Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Januari 12, 1964 mizani ya utawala ya Visiwa vya Zanzibar ilibadilishwa daima; waliokuwa watawala wa miaka mingi walijikuta wakiwa hawana nafasi tena na Sultani akatimuliwa na uzao wake kunyang'anywa kiti cha Usultani wa Zanzibar. Lakini zaidi serikali ya Waarabu wengi ya Waziri Mkuu Shamte ilipinduliwa na serikali ya wananchi chini ya Abein Amaan Karume kusimikwa. Katika kuyalinda mapinduzi hayo Zanzibar ikaingia/ingizwa katika Muungano wa TAnganyika ambao ni nchi kubwa yenye uwezo mkubwa na hivyo kuyaweka salama mapinduzi yale. Kwa miaka karibu hamsini sasa mapinduzi ya Zanzibar yamelindwa zaidi na uwepo wa Muungano. Nje ya Muungano - wapo ambao tunaamini hivyo - mapinduzi ya Zanzibar hayasalimiki - tishio lake bado likiwa dhahiri kama lilivyokuwa 1964 au 1972 kufuatia mauaji ya Abeid Karume.
Mauaji ya Karume yangeweza kabisa kufanya counter revolution na kama tulivyoona kwenye ile clip ya Video Sultani Jamsheed alikuwa na matumaini kuwa "watu wake" wangeweza kumtaka arudi. Bila ya shaka alijisahau kuwa Zanzibar iko ndani ya Muungano na serikali ya Muungano isingeweza kuruhusu kutokea kwa counter revolution. Hadi hivi sasa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko salama - baadhi yetu tunaamini - kwa sababu ya Muungano; nje ya Muungano serikali hiyo iko matatani?
Je, yawezekana basi kuwa juhudi za kutaka kuvunja Muungano ni juhudi za kupinga mapinduzi? Kwamba, endapo Zanzibar ikafanikiwa kutoka kwenye muungano katika kile kinachoitwa 'umoja, udugu, na historia ya pamoja' mapinduzi ya Zanzibar yatakuwa hatarini? Je, Nje ya Muungano Mapinduzi ya Zanzibar yanaweza kulindwa?
Lakini swali kubwa - ambalo inshallah nitajaribu nami kulitafutia jibu ni hili: Kwanini Serikali ya Tanganyika itumike kulinda mapinduzi ya Zanzibar? Ni lini Wazanzibar wataanza kuwa tayari kulinda mapinduzi yao wao wenyewe bila kuwa ndani ya Muungano?
Je, tukiendelea na kampeni ya "Let Zanzibar Go" wananchi wa Zanzibar wataharakisha kutoka kwenye Muungano ili walinde mapinduzi yao - kama bado wanayathamini? Kama mtu wa bara naamini tumeshatumia kiasi cha kutosha kulinda mapinduzi haya na kuleta utulivu mkubwa visiwani bila jaribio lolote kubwa la counter revolution. Kwa vile hili ni kweli na kwa vile wapo Wazanzibari ambao wanaamini kuwa wako tayari kuyalinda na "kuyaenzi" mapinduzi haya vikundi vya Uamsho na mihadhara vitajipatia uhalali zaidi kama watahubbiri sifa za mapinduzi na kuwa wao watayalinda na kuyatunza kwani hawauhitaji Muungano kulinda mapinduzi hayo!
I was just saying....