Je, Tanzania kuna Yoabu? Yoabu huyu hapa, ana nguvu sana

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,904
44,035
Utangulizi:

Yoabu alikuwa ni Mkuu wa Majeshi au Jemedali wa Jeshi la Israel wakati wa Mfalme Daudi.

Habari za Yoabu na Mfalme Daudi utazipata kwa kina ktk Kitabu cha Biblia cha Samweli wa kwanza na Wapili, Mambo ya Nyakati wa kwanza na Wa Pili lakini pia Habari zake zinaanzia Katka kitabu cha Mambo ya walawi.

Yoabu alikuwa ni mmoja wa watoto wa Seruya, wengine ni Asaheli na Abishai( wana wa Seruya).

Matukio muhimu ya Yoabu ktk Nchi ya Israel na Rais Daudi wa Israel.

1. Yoabu anamlaghai Daudi kuwa si vema kumwacha mwanaye Absalom ajitenge na familia hata kama alikosea na kumuua Ndugu yake Amnoni.

2. Yoabu anamuua Absalom mwana wa Mfalme Daudi kwa kumchoma mkuki Mgongoni wakiwa vitani kipindi ambacho Rais Daudi alimuonya Yoabu asimuue mwnaye. Hata hivyo Daudi hakuwa na cha kumfanya Yoabu.

3. Yoabu anamuua Abneli mwana wa Neli mbele ya Mfalme Daudi muda mchache tu wakitoka kwenye Kikao cha Maridhiano Ikulu ya Mfalme Daudi. Daudi aliishia kulia tu na kutoa machozi bila kujua cha kumfanya Yoabu.

4. Yoabu anatumika kwenye mkakati wa uovu wa kusababisha kifo cha mwanajeshi Uria vitani ili asiweze kurudi nyumbani akiwa hai maana Mfalme Daudi kampa mimba mke wa askari wake.

5. Yoabu anaungana na Adoniya( mwana wa Daudi) ili kupora haki ya Suleiman ya kurithi ufalme. Alifanya hivyo kwa kuungwa mkono na manabii wasio wachamungu akina Kuhani Abiathai. Huku Rais Daudi akiona mienendo ya Mwanaye Adoniya na asichukue hatua yoyote.

Je, Tanzania kuna Yoabu?

Je, Yoabu alikuwa na nguvu sana kuliko Mfalme Daudi?

Kwanini Yoabu alitamba na kutenda kama alivyotaka na asifanywe chochote?

Daudi alimuogopa nini Yoabu?

Je, ni kwa vile Yoabu alikuwa jemedali mwenye nguvu na ujuzi wa kupigana? Au ni sababu ya Madhaifu ya Daudi yalijulikana sana kwa Yoabu ikiwemo matendo machafu ya kulala na wake za maaskari wake?

Sote tunajua Katiba iliyopo ni mbovu na imeleta hasara kubwa kwa Taifa, nini kinafanya watu kusua sua kuhusu mchakato wa kuiponya Tanzania?

Nani ananufaika na mfumo huu?

Wizi wa mali za Umma miaka nenda rudi kwanini hapajatokea Rais hata mmoja wa kukomesha haya? Marais woote wanamwogopa Yoabu wa Tanzania?

Yoabu alikuwa mtu mzuri sana mbele ya Mfalme Daudi. Alikuwa mtu aliyemuumiza sana moyo mfalme wake Daudi hata kumuua mwanaye na bado asichukue hatua yoyote.

Yoabu alimpendeza sana Daudi pale tu alipokuwa akishindana vitani dhidi ya Wapinzani na kuwa kidedea na kuokoa Utawala wa Israel kurudi mikononi mwa Daudi. Kila mpinzani aliyeinuka ndani ya Israel akitaka kumpindua Daudi alikipata cha moto. Na ushindi wa Yoabu ulikuwa ni ushindi wa Daudi.

Kupenda madaraka kwa Daudi kulimkosti sana kiasi akaishi bila amani hadi kupoteza uhai wa mwanaye mpendwa Absalome.

Je, Tanzania kuna Yoabu?
 
Daudi anaishia kulalamika na kulia tu. Huku yeye ndiye mwenye mamlaka.

Sio kweli!
Mfalme Daudi alikuwa halalamiki hata kidogo!
Mfalme Daudi alikuwa anamlalamikia Mwenye Enzi Mungu amsamehe kwa makosa yake makubwa ambayo aliya fanya mbele ya macho ya Mwenye Enzi Mungu!
Mfalme Daudi alipigana vita vingi sana na ndio maana Mwenye Enzi Mungu akamwambia ‘huwezi kunijengea nyumba yangu maana mikono yako imejaa damu nyingi sana bali mwanao Mfalme Selemani ndio atakaye ijenga na nitambariki kwa baraka zote’
 
Hiyo ni angle nyingine ya Mfalme Daudi
 
Ndio akina nani hao? Ndio wanaozuia kupata Katiba Bora kwa maendeleo na Ustawi wa Nchi?
Hapa ndo ulipo chemka, ulianza vzr then comment zako unakosea,katiba ndiyo nini inayoweza kuwazuia hao kina Yoabu?kweni Daudi alibadili katiba?katiba ni sheria na inaweza ikavunjwwa kwa wanadamu
 
Sisi wengine tunaamini Katiba kama mfumo wa Kisheria( mama) inaweza kuwa na matunda kwa Taifa
 
Sijaona relevance ya story ya Yoab na issue ya katiba.
Katiba ndio hulete mwongozo wa namna ya kusimamia maslahi mapana ya Taifa.

Maslahi mapana inabeba uwanja mpana, nyanja ya siasa, maendeleo, ustawi,uchumi na amani.
 
Sisi wengine tunaamini Katiba kama mfumo wa Kisheria( mama) inaweza kuwa na matunda kwa Taifa
Yoabu na Daudi walihangaika na katiba?watu wanawweza wakakubali kukutengenezea katiba na bado ikavunjwa tu kama ya sasa,kweni unadhani ilihopo haifai?mnajidanganya tu...ukiniambia deesturi na hulka ya sisi weusi ndiyo mbaya ntakukubalia,lakini katiba!!! Hakuna lolote
 
Mr G'tax unakubali kuwa sisi wafrika ndio wenye hulka mbaya? Sasa hizo hulka mbaya zimeruhusiwa kuwepo kutokana na loopeholes za katiba za Nchi zetu za Afrika.
 
Utangulizi:

Yoabu alikuwa ni Mkuu wa Majeshi au Jemedali wa Jeshi la Israel wakati wa Mfalme Daudi.

Habari za Yoabu na Mfalme Daudi utazipata kwa kina ktk Kitabu cha Biblia cha Samweli wa kwanza na Wapili, Mambo ya Nyakati wa kwanza na Wa Pili lakini pia Habari zake zinaanzia Katka kitabu cha Mambo ya walawi.

Yoabu alikuwa ni mmoja wa watoto wa Seruya, wengine ni Asaheli na Abishai( wana wa Seruya).

Matukio muhimu ya Yoabu ktk Nchi ya Israel na Rais Daudi wa Israel.

1. Yoabu anamlaghai Daudi kuwa si vema kumwacha mwanaye Absalom ajitenge na familia hata kama alikosea na kumuua Ndugu yake Amnoni.

2. Yoabu anamuua Absalom mwana wa Mfalme Daudi kwa kumchoma mkuki Mgongoni wakiwa vitani kipindi ambacho Rais Daudi alimuonya Yoabu asimuue mwnaye. Hata hivyo Daudi hakuwa na cha kumfanya Yoabu.

3. Yoabu anamuua Abneli mwana wa Neli mbele ya Mfalme Daudi muda mchache tu wakitoka kwenye Kikao cha Maridhiano Ikulu ya Mfalme Daudi. Daudi aliishia kulia tu na kutoa machozi bila kujua cha kumfanya Yoabu.

4. Yoabu anatumika kwenye mkakati wa uovu wa kusababisha kifo cha mwanajeshi Uria vitani ili asiweze kurudi nyumbani akiwa hai maana Mfalme Daudi kampa mimba mke wa askari wake.

5. Yoabu anaungana na Adoniya( mwana wa Daudi) ili kupora haki ya Suleiman ya kurithi ufalme. Alifanya hivyo kwa kuungwa mkono na manabii wasio wachamungu akina Kuhani Abiathai. Huku Rais Daudi akiona mienendo ya Mwanaye Adoniya na asichukue hatua yoyote.

Je, Tanzania kuna Yoabu?

Je, Yoabu alikuwa na nguvu sana kuliko Mfalme Daudi?

Kwanini Yoabu alitamba na kutenda kama alivyotaka na asifanywe chochote?

Daudi alimuogopa nini Yoabu?

Je, ni kwa vile Yoabu alikuwa jemedali mwenye nguvu na ujuzi wa kupigana? Au ni sababu ya Madhaifu ya Daudi yalijulikana sana kwa Yoabu ikiwemo matendo machafu ya kulala na wake za maaskari wake?

Sote tunajua Katiba iliyopo ni mbovu na imeleta hasara kubwa kwa Taifa, nini kinafanya watu kusua sua kuhusu mchakato wa kuiponya Tanzania?

Nani ananufaika na mfumo huu?

Wizi wa mali za Umma miaka nenda rudi kwanini hapajatokea Rais hata mmoja wa kukomesha haya? Marais woote wanamwogopa Yoabu wa Tanzania?

Yoabu alikuwa mtu mzuri sana mbele ya Mfalme Daudi. Alikuwa mtu aliyemuumiza sana moyo mfalme wake Daudi hata kumuua mwanaye na bado asichukue hatua yoyote.

Yoabu alimpendeza sana Daudi pale tu alipokuwa akishindana vitani dhidi ya Wapinzani na kuwa kidedea na kuokoa Utawala wa Israel kurudi mikononi mwa Daudi. Kila mpinzani aliyeinuka ndani ya Israel akitaka kumpindua Daudi alikipata cha moto. Na ushindi wa Yoabu ulikuwa ni ushindi wa Daudi.

Kupenda madaraka kwa Daudi kulimkosti sana kiasi akaishi bila amani hadi kupoteza uhai wa mwanaye mpendwa Absalome.

Je, Tanzania kuna Yoabu?
Jemedali ✖️
Jemedari✔️
 
Back
Top Bottom