Je, ni vibaya kunyonyesha ukiwa mjamzito?

Jamani ni siku ya tatu sasa tangu niweke huu uzi lakini hadi sasa sijapata msaada wowote,sijui huu uzi hauonekani au swali langu sio la msingi hata sielewi!!
 
Wadau,

Naombeni mnijuze kama kuna madhara yoyote kwa mtoto endapo mama atamnyonyesha huku akiwa na ujauzito mwingine.

Na je,ni baada ya kipindi gani mama anatakiwa kusitisha kunyonyesha akishajigundua kuwa ana ujauzito?

Hakuna tatizo.

Muhimu jitahidi sana wewe binafsi upate lishe ya kutosha.
Vile vile umwongezee mwanao wigo wa vyakula unavyompa ili kunyonya iwe ni ziada tu.
 
mpaka miezi saba wala usihofu acha mtoto anyonye ila mama ale vizuri na mtoto naye apewe vyakula vingine vizuri
 
Nilipata uja uzito mwanangu akiwa bado ananyonya akiwa na mwaka na miezi saba.

Research niliyofanya ni kuwa unaweza kunyonyesha ila ujue sasa calories zinazohitajika ni za alie tumboni, anaenyonya na wewe mwenyewe.

Pamoja na kuwa napenda sana kunyonyesha ilibidi tu nimuachishe mtoto nyonyo.
 
Kuwa makini..kuna wengne akinyonyesha hku akiwa ana ujauzito mara nyng huwa yule mtoto anadhoofika na kuharisha sana..ila sijafahamu ni kwanini.
 
Salaam wakuu,

Mimi ni mama mwenye mtoto mmoja wa kiume ambaye ana mwaka mmoja kamili sasa. Sasa hivi majuzi nikawa sijielewi elewi siku zangu hazikuwa sawa, jana ikabidi ninunue kipimo nipate kupima nikaona ni postive yaani nilishtuka sana kwa kweli kwasababu njia ya uzazi niitumiayo ni withdraw.

Sikutegemea kukuta hivyo nilivyokuta. Sasa maswali yangu ni haya;
Je niendelee kumnyonyesha mtoto wangu hatopata madhara
Na vipi suala la kuwa nae karibu sababu nilisikia joto langu linaweza muathiri. Je ni kweli.

Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu

Asante
 
Dada kuchomoa sio mchezo mana kuna zile maji maji za shahawa so mimba possibility lazma jamaa alijisahau akakojoa kidogo halafu akatoa shahawa za kwanza ndo zinatunga mimba
 
Ungekuwa jirani ningekupa dawa kutoka wa bibi yangu,ukiyumia hiyo utanyonyesha na kuwa karibu na motto kwa muda wa miezi sits zaidi mpaka unakaribia kujifungua pasipo kumletea madhara mtoto.

N.B ni mitishamba
 
Kapate ushauri kwa Daktari, lakini as a general rule Hakuna madhara.
 
Mpendwa pole na hongera na hali ambayo hukuitarajia. Ngoja nikupe experience yangu. Mimi yalinikuta kama yako wakati first born wangu akiwa na miezi kumi na moja hivi. Nilijaribu kumwachisha mtoto ziwa mtoto akagoma kabisaaaa. Watu wakaniambia nikomae hivyohivyo, nikashindwa maana mtoto akagoma sasa kula chochote.

Nikaamua tu nimnyonyeshe hivyo hivyo. Mpaka mimba imekua kubwa nilikua namnyonyesha, ila kwa vile nilikua naamini kua maziwa yangu hayatakua na ubora kwa ajili ya ujauzito nikawa pia namfeed chakula kizuri, mayai ya kienyeji, supu za samaki na maharage, maboga, pudding za matunda, kifupi niliwekeza kwenye chakula chake.

Huwezi amini last time kumnyonyesha usiku, alfajir yake naingia leba. Watu walikua wananishangaa sana before, niko na mimba kubwaaa halaf nanyonyesha, nilikua nasemwa sana hata nikienda clinic wamama wengine wamejijengea hiyo imani eti namwaribu mtoto, ila walikua wanashangaa, katoto kamenawiri kana afya, kachangamfuu, basi wanakaa kuitana kunishangaa.
 
Kwahiyo binafsi sijaona madhara yoyote, mtoto nilikua nalala nae beneti namkumbatia, nilikua karibu yake na kumjali vizuri kama before, nilipotoka hosp na mdogo wake nikamwambia sahivi nyonyo ni ya toto, kakaelewa kenyewe maisha yakasonga. Ingawa nilichoka, kunyonyesha mfululizo sio kazi rahisi, lakini niliona nikiwa mzembe na kuendeleza imani ambayo sikua na uhakika nayo mtoto angeyumba kiafya.
So, jiangalie mwenyewe, kama wewe ni mfanyakazi na kazi yako ni very demanding na mimba inakuchosha sana jaribu kumwachisha ila umsupplement mtoto na chakula bora, nikimaanisha mlo kamili, lakini vinginevyo unaweza tu kufanya kama mimi ika na wewe ule vizuri, mlo kamili. Wish u all the best
 
Hongeara mumy na pole it happened th same to mi..
Mimi nilianbiwa niweke maji kwny kitovu then nikamnywesha anaenyonya hlf nikasema wanangu nawaunganisha maziwa yasimdhuru..Mungu awajaalie.
They grew up very healthy n happy
Na vitu vingine ni imani tu na sala km alivyosema mdau hapo juu alinyonyesha hadi anaenda labour
 
Back
Top Bottom