Je, Rais au Mfalme kuna watu anaowaogopa?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,432
52,078
JE RAIS AU MFALME KUNA WATU ANAOWAOGOPA?

Anaandika, Robert Heriel
Jemadari

Huenda nawe ni miongoni unaofikiri kuwa Rais au Mfalme ni mtu asiyemuogopa yeyote, lakini sivyo. Rais au Mfalme ni Binadamu Kama binadamu wengine. Cheo chake kisikuzuzue ukadhani kuwa hakuna anayemuogopa. Hata ukisikia Rais au Mfalme akisema kuwa hamuogopi mtu yeyote ujue anajikosha. Ingawaje Kwa sehemu kubwa anaweza kuwa kweli, Ila elewa kuwa kuna mtu au watu Fulani katika nchi au kwenye mfumo ambao atakuwa anawahofia, anawaogopa na Kundi hilo Kwa sehemu kubwa ni watu wasiomuogopa Rais au Mfalme.

Zipo sababu nyingi zinazopelekea Rais au Mfalme kumuogopa Mtu au kundi la watu Fulani. Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na hizi;

I. Waliomuweka na kumpa Madaraka

Ufalme au Urais hauji tuu Kama usingizi, unatafutwa Kwa nguvu nyingi, Kwa damu na jasho, Kwa watu kujitoa kafara.

Rais au Mfalme yeyote unayemuona anaongoza nchi au taifa Fulani elewa kuwa kuna watu wapo nyuma yake waliomfanya awe hapo. Iwe Kwa njia ya Demokrasia au njia ya mapinduzi.

Watu hao huogopwa na Rais au Mfalme. Situmii neno "kuheshimika" Kwa sababu Heshima na woga ni mambo mawili tofauti ingawaje yanakaribiana kimaana.

Sio ajabu kwenye mapinduzi yakifanyika, Rais au Mfalme atakayechukua Utawala Jambo la kwanza kufanya baada ya kuyapata Madaraka na kuituliza nchi ni kuwaua wale vijeba waliomsaidia kuyatwaa hayo Madaraka. Kwa maana ni hakika hataweza kutawala Kwa Amani watu hao wakiwepo. Hivyo kuwaua ndio Suluhu ya yeye kutaka kutawala Kwa Uhuru bila kumuogopa yeyote na bila kufuata amri ya yeyote.

Katika mataifa ya Demokrasia, lile kundi lililokuwepo madarakani utake usitake lazima litakuwa na nguvu juu yako. Ukikaidi basi kama waliweza kukuweka madarakani ni wazi wanauwezo wa kukuondoa kwenye hicho kiti. Hiyo ndio sababu Rais au Mfalme kuogopa baadhi ya watu ndani ya Nchi.

ii. Mpiganaji shujaa wa Vita

Wapo majemadari majasiri na wasio na mchezo ambao wamefanya matukio makubwa ambayo Rais au Mfalme waliyashuhudia Kwa macho Yao. Hii huwafanya baadhi ya Rais au Wafalme kuwaogopa baadhi ya majemadari.

iii. Waganga wa Hali ya juu au Manabii.
Mfalme au Rais sio kila mganga atamuogopa, na sio kila Nabii au mtumishi wa Mungu atamuogopa. Ila kuna zile chata, namba chafu za kiwango cha juu ambao Wanafanya matukio ya ajabu ajabu. Hao Rais na Wafalme huwaogopa. Ingawaje hawa huwaga ni wachache Sana lakini wakitokeaga Wafalme na Marais huwahofia.

Katika Historia ya Dunia wapo baadhi ya Wafalme ambao waliogopa makundi au watu Fulani Fulani. Mfano;

1. MFALME DAUDI Vs JEMADARI YOABU
Daudi licha ya ujasiri wake wote, CV yake ya kumuua Goliath lakini yupo mtu mmoja aliyeitwa Yoabu ambaye Mfalme Daudi alimuogopa.

Yoabu alikuwa ni Shujaa wa vita ambaye ndiye aliyekuwa bega Kwa Bega na Daudi katika harakati za kusaka Ufalme.

Kimahusiano Yoabu ni Mpwa wa Daudi kwani Yoabu amezaliwa na Dadaake Daudi aitwaye Seruya. Hii ni kusema Yoabu alimuita Daudi Mjomba. Seruya(Dadaake Daudi) alizaa watoto watatu nao ni Yoabu, Abishai na Asaheli.

Kilichofanya Daudi aonekane anamuogopa Jemadari Yoabu ni kipindi Jeshi la Daudi ambalo linaongozwa na Yoabu walivyoenda kupigana na Jeshi la Mfalme ishbotheshi(mwana wa Mfalme Sauli) likiongozwa na Jemadari Abneri(mjomba wake Mfalme Sauli).

Katika vita hiyo Jeshi la Daudi lilipata ushindi mnono kupitia Kwa Jemadari Yoabu lakini kulikuwa na tatizo.

Nalo ni wakati vita inaendelea, Asaheli mdogo wake Yoabu alikuwa akimkabili Jemadari Abneri.

Abneri akiwa katika mapambano akamuona Asaheli akimjia Kwa Kasi bila kuenda kushoto wala kuenda Kulia(yaani akimkabili) abneri akapaza sauti yake kumkanya Asaheli kuwa asimfuate kwani atamuua, abneri hakutaka kumuua Asaheli kwani alijua ni mdogo wake Yoabu.

Kumbuka hawa wote ni Waisrael(ilikuwa Civil War)
Lakini Asaheli akakazana kumkabili Abneri. Abneri akarudia tena kusema akimkataza. Lakini Asaheli hakumsikiza, Ndipo Abneri akamuua Asaheli.

Unajua Abneri ni shujaa wa vita, uwezo wake ni Mkubwa, hivyo alijua kuwa Asaheli Hana uwezo wa kumkabili. Lakini angefanya nini sasa.

Licha ya Jeshi la Daudi kushinda kupitia Jemadari Yoabu, na Jeshi la Ishbotheshi kushindwa kupitia Jemadari Abneri lakini Yoabu hakuridhika na ushindi huo ulioondoka na Roho ya mdogo wake Asaheli.
Napenda Sana Aya hizi
2 Samweli 2:19
Naye Asaheli akamfuatia Abneri; na katika kwenda kwake hakugeuka kwenda mkono wa kuume wala mkono wa kushoto katika kumfuatia Abneri.

2 Samweli 2:20
Basi Abneri akatazama nyuma yake, akasema, Ni wewe, Asaheli? Akajibu, Ni mimi.

2 Samweli 2:21
Basi Abneri akamwambia, Geuka mkono wa kuume au mkono wa kushoto, ukamshike mmoja wa vijana, ukazitwae silaha zake. Lakini Asaheli hakukubali kugeuka na kuacha kumfuata.

2 Samweli 2:22
Abneri akamwambia Asaheli mara ya pili, Geuka, acha kunifuatia mimi; kwa nini nikupige hata chini? Hapo ningewezaje kuinua uso wangu mbele ya Yoabu, ndugu yako?

2 Samweli 2:23
Lakini akakataa kugeuka; kwa hiyo Abneri akampiga tumboni kwa ncha ya nyuma ya mkuki wake, ule mkuki ukamtoka kwa nyuma; naye akaanguka hapo, akafa papo hapo; ikawa, watu wote waliofika hapo, alipoanguka Asaheli na kufa, wakasimama.


Baadaye muda umepita Abneri akakosana na Mfalme Ishbotheshi kisa na mkasa ni Abneri kumchukua/kumuoa Moja wa Masuria wa Sauli(Baba yake Mfalme Ishbotheshi) Mfalme Ishbotheshi hakupendezwa na Mama yake mdogo kuolewa na Jemadari Abneri lakini Mfalme alimuogopa Abneri. 😀😀
soma kidogo Aya hizi nazipenda; iliyokolezwa;
2 Samweli 3:7
Basi Sauli alikuwa na suria, jina lake akiitwa Rispa, binti Aya; Ishboshethi akamwuliza Abneri, Kwa nini umeingia kwa suria ya babangu?

2 Samweli 3:8
Basi Abneri akakasirika kwa maneno ya Ishboshethi, akasema, Je! Mimi ni kichwa cha mbwa, aliye wa Yuda? Hata leo hivi nawafanyia fadhili nyumba ya Sauli babako, na ndugu zake, na rafiki zake, nisikutie wewe mkononi mwa Daudi; nawe hata hivyo wanitia hatiani leo kwa mwanamke huyu.

2 Samweli 3:11
Wala hakuweza kumjibu Abneri tena, kwa sababu alimwogopa.

Baadaye Yoabu anakuja kumuua Abneri, lakini Daudi anashindwa chakufanya zaidi ya kumuachia Mungu Jambo ambalo Kwa tunaomjua Daudi na visa vyake Hilo lisingewezekana.
Daudi hapo nyuma ameshaua watu wengi Sana bila kumuachia Mungu lakini Leo hii Daudi anajikuta akiongea Kauli ya kutia huruma bila kuchukua hatua yoyote Kwa Yoabu.
2 Samweli 3:39
Nami leo nimedhoofika, hata nijapotiwa mafuta niwe mfalme; na watu hao, wana wa Seruya, ni wagumu kwangu mimi; BWANA amlipie mwovu sawasawa na uovu wake.

Mfalme Daudi anashindwa kumuwajibisha Yoabu kama anavyofanyaga Kwa wengine.
Anakaa na hiko kinyongo mpaka uzee wake, mpaka siku anakaribia kufa akiwa anamkabidhi Suleiman mwanaye Ufalme anampa majukumu.
Msikilize Daudi hapa😀😀 zingatia Aya zilizokolezwa;
1 Wafalme 2:1
Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema,

1 Wafalme 2:2
Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume;

1 Wafalme 2:3
uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;

1 Wafalme 2:5
Na zaidi ya hayo, umejua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani, alivyowatenda majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa Yetheri, ambao aliwaua, na kuimwaga damu ya vita wakati wa amani, akautia damu ya vita mshipi uliokuwa viunoni mwake, na viatu vilivyokuwa miguuni mwake.

1 Wafalme 2:6

Kwa hiyo ufanye kama ilivyo hekima yako, wala usimwachie mvi zake kushukia Ahera kwa amani.

Hizo ni Siasa na mambo ya Ufalme na Urais. Daudi anaacha kiporo cha miaka nenda Rudi kiliwa na Mwanaye Suleiman.
Hivyo moja ya majukumu makubwa aliyopewa Suleiman ni kumuua Yoabu Kwa Upanga ili akupe kisasi cha Abneri na Amasa( huyu sijawaelezea kisa chake).


2. Mfalme Ishboshethi Vs Jemadari Abneri
Tukio hili tayari nimeshalieleza hapo juu.
2 Samweli 3:11
Wala hakuweza kumjibu Abneri tena, kwa sababu alimwogopa.

Hii ni kusema, kwenye nchi au taifa lolote kuna watu au kundi Fulani la watu linaweza likafanya Jambo lolote na Rais au Mfalme asiwe na chakufanya akabaki na kinyongo rohoni mwake.

Andiko hili linamaanisha Jambo gani au linatufundisha nini?
I. Usimtegemee mwanadamu Bali mtegemee Mungu
Huyo unayemtegemea kuna watu anaowaogopa. Ila Mungu pekee ndiye asiyetishwa na yeyote na chochote.

ii. Siasa ni mchezo hatari Sana uliogubikwa na matukio ya umwagaji wa damu.

iii. Heshimu mamlaka au wakubwa Kwa sababu kuna watu ukiingia kwenye 18 zao hakuna atakayekusaidia sio Rais au Mfalme au Serikali. Hiyo ipo Duniani kote.
Usidanganywe na media au propaganda za demokrasia.

iv. Uongozi na utawala unahitaji watu wacha Mungu ili Kupunguza maumivu na kuongeza Haki.

V. Sio kila Jambo linalotokea Rais au Mfalme ameamua litokee kuna mtu au kundi Fulani wanaweza kuamua Jambo Fulani litokee na Rais au Mfalme asiweze kufanya lolote.

Mwisho; andiko hili halimaanishi watu wawe waoga hata wakiumizwa isipokuwa waangalie uhalisia wa mambo, ikiwa kunanafasi ya kujitetea na kupata Haki wafanye hivyo, ikiwa ni wakati WA kusubiri basi wasubiri.

Ni Yule Jemadari wa vita.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ufalme na Urasi vyanzo vyake ni tofauti!

Ufalme ni Utawala wa kurithi
Ufalme ni mfumo wa utawala ambapo mfalme, malkia au mtu mwingine aliyerithi cheo chake ni mkuu wa dola. Vyeo vingine vya mkuu katika ufalme ni pamoja na kaisari, shah, tenno, sultani, amiri au mtemi. Kwa kawaida mfalme amerithi cheo chake kutoka kwa baba yake au mama yake, kwa hiyo alizaliwa kama mfalme mteule na ataendelea kuwa na cheo hicho hadi kifo chake. Lakini kama mfalme aliyetangulia hakuwa na mrithi inawezekana ya kwamba mfalme mpya amechaguliwa. Mfano wa dola lenye mfumo wa ufalme ambapo mkuu anachaguliwa mara kwa mara ni Vatikani ambapo Papa ni mkuu wa dola.

Na Utawala wa Urais ni wa Jamhuri!

Kinyume na ufalme kuna Jamhuri inayoongozwa na mkuu, mara nyingi kwa cheo cha rais au katika nchi kadhaa na kamati ya watu wanaochaguliwa na kwa kawaida kwa kipindi fulani. Mara nyingi rais wa nchi huchaguliwa kwa kipindi cha miaka 4-6 na katika nchi nyingi kuna uwezekano Wa kwamba anarudi tena kwa kipindi kingine. Kuna jamhuri ambapo vongozi wanalenga kuhakikisha ya kwamba mtoto wao anaendelea na cheo cha mkuu wakiacha kutawala, lakini hii kwa kawaida si utaratibu wa kisheria katika jamhuri; mfano wa kisasa ni Korea Kaskazini ambayo ni jamhuri inayotawaliwa na familia Kim katika kizazi cha pili ilhali mtoto wa kiongozi Kim Jong Il anateuliwa kumfuata baba

Urais na mifumo yake!
Rais wa nchi huwa anachaguliwa ama na wananchi wote au na bunge. Katika nchi kadhaa kuna pia mkutano maalumu unaoitishwa kwa uchaguzi wa rais pekee, kama vile Marekani au Ujerumani.

Kuna aina mbili za rais kufuatana na katiba za nchi mbalimbali:

rais kama mkuu wa serikali, jinsi ilivyo Marekani na pia katika nchi nyingi za Afrika (serikali ya kiraisi).rais kama mkuu wa nchi asiyeshughulikia mambo ya serikali, jinsi ilivyo Ujerumani au Uhindi (serikali ya kibunge)

Katika muundo wa serikali ya kibunge shughuli za serikali zinasimamiwa na waziri mkuu. Madaraka ya rais katika muundo huo hufanana na madaraka ya mfalme wa kikatiba isipokuwa hayupo kama rais kwa muda wa maisha yake kama mfalme.

Katika nchi chache, yaani Uswisi, San Marino na Uruguay, kazi za rais hazitekelezwi na mtu mmoja bali na kamati ya viongozi kwa ujumla, kama Halmashauri ya Shirikisho ya Uswisi.

Sisi kama Taifa,tunapaswa kuchagua sina ya Siasa za kutufanya kwanza tutambue umuhimu wa Uongozi na Mamlaka.

Kisha viongozi nao watambuwe umuhimu wa wananchi wanaowaongoza,jinsi ya kuishi na kuwaongoza badala ya kuishi kwa kuwatawala.

Kwa Bahati mbaya sana.
Afrika tumejaaliwa Watawala Wengi kuliko Viongozi.

Nashukuru kwako .....
ROBERT HERIEL Fasihi yako ni Fikirishi na ya Ki-Mafundisho zaidi.

Wa kukuelewa tunakuelewa vizuri.
 
Mifumo ya kijamaa mtawala huwa anahakikisha anawaondoa wote anaohisi wanaweza kuwa tishio kwa utawala wake.
 
Sisi huku kwetu tuna makundi hatari kweli kweli! Msoga gang, sukuma gang, ccm asili, ccm makinikia, nk.

Kila kundi hapo, ukiingia tu kwenye 18 zake; huchomoki.
 
Back
Top Bottom