Je, ni umbali gani unatakiwa kupandwa miti ifuatayo pembeni ya fensi ili mizizi isipasue msingi, mwisho ukuta?

Mizizi ya miti inaweza kutembea zaidi ya mita 15. Kwa viwanja vyetu vya 20x20, 30x30 ukipanda mti bado ni hatari kwa nyumba yako kama sio leo wakati wa uhai wako huko mbele lazima mizizi itamalaki eneo la nyumba yako. Cha muhimu jenga msingi imara wa nyumba angalau foot 3 (mita 1) kutoka usawa wa ardhi.

Pia janvi liwe la upana wa angalau inch 5 au 6 (unene) wa tofari na lishindiliwe vizuri. Mafundi wengi janvi ni inch mbili wanalipua huwe na uhakika mzizi utatokeza sebuleni au kwenye ukuta. Kwa tahadhari zaidi kama unataka nyumba yako izungukwe na miti mingi, zingushia msingi plaster ya zege kali.
 
Kuna baadhi ya miti ya matunda ina mizizi korofi sana. Mmoja wapo ni parachichi. Hasa hizi parachichi za asili. Pia kuna mti unajulikana kama grevilia(uchagani miti hii imejaa sana). Mizizi ya grevilia inajua sana kujipenyeza. Hii miti miwili usipande kabisa karibu na nyumba.

Mwembe wacha angalau mita 7 hadi 10 kutoka ukutani. Ukiachana na suala la mizizi pia matawi yake hujiachia sana kadri mti unavyozidi kukua.

Fenesi nao huwa unakua mkubwa sana. Huu panda shambani huko.

Jamii yote ya michungwa(chungwa, ndimu, chenza, limao). Kuanzia mita 4 hadi 7 toka usawa wa ukuta haisumbui.

Topetope, komamanga, nayo yote umbali kama wa michungwa tu bila kusahau mapera.

Stafeli huwa inarefuka sana. Zambarau pia weka shamba huko huu unakuaga mkubwa mno.

Mtanisahihisha kama kuna sehemu nimekosea
 
2. Miparachichi uwe na eneo kubwa panda katikati ila siyo karibu na kuta

3. Miembe - kapande shambani ...ukubwani inapasua kuta

Natanguliza shukrani!
Miti hatari hapo ni hiyo yenye red, mingine yote haina shida
 
Lima mipapai mizizi yake haina shida,kuhusu distance inategemea na aina ya miti ukuaji wake na aina ya mizizi
 
Hapo kwenye muembe nasubiri jibu.. Kuna muembe wangu matunda yake matamu... Kila nikifikiri kuukata nijenge msingi naona ugumu. Had nkawaza nipitishe msingi kwa pemben. Naiche cm 5 frm mti
we acha tu mi mwenyw nina mwembe dodo upo karibu.., nguvu za kukata imeniishia.., nilinunua kiwanja na miti kadhaa ndani yake
 
Panda mipapai tu, maana naona kama umelenga kupanda miti ufaidi matunda
 
Kuna baadhi ya miti ya matunda ina mizizi korofi sana. Mmoja wapo ni parachichi. Hasa hizi parachichi za asili. Pia kuna mti unajulikana kama grevilia(uchagani miti hii imejaa sana). Mizizi ya grevilia inajua sana kujipenyeza. Hii miti miwili usipande kabisa karibu na nyumba.

Mwembe wacha angalau mita 7 hadi 10 kutoka ukutani. Ukiachana na suala la mizizi pia matawi yake hujiachia sana kadri mti unavyozidi kukua.

Fenesi nao huwa unakua mkubwa sana. Huu panda shambani huko.

Jamii yote ya michungwa(chungwa, ndimu, chenza, limao). Kuanzia mita 4 hadi 7 toka usawa wa ukuta haisumbui.

Topetope, komamanga, nayo yote umbali kama wa michungwa tu bila kusahau mapera.

Stafeli huwa inarefuka sana. Zambarau pia weka shamba huko huu unakuaga mkubwa mno.

Mtanisahihisha kama kuna sehemu nimekosea
Umemaliza maelezo yote mkuu,ilibidi wakuandikie Excellent
 
Miti kando ya ukuta hutumiwa na wezi Kama ngazi/kivuko Cha kuingilia/kutorokea wakati wa kumtembelea mlengwa
Inafikirisha sana. Nje ukipiga michongoma bila ukuta halafu ndani ukaweka miti, na hiyo miti matawi yawe juu ninadhani itapunguza hii risk
 
Ili mizizi ya miti yoyote isisumbue kuta za nyumba au uzio chima mashimo yenye kina cha tuti3 *(mita 1 au zaidi) kwenda chini. Hii itasaidia miziz itakapo anzaa kutanuka na kusambaa kusambalia chini zaidi ya ardhi ambapo haifikii kuta za nyumba au uzio.
Tofauti na hapo utakuja ikata na kuacha ubovu wa nyumba na uzio ambao utakutesa.
Yamesha tukuta wengine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom