Je Star tv itamuonyesha mbunge wa Ilemela atakapokuwa anasoma hotuba ya upinzani?

Vancomycin

Senior Member
Jan 7, 2011
171
111
Salaam wakuu...!

Asubuhi kabla sijainua miguu yangu kueleke kutafuta riziki ya kila siku nimeona mwendelezo wa kile wananchi wengi wakistaajabu kwa kituo cha luninga cha Star kutomuonyesha mbunge wa Ilemela (CHADEMA), Mh.HIGHNESS KIWIA alipokuwa akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani akiwa ni waziri kivuli wa Maji. Swali je atakapokuwa anasoma bajeti hii hawatamuonyesha?

Nadhani siasa ni kupingana kwa hoja na sio uadui. Ndugu zangu tujadili kama jambo hili ni sawa hata kama kituo cha tv ni mali yako.

Ngoja tuone mkuu itakuaje,lakn nafikiri Diallo hafanyi vizuri huyu Mbunge kachaguliwa na wananchi kwa hyo hakukua na haja ya yeye kuelekeza wafanyakazi wake wasimuoneshe huyu Mh Kiwia kwani madoa ya uchaguzi yasiendelee kumtesa kiasi hicho

Mimi nimeshangaa mara baada ya mwenyekiti wa kamati kumaliza akaingia yeye akapotezewa ikabidi nirudi TBC

Duh! Lakini haisaidii kwa kuwa vituo vipo vingi, pia hata asipoonekana
wakati wa majadiliano anaweza kuonekana wakati wa taarifa za habari.
Pia magazeti yapo ya kumwaga...

Duh! Lakini haisaidii kwa kuwa vituo vipo vingi, pia hata asipoonekana
wakati wa majadiliano anaweza kuonekana wakati wa taarifa za habari.
Pia magazeti yapo ya kumwaga...

Ule msingi mkuu wa uwepo wa vyama vingi kuleta ushindani wa hoja,sera na kadhalika ili kuchagiza maendeleo na kugeuka uadui unauzungumziaje?

mtu anasoma hotuba pg 15 humuonyeshi?? hapo hata wandishi na warusha matangazo dhamira zenu haziguswi???

Ule msingi mkuu wa uwepo wa vyama vingi kuleta ushindani wa hoja,sera na kadhalika ili kuchagiza maendeleo na kugeuka uadui unauzungumziaje?

Unajua kilichofanyika hapa nchini, serikali haikuukubali mfumo
huu wa vyama vingi bali kwa shinikizo la kimataifa kwa kuwa
ingekosa misaada, hivyo vyama vingi vimegeuka kuwa adui
wa serikali hasa vile vinavyoikosoa, ndiyo maana wanaviita
vyama vya upinzani. Ukiangalia maana hasa ya upinzani ni
kupinga kila kitu jambo linaloleta tafsiri mbaya kwa vyama
visivyoshikilia dola. Hata hivyo Watanzania wa sasa si wale
wa enzi za "Zidumu fikra za mtu mmoja..." kwa hiyo
wanaelewa...

mtu anasoma hotuba pg 15 humuonyeshi?? hapo hata wandishi na warusha matangazo dhamira zenu haziguswi???

Duh...inamaana kile ambacho nilikuwa nawasiwasi nacho kutukia kimejiri,hebu tupatieni taarifa sisi wengine tuko mbali na TV kwa sasa

Ngoja tuone mkuu itakuaje,lakn nafikiri Diallo hafanyi vizuri huyu Mbunge kachaguliwa na wananchi kwa hyo hakukua na haja ya yeye kuelekeza wafanyakazi wake wasimuoneshe huyu Mh Kiwia kwani madoa ya uchaguzi yasiendelee kumtesa kiasi hicho
Wakati mwingine unaweza kukuta Diallo hahusiki ila ni hao watangazaji na waandishi wake kwa vile elimu wakati mwingine ni za kuungaunga wanadhani kwa kufanya hivyo watamfurahisha mwajiri.

Wakati mwingine unaweza kukuta Diallo hahusiki ila ni hao watangazaji na waandishi wake kwa vile elimu wakati mwingine ni za kuungaunga wanadhani kwa kufanya hivyo watamfurahisha mwajiri.

sikubalian nawe,Dialo ana mkono hapa

sikubalian nawe,Dialo ana mkono hapa

Kama wananchi wa Ilemela walimchagua Kiwia bila kumuona kwenye tv ya Dialo,hata kama sasahivi wamesusa kumuonyesha haitampunguzia chochote. Jambo la msingi ni Kiwia kutekeleza wajibu wake na ilani yake ya uchaguzi kwa wapiga kura wake Dialo ataisoma namba tu 2015.

Tena Diallo anamuongezea umaarufu mb. Highness Kiwia yaani anazidi kuwapa kasi wapiga kura wake yakumsaka ktk source nyingine hata mm mwenyewe amezipasha moto juhudi zangu. Keep up Diallo na hau wanaokudanganya kufanya upuuuzi. Isitoshe wapiga kura wake hawakumuona star tv ndo wakampigia kura hapo. Pia ujue siku hizi kuna source nying za information na zipo accessible mpaka kwny simu zakichina.

Hivi kuna star tv siku hizi? Mara ya mwisho kuiangalia nadhani 2009. Hizi tv za makada wa ccm shida tupu. Kiwia sisi tunamwona kila siku kupitia source nyingine nyingi za habari. Dialo anajidanganya. Uchaguzi ulishaisha visa vya nini?

Back
Top Bottom