Je sisi watanzania ni taifa la wachapa kazi?

Teroburu

Member
Aug 6, 2009
41
3
Je Watanzania sisi ni taifa la wapendao kufanya kazi kwa bidii au ni taifa la walalamishi?

Jamii forum inajiita kuwa ni jumuiko la wanaofikiri {GREAT THINKERS}. Kwa bahati mbaya Great thinkers wa JAMII FORUM wamejikita katika siasa, sio uchumi na uzalishaji wa mali na utajiri kwa mtanzania wa kawaida. Maslahi ya Mtanzania hayataongezeka kwa kushinda kutwa nzima kuzungumzia KATIBA bila kuongeza jihudi za kufanya kazi na kuzalisha. Tusiwe wepesi kuwalaumu viongozi bila kujiuliza JE SISI NI TAIFA LA WAFANYAO KAZI KWAA BIDII NA KUJITUMA. China imepiga hatua kubwa sana kiuchumi kwa muda mfupi sana. Wachina hawakupoteaza muda wao mwingi sana kuimba KATIBA MPYA, KATIBA MPYA. Tanzania tutapata hiyo katiba MPYA. Tena itakuwa mpya sana, lakini hiyo KATIBA MPYA haitatuongezea pato la taifa endapo tutaendelea kuwa watu wa LALAMA na watu LAUMU.

Great THINKERS katika JAMII FORUM nusu saa iliyopita, JAMII FORUM ilikuwa na VIEWERS wengi katika MICHAPO YA KISIASA na sio katika Anga za uchumi, teknolojia, elimu ambazo zinaweza kutuondolea umaskini:

Siasa- 1177 viewers {thinkers!!}
Elimu- 84 viewers

International forum- 69 viewers
Business & Economy- 119 viewers
Nafasi za Kazi na tenda- 150 viewers
Technology, Gadgets & Science Forum- 79 viewers
Sheria- 16 viewers

Kwa hiyo, baada ya Katiba Mpya watanzania tutaanza kulalamika kuhusu Jumuiya.

Vile vile wasomi wetu wa vyuo vikuu ni wepesi sana kulaumu na kutoa mapendekezo ya kiujumla jumla {wananchi washirikishwe}. Walilaumu sana Mswada uliopita. Lakini ni wajanja sana katika kutoa mapendekezo ni namna GANI WANANCHI WAJADILI katiba. Je tuache shughuli zote za kiuchumi na kimaendeleo ili tujadili Katiba mpya? Je fedha za mijadala itokane na kodi na mipango mingine yote isimame ili tuishughulike Katiba? Mungu ibariki Tanzania.
 
Kaka hujui umuhimu wa katiba na siasa ngoja nikusaidie:KATIBA INATOA MWONGOZO WA HAKI ZA RAIA NA WAJIBU WAO PIA MFUMO WA UONGOZI NA SIASA NI MFUMO unaoamua nani apate kipi kwa utaratibu upi mfano mwananchi apate maendeleo kwa utaratibu upi,kiongozi apate madaraka kwa utaratibu upi na siasa ya nchi inazaliwa kwenye sheria mama ya nchi yaani katiba.Siasa ya Tanzania ipo kwenye katiba ya Tanzania na ile ya Rwanda,KENYA,USA,UK zipo kwenye katiba na wasomi wa vyuo vikuu hasa vijana ambao ccm imeshindwa kuwashawishi duniani kote ndio wanaleta maendeleo ndio maana viongozi wa nchi zilizoendelea wanawajali mfano Obama akiwa Uturuki aliomba kuzungumza na wanavyuo,akiwa cAIRO ALIFANYA HIVYO juzi akieleza mkakati wa kupunguza matumizi alihutubia wanavyuo hivyo wasomi walipokataa muswada mpovu walikuwa sahihi ndio maana umerudishwa kwa wananchi kwa leo niishie hapa
 
People are not going to like this thread, hehe. But 'WE' Great Thinkers verily recognize that statistics dont lie and those up there say it all.
 
Back
Top Bottom