwa kasi kwenye Nchi wanachama na kufikia malengo ya nchi husika hapo baadae. BRIC walipoanzisha Marketing Ploy ili vutia wawekezaji wengi na ikakua zaidi kufikia kuwa " platform for intergovernmental cooperation" kama vile ilivyo G7. Nchi hizo kwa mara ya kwanza walifanya mkutano Nchini Russia's Yekaterinburg mwaka 2010, ambapo Nchi ya Afrika ya Kusini ilialikwa kujiunga uanachama rasmi nakuongeza kale ka "S" hivyo na kuwa BRICS.
BRICS kuipa Changamoto mifumo ya Benki ya Dunia.

Mwaka 2014, Mataifa ya BRICS ilianzisha Benk Mpya ya Maendeleo (New Development Bank, NDB) ambayo ni mbadala wa sera za kinyonyaji za Benki ya Dunia na Mfuko wa Kimataifa wa Fedha (IMF), Benki hiyo ilianza na mtaji wa Dollar za kimarekani $Billioni 50 sawa na €46 Billions. Cha kuongezea New Development Bank ilweka liquity mechanism iliyoitwa Contingent Reserve Arrangement to support members struggling with payment. Ofa hii haitainufaisha nchi za Umoja huo pekee tuu bali kwa Nchi zote zilizopitia machungu ya IMF's Structural Development Program (SAP) na austerity measure (kipimo Cha ukali)
Hii ndivyo inqvyopendezewa na nchi tofauti tofauti Ulimwenguni kutaka kujiunga na huo umoja wa BRICS.

5864f4e0-ca27-11ed-be2e-754a65c11505.jpg
Makao makuu ya umoja wa BRICS huko Shanghai huko ndipo ilipo New Development Bank. Benki ya BRICS imefunguliwa kwa wanachama wapya kuanzia 2021, Ambapo nchi za Egypt, the United Arab Emirates, Uruguay na Bangladesh walichukua Shares zao(hisa). However, these were much lower than the respective $10 billion investments made by the bank's founding members.

Nchi nyingi zavutiwa na Umoja wa BRICS.
Waziri wa mambo ya nje ya South Africa Naledi Pandor, alisema akiwa kwenye interview ya Television fulani kuwa Nchi Nyingi Ulimwenguni zina matamanio ya kujiunga uanachama. Takribani barua 12 nimezipokea zimeonyesha nia ya kujiunga na Umoja wetu wa BRICS kama vile Saudi Arabia is one, United Arab Emirates, Egypt, Algeria, na Argentina," vile vile na Mexico na Nigeria. Nchi hizo 5 za umoja huo ni Nchi ya China pekee ambayo GDP yake imekuwa kwa kasi kutoka $6 Trillion mwaka 2010 mpaka $18 Trillion mwaka 2021, ila uchumi wa Urusi, Brazil na South Africa ukiwa katika hali ile ile ya wastani. Pia Pato la Taifa la India liliongezeka kutoka $1.7 Trillion mpaka kufikia $3.1 Trillion.

Pesa ya Marekani US$ kutumika kimabavu.

Kuhusu tarehe ya kuanza kutumika kwa dola ya Marekani kibiashara kimataifa, hii ilianza kujitokeza kuanzia mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia. Hii ni kutokana na kuwa Marekani ndio nchi iliyokuwa na uchumi mkubwa na ulioendelea zaidi baada ya vita na hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya biashara kimataifa. Hata hivyo, dola ya Marekani ilianza kutumika rasmi kama sarafu ya kibiashara kimataifa mwaka 1944 wakati wa mkutano wa Bretton Woods, ambapo nchi zilizokutana zilikubaliana kutumia dola ya Marekani kama sarafu ya kubadilisha katika mfumo wa kubadilishana fedha kati ya nchi hizo.

Nchi nyingi masikini zinategemea sana dola ya Marekani ili kufanya biashara ya kimataifa. Hii inamaanisha kwamba wakati wa kufanya biashara, pesa nyingi za kigeni zinabadilishwa kwa dola ya Marekani, na kwa hiyo Nchi masikini zinapaswa kumiliki dola za kutosha ili kuendesha biashara zao. Marekani pia inaweza kutumia dola yao kama njia ya kushinikiza Nchi nyingine.

Kwa mfano, Marekani inaweza kutumia vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Nchi ambazo hazifuati sera yao ya kigeni au za usalama, Mfano wa nchi hizo ni North Korea tangu 1950's, Nchi ya Iran tangu 1979, Nchi ya Urusi tangu 2014, Nchi ya Venezuela, Cuba, Zimbabwe na Syria. Hii inaweza kusababisha kuporomoka kwa uchumi wa Nchi hizo na kusababisha shida kwa wananchi wake.

STRUCTURAL ADJUSTMENT PROGRAM

Wazungu wametuletea program za ajabu na za kudidimiza uchumi wetu lakini wanaturubuni kwa njia ya kutusaidia na kutupa misaada,kumbe hawana nia ya kutusaidia bali kutuibia. Kwa sababu tumeletewa programu ya SAP ambayo kirefu chake ni STRUCTURAL ADJUSTMENT PROGRAM. Wanasema ni kwa lengo la kutusaidia Afrika lakini kwa akili ya kawaida hebu jiulize tunanufaika vipi ama tutaendelea vipi, wakati wanatuambia ili tupate hiyo misaada, zawadi ama mikopo tuzingatie mambo yafuatayo;

1. TUSHUSHE THAMANI YA PESA ZETU
Yaani pesa zetu sisi kama Waafrika tushushe thamani yake ukilinganisha na dola yao. Tena kitu ambacho wazungu wamefanikiwa sana kwa Waafrika ni kubadilisha kila kitu kuwa katika mtindo wa pesa ndiyo upate huduma ama kitu Fulani unachohitaji (International Trade)

2. LAZIMA TUPUNGUZE MATUMIZI
Serikali zetu za Kiafrika ili zipate mikopo, misaada na zawadi mbalimbali kutoka kwa Benki ya dunia au shirika la fedha duniani lazima matumizi ya nchi yawe chini. Hivyo mataifa ya Afrika tunapangiwa matumizi katika nchi zetu. Sasa kama hata matumizi ya taifa tunapangiwa na wazungu tutaweza vipi kuendelea ama kufanikiwa?

3. LAZIMA TUFANYE UBINAFSISHAJI
Lazima tusaidie au kuanzisha na kufanya ubinafsishaji, ambapo huko wametuweza kabisa, yaani wanasema wanafanya uwekezaji, jambo ambalo lipo kimaslahi zaidi. Lakini cha kushangaza serikali za nchi za Afrika tunakubali uwekezaji huo katika nyanja mbalimbali ikiwemo viwanda, ujenzi na uchukuzi, utalii, madini, teknolojia nk

Hitimisho; Kipindi SAP zinaanzishwa Tanzania Baba wa Taifa letu Marehemu Julius K. Nyerere alipinga sana hii Agenda ila kwa sababu ya umasikin wetu na vile siasa za ujamaa na kujitegemea zilipofeli ndipo USA ikafanikiwa na mpango wake uo wa SAP wa unyonyaji kupitia WB na IMF miaka ya 1970's. Namalizia na nukuu hii 👇✍️
1985 THOMAS SANKARA alipokuwa Raisi
wa Bukinafaso, alitoa hotuba nzuri sana katika mkutano wa umoja wa nchi za Afrika, ambapo alisema, "Afrika tunapaswa kupunguza kukopa
madeni, madeni sio mazuri tutumie rasilimali zetu za ndani katika kuendeleza mataifa yetu."


Hii ni kweli, kwa sababu madeni tunayodaiwa yamepelekea kila mwananchi katika taifa kudaiwa hadi watoto walio tumboni. Ni ngumu sana taifa kuwa na mgawanyo sawa wa
rasilimali ama pato la taifa, ni nchi chache Afrika zenye kufanya wananchi wake kufurahia pato la taifa.
 

Attachments

  • 65117333_902.jpg
    65117333_902.jpg
    19.1 KB · Views: 7
Lakini tumefungamana informal
Yaap mkuu nikikumbuka idea ya Afrika to unite iliyotoka kwa Kwame Nkrumah wa Ghana, halafu Hayati Nyerere akaipokea kutekeleza ukombozi wa Nchi za kusin mwa Afrika miaka ya 1973-1978 Nchi ya Urusi iliwapa mafunzo wanaharakati wa Afrika ila sasa hawa USA wanatembelea kwny legacy zetu wameanza Ghana na sasa Tanzania halafu Zambia daaah💔😔
 
Tusijiunge tu imradi tumejiunga, lazima tujue tutafaidika vipi
Yaap ni kweli kabisa kama manufaa yapo situnaona India na Tanzania wameacha kutumia Us$ Dollar kwny International trading kati yao nakutumia currencies zao TSH na Rupee
 
Kamala Harris amemwaga packages za kutosha kabisa hadi bibi mfuga kuku kule kijijini atafaidika; hadi wagonjwa wa ukimwi na murbug kwenye famili zenu wataguswa!

Urusi? China? India? You're joking!
 
Inshu sio kumwaga pesa angalia baada ya miaka ijayo mbele vizazi vijavyo, unajua mikataba walioingia hapo ili kupokea izo aids?
 
Kajifunze kuhusu tigers of the east! Mkipeleka kununulia t-shirts za kampeni hilo sio la Marekani.
Sasa izo Asian Tigers hawafungamani na USA hata kidogo labda Taiwan ikumbukwe izo Asian Tigers miaka ya 1950's to 1960's walianzisha sera zao Binafsi na walikuwa na Uchumi kama Tanzania kipind Iko na walijikwamua kiuchumi bila kumtegemea West uko. Sisi huko ujamaa ulifeli capitalism ikatek place privatization ikamaliza Future ya Tanzania yetu
 
Sasa izo Asian Tigers hawafungamani na USA hata kidogo labda Taiwan ikumbukwe izo Asian Tigers miaka ya 1950's to 1960's walianzisha sera zao Binafsi na walikuwa na Uchumi kama Tanzania kipind Iko na walijikwamua kiuchumi bila kumtegemea West uko. Sisi huko ujamaa ulifeli capitalism ikatek place privatization ikamaliza Future ya Tanzania yetu
Tigers of the east plus China kuna mikono mingi sana ya west mule! Nafuu yao tofauti na sisi walitumia vizuri fursa.
 
Saudia Arabia ikijiunga na United Emirates ujue mwisho wa marekani umefika
😅😅Lazima atape tape ila USA anajivunia nguvu ya US$ Dollar labda mifumo ya kibenki yote ya kutumiana pesa ibadilishwe maana visa ,master card etc inatumia teknolojia ya Marekani ya Swift na Tanzania since 2020 tulianza kutumia mifumo yetu ya kifedha ya TIPS
 
Back
Top Bottom